Katika maisha watu hujiwekea malengo
mbalimbali kama vile, kufunga harusi, kwenda kusomea kozi fulani, kununua
kiwanja, kununua gari, kujenga nyumba, kufungua biashara na malengo mengine
mengi binadamu anayoweza kupanga kichwani mwake.
Hapa nimekuletea hatua 3 rahisi sana ambazo
mtu unaweza ukazitumia katika kuandaa bajeti itakayokuwezesha kutimiza lengo
lolote lile ulilojiwekea kwani duniani hakuna malengo yasiyokuwa na bajeti.
Fedha ni muhimu karibu kwenye kila tukio siku hizi iwe ni shughuli au kitu
kingine chochote kile.
Ili kuweza kutekeleza mpango wowote ule ni
lazima kwanza uwe umejiwekea malengo. Hivyo basi huna budi kutambua kiasi cha
fedha utakazohitaji pamoja na muda katika kutekeleza mpango wako. Tuchukulie
mfano labda kwa kipindi hiki cha kiangazi ungetaka ununue Friza kwa ajili ya
kutengeneza Icecream za kuuza pale nyumbani kwako.
Unataka hadi kufikia mwezi Desemba mwezi wa (12)
basi uwe umeshapata shilingi laki 4 kwa ajili ya kununulia hilo friza. Hii
inamaanisha kwamba katika kila mwezi kuanzia mwezi huu ujao wa 9 utajiwekea
shilingi laki moja.
Baada ya kuhakikisha lengo hili uliloliweka
ni la kweli na linatekelezeka, kitakachofuata sasa ni kuamua hatua
utakazozichukua ili kulifikia lengo hilo. Zoezi hili litahusisha hatua kubwa 3
zifauatazo;.........
...............................................................
Somo hili ndugu msomaji tutajifunza leo tarehe 20/8/2018 katika group la whatsap la MICHANGANUO ONLINE ambalo tunakuwa na masomo yahusuyo fedha kila siku kuanzia saa 3 hadi saa 4 usiku. Pia tunakuwa na semina za kuandika Michanganuo ya biashara kila mwezi.
Unapojiunga tunakupa masomo na semina zote zilizokwishapita, vitabu na michanganuo halisi ya biashara mbalimbali ikiwemo ya ufugaji wa kuku aina zote na kilimo cha matikiti maji.
Ukitaka kujiunga unalipia kiingilio sh. elfu 10 kwenye namba 0712202244 au 0765553030 kisha unatuma kwa meseji anuani yako ya email ikiambatana na ujumbe, "NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO" Tutakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia kila kitu. Namba yetu ya whatsap ni 0765553030
0 Response to "KUFIKIA NDOTO NA MALENGO YAKO, HIZI HAPA NI HATUA 3 ZA KUTENGENEZA BAJETI YA JAMBO LOLOTE MAISHANI "
Post a Comment