Nishati ndiyo msingi wa asili, ambao kutoka
kwake asili hutengeneza kila kitu kilichopo Ulimwenguni, akiwemo binadamu na
kila aina ya wanyama na maisha ya mimea. Kupitia mchakato wa asili ambao ni asili
tu inayoufahamu kikamilifu unaigeuza nishati kuwa maada.
Viasili vya uumbaji hupatikana kwetu katika
nishati inayohusika katika kufikiria. Ubongo unaweza ukafananishwa na betri ya
umeme. Hunyonya nishati kutoka angani, ambayo husambaa katika kila atomu ya
maada na na kujaza Ulimwengu mzima. Kundi la betri za umeme zitatoa nishati
kulingana na idadi na uwezo wa seli zilizokuwa nazo. Ubongo hufanya kazi kwa
namna inayofanana.
Hii ni sababu ya baadhi ya ubongo(akili) kuwa
na ufanisi kushinda nyingine, na kusababisha kauli hii muhimu – kundi la
akili(ubongo) zilizoratibiwa(au kuunganishwa) katika roho ya masikilizano
litatoa nishati nyingi zaidi ya mawazo kuliko ubongo mmoja kama tu ilivyo kwa
kundi la betri za umeme zitakavyotoa nishati zaidi kushinda betri moja. Kupitia
huu mfano mara moja inakuwa dhahiri kwamba kanuni ya ushirika hubeba kanuni ya
nguvu iliyotwaliwa na watu ambao hujihusisha wenyewe na watu wenye akili.
Inafuata sasa kauli nyingine ambayo itaongoza
bado karibu na uelewa wa kiroho wa ushirika: Kundi la akili za watu
linaporatibiwa na kufanya kazi kwa masikilizano, nishati ya ziada
inayotengenezwa kupitia ushirika huo hupatikana katika kila ubongo(akili) ya
mtu mmojammoja ndani ya kundi hilo.
Henry Ford alianza biashara yake akiwa na
kilema cha umasikini, kutokuwa na elimu na ujinga. Ndani ya kipindi kifupi
kisichofikirika cha miaka 10 Bwana Ford alivishinda vilema hivi vitatu, na
ndani ya miaka 25 aliweza mwenyewe kuwa mmoja wa watu matajiri zaidi Marekani.
Unganisha na ukweli huu ujuzi wa ziada kwamba, hatua za haraka alizopiga Bwana
Ford zilianza kuonekana tokea muda alipoanza urafiki na Thomas A. Edison na
utaanza kutambua athari ambazo ubongo mmoja unaweza ukawa nazo dhidi ya
mwingine.
Nenda hatua moja zaidi na zingatia ukweli
kwamba, mafanikio makubwa ya Bwana Ford yalianza tokea muda alipoanza
kufahamiana na Henry Fireston, John Burroughs na Luther Burbank(kila mmoja
akiwa ni mtu wa akili yenye uwezo mkubwa) na utakuwa na ushahidi zaidi kuwa
nguvu hiyo inaweza ikapatikana kupitia ushirikiano wa kirafiki wa
ubongo(akili).
Itaendelea......
Usikose somo la leo 20/8/2019 usiku saa3 katika Group letu la
Whatsap na mada itakuwa ni;
“KUFIKIA
NDOTO NA MALENGO YAKO, HIZI HAPA NI HATUA 3 ZA KUTENGENEZA BAJETI YA JAMBO
LOLOTE MAISHANI”
Masomo ni kila siku, kujiunga namba ya wasap ni 0765553030 *kuna kiingilio sh. 10,000/-*
Masomo ni kila siku, kujiunga namba ya wasap ni 0765553030 *kuna kiingilio sh. 10,000/-*
0 Response to "MAFANIKIO MAKUBWA YA HENRY FORD YALIANZA PALE ALIPOANZA USHIRIKIANO NA MATAJIRI WENGINE"
Post a Comment