Semina yetu ya kuandika michanganuo ya biashara zilizo na
fursa kubwa ya kutengeneza faida inaendelea ndani ya Group la Whatsap la
MICHANGANUO-ONLINE. Mchanganuo tunaoandika leo unahusu Biashara ya kilimo cha
matikiti maji katika eneo la Kibada Kigamboni jijini Dar es salaa. Ni
mchanganuo wa 3 kati ya 12 tutakayochanganuo katika kipindi cha miezi 6 ijayo.
Semina imeanza leo tarehe 9/8/2018 na itamalizika rasmi siku ya tatu hapo
tarehe 11 siku ya Jumamosi.
MAELEZO
YA BIASHARA.
Kibada
watermelon Fruits ni shamba jipya la heka 2 lililoanzishwa kwa
lengo la kuzalisha na kuuza matunda ya tikiti maji yenye ubora wa hali ya juu
katika jiji la Dar es salaam. Matikiti maji yetu yatakuwa na ukubwa utakaomvutia
mteja kutokana na utunzaji makini na uwekaji wa virutubisho vya kutosha katika
mimea ya matikiti maji.
Kampuni itakuwa na makao yake eneo la Kibada
Kigamboni na itasajiliwa rasmi kwa msajili wa Makampuni ili kuweza kukidhi
vigezo vya kufanya biashara na kila mtu yakiwemo makampuni yanayomiliki
mahoteli pamoja na supermarkets.
Dhamira
kuu.
Dhamira yetu ni kuzalisha matikiti maji
makubwa yaliyo na ubora wa hali ya juu yatakayomvutia kila mteja kwa kutumia
njia za kisasa kabisa za kilimo cha matikiti maji.
Dira
Dira yetu ni kuwa kampuni kubwa kabisa
itakayouza matikiti maji yaliyo na ubora wa hali ya juu katika ukanda mzima wa
Pwani ya Afrika Mashariki.
Malengo.
· Kulima
heka moja kwa kila mzunguko mmoja itakayotoa matikiti maji yapatayo 5500
· Kupata
faida ya shilingi milioni 11 kwa mwaka
· Kulima
matikiti maji mizunguko 3 ya siku 90 kwa mwaka.
· Kulima
matunda na mbogamboga za aina nyingine siku za baadae katika maeneo ya mashamba
tunayoyapumzisha katika mzunguko wa matikiti maji.
Siri
za mafanikio
· Kutumia
mbolea ya samadi sambamba na zile za viwandani kwa kiasi cha kutosha
kuhakikisha matunda makubwa na yaliyo na ubora wa hali ya juu.
· Kuwapelekea
matikiti maji wateja hasa hoteli kubwa na supermarkets mpaka mlangoni.
· Kuhakikisha
soko la uhakika lipo pindi tu matikiti maji yanapoanza kutoa maua.
Umiliki
wa biashara........
...................................................................................
Kujiunga na Group hili kwa ajili ya semina zote
zitakazofuata na zile zilizokwishafanyika pamoja na masomo ya kila siku jiunge
na group hili kwa kutoa kiingilio shilingi elfu 10 kupitia namba zetu za simu,
0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo.
Baada ya malipo tuma namba unayotumia wasap na anuani yako ya email kisha
ujumbe unaosema, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”
0 Response to "MCHANGANUO WA BIASHARA YA KILIMO CHA MATIKITI MAJI KIBADA KIGAMBONI"
Post a Comment