Kwenye Ulimwengu wa biashara upo usemi usema, “Cash
is a king” au Pesa taslimu ni
kama mfalme, Usemi huu una maana kubwa sana hasa ukizingatia kwamba ili
biashara iweze kuendelea vizuri inahitaji fedha taslimu kwanza za kulipia
gharama mbalimbali kabla mauzo hayajafanyika, pia yanaweza yakawa ni mauzo kwa
mkopo ambapo hapa biashara inakuwa bado haijaingiza pesa taslimu.
Tuchukulie mfano mmoja wa mtu aitwae Juma aliyeamua
kuanzisha biashara ya kuuza kuku wa kienyeji ambao anawafuata mikoani na kisha
kuja kuwauza jijini Dar es salaam. Juma baada ya kugundua kwamba biashara hii
ya kuku ina faida nzuri na nono, aliamua kuanza kuifanya lakini mtaji aliokuwa
nao ulikuwa ni kidogo mno, hivyo alimkopa mtu shilingi laki 3 kwa lengo la
kwenda kununulia kuku wakubwa 300 kwa bei ya shilingi elfu 10 kila mmoja halafu
baadae ndipo amrudishie mwenyewe pesa zake.
Alitarajia atakapowafikisha hao kuku katika masoko ya Dar
es salaa angewauza kila mmoja kwa shilngi elfu 20 mpaka elfu 25 na hivyo
kutengeneza jumla faida ya shuilingi laki 3 juu, tena chapchap.
Lakini ilikuwa rahisi kiasi hicho Juma kutengeneza kiasi
kikubwa namna hii cha cha faida katika muda mfupi hivyo? Huu ndiyo mtego ambao
wajasiriamali wengi huingia pasipo kujua na baadae kuja kujutia sana kwanini
walianzisha biashara kwa msukumo tu wa faida kubwa kabla kwanza ya kutafiti au
hata kuingia kidogo kwanza katika uhalisia wa mambo ulivyo ndipo waweke fedha
zao nyingi.
Mdudu hatari tunayemzungumzia leo hii hapa siyo mwingine
bali ni UKOSEFU WA FEDHA TASLIMU ZA UENDESHAJI KWENYE BIASHARA(WORKING CAPITAL)
au kwa lugha nyingine tunaweza tukasema mzunguko mdogo wa fedha taslimu
unaosababisha biashara kushindwa
kujiendesha na hatimaye kufa ingawa faida ipo nyingi tu. (Masomo kama haya na mengineyo
kuhusiana na fedha kwa undani kabisa ndiyo tunayojadili kila siku usiku saa 3
katika Group la MICHANGANUO-ONLINE.)
Juma anapokwenda zake Morogoro kufuata kuku kwa fedha za
mkopo shilingi laki 3 kumbuka anatakiwa pia mbali na kwenda kuwalipia hao kuku,
ale chakula na maji njiani, akalale nyumba ya wageni pale Moro, alipe nauli ya
basi, awalipie hao kuku usafiri kutoka hapo Moro mpaka Dar na ushuru wa soko au
njiani. Akiwafikisha Dar kuna gharama za kuwalisha siku mbili tatu watakazokuwa
wakisubiri wanunuzi nk.
Si hivyo tu wakati wa kuwauza wataibuka wateja wengine
ambao watataka kuchukua kuku kwa mkopo na kisha kuja kulipa baada ya siku
kadhaa au hata mwezi na kwa kuwa ni wateja wenye ofizi zao kama migahawa,
huwezi kuwakatalia au kuhofia watakuzima pesa zako. Lakini Juma mategemeo yake
ya haraharaka yalikuwa kwamba, laki 3 angenunua hao kuku 30 atakaouza kila mmoja kwa shilingi
elfu 20-25 apate faida laki 3 na ushee ndani ya siku chache tu kisha arudi tena
Moro kufuata mzigo mwingine wa ‘ndege’. Kwa kifupi ni kwamba Juma mawazoni
mwake alikisia umilionea kumnyemelea ndani ya miezi michache tu ijayo.
Badala yake Juma alipofika Morogoro alitahamaki mfukoni
amesaliwa na shilingi laki moja na elfu sabini tu, fedha ambazo hazikuweza tena
kununulia kuku 30 kama alivyokuwa amepanga awali.Aliishia kununua kuku 25 na
mfukoni akabakiwa na elfu 30 hivi. Alipokuja kwenye malori ya mizigo
wakamwambia mzigo ili uweze kufika Dar es salaam walitaka shilingi elfu 50
ambazo Juma hakuwa nazo, alikuwa na elfu 30 peke yake.
Ilimbidi Juma akimbie tena kwenda kwa rafiki yake mmoja
anayeuza kuku pale Morogoro na kumkopa shilingi laki moja nyingine ili
atakaporudi kutoka Dar amrejeshee fedha zake, kwa bahati njema jamaa alikubali
akampatia laki moja.
Juma alifanikiwa kuufikisha mzigo Dar salama na kesho
yake ilimkutia pale Manzese darajani kando kando kabisa ya daraja kwenye banda
la kukodi la kuuzia kuku wa kienyeji. Alitakiwa kila siku alipe shilingi elfu 5
auze asiuze, na kuku wale mpaka kuja kumalizika ilimchukua siku 5 huku akiwa
amekopesha kuku 8 kwa mwenye hoteli moja pale pale Manzese.
Ingawa mzigo haukuchukua muda mrefu lakini Juma hakuwa
tena na fedha za kutosha kwenda kufuata
mzigo mwingine Morogoro. Huku nyuma mdai wake aliyemkopesha laki tatu alimjia
juu ile mbaya akitaka angalao amrudishie hata laki moja na nusu kwanza kiasi
kingine aje kumalizia akiuza mzigo wa pili. “Si umeuza mzigo wote wewe, sasa
kwanini usinipe hela yangu?” jamaa
alimfokea Juma kwa ghadhabu.
Ulikuwa ni ugomvi mkubwa. Siku hiyohiyo rafiki wa Morogoro
naye aliyemkopesha laki moja alikuwa akipiga simu utadhani kapagawa vile, “Juma
chondechonde nakusubiri hapa stendi nimekwama kishenzi, njoo haraka na kale
kamzigo kangu”
Biashara ya Juma ya kuku kama angelikuwa na mtaji wa
kuiendeshea (Working capital) kwa kweli angeweza kutajirika haraka sana
kama alivyokuwa amedhamiria mwenyewe. Lakini kwa kuwa hakuwa nao, alitegemea
mtaji wa kuungaunga tena wa kukopa, sasa anazidi kujiongezea umasikini, kaingia
migharama kibao wakati biashara si endelevu inaishia njiani na kubaki na mideni
lukuki ambayo hata yanaweza kumsababisha ahame mji au hata kufikia hatua mbaya
zaidi ya kujitoa uhai wake shauri ya madeni.
Juma alipaswa angalao kuwa na kiasi cha fedha zake
mwenyewe kwanza kama shilingi laki 3 ndipo sasa akaazime nyingine tena laki 3.
Hapo biashara hii yenye faina nono na nzuri ingeliweza kufanikiwa. Au pia kama
ni kukopa basi alipaswa kuhakikisha anakopa kiasi kinachotosheleza mahitaji
yote ya biashara hiyo na siyo tu kukubali kupokea hela ya mkopo kinjaa njaa kwa
vile kaona pesa halafu anakuja kukwama na fedha za wenyewe nazo kukatikia
humohumo.
Kosa la kuingia mikopo isiyokidhi mahitaji ni watu wengi
hulifanya na husababishwa na watu hao kutokufanya tafiti za biashara zao kabla
na kuandaa japo mpango rahisi tu unaoonyesha wanahitaji mtaji kamili kiasi gani.
Wala mpango huo si lazima kuuandika, unaweza hata kuupangia ndani ya kichwa
chako ingawa kuuandika kuna faida za ziada.
…………………………………………………
UKWELI
KUHUSU KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA
1. Mpango
wa biashara siyo kitu cha ajabu, ni vile unavyofikiria juu ya biashara yako tu
basi, hakuna cha zaidi ya hapo.
2. Kila
mtu mwenye uwezo wa kufanya biashara, moja kwa moja ‘automatically’ anao uwezo
pia wa kuandaa au kuandika mpango wa biashara yake.
3. Ushahidi
kwamba mpango wa biashara kila anayefanya biashara anaweza pia kuandaa, tazama
watu matajiri wengi wa zamani waliofanikia wengine hata shule hawakwenda kabisa
halafu ujiulize mipango ya biashara zao waliandika wapi na lini? Kama hawakuandika
sasa waliwezaje kufanikiwa?
4. Ukweli
ni kwamba watu wengi mipango ya biashara zao huipangia kichwani tu kitu ambacho
ni sahihi kabisa lakini uwezo wa vichwa vya wanadamu hutofautiana na ndiyo
maana mwingine anapoandika mahali mipango yake ndiyo huweza kuitekeleza na
kunyooka vizuri zaidi.
5. Ikiwa
wewe uwezo wako wa kupanga kichwani tu peke yake si mkubwa jaribu pia kutumia
karatasi na kalamu kuweka mipango yako. Wenzetu Wazungu kwa hili wametupita
sanan na pengine ndiyo sababu kubwa ya maendeleo yao makubwa kutuzidi sisi
Waafrika.
Katika GROUP LA MICHANGANUO ONLINE ambapo washiriki
hujifunza kupitia WASAP na EMAIL tunajifunza masomo ya namna ya kuandaa mpango
wa biashara yeyote ile kwa kichwa na pia kwa kuandika katika karatasi. Hata uwe
mvivu kiasi gani kwenye mambo ya kuandika-andika, course hizi unaweza tu
kujifunza kupitia kusoma michanganuo ya biashara mbalimbali na ukajijengea
uwezo mkubwa wa kuandaa mpango wa biashara yako yeyote ile kichwani tu pasipo
hata kuandika mahali.
KIFURUSHI
(PACKAGE) CHA MASOMO YA MICHANGANUO YA BIASHARA.
Kuna kozi kamili ya kuandika mpango wa biashara yenye
masomo 11, vitabu, cha kiingereza na cha Kiswahili, michanganuo halisi
mbalimbali iliyokamilika kila kitu kuanzia Kasha la nje(jalada) mpaka makisio
ya hesabu zote na vielelezo halafu kuna semina 12 za kuandika michanganuo yabiashara bunifu hatua kwa hatua ambazo semina ya tatu tunakwenda kuifanya siku
ya Alhamisi wiki hii tarehe 9/8/2018. Nyingine zitafuata mpaka mwisho wa programu
hii Februari 2019 kabla hatujaanza kampeni nyingine tena.
Ukipata package(kifurushi) hiki chote kizima unakuwa
umejijengea uwezo mkubwa wa kupanga biashara yeyote ile utakayoianzisha na
utakuwa vilevile umeongeza mara dufu uwezekano wa kufanikiwa biashara yeyote
ile utakayoifanya kwani unakuwa umemaster ‘ABCD’ zote za biashara.
Kwa habari zaidi kuhusiana na semina ya Alhamisi tarehe 9/8/2018 fungua hapa, SEMINA 12 ZA KUANDIKA MICHANGANUO BUNIFU YA BIASHARA.
Usisahau pia kuwa leo 4/8/2018 kwenye group la ICHANGANUO-ONLINE tutakenda kujifunza somo muhimu sana la pesa lisemalo,
JE, UNAIFAHAMU THAMANI YAKO HALISI KATIKA FEDHA, UTAJIRI NA MALI UNAZOMILIKI?
Usikose somo hili na ikiwa utachelewa kujiunga basi bado unayo nafasi ya kupata somo hili na mengine yote toka January mwaka huu lakini kabla ya february mwaka ujao. Simu 0712202244 na wasap ni 0765553030.
0 Response to "MDUDU HATARI ANAYEWEZA KUUA BIASHARA YAKO HARAKA LICHA YA KUWA INAINGIZA FAIDA KUBWA"
Post a Comment