Biashara ndogo inayostawi inamhitaji mmiliki
wake kuwa na malengo na umakini wa hali ya juu katika usimamizi. Hiyo ndiyo
kazi ya mjasiriamali ya kwanza kabisa ikiwa atapenda biashara yake kukua haraka
na kufikia kuwa biashara kubwa au ya kati. Umakini huo pia unahitajika katika
matumizi mazuri ya muda na utekelezaji sahihi wa majukumu katika kuongeza kasi
ya mafanikio ya biashara.
Ni bahati mbaya kwa wajasiriamali wengi
wakati wangependa kutekeleza majukumu ya biashara zao kwa ubunifu mkubwa
huibuka vidakizi ambavyo vinarudisha nyuma kasi ya utendaji wa shughuli muhimu
za biashara na hata wakati mwingine kuwa ndiyo chanzo cha vifo vya biashara
nyingi zinazoanza kabla hata hazijatimiza umri wa mwaka mmoja.
Kabla hatujaenda kuona jinsi ya kukabiliana
na tatizo hili la vidakizi hebu kwanza tuone vidakizi ni kitu gani, Vidakizi ni
kitu chochote kile kinachoingilia kati wakati mtu akitekeleza kazi au jukumu la
msingi la biashara. Hivyo tunapomzungumzia mjasiriamali mdogo na biashara yake
ni vile vitu vinavyomfanya kuachana na mambo ya msingi anayopaswa kuyafanya na
kuelekeza usikivu wake na akili kwavyo. Mara nyingi vidakizi huwa havina faida
yeyote ile zaidi ya kula tu muda wa mjasiriamali na kusababisha ufanisi wake
kuwa mdogo.
Kwa mfano mtu anakuwa anachapa kazi za
ofisini mara meseji, sms ya mapenzi inaingia kwenye simu yake ya mkononi,
meseji hii ni kidakizi kwani imeingilia kati kazi ya msingi ya biashara.
Vidakizi pia vyaweza kuwa ni moja kati ya vitu hivi vifuatavyo;
· Kupigiwa
simu
· Kusoma
gazeti au kitu kingine chochote kile ambacho hakihusiani na kazi
· Email
· Mitandao
ya kijamii
· Kusikiliza
redio,muziki au kutazama TV.
· Kutazama
video na picha mbalimbali.
· Mazungumzo
na watu wengine muda wa kazi
· Kuchati
na marafiki
· Na
hata maombi na sala ikiwa siyo muda wake inaweza kuwa ni kidakizi pia.
Chanzo cha mafanikio yeyote yale yawe ni
katika biashara, mafanikio kieleimu na hata mafanikio katika kazi mbalimbali ni
umakini(focus). Na ili mtu kuweza kuwa makini hapaswi kabisa kuviendekeza
vidakizi wakati anapokuwa akitekeleza majukumu yake ya msingi ya biashara au
kazi. Kwakuwa vidakizi hatuwezi kuvikwepa kabisa kwa asilimia 100%, lakini zipo
njia mjasiriamali anaweza akazitumia na hatimaye kuvipunguza kabisa na kuwa
mjasiramali aliyefanikiwa. Njia hizo ni hizi hapa chini;
1.Kuzingatia
ratia
Kamwe usikubali kuondoka kwenye jukumu ambalo
tayari ulishalipangia muda wa kulifanya. Zingatia unakamilisha kwanza jukumu
hilo hata kama vidakizi vitaibuka kwa njia gani. Wajulishe marafiki na wale
wanaokutumia ujumbe muda wa kazi kuwa huna nafasi muda huo na ikiwezekana zima
kabisa vifaa vinavyohusika katika kukuletea vidakizi mfano simu, redio, kompyuta
nk.
2.Gawa
majukumu.
Siyo kila wakati utafanya kila kitu wewe
mwenyewe, mjasiriamali makini anayefahamu vyema ni nini maana ya ujasiriamali
ni lazima wakati mwingine akubali kuwa ili mambo yaweze kwenda mbele basi
anatakiwa kusaidiwa majukumu na watu wengine . Kugawa majukumu kwa watu wengine
kwanza kunaonyesha unawajali wengine na pia kunazidisha hali ya kuaminiana
katika biashara au kampuni. Hupunguza vidakizi kwa kiasi kikubwa.
3.Simamia
kikamilifu malipo ya bili mbalimbali.
Hili ni eneo nyeti sana katika biashara
yeyote ile ndogo kwani linahusika moja kwa moja na mtiririko wa pesa kwenye
biashara yako. Mafanikio na afya ya biashara ndogo hutegemea sana mtiririko
mzuri(chanya) wa fedha kwani ndiyo kitu kinachoweza kuamua ikiwa biashara ife
au iendelee kuwa hai, Kwahiyo hakikisha kwamba kama kuna mazingira
yatakayokulazimisha ukopeshe , vilevile basi kuwe na utaratibu mzuri na
unaoeleweka wa kudai madeni kwa wakati.
SOMA: Ikiwa huwezi kusimamia mahesabu ya biashara yako ni bora ukaachana nayo vinginevyo utavuna mabua.
SOMA: Ikiwa huwezi kusimamia mahesabu ya biashara yako ni bora ukaachana nayo vinginevyo utavuna mabua.
Hali kadhalika ikiwa wewe (biashara yako)
italazimika kukopa mahali, hakikisha pia unasimamia kikamilifu deni lilipwe kwa
wakati muafaka. Kwa malipo ya zile bili zinazojirudia kama vile umeme na maji ili kuokoa muda unaweza
ukaweka mfumo utakaokata madeni hayo moja kwa moja(automatically) katika
akaunti yako ya benki muda wa malipo unapofika.
Hizo ni njia chache za kupambana na vidakizi
katika biashara ndogo. Kila biashara na kila mjasiriamali ni tofauti na hivyo
kila mmoja anaweza akawa na vidakizi tofauti vinavyoweza kuiba muda wake wa
thamani katika biashara. Fikiria ni kitu gani kwa upande wako kinachoweza kuwa
kinadakia majukumu yako zaidi na
kukupunguzia ufanisi wa kazi.
Kufanya marekebisho madogo lakini muhimu
katika mfumo na mtindo wako wa uendeshaji biashara kunaweza kukasababisha
tofauti kubwa itakayokuletea matokeo bora kabisa katika mafanikio ya biashara
yako.
...........................................................................
Ukitaka vitabu vya ujasiriamali kwa lugha ya kiswahili tembelea hapa; SMART BOOKS TANZANIA
Kujiunga na group letu la whatsap la masomo ya kila siku na semina za kila mwezi za michanganuo ya biashara lipia kiingilio kupitia namba zetu, 0712202244 au 0765553030 whatsap 0765553030
Kuandikiwa mchanganuo wa biashara yako bonyeza hapa, HUDUMA ZETU
Leo tarehe 22 August katika group la wasap tutakuwa na somo lihusulo, "JINSI YA KUSIMAMIA HESABU KWENYE BIASHARA NDOGO UNAYOMWACHIA MFANYAKAZI" Ni saa 3 mpaka saa 4 usiku, usikose.
Leo tarehe 22 August katika group la wasap tutakuwa na somo lihusulo, "JINSI YA KUSIMAMIA HESABU KWENYE BIASHARA NDOGO UNAYOMWACHIA MFANYAKAZI" Ni saa 3 mpaka saa 4 usiku, usikose.
0 Response to "NJIA YA MAFANIKIO NI NYEUPE KWA MJASIRIAMALI MDOGO ANAYEWEZA KUVIKWEPA VIDAKIZI HIVI."
Post a Comment