Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa wahi kiti chako hapo! Ndiyo leo ninavyoanza ndugu msomaji wangu nikitaka kukujulisha kule tulikotokea na tunakoelekea nusu hii ya 2 ya mwaka huu wa 2018.
Tangu mwaka huu uanze tumekuwa tukitangaza na kuhubiri semina za michanganuo ya biashara zile zilizokuwa na fursa kubwa ya kutengeneza faida, tukasema kwamba kila mwezi tungekuwa na semina moja huku masomo ya mzunguko wa pesa yakitolewa kila siku, hayo ndiyo yaliyokuwa malengo yetu ya mwaka 2018.
SOMA: Mzunguko mzuri wa fedha ndiyo njia bora zaidi ya kufikia malengo yako mwaka 2018
Kwa yule anayetufuatilia kwa karibu hususani wateja wetu
waliojiunga na GROUP LA WATSAP LA MICHANGANUO ONLINE kwa kweli wanaweza
wakafikiri labda tuliwahadaa kwa kuwatangazia kitu ambacho hatuwezi kukitekeleza.
Lakini naomba nichukue nafasi hii kwa heshima na taadhima kuwaomba kwamba,
wasikasirike kwani sasa nusu hii ya pili ya mwaka 2019 tunakwenda kumalizia
kila kitu tulichoahidi kama Mwenyezi Mungu atatupa uzima, nasema hivyo kwani
kama ujuavyo ‘Mipango si matumizi’ japo haiepukiki ni lazima binadamu tupange
karibu kila kitu tunachokifanya ili kiweze kwenda vizuri.
SOMA: Ratiba ya masomo ya semina hii hapa.
SOMA: Ratiba ya masomo ya semina hii hapa.
Nashukuru kwa upande wa masomo ya siku, tulijitahidi sana
japo pia siku chachechache hatukuweza kutimiza. Programu yetu kwa mwaka huu
ijulikanayo kama MZUNGUKO WA FEDHA NDIYO NJIA BORA ZAIDI YA KUFIKIA MALENGO
YAKO MWAKA 2018 ilianza rasmi hapo mwezi Februari mwaka huu na itamalizika
rasmi mwakani mwezi Februari 2019. Kampeni ya mwaka jana iliyokuwa imeitangulia
hii ilijulikana kama, MAKE YOUR SELF GREAT AGAIN au JIRUDISHIE UKUU WAKO TENA na
nakumbuka ilikuwa nzuri sana na watu wengi walihamasika mno nayo.
SOMA: Ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena(MAKEYOURSELF GREAT AGAIN)
SOMA: Ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena(MAKEYOURSELF GREAT AGAIN)
Ninachotaka hasa kusema leo ni kwamba, kama tulivyokuwa
tumeahidi wakati kampeni hii inaanza, Michanganuo bunifu 12 mwaka huu ni lazima
wale wote waliojiunga na Group letu Whatsap na wale wanaoendelea kujiunga sasa
hivi mpaka itakapofika hiyo Februari, wajifunze na kuipata ili kuwa nayo yote
12.
Tutaandika nao hatua kwa hatua kama tulivyoanza pale
mwanzoni. Kumbuka tayari tulikwishaandika Michanganuo mingine 3 ya Kuku wa
mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji. Yote hiyo kwa aliyewahi kuisoma siyo
michanganuo ya kawaida tu kama ilivyozoeleka bali ni michanganuo YA BIASHARA
BUNIFU ZENYE UWEZO WA KUZALISHA FAIDA KUBWA NA YA HARAKA.
Siku ya Alhamisi ya tarehe 9 August, 2018 tutakwenda kuwa
na semina yetu ya tatu 3 na Jina la biashara bado lipo kapuni halijatajwa,
tutalizindua rasmi siku hiyo hiyo kwa wale washiriki wa semina. Ni biashara ambayo
kila mtu atatamani kuifanya. Wanasema wazo la biashara haliigwi, ni kweli,
lakini tusidanganyane bwana kama biashara inalipa kwanini mtu usiige na
kuongeza maboresho?
SOMA: Ukibuni kitu kizuri ni kwanini watu lazima wakopi?
SOMA: Ukibuni kitu kizuri ni kwanini watu lazima wakopi?
Ni nani anayependa kuuza kitu ambacho kutwa kucha haoni
mteja wakati wenzake wanapiga hela kila dakika? Nani wa kufa njaa usawa huu ulivyokuwa mgumu,
ni lazima tukubali kuwa wabunifu lakini pia tuangalie na vile vitu ‘hot cake’ vinavyotoka chapchap kama tunapenda
kutoka haraka kimaisha.
Semina yetu ni ya siku 3 na itaanza rasmi saa 4 asubuhi
mpaka saa 8 mchana kila siku kwa siku hizo 3 mpaka Jumamosi.
Kwa masaa hayo manne wakufunzi wako tutakuwa macho muda
wote hewani(online) tukifuatilia darasa kwa karibu kabisa huku tukiwa tayari
kwa swali lolote lile kutoka kwa mshiriki yeyote atakalouliza. Siyo semina ya
kitoto kabisa kwani tumepata uzoefu mkubwa kutokana na semina zilizopita huko
nyuma, tunaelewa wateja wetu wanataka kitu gani na tunawapatia kile
wanachokitaka vilevile bila kupunguza chochote, zaidi tunawaongezea.
SOMA: Utambulisho rasmi wa semina ya kuandaa mpango wa biashara.
SOMA: Utambulisho rasmi wa semina ya kuandaa mpango wa biashara.
Baada ya semina hii ya Alhamisi, tutakuwa na mfululizo wa
semina nyingine karibukaribu ili kutimiza azma yetu ya kuwa na semina 12
itakapofika tamati ya kampeni yetu hii mwezi wa 2 mwakani. Unajua bwana, mpango
wa biashara kuna watu hubeza kwamba eti, oo.. mipango si matumizi…, utapangaje
wakati mambo hubadilika kila mara kwa kasi ya ajabu….., mpango wa biashara ni
kupoteza muda bure……., na bla bla nyingine kibao. Lakini mimi napenda tu
kuwaeleza hao rafiki zangu kwamba, hebu waache kuwadanganya watu kwani hakuna asiyepanga mipango kichwani mwake hata
kama anataka kuanzisha genge sembuse biashara ya mamilioni ya shilingi.
Utakuta mtu anaponda mipango wakati yeye biashara zake
zinamuendea vizuri kutokana na mipango mizuri anayoandaa kabla ya kutekeleza
biashara zake. Siri moja niliyogundua ni kwamba watu wengi hasa sisi Waafrika
ni wazuri sana kupanga vichwani mwetu kuliko kwenye kipande cha karatasi.
Wenzetu wazungu unajua ni kwanini karibu kila sekta wametuzidi?......... Njoo
kwenye group bwana mambo haya tuje tuyadiscuss pamoja naona hapa muda hautoshi.
Mimi rafiki yako Peter Augustino Tarimo, nakuthamini sana
msomaji wangu, uwe unasoma makala kwenye blogu ya jifunzeujasiriamali, uwe ni
kwenye makala ninazotuma kwa njia ya email au hata katika mitandao mingine ya
kijamii ninakopost post makala zangu. Lakini naomba nikuambie kwamba Binadamu
hata uwe na ufanisi wa kiasi gani ndugu yangu kamwe huwezi ukamridhisha kila
mtu hapa duniani. Makala zangu hata zingekuwa nzuri kiasi gani, bado kuna watu
watakaoziponda na kuziona hazina maana. Kwahiyo kuna njia moja tu hapa duniani
mtu unaweza ukawapa zaidi wale wanaochagua kukufuata au kuthamini zaidi kile
unachotoa.
SOMA: Ingawa mipango si matumizi lakini haiepukiki kwenye maisha na biashara.
SOMA: Ingawa mipango si matumizi lakini haiepukiki kwenye maisha na biashara.
FOCUS,
sijui niliweke vipi neno hili kwa Kiswahili lakini nadhani ni kuamua kuchagua
vitu vichache vyenye ufanisi zaidi utakavyodili navyo. Sina maana kwamba basi
nisithamini tena wasomaji wangu wa blogu ya jifunzeujasiriamali hapana, bali
niwe na kipande maalumu “Segment” ambayo nitawapatia kile
watakachoniambia wenyewe niwape bila mimi kuwasukuma au kuwakazania. Hii ndiyo
sababu kubwa ya kuanzisha GROUP LA WATSAP LA MICHANGANUO ONLINE.
Group ni la wasap lakini siyo lazima uwe unatumia wasap
ndipo uweze kupata masomo na semina zinazotolewa hapana, tunatuma pia masomo
hayo kwa njia ya Email na hata tuna blogu maalumu ya private tunakoyaweka
masomo yote na semina tunazozitoa. Halikadhalika ndiyo maana tukawa na email
list ambayo kwa mtu kujiunga/kusubscribe, basi mtu huyo anaonyesha kile
unachokitoa anakithamini zaidi na hivyo huna budi pia kuongeza umakini wako
kwake kwa kuhakikisha hata huduma zako kwake zinakuwa tofauti na za kipekee
pia.
Kwahiyo niseme tu kwamba wewe unayesoma Blogu ya
jifunzeujasiriamali na wewe unayepokea makala kwa email, kuna fursa nyingine
zaidi ambayo mimi na wewe tunaweza tukawa karibu zaidi na nakuhakikishia hapa
ndipo ninakoweka maarifa yangu yote ninayohangaika kuyatafuta kila siku kwani
mimi nimejitolea kufanya kazi hiyo sawasawa tu na jinsi wewe mwenyewe
ulivyojitolea kuifanya ile kazi unayoifanya kila siku.
Kwahiyo sioni sababu kwanini uhangaike kutafuta maarifa
ya ujasiriamali hususani namna ya kupanga biashara zako wakati tayari mimi
nipo. NJOO JIUNGE LEO NA GROUP LETU KWA ADA YA SHILINGI ELFU 10 TU, TUJIFUNZE
MPAKA MWAKANI NA BAADA YA HAPO TUTAANZISHA KAMPENI NYINGINE.
Ili kujiunga, lipia kiingilio chako sh. Elfu 10(10,000/=)
kupitia namba za simu 0712202244 au
0765553030 na jina litakalotokea ni
Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma kwa meseji anuani yako ya barua pepe/email
pamoja na namba unayotumia WASAP kama unatumia lakini, ikiwa hutumii wasap
Email inatosha. Kisha tuma ujumbe usemao; “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”
Baada ya hatua hizo, nitakuunganisha mara moja na group
muda huohuo pamoja na kukutumia masomo yote yaliyopita, semina, vitabu na
michanganuo tuliyokwishachanganua katika semina zilizopita. Hatujawahi na wala
hatutakaa tumwangushe mtu, fedha yako inapofika kwetu tunaithamini kwani
tunafahamu fika fedha haijawahi kuwa rahisi kupatikana hata siku moja. Tutakupa
pia thamani ya fedha yako na zaidi yake.
KARIBU SANA RAFIKI YANGU KAMATA KITI CHAKO HAPO USICHELEWE ILI TUWEZE KUWA
PAMOJA ‘LIVE’ KWENYE HIZO SEMINA, KUNA UZURI WAKE NA FAIDA NYINGI KUWA PALEPALE
WAKATI SEMINA ZIKIENDELEA.
0 Response to "SEMINA 12 ZA KUANDIKA MICHANGANUO YA BIASHARA ZA KIPEKEE ZENYE FURSA KUBWA YA KUTENGENEZA FAIDA"
Post a Comment