TUKIO HILI LIMENIFUNDISHA KWAMBA HOFU HAIJAWAHI KUTATUA TATIZO LA PESA KWA MTU YEYOTE. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

TUKIO HILI LIMENIFUNDISHA KWAMBA HOFU HAIJAWAHI KUTATUA TATIZO LA PESA KWA MTU YEYOTE.


Nazungumzia uzoefu niliowahi kuupitia mwenyewe binafsi na wala siyo hadithi. Miaka kadhaa iliyopita kuna kipindi nilikabiliwa na deni lililoniumiza sana kichwa lakini mwishowe nilifanikiwa kulitatua tatizo lile kwa njia ya kustaajabisha sana kiasi kwamba mpaka leo hii sijaelewa kama ilikuwa ni muujiza, bahati au ni kitu gani.

Nilikuwa na biashara niliyokuwa nikiifanya kwenye fremu ya kukodi hapahapa jijini Dar es salaam. Muda wa kulipia upya kodi ya pango la fremu hiyo ulikuwa umefika na mwenyenyumba hakuwa na chembe ya huruma, alikuwa anataka kodi  yake akawalipie wanawe ada ya shule. Nilitakiwa kulipa shilingi laki tisa(900,000) kodi ya miezi 6. Wakati huohuo sikuwa na fedha na biashara ilikuwa imedorora kiasi ambacho sikuwa na uwezo hata wa kununua bidhaa kwa ajili ya kuuza pale dukani.

SOMA: Ukisoma hapa hutokaa tena uwalaumu benki au taasisi za fedha.

Sababu za kudorora kwa biashara hiyo zilitokana na matatizo mengine ya kifamilia yaliyokuwa yakiniandama ikiwemo ugonjwa. Tegemeo langu kubwa lilikuwa ni mkopo katika benki moja ambayo tayari nilishakuwa mteja wao kwa karibu mwaka mmoja. Nilikuwa ndiyo namalizia mkopo wa zamani niliokuwa nimekopa wa shilingi milioni moja, nikapanga safari hii kwenda kukopa shilingi milioni mbili kusudi niweze kulipa kodi ya watu laki 9 na zinazobakia milioni moja na laki moja niongeze bidhaa katika biashara yangu kama mtaji.

Mkopo wa zamani niliokuwa namalizia nilikuwa nimedhaminiwa na mtu mmoja ambaye alikuwa anamiliki kampuni moja ya ulinzi na safari hii nilikuwa nimepanga tena kumuomba aendelee kunidhamini. Sikuwa na mashaka yeyote kuwa angeweza kukataa kwani katika marejesho sikumsababishia usumbufu wa aina yeyote ile, nilirejesha kila mara rejesho kamili na kwa wakati. Nilimueleza mdhamini wangu azma yangu hiyo, akanijibu hakuna shida yeyote ile, niendelee tu na process za benki siku ikifika nimjulishe tuende akanisainie kama kawaida.

SOMA: Kutumia nyumba, kiwanja au ardhi kama rehani kupata mkopo ni sahihi? Naomba ushauri

Niliendelea na harakati zangu huku hali ikizidi kuwa ngumu kipesa, biashara ilikuwa imezorota kiasi kwamba wateja walikuwa wakiniuliza ni wapi nilikuwa nimepeleka mtaji. Muda huo wote ijapokuwa matatizo yalikuwa mengi lakini sikupoteza kabisa matumaini, niliamini kuwa ningetatua tatizo lile la pesa vyovyote vile hata kama benki wangeamua kunitosa. Niliifundisha akili yangu kwamba nilikuwa na uwezo wa kupata kiasi cha shilingi milioni 2 na kutatua matatizo yaliyokuwa yananikabili.

Wakati nikiwa naendelea na mchakato wa kuprocess ule mkopo, pale mtaani ulizuka uvumi mbaya kuwa, eti mimi nilikuwa  na mpango wa kuifunga ile biashara  kisha nihame mji kurudi kijijini  na mkopo niliotaka kuomba benki nilikuwa na njama za kukimbia nao kisha nimwachie yule mdhamini jumba bovu akahangaike nalo. Mdhamini kusikia vile alianza kuingiwa na wasiwasi, nikamwona mara akija kwa yule mwenye nyumba wangu wakiteta kitu nisichokijua na kisha kuondoka zake. Baadae nilikuja kubaini kumbe vile vilikuwa ni vikao vya kunijadili mimi kwamba nataka kumuingiza mdhamini wangu choo cha kike kwa kumwachia deni la benki.

SOMA: Naanza utumishi Januari, nifanyeje kuwa huru kifedha au nikakope? 

Mwenye nyumba naye kwa upande wake alianza kunionyesha wazi kuwa hakuwa ananihitaji tena pale akanipa notisi ya mwezi mmoja niwe nimemwachia chumba chake. Kule benki niliendelea na process kama kawaida, nikakamilisha makaratasi yote huku nikifocus kupata pesa ingawa nilishaanza kuingiwa na woga kiasi fulani juu ya mdhamini wangu. Hata hivyo nilijitahidi sana kupuuzia hofu ile.

Siku mbili kabla ya siku ya kwenda kusaini mikataba ya mkopo, nilimpigia simu mdhamini wangu, kwanza simu iliita weee…..bila majibu. Nikaamua kumtumia meseji baadae akanijibu kuwa hakukuwa na tatizo lolote na siku ya kusaini fomu atafika tukutane benki. Hapo tena wasiwasi ulitaka kuninyemelea lakini nikapiga moyo konde na kusema, “Nitapata milioni 2 nitatue matatizo yanayonikabili” Niliziona milioni mbili nikiwa nimezishika kwa mikono yangu akilini.

Jioni ya kuamkia siku ya kwenda kusaini nilipompigia simu mdhamini ili kumkumbusha, simu yake ilikuwa imezimwa kabisa. Bado pamoja na hayo sikuruhusu kabisa kuchanganyikiwa japo nilifahamu fika fedheha ambayo ningeweza kwenda kuipata benki baada ya kuulizwa mdhamini wako yuko wapi. Nikajipa moyo kuwa mpaka kesho yake asubuhi kama asingepatikana kwenye simu basi ningejihimu asubuhi sana nyumbani kwake kabla hata hajakwenda ofisini japo nyumbani kwake palikuwa mbali nikajue hatma ya suala lile.

SOMA: Jinsi wanavyochukua hatari kubwa kwenye biashara wanavyofanikiwa haraka.

Asubuhi nilijaribu tena kumpigia simu safari hii akapokea na kunihakikishia kuwa saa nne asubuhi muda afisa wangu alioniambia tuende atakuwa amewasili benki. Niliwahi pale benki saa 2 na nusu nikakuta hata maafisa wenyewe wa benki bado hawajafika, kulikuwa na walinzi tu.

Mpaka majira ya saa tano asubuhi mdhamini wangu alikuwa hajaonyesha dalili zozote za kufika pale benki nikaamua tena kumtumia meseji, “upo wapi mkuu” akanijibu hivi, “Nimepata safari ya dharura, wewe nenda tu wakupe  mkopo halafu mimi kesho au keshokutwa nitafika hapo kusaini hizo fomu”

Badala ya kupatwa na mshituko nilishangaa ni kwa vipi benki inaweza kukupa mkopo kisha mdhamini aje siku yeyote ile anayotaka yeye kuja kukusainia mkataba. Hata pamoja na hivyo bado akili yangu mpaka nukta ile ilikuwa timamu, ikilenga tu kupata milioni 2 siku ileile hata kama mdhamini asingetokea, sikuamini kabisa kama ningekosa ule mkopo.

Majira ya saa saba mchana yule afisa wangu naye alianza kuingiwa na wasiwasi akaniita na kuniomba nimpe simu ili aongee na yule mdhamini moja kwa moja kujua tatizo lilikuwa wapi. Majibu ya mdhamini kwa afisa wa benki yalikuwa ni yaleyale aliyonipa mimi, “Mpe hela mimi nipo safarini nitafika kesho au keshokutwa kuja kusaini hizo fomu” akakata simu.

Hatma ya mkopo wangu sasa ilibakia mikononi mwa yule afisa na uongozi wa benki. Punde kidogo afisa aliniita chemba akaniuliza, “kwani imekuwaje tena bro?” Nikamjibu, “hata mimi nashangaa sielewi kwani tangu juzi tumekuwa tukiwasiliana na leo asubuhi kanihakikishia tutakutana hapa benki” Majibu yangu kwa yule afisa niliyatoa kwa ujasiri mkubwa bila kuonyesha woga wala wasiwasi wowote ule, na hadi leo hii bado nashangaa ule ujasiri ulitoka wapi…………….


…………………………………………..

Mpenzi msomaji wa makala hizi, somo hili ni kipande kidogo tu, somo zima tutajifunza leo hii tarehe 28 Mei 2020, muda ni saa 3 usiku mpaka saa 4 ndani ya Group la Whatsap la MICHANGANUO-ONLINE. Group hili lina kiingilio ambacho ni shilingi elfu 10 tu, na unatumiwa masomo yote yaliyokwishapita, offa ya vitabu na michanganuo ya biashara mbalimbali pia fursa ya kushiriki semina nyingine zote mpaka mwisho wa programu ya mwaka huu ambayo itamalizika baada ya mwakani mmoja.

Huwa tunakuwa pia na semina za mara kwa mara za kuandika Michanganuo ya biashara bunifu hatua kwa hatua ambayo mwishoni mwa semina tunakuwa na mchanganuo uliokamilika kila kitu unaoweza kuuedit kulingana na mahitaji yako mwenyewe.

Kujiunga tuma kiingilio chako sh. Elfu 10, kupitia namba 0712202244  au 0765553030  jina hutokea Peter Augustino Tarimo. Baada ya kutuma, tuma pia na namba yako ya wasap na anuani yako ya email. Na muda huohuo tunakuunganisha na kukutumia kila kitu ndani ya dakika 5 tu. Ikiwa hutumii wasap hamna shida yeyote kwani masomo na kila kitu tunatuma kwa njia ya email.  

Kwa vitabu pia vya Ujasiriamali na Biashara katika lugha ya Kiswahili, tembelea, SMART BOOKS TANZANIA.


Vitu mbalimbali, vitabu na masomo yaliyopita tunayokutumia pindi tu ujiungapo ni haya hapa chini;


1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.


3.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

4.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.


6.  Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

7.  Masomo yote yaliyopita katika group kuhusu MICHANGANUO NA MZUNGUKO WA FEDHA.

8.  Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

9.  Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

10.      Ukurasa mmoja wa mchanganuo.





0 Response to "TUKIO HILI LIMENIFUNDISHA KWAMBA HOFU HAIJAWAHI KUTATUA TATIZO LA PESA KWA MTU YEYOTE."

Post a Comment