Binadamu kila wakati tumekuwa tukisaka siri
za mafanikio maishani lakini chakushangaza sana ni kwamba wengi wetu badala ya
kulenga yale mambo ambayo ndiyo yanayoweza kutufikisha kwenye mafanikio ya
kweli tunakuwa tukihanganika na vitu vidogovidogo sana ambavyo havina uwezo wa
kutuletea maendeleo yeyote yale ya maana.
Matone ya kawaida ya mvua hayajawahi kumuua
wala kumuumiza mtu lakini si ajabu hata kidogo kumkuta mtu akikimbia mvua
barabarani kwa kasi ya ajabu akitafuta mahali pakavu pa kujificha lakini wakati mwingine
akiwa katika barabara hiyohiyo haogopi kabisa kupishana kwa karibu na magari
ambayo yana uwezekano mkubwa wa kukatisha uhai wake.
Hali ni hivyohivyo ilivyo kwa upande wa afya
zetu, unaweza ukamkuta mtu anajali kupita kiasi kujikinga na magonjwa madogomadogo
hata yale yanayotibika kirahisi kabisa kama kikohozi na mafua(simaanishi
tusijikinge na magojwa hapana) lakini cha kushangaza mtu huyohuyo ndiye
utakayemkuta akifanya ngono zembe(mapenzi holela na watu tofautitofauti) bila
hata ya kuchukua tahadhari yeyote kama kuna magonjwa hatari ya zinaa yanayoua
kama ukimwi nk.
Nimetoa mifano hiyo 2 makusudi nikitaka
kuonyesha kwamba hata katika suala zima la mafanikio yetu binadamu kiuchumi
bado wengi wetu tunalenga mno katika vitu vidogovidogo ambavyo katu haviwezi
kuwa na uwezo wa kututoa pale tulipo na kutufikisha kwenye ‘nchi ya ahadi’
mahali pazuri zaidi au palipo na mafanikio.
Hebu jiulize, unaweka vipaumbele vyako katika
vitu gani linapokuja suala la pesa na mafanikio?. Mfano kijana anayemaliza
shule au chuo sasa na kuanza mara moja kuweka malengo ya kujiwekea akiba kwa
ajili ya ununuzi wa rasilimali(asseti) zenye uwezo wa kumzalishia pesa baadae,
miaka kumi mbele utakuja kumshangaa kijana huyu hutampata tena atakuwa mbali
kiuchumi kuliko yule anayewaza kutumia kila senti anayoipata kula raha.
Mtu kufikiria namna unavyoweza kuwekeza pesa
zako na ni wapi uziwekeze ni moja ya kitu muhimu sana katika maisha ya binadamu
kwani ndiyo hatimaye huamua mustakabali mwema wa maisha yake kiuchumi.
Lakini utakuta mtu badala yake anaanza
kufikiria vitu vidogovidogo vya muda
mfupi mfupi tu kwa mfano, “nitakula nini kesho”, “mpenzi wangu anataka
nimnunulie rasta na hereni za dhahabu, nitapata wapi pesa za kumnunulia”, “nyumbani
hatujala nyama huu ni mwezi wa pili sasa..”.nk. Mtu anahofia vitu ambavyo wala
sio tishio kabisa katika maisha yake na ni vya kupita muda mfupi. Imefikia
mahali watu sasa tuweke hofu zetu katika mambo yanayotutisha kweli na kuweka
mipango na mikakati ya kukabiliana nayo
Kuna matishio ya ukweli kama vile homa,
kuugua magojwa yanayohitaji gharama kubwa, badala ya kuwaza tu vitu
vidogovidogo kama michango ya harusi, vipaimara au ngoma za viduku mitaani, tuanze
kufikiria utaratibu wa kujikatia bima za afya kwa familia zetu na sisi wenyewe,
matishio ya magojwa yanayohitaji fedha nyingi ni ya ukweli wala siyo hadithi
kama wengi tunavyoweza kufikiria. Umeshashuhudia mara ngapi wapendwa wako au
hata watu unaowajua wakipoteza maisha kisa tu kukosa gharama za matibabu zinazoeleweka?
Si kama nahukumu au kutishia hapana, bali hii ndiyo asili
yetu sisi binadamu kuhangaika na vile vitu vilivyopo mbele yetu kwa wakati ule
tulio nao tu hata kama havina umuhimu kihivyo. Watu wanaofanikiwa mara nyingi
hulenga katika yale mambo mazito yaliyo na umuhimu mkubwa katika maisha yao
hata ikiwa mambo hayo wanayatarajia miaka mingi ijayo. Mfano wa mambo hayo ni
kama haya yafuatayo;
1. Kupata
kazi nzuri
2. Kuwekeza
katika vitegauchumi na biashara zitakazowalipa vizuri baadae
3. Kujenga
mahusiano mazuri na watu wale uwapendao na mnaoonana mara kwa mara.
4. Kuwa
na afya nzuri
5. Kuishi
maisha unayoyataka kila siku
Mambo haya makubwa, kila mtu anaweza akawa
nayo yakwake tofauti na mwingine lakini yote kwa yote mtu anatakiwa kuwa na
malengo yake makubwa maishani atakayohakikisha akili yake yote inayawaza mpaka
pale atakapoyatimiza na wala siyo mambo madogomadogo yasiyokuwa na tija yeyote
maishani.
……………………………..
Ndugu msomaji wangu, makala zako kuhusiana na Mzunguko wa fedha
na Michanganuo ya biashara katika group la Wasap la MICHANGANUO-ONLINE bado zinaendelea
kila siku, karibu njoo ujiunge kwa shilingi elfu 10 tu upate na masomo mengine
yote yaliyopita pamoja na kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
free of charge.
Tunakupa na michanganuo maarufu 3 ya ufugaji wa kuku aina zote
pamoja 1 wa kilimo cha matikiti maji bila malipo yeyote ya ziada. Pia
utaunganishwa na group hilo la wasap na kuwa miongoni mwa wajasiriamali makini karibu 100 wanaojua kile wakitakacho maishani(MASTERMINDGROUP)
Ikiwa hutumii wasap hamna shida kwani masomo utapata kupitia email
yako.
Leo Septemba 10 2018
usiku saa 3 tutakuwa na somo lisemalo; “BIASHARA YENYE FURSA KUBWA NA YA
KIPEKEE NCHINI ISIYOJULIKANA BADO NA WATU WENGI”
ASANTE SANA,
Peter Augustino Tarimo
self help books Tanzania
0765553030
ASANTE SANA,
Peter Augustino Tarimo
self help books Tanzania
0765553030
0 Response to "JINSI UNAVYOZUIA MAFANIKIO MAKUBWA MAISHANI KWA KUHANGAIKA NA VITU VIDOGOVIDOGO"
Post a Comment