Biashara ya bucha la kuuza nyama au samaki kama
zilivyokuwa biashara nyingine za rejareja siri yake kubwa ya mafanikio ni eneo
utakalofungua biashara yako. Eneo zuri la biashara ya bucha unayoweza kupata
wateja wengi wa kutosha ni maeneo yale yaliyokuwa na mzunguko wa watu wengi ama
yaliyozungukwa na makaazi mengi ya watu. Bucha za kisasa nyingi utakuta
zimewekwa maeneo wanakopita watu wengi kama stendi za magari na sokoni.
Kigezo kingine kinachoweza kuamua bucha lako lipate
wateja wengi ni kipato cha wateja walioko katika eneo utakalochagua kufungua
bucha. Kuna wateja wa aina tatu kulingana na kipato, wapo wateja wa kipato cha
juu, kipato cha kati na wale wa kipato cha chini. Kwa mfano eneo linapokuwa na wakaazi
wengi wa kipato cha juu, biashara ya bucha inalipa sana kwani wateja watakuwa
wengi tofauti na eneo lenye watu wa vipato vya chini.
Si kama watu wa vipato vya chini hawapendi kula nyama na
samaki hapana, bali uwezo wao wa kununua bidhaa hizo ni mdogo jambo
linalowafanya wengi kununua mara chache sana kwa mwezi. Unaweza ukakuta mtu
anapitisha hata miezi miwili bila kugusa kabisa nyama. Sanasana utakuta
akinunua dagaa na samaki mara chachechache.
Ni katika mtaa mmoja maeneo ya Mbezi ya Kimara, eneo
ambalo wakazi wake wengi ni watu wa
kipato cha chini na cha kati mjasiriamali mmoja mmiliki wa bucha la nyama
ajulikanae kwa jina la Mushi amebuni mbinu mpya ya kuongeza mauzo kutoka kwa
wateja wa kipato cha chini, mbinu hiyo hapo kabla hakuna mtu mwingine aliyekuwa
amewahi kuitumia katika kitongoji hicho.
Kabla ya ujio wa mjasiriamali huyu mbunifu,
wafanyabiashara wengine wa mabucha ya nyama na samaki katika eneo hili waliwahi kufungua mabucha lakini wengi “walichemka”
kutokana na wateja kuwa wachache mno. Mpaka anakuja palikuwa na bucha moja tu
eneo hilo na wateja wake wengi walikuwa ni watu wachache sana wa vipato vya
kati wanaoishi eneo lile. Hapakuwa na butcher la nyama wala bucha la saki
lolote lililokuwa likiwalenga wateja wa kipato cha chini.
MBINU
YENYEWE ALIYOKUJA NAYO HUYU JAMAA NI HII HAPA.
Nilipofanya naye mazungumzo ya kirafiki, Bwana Mushi
alianza kunieleza hivi;
“Kabla sijafungua
bucha katika eneo hili wala kununua vifaa vya bucha kitu cha kwanza nilifanya
utafiti kujua kama kuna wateja wa kutosha kuniwezesha niweze kupata faida.
Katika utafiti huo niligundua kwamba watu wengi hasa wale wenye vipato vidogo
wanapenda sana kula nyama na samaki kama vitoweo lakini kikwazo kikubwa
kinakuwa ni uwezo wa kununua, wanaishia tu kununua dagaa mchele wa buku, dagaa
wa kigoma na wale wa mwanza, maharage na mbogamboga za majani kama vile
mchicha, spinachi, matembele, majani ya maboga, majani ya kunde, matembele,
kabichi nk.
Ukichunguza
vitoweo vyote hivyo nilivyovitaja bei zake hazizidi shilingi elfu moja(1000)
kwa mlo mmoja lakini ili mtu aweze kupata nyama kiwango cha chini kabisa
anachoweza kununua ni robo kilo ¼ na atalazimika kulipa shilingi elfu moja na
mia tano(1500), tena mwenye duka naye akigundua tu hana washindani wengi hupandisha
na kuuza nyama robo kilo kwa shilingi elfu mbili( 2000), hii sasa inakuwa ni
kama kuwakomesha wateja ili wakome kununua roborobo, wanunue kuanzia nusu kilo,
kilo moja na kuendelea.
Baada
ya kubaini hali hii, niligundua fursa kubwa ya soko la nyama ya ng’ombe na
samaki wa mwanza kama vile sangara na sato kwa watu wa hali za chini ambao
vipato vyao si vya uhakika sana. Nilifikiri kwamba kama nitaanzisha biashara ya
bucha la kuuza nyama ya ng’ombe, nyama ya kuku na samaki kisha nikaweka bei ya
kawaida lakini nianze kupima kiasi kidogo kadiri iwezekanavyo basi ningeweza
kuwanasa wateja wengi sana wa kipato cha chini na wale wa kati pia.
Mwanzoni
nilipanga kuuza kuanzia robo kilo kwa bei ileile ya kawaida nisiwakomoe wateja
kwa kuwauzia elfu mbili bali kama kilo moja ya nyama ni shilingi elfu 6 basi
robo kilo niuze shilingi elfu moja na mia tano(1500). Na samaki hivyohivyo,
kama kilo moja ya sato ni shilingi labda elfu tisa(9) basi robo kilo ya samaki
hao niuze shilingi elfu mbili na mia mbili na hamsini(2250) tu pasipo
kumbugudhi mteja kuhusiana na chenchi wala nini.
Nilipofungua
bucha langu nilianza na mzani wa mawe huu wa kawaida wenye jiwe la kuanzia robo
kilo mpaka kilo 5, lakini pamoja na mbinu hiyo niliyoazimia kuitumia bado
sikuona wateja wengi wakija kununua nyama na samaki kama nilivyokuwa
nikifikiria. Nilijitahidi kubandika tangazo ukutani(TUNAPIMA NYAMA KUANZIA ROBO
KILO KWA SHILINGI 1500) ;lakini wapi, wateja wala hawakuongezeka kama
nilivyodhania.
Mwishoni
katika pitapita yangu mjini siku moja nikaingia duka moja Kariakoo linalouza
vifaa mbalimbali ikiwemo mizani kwa ajili ya kupimia vitu mbalimbali.
Niligundua kuna mzani mmoja wa kichina wenye uwezo wa kupima kiasi chochote
kile cha bidhaa bila kutumia mawe ya kawaida, ni mzani wa kielektroniki na
unasoma mahali kama vile unavyosoma saa au mashine zinazotumika shelli za
mafuta ya magari. Unaweza kupima kitu kuanzia uzito wa chini kabisa kuliko hata
robo kilo na cha kushangaza zaidi ni kwamba mzani huo una mahali unapoandika
bei moja kwa moja kulingana na utakavyo useti.
Kama
umeseti kilo moja ya nyama kuwa ni shilingi elfu 6 basi kiasi chochote kile cha
nyama utakachoweka kwenye bakuli la mzani, mzani utakuandikia ni gramu ngapi na
kiasi cha fedha kinachoendana na gramu hizo moja kwa moja (automatically) wala
hupati shida ya kuanza kukokotoa mwenyewe tena kwa mashine ya hesabu. Hata
uweke gramu moja ya nyama itakuonyesha bei yake ni shilingi ngapi.
Kwa
mtindo huo mteja wa nyama au samaki hata akitaka nyama ya shilingi mia tano
anaweza kupata bila kumpunja wala wewe muuzaji kupunjika kwani mzani unapima na
kutoa bei sawasawa kulingana na kiasi kile ulichoweka pale kwenye bakuli.
Baada
ya wateja wengi kugundua vile, nilianza kuona wateja wengi wakimiminika kuja
wakitaka kupimiwa nyama na samaki za shilingi elfu moja(1000), wengine hata
huja na pesa kiasi chini ya hapo na mimi wala sikatai nawapimia kwani nafahamu
sipotezi kitu chochote na mwisho wa siku nyama na samaki vikiisha hesabu zangu
hubakia vilevile sahihi sawasawa tu kama ningeuza kwa kupima kilo mojamoja.
Siku
hizi buchani kwangu nyama na samaki wabichi hazikai tena muda mrefu nikileta
leo kesho nimemaliza na wateja wangu wengi ni akina mama wa familia za kipato
cha chini na kidogo wale wa kipato cha wastani. Badala ya kwenda sasa kununua
dagaa za shilingi elfu mojamoja au samaki wa kukaanga wanakuja nawapimia nyama
ya shilingi elfu moja. Wapo wengine husema niwapimie ya elfu mbili, 1500 au
kiasi chochote kile kulingana na hela aliyokuwa nayo mteja.
Mzani
huu umewapa wateja uhuru mkubwa wa kuchagua wanunue nyama na samaki kiasi gani
bila vikwazo vyovyote vile visivyo na msingi. Unajua wateja wana kawaida moja
ya kupenda kuwa huru wanapofanya manunuzi yao ya aina yeyote ile pasipo
kubanwabanwa. Mfanyabiashara ukigundua hili na kuwapa wateja uhuru huo
utashangaa vile watakavyokuwa marafiki zako.” Alimaliza Bwana
Mushi maelezo yake.
.............................................
Ndugu msomaji wa makala hizi napenda kukujulisha pia kwamba kila siku tunakuwa na masomo yahusuyo fedha katika group la MICHANGANUO-ONLINE ambalo kiingilio chake ni shilingi elfu 10.
Unakuwa mwanachama wa kudumu na pia mbali na masomo hayo ya kila siku na semina za mara kwa mara za kuandika michanganuo ya biashara mbalimbali zenye fursa, tunakutumia masomo yote na semina zilizopita, vitabu na michanganuo kama ilivyorodheshwa hapo chini.
Somo la leo usiku tarehe 22/9/2018 linasema hivi;
"HUWEZI KUAMINI KAMA SIRI YA KUPATA UTAJIRI NI KITU KIDOGO NAMNA HIII !"
Malipo ni kupitia namba hizi, 0765553030 au 0712202244 na baada tu ya kulipia tuma ujumbe kwa wasap 0765553030 usemao "NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO" na tutakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia vitu mbalimbali vifuatavyo;
.............................................
Ndugu msomaji wa makala hizi napenda kukujulisha pia kwamba kila siku tunakuwa na masomo yahusuyo fedha katika group la MICHANGANUO-ONLINE ambalo kiingilio chake ni shilingi elfu 10.
Unakuwa mwanachama wa kudumu na pia mbali na masomo hayo ya kila siku na semina za mara kwa mara za kuandika michanganuo ya biashara mbalimbali zenye fursa, tunakutumia masomo yote na semina zilizopita, vitabu na michanganuo kama ilivyorodheshwa hapo chini.
Somo la leo usiku tarehe 22/9/2018 linasema hivi;
"HUWEZI KUAMINI KAMA SIRI YA KUPATA UTAJIRI NI KITU KIDOGO NAMNA HIII !"
Malipo ni kupitia namba hizi, 0765553030 au 0712202244 na baada tu ya kulipia tuma ujumbe kwa wasap 0765553030 usemao "NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO" na tutakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia vitu mbalimbali vifuatavyo;
Ukihitaji vitabu vya ujasiriamali na biashara
katika lugha ya kiswahili pia tembelea hapa, >> SMART BOOKS TZ
0 Response to "Mmiliki biashara ya bucha la kuuza nyama na samaki agundua siri ya kupata wateja wengi wa kipato cha chini"
Post a Comment