Wanaosema nikishinda bahati na sibu milioni 100 nitafanya hiki na kile wakishinda hufanya kinyume chake | JIFUNZE UJASIRIAMALI

Wanaosema nikishinda bahati na sibu milioni 100 nitafanya hiki na kile wakishinda hufanya kinyume chake

Ni karibu kila mtu katika nyakati tofauti maishani huwa na ndoto na ahadi mbalimbali. Siyo jambo baya kuwa na ndoto au malengo katika vitu mbalimbali lakini ahadi nyingi za watu katika matumizi ya fedha ni za uwongo. Waotaji ndoto za fedha mara nyingi ndoto zao zinapokuwa zimetimia au kufanikiwa hugeuka jiwe la chumvi na kusahau kabisa yale waliyokuwa wakiyaahidi au kutamani kuyafanya pindi tu wakipata pesa walizokuwa wakitamani kuzipata. 

Nadhani hii inaweza kuwa ndiyo sababu kubwa hata makampuni mengi ya michezo ya kubahatisha kuamua kuweka utaratibu wa washindi kuchagua mapema watu wa karibu watakaowashirikisha sehemu fulani ya zawadi wanazoshinda kwani wangeliachwa tu hivihivi sidhani kama wangemgawia mtu senti tano hata kama  ikiwa ni watu wao wa karibu sana kama mzazi, mtoto, mwenza nk.

SOMA: Kama pesa haijawahi kuwa rahisi kupatikana kwanini uchezee pesa?

Unamkuta mtu akijinasibu kuwa, nikishinda bahati na sibu hii shilingi milioni 100 au milioni 10 kwanza nitawagawia watu wangu wote muhimu wa karibu kiasi cha shilingi laki 5 kila mmoja kisha nitafanya bla bla blaaa…, lakini cha ajabu mtu huyu akija kushinda kweli  bahati na sibu atasahau yoote aliyoahidi.


Mwingine utamsikia akisema, “Nitakapofanikiwa kuupata mkopo wangu wa shilingi milioni tano tu hivi, nitafanya hiki, nitafanya kile, nitabana matumizi, nitaboresha biashara yangu nk. Lakini siku lengo likitimia tu hivi, mtu huyo ndiyo kwanza atafanya kinyume na vile alivyokuwa akiahidi kufanya. Wapo pia wanaopanga kutoa misaada kwa wasiojiweza, wengine huahidi kuanza kuwa na nidhamu ya pesa ili kulinda utajiri wa pesa watakaoupata usipotee.

SOMA: Ingawa mipango si matumizi lakini haiepukiki kwenye maisha.

Kwa ujumla sisi binadamu tunapendelea kufikiria maisha yetu yajayo kama vile ni kitu kikamilifu lakini tunasahau jambo moja kubwa sana na ambalo ndilo linalotusababisha mara zote kwenda kinyume na  ahadi zetu tunazozitoa maishani hasa juu ya pesa.

Uliwahi kujiuliza swali jingine hili?
Hivi ni kwanini watu waliofanikiwa kimaisha inakuwa vigumu hivyo kuwafundisha watu masikini njia zote za mafanikio walizopitia wakati wanazijua fika na walishawahi kuzipitia? Ikiwa watu kama kina Aliko Dangote, Said Salim Bakhresa, Reginald Mengi, Mohamed Dewj na wengineo walitumia miaka zaidi ya 20 kufikia mafanikio waliyonayo, ni kwanini basi washindwe kuwamegea watu wa hali za chini siri zao kwa urahisi ili badala ya kuchukua miaka mingi kama wao wachukue angalao miaka 3 au 5 tu kufanikiwa? Swali hili litajibiwa karibu na mwisho wa makala hii hivyo tafadhali ‘stay tuned’ fuatana nami mpaka mwisho.

Vipi wale watu wanaorithi utajiri na mali nyingi kutoka kwa wazazi au walezi wao? Sawa sawa tu na wale wanaoshinda michezo ya kubahatisha watu hawa eti inasemekana wengi wao utajiri wanaoupata kwa njia hizo haudumu hutoweka ndani ya kipindi kifupi tu. Sasa sababu hasa ni kitu gani? Kuna sababu kubwa inayozunnguka miongoni mwa mambo yote haya niliyoyataja na ni vizuri mtu kuifahamu kwani inaweza kutusaidia kutegua vitendawili vingi vinavyotusumbua katika harakati za utafutaji wa pesa na maisha kwa ujumla.    

Mtabiri wa kweli wa ahadi na ndoto zako si mwingine bali ni.............

Mpenzi msomaji wa makala hizi, makala hii nzima tutajifunza leo usiku Ijumaa ya Septemba 21 saa 3 mpaka saa 4 pale katika Group la watsap la Michanganuo-online. Kujiunga na group hili kuna kiingilio kidogo cha sh. elfu 10 lakini pia utapata vitu vingi  ikiwa ni pamoja na kuwa mwanachama wa kudumu. Malipo hufanywa kwa njia ya simu, 0712202244  au 0765553030

Mara baada ya kulipa unatumiwa hapohapo vitu mbalimbali vifuatavyo pamoja na kuunganishwa na group;

0 Response to "Wanaosema nikishinda bahati na sibu milioni 100 nitafanya hiki na kile wakishinda hufanya kinyume chake"

Post a Comment