Kama ilivyokuwa kwa samaki unapomtoa kwenye maji, hawezi
kufanya tena lolote, na mimi ilikuwa ni hivyohivyo tatizo lililonikuta najifananisha
na samaki aliyetupwa nchi kavu kwani lilinifanya nishindwe kabisa kufanya
majukumu yangu niliyozoea kuyafanya ikiwemo kuandika.
Ni stori binafsi mno na sidhani hata kama ilikuwa ni sahihi
sana kuisimulia hapa lakini kuna vitu kadhaa nilivyoona kama uzoefu wangu
binafsi ingefaa kuwashirikisha wasomaji wangu.
SOMA: Umekata tamaa ya maisha? hebu soma maajabu ya mwanasayansi huyu mkubwa duniani.
SOMA: Umekata tamaa ya maisha? hebu soma maajabu ya mwanasayansi huyu mkubwa duniani.
Mimi ni mwandishi nategemea kubadilisha maisha ya watu
wengine kwa kile ninachokiandika hivyo si jambo baya kama nitaandika pia mambo
ninayokutana nayo binafsi kama kuna la kujifunza kuliko tu kubakia kuandika mambo
ninayosikia kutoka kwa watu wengine. Ndio maana nimeshawishika kuandika kisa
hiki hapa, ikiwa hakitokupendeza tafadhali sana natanguliza samahani kwako.
Na pia ikiwa kama hutaweza kusoma blah..blah.. nyiingi nilizoweka
hapa katikakati, basi nakusihi tu moja kwa moja uruke mpaka mwisho wa makala
hii, utakuta hitimisho nililoweka pale lenye dondoo kama 6 hivi, zisome hizo
dondoo inatosha. Utakuwa umepata ujumbe wote niliokusudia kuutoa kwako leo hii.
Zimepita wiki mbili sasa tokea mkasa huu uanze, ilikuwa
ni asubuhi ya tarehe 22 Septemba 2018 asubuhi baada tu ya kuamka, ghafla nilianza kuhisi maumivu kwenye jicho langu la kulia
yaliyokuwa yakiongezeka pindi nitazamapo mwanga mkali au chanzo chochote kile
cha mwanga kama vile taa au upande inakochomoza miali ya jua. Maumivu hayo
yaliambatana na jicho kubadilika rangi na kuwa rangi ya pinki inayoelekea kuwa
nyekundu.
SOMA: Dengue ni kama tauni na ukoma zama za Yesu Kristo
SOMA: Dengue ni kama tauni na ukoma zama za Yesu Kristo
Hali ile ilinifanya niwe nalazimika kufunga jicho la
kushoto kusudi niweze kuona, lakini hata hivyo miale ya mwanga ilipopenye
katika jicho la kushoto bado nilihisi kama vile inapenya pia kwenye jicho la kulia
lililokuwa linauma hivyo kulifunga wala haikusaidia sana. Nilifikiria njia ya
kuvaa miwani nyeusi ya jua na kweli nilipojaribu ikanisaidia kwa kiasi fulani kupunguza
maumivu nikitazama mwanga japo siyo sana. Miwani pia ilinisaidia watu wengi
wasitambue kama nilikuwa naumwa jicho kwani ilificha ule wekundu.
Siku iliyofuata iikuwa Jumapili na bila ya kujali kama
ilikuwa ni siku ya mapumziko niliamua kwennda kumuona daktari wa macho
hospitali ya serikali Magomeni kwa ajili ya tiba ya macho. Nilitoka zangu Mbezi
ya Kimara kwa mwendokasi mpaka Magomeni Mapipa. Pale mapokezi waliniuliza kama
natumia bima nikasema nitalipa mwenyewe. Kwakuwa haikuwa siku rasmi ya kazi
hapakuwa na foleni kubwa kwenda kumuona daktari. Pale mapokezi pia waliniambia
kuwa siku ya jumapili huwa hamna cliniki ya macho hivyo nikaonane tu na daktari
wa kawaida(general)
SOMA: Ebola, tuachane na dawa za kizungu turudi kwenye muarobaini na kikombe cha babu?
SOMA: Ebola, tuachane na dawa za kizungu turudi kwenye muarobaini na kikombe cha babu?
Daktari baada ya kunitizama kidogo kwenye jicho
alinieleza kuwa nirudi siku iliyofuata yaani Jumatatu ili niweze kuwaona
wataalamu wa macho katika kliniki ya macho huku akiniandikia nikanununue famasi
dawa ya mafuta ya kuweka kwenye jicho kama
huduma ya kwanza. Kwa maumivu niliyokuwa nikiyasikia sikusubiri mpaka nifike
nyumbani ndipo niweke ile dawa,
nilitafuta mahali palepale hospitalini na kuanza kuitumia.
Siku iliyofuata Jumatatu tarehe 24 nilijihimu asubuhi na
mapema nikawa mtu wa pili kwenye foleni ya kliniki ya macho pale Magomeni
hospitali. Daktari mmoja mwanaume alinichunguza ikiwa ni pamoja na kupima uwezo
wa macho yote mawili wa kuona na yote bado yalikuwa yakiona vizuri kwani
niliweza kusoma herufi zote nilizowekewa mbele nisome, isipokuwa tu zamu ya
jicho la kulia nilisoma kwa taabu kidogo, kulikuwa na mchanganyiko wa
mawingumawingu kidogo na maumivu makali.
SOMA: Uwezo wa akili ya binadamu ni wa ajabu na usiokadirika
SOMA: Uwezo wa akili ya binadamu ni wa ajabu na usiokadirika
Dokta yule aliniambia kuwa jicho langu lilikuwa jekundu
sana na lilikuwa limeshambuliwa na aina ya ugonjwa wa macho utokanao na virusi ujulikanao
kitaalamu kama (pink eyes au conjactivitis) hivyo alinipa dawa(antibiotic)
nikaweke kuzuia maambukizi mengine zaidi ya bakteria na baada ya siku kadhaa
lingeacha tu lenyewe kwani virusi hawana
tiba ni kama yalivyokuwa mafua, hutoweka vywenyewe kwa kinga ya mwili kuimarika.
Nilipoenda duka la dawa nikakuta kumbe dawa ya macho
aliyoniandikia yule dokta wa macho ni sawasawa na ile niliyoandikiwa na daktari
wa kawaida jana yake hivyo ilinibidi niache kununua nikatumie tu ileile ya jana.
Niliwahi kuugua macho siku za nyuma lakini kitu cha ajabu
nilichoona safari hii ni kwamba jicho moja tu ndilo lililokuwa likiuma na kuwa
jekundu, nilitegemea kama kweli ni maambukizi basi baada ya muda mchache na jicho jingine nalo lingeanza kuathirika
lakini haikuwa hivyo. Kadiri siu zilivyozidi kupita ndivyo jicho langu nalo
lilivyokuwa “likiwiva”(likiwa jekundu) sambamba na maumivu makali yasiyotaka
kabisa mwanga licha ya kuendelea na
matumizi ya ile dawa ya macho ya tube aliyoniandikia daktari wa Magomeni.
SOMA: Hivi unajua mswaki ni hatari unaweza kukuua?
SOMA: Hivi unajua mswaki ni hatari unaweza kukuua?
Sasa ilikuwa ikipindukia siku ya nne tangu nianze
matibabu hayo pasipo kuona nafuu yeyote ile. Ilifika mahali nikawa hata nakiuka
masharti ya ile dawa na kuongeza kiasi cha dawa machoni kwa matumaini labda
ingenisaidia lakini wapi!
Shughuli zangu zote ziliathirika, kazi za kuandika makala
katika blogu ya jifunzeujasiriamali, kwenye email list na hata katika group la
watsap la michanganuo-online zote niliona kama kituo cha polisi vile. Kila
nilipojaribu kutizama kwenye kioo kiwe ni cha kompyuta au simu miali ilichoma
kwenye jicho utadhani nimetazama mlipuko wa bomu la atomiki.
Ningelikuwa na imani haba nigeliweza kufikiria labda kulikuwa na mtu ameniloga ili nishindwe
kutimiza majukumu yangu, “Kwanini macho
tu, ambayo ndiyo huniwezesha kufanya kazi zangu muhimu? si bure lazima kuna
mkono wa mtu hapa” ningeliweza kuwaza hivyo lakini katu sikuruhusu kitu cha
namna hiyo akilini mwangu.
Maumivu ya jicho yalinifanya nikumbuke vitu vingi vilivyokuwa vimetokea siku chache jirani na
ninapoishi.
Kwanza
ulikuwa ni msiba wa kuhuzunisha mno wa kijana mmoja mtoto wa jirani yangu(mama
mmoja) aliyekuwa ndio tu katoka kumaliza kidato cha sita(form six) mwaka huu na
kufaulu mtihani wake vizuri.
SOMA:Unawezaje kuyakabili magumu, maanguko na mikasa ya kutisha maishani kama hii?
SOMA:Unawezaje kuyakabili magumu, maanguko na mikasa ya kutisha maishani kama hii?
Akiwa
anasubiri kupangiwa chuo kikuu alikwenda Mbagala kwa ndugu zake alipokaa wiki
kadhaa kabla ya kurudi kwa mama yake Mbezi akiwa analalamika kichwa kumuuuma
sana pamoja na taya na misuli ya shingo kukaza. Tangia utotoni alilelewa na
mama yake pekee kwa shida ikiwa ni pamoja na kuhangaika naye kwa kila kitu
zikiwemo gharama zote za masomo. Alikuwa ndio tegemeo pekee kwa mama yake.
Mama
yake alimpeleka hospitali za kawaida pale mtaani ambapo walimpima na kugundua
alikuwa na malaria wakampa dawa alizotumia bila nafuu yeyote ile. Alipelekwa
hospitali ya Mwananyamala na walipompima hawakuona ugojwa wowote. Wakampa tu
dawa za maumivu na kumfanyia kipimo cha kichwa walichomwambia arudi baada ya
siku kadhaa kuchukua majibu.
Kwa
karibu wiki mbili sasa tangu aanze kuugua, hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya
mpaka akawa sasa anaanza kupoteza fahamu na kupata kitu kama degedege ndipo
watu wakamshauri mama yake amrudishe tena hospitali ya Mwananyamala labda
watampa rufaa aende Muhimbili kwa vipimo zaidi.
Kutokana
na hali ya kiuchumi ya mama yule hata nauli ya safari za hospitalini ilikuwa ni
mtihani, pia ndugu wengine na jamaa walikuwa wakikazana kumshawishi kuwa
mwanaye atakuwa alikuwa anasumbuliwa na maswala ya kienyeji(kulogwa au kutupiwa
majini) hivyo nguvu zikawa zinagawanyika hospitalini na katika maswala ya
kienyeji na maombezi. Mwishowe lakini mama alikubali kumrudisha mwanaye
hospitali ya Mwananyamala baada ya hali kuzidi kuwa mbaya.
Moja
kwa moja Mwananyamala walimuandikia rufaa apelekwe hospitali ya Mloganzila,
iliyo chini ya Hospitali kubwa ya Muhimbili. Madaktari pale walijitahidi
kuchukua kila aina ya vipimo siku hiyohiyo huku mama yake naye akienda kuhangaika
kutafuta fedha kwani hakuwa na bima ya afya. Kwa bahati mbaya siku ya pili yake
kabla hata ya kuanza matibabu kamili kijana yule alizidiwa na kuaga dunia kifo
kilichoacha simanzi kubwa si kwa mama yake mzazi tu bali kwa kila mtu
aliyemfahamu yule kijana.
SOMA: Ukweli mchungu kila mtu anaopaswa kuukubali maishani kabla hajaiaga dunia.
SOMA: Ukweli mchungu kila mtu anaopaswa kuukubali maishani kabla hajaiaga dunia.
Ripoti
ya madaktari wa Mloganzila ilikuja kuonyesha kwamba kjijana yule kilichomuua ni
ugojwa wa Tetanus au Pepopunda. Ugojwa huu watu wengi huuhusisha na kukatwa au
kutobolewa na kitu chenye kutu kama msumari au bati lakini ukweli ni kwamba
unasababishwa na bacteria fulani ambao hupenda kuingia mwili wa binadamu
kupitia vidonda au michubuko na huishi katika udongo, vinyesi vya binadamu na
wanyama. Hauna tiba maalumu ila mgojwa akiwahi matibabu kuna uwezekano wa
kupona. Huzuilika kwa kinga hasa watoto wachanga wanapozaliwa, mama zao wakiwa
wajawazito na mtu yeyote yule anapohisi yupo hatarini kupata hao bacteria.
Haijulikani
kijana huyu alipatapata vipi hao bacteria na mama yake anadai inawezekana
kipindi akiwa kwa ndugu zake huko Mbagala labda aliwahi kuumia mahali au kupata
kidonda bila kujua kama kingeliweza kumletea madhara hayo. Hata hivyo hakuwa na
jeraha lolote kubwa mwilini.
Maumivu makali ya jicho pia yalinifanya nikumbuke watu
kadhaa waliowahi kupata ulemavu wa macho yote mawili au jicho moja na
kutafakari ni maumivu na mateso kiasi
gani waliyopitia kipindi cha mpito walipokuwa wakitoka kwenye uoni wa kawaida
kuelekea ulemavu kamili wa macho.
SOMA: Punde kabla hujakata tamaa ya maisha soma hapa.
SOMA: Punde kabla hujakata tamaa ya maisha soma hapa.
Nilimkumbuka mwandishi na mhariri maarufu wa magazeti
Absalon Kibanda aliyepoteza jicho lake moja baada ya kushambuliwa na majambazi
wasiojulikana akitokea kazini usiku karibu na nyumbani kwake. Mungu mkubwa
jicho moja lilipona halikudhurika. Sipati picha kama angewezaje kuendelea na
majukumu yake ya uandishi wa habari.
Isingelikuwa tofauti tena na kumtoa samaki kwenye maji na kumweka nchi kavu.
Nilimkumbuka pia yule mtu aitwaye Saidi aliyetobolewa
macho yake yote mawili na mtu hatari aliyejulikana kama Scorpion maeneo ya
Buguruni Sheli, nikajaribu kuvaa viatu vyake lakini nikaona havinitoshi ni
vikubwa mno! Hata kama ni ulemavu wa macho kwa upande wangu bado ingelikuwa ni
jicho moja siyo mawili kama ilivyokuwa kwa bwana Said. Nilizidi kupiga picha na
kujaribu kufikiria changamoto walemavu wa macho wanazokutana nazo wawapo
barabarani nikathibitisha wana changamoto za kweli.
SOMA: Historia ya siku ya kutokomeza umasikini duniani ni ya kusisimua.
SOMA: Historia ya siku ya kutokomeza umasikini duniani ni ya kusisimua.
Siku ya Ijumaa, siku ya 6 baada ya matibabu pale Magomeni
kutoonyesha nafuu yeyote, nilifikiria nirudi tena palepale nikawaeleze ili
wanipe ushauri iwapo niende hospitali nyingine au la. Nilitoka nyumbani asubuhi sana kusudi nisije kukutana na miale
ya jua linapochomoza kabla sijafika hospitali kwani sasa jicho lilikuwa ndio
limezidi kabisa kukataa mwanga hata uwe kidogo, hata miwani ya jua nayo ilikuwa
haiwezi tena kunifanya nisisikie maumivu makali. Lilikuwa likitoa machozi
mfululizo na nafuu pekee sasa ikawa ni kuweka kitambaa juu ya miwani tena kwa
kufunika macho yote mawili huku nikigeukia upande usiokuwa na miale ya jua
kwani hata mwanga kidogo tu kwenye jicho la kushoto nao ulionekana kama vile
unapenya kwenye jicho la kulia. Chumbani taa ilizimwa muda wote usiku na mchana
na mchana mapazia yalifungwa yote kusiingie mwanga wowote ule mkali.
Siku hiyo ya Alhamisi nikiwa kwenye daladala la
Mbezi-Kimara ili nikapande mwendokasi, nilimpa kondakta nauli shilingi elfu
moja akanirudishia chenchi sh. 600. Mara kondakta yule aliniita akiniuliza, “bro,bro, kwani una matatizo ya macho?” nikamjibu ndiyo huku nikikazana kufunika vizuri jicho la kulia kwa kile
kitambaa. Alinitaka nimpe ile shilingi mia sita kisha na yeye akanirudishia ile
elfu moja niliyompatia. Badala ya kufurahi kitendo kile kilinishtua kwani
nilianza rasmi kuhisi namna ambavyo walemavu hutendewa na baadhi ya wasamaria
wema. Ndio muda nilioanza rasmi kuonja hali ya kuwa mlemavu wa macho.
Sikushuka Kimara mwisho shauri ya kukwepa kupanda daraja
nikashuka Korogwe na kuingia moja kwa moja kwenye Mwendokasi lililokuwa limejaa
sana abiria. Nikasimama kwa shida na miwani yangu ya jua huku kitambaa nacho
hakibanduki machoni kuhakikisha mwanga wa jua ambalo tayari lilikuwa
limekwishaanza kuchomoza hauingii moja kwa moja machoni.
SOMA: Pipi ya kijiti yaweza kuwa hatari sana kwa mwanao, chukua tahadhari.
SOMA: Pipi ya kijiti yaweza kuwa hatari sana kwa mwanao, chukua tahadhari.
Gari likiendelea na safari nilihisi mkono wa mtu
ukinigusa begani, “Kaka, kaka, njoo ukae
hapa inaonekana unaumwa ” Dada mmoja aliyekuwa ameketi kwenye siti
alivyoona hali niliyokuwa nayo akashindwa kujizuia na kuniita nikakae kwenye
kiti alichokuwa amekalia. Hili nalo pia lilinishitua sawasawa tu na lile la
kurudishiwa nauli na konda, nikazidi kuona dhahiri sasa naelekea kuwa na
ulemavu kamili wa macho.
Nilipofika kwa daktari wa Magomeni, alishtuka kuniona
tena huku hali ikiwa mbaya zaidi. Nikamsikia akimuita daktari mwingine wa macho
mwanamke wanayefanya pamoja, “Mama hebu
mcheki huyu” Nilimpa lile kadi akalisoma kisha akanichunguza jicho, hawana
vifaa vingi sana vya kupimia macho, akachukua smartphone yake na kuwasha tochi
kisha akanimulika kwenye jicho kama anapiga picha vile. Mama alionyesha kama
kushtuka hivi halafu akaniambia niketi kwenye kiti kingine maalumu kwa ajili ya
kupima uwezo wa macho kuona.
Nilitakiwa kusoma maandishi kama ile siku ya kwanza
lakini jicho lililokuwa na ugonjwa safari hii lilipoteza kabisa uwezo wake wa
kuona kwa karibu asilimia 50. Ina maana nilipofunga jicho la kushoto, jicho la
kulia halikuwa na uwezo wa kutambua nusu
ya herufi za maandishi yaliyokuwa yamewekwa mbele yangu.
Yule mama Daktari aliniambia kuwa tatizo langu pale
wasingeweza kuendelea tena kulitibu kutokana na jicho kuanza kupoteza uwezo wa
kuona hivyo angeniandikia rufaa niende hospitali kubwa, mwananyamala au Muhimbli lakini alifikiria kidogo kisha
akaniambia, “ Sijui lakini ninavyokuona
sidhani kama utashindwa kwenda pale Mikocheni CCBRT, kama utaweza ni bora uende
pale moja kwa moja kwani ukisema uendelee kuhangaika hospitali za kawaida huku
jicho likiendelea kupoteza uwezo wa kuona namna hii ni hatari, unaweza
ukalipoteza jicho lako kabisa”.
SOMA: Ua zuri lakini hatari linaloweza kuua dakika kumi na tano tu
SOMA: Ua zuri lakini hatari linaloweza kuua dakika kumi na tano tu
Aliandika andika pale kwenye kadi, nikatoka zangu
kuelekea CCBRT Iili pamoja a vipimo vingine wakanipime na ugojwa wa presha ya
macho(glakoma) ambao daktari huyu alihisi naweza kuwa nao kwani dalili za
presha ya macho nazo ni pamoja na maumivu na macho kuwa mekundu. CCBRT hutoa matibabu ya matatizo ya macho kwa
walemavu na watu wengine wa kawaida,
hutibu aina zote za magojwa ya macho ikiwemo glakoma, upasuaji, miwani, uoni
hafifu, mtoto wa jicho na dalili za
matatizo ya macho za aina zote.
Niliingiwa na hofu kubwa sana baada ya kusikia naenda
kupima presha ya macho, nikaanza kufikiria kama nitakuwa nayo itakuwaje kwani
ugojwa huo ni serious sana hasa ukishaanza kusikia dalili kama nilizokwishaanza
kuziona. Mara nyingi unaweza kutibu athari zake tu usipofuke iwapo utawahi
kuzigundua mapema. Isitoshe inasemekana huanza na jicho moja kisha muda mfupi
baadae la pili nalo hufuatia.
Nilipanda basi la Msasani nikashuka ilipo hospitali ya
macho CCBRT, nilikata kadi na moja kwa moja nikaelekezwa kuketi kwenye viti
kusubiri namba yangu ya faili iitwe nikaonane na dokta. Kabla ya kuwaona
madaktari kwanza unafanyiwa vipimo na manesi kikiwemo hicho kipimo cha presha
ya macho. Foleni ilikuwa ndefu na mpaka kufikia saa 9 nilikuwa bado sijaitwa.
Ila uzuri wa pale ni kwamba hawaruki namba ya mtu, aliyewahi amewahi na
ukichelewa umechelewa.
SOMA: Kwanini chanjo ya malaria imekuwa ngumu hivyo kupatikana?
SOMA: Kwanini chanjo ya malaria imekuwa ngumu hivyo kupatikana?
Zamu yangu ilipofika, mtaalamu alinipima presha ya macho
kwa kidude mfano wa bunduki ya ‘toy’ kisha akajaza katika kadi langu nambanamba
fulani, sikuelewa namba aliyoandika ilimaanisha kitu gani hivyo nikawa bado na
wasiwasi ambao hatima yake ingeenda
kujulikana kwa daktari mwenyewe. Nilielekezwa na yule mtaalamu(nesi) nielekee
chumba namba 12 wanakopatikana madaktari. Huko nako nilikuta foleni ni ndefu
lakini ilikuwa ikitembea harakaharaka. Kuna kama hall hivi ambalo wapo
madaktari wengi kila mmoja na kizimba chake. Mbele ya Daktari ipo mashine kubwa
ya kisasa ya kioo kwa ajili ya kuchunguzia macho inayofanana na darubini kubwa.
Mfano wa mashine hiyo wanayotumia
madaktari kupimia macho, mwanaume aliyeko kulia ndio daktari, kushoto ni mgonjwa wa macho akichunguzwa.
|
Daktari aliyenitibu alikuwa mwanaume wa makamo, alianza
kulichunguza jicho langu kwa kuniambia niingize kichwa kwenye mashine ambapo
macho hulenga katika chombo kinachomwezesha kuyachunguza. Alinitaka niangalie juu,
chini kisha kila upande na baada ya hapo
akaandika kwenye kadi. Aliniambia kuwa jicho langu lilikuwa na maambukizi
(infection), hivyo ataniandikia dawa za matone(aina mbili) nitakazokwenda
kutumia kwenye jicho lililokuwa na tatizo tu mpaka tarehe ya kurudi tena kwa
uchunguzi.
SOMA: Vitu vitano (5) vitakavyokupa utulivu wa nafsi na amani ya moyo katika maisha yako
SOMA: Vitu vitano (5) vitakavyokupa utulivu wa nafsi na amani ya moyo katika maisha yako
Mpaka naondoka pale hospitalini ilikuwa yapata kama saa
11 jioni hivi, muda ulikuwa umekwenda sana lakini sikujali kwani nilikuwa
angalao nina matumaini kwamba nimepata matibabu. Muda ule nadhani hata
madaktari na wahudumu katika ile hospitali wengi wao walikuwa wakiondoka
makwao. Hili ungeweza kuliona dhahiri hata kwa madaktari mle chumbani kwani
walionekana wamechoka kwa kazi nyingi na foleni ndefu ya wagojwa. Hata hivyo niliwasifu
kwa uvumilivu wanaouonyesha kwa wagojwa kwani mgojwa faraja yake ni kuona
anapata huduma bila kujali muda atakaosubiri.
Nilikwenda kuzitumia zile dawa za macho kama
nilivyoelekezwa na daktari na baada ya siku tatu (3) nikaanza kupata nafuu.
Wiki moja baadae sasa jicho langu limeanza kurudia tena katika hali yake ya
kawaida.
HITIMISHO:
VITU
NILIVYOTAKA MSOMAJI UJIFUNZE KWA KIFUPI KUTOKANA NA MKASA HUU ULIONIKUTA
1. KABLA HUJAFA HUJAUMBIKA.
Ukiwa
ungali bado unaishi hapa duniani tegemea lolote kukukuta na wala haijalishi
kama ulizaliwa na viungo vyako vyote kamili, hivyo wajali wale waliokuwa na
mapungufu mbalimbali katika viungo vyao au akili kwani hawakupenda kuwa kama
vile walivyo, wengi walikuwa tu kama ulivyokuwa wewe sasa. Wenye macho mekundu
hawajapenda kuwa vile hata wewe unayemuua kikongwe mwenye macho mekundu leo
ukisema ni mchawi unaweza kuja kuuwawa pia na wewe hivyohivyo hali hiyo
itakapokuja kukukuta
Walemavu
wasioona, wasiosikia, walewmavu wa ngozi, wenye ulemavu wa miguu au kiungo
kingine chochote kile, changamoto wanazozipata ni za kweli wala si kama
wanadeka kama watu wengi wanavyowachukulia. Taabu wanazozipata wakiwa kwenye
vyombo vya usafiri, majengo ya umma, tasisi na hata maeneo mengine mbalimbali
wanastahili kupewa msaada na upendeleo wa kipekee kuwapunguzia makali ya taabu
hizo.
2. UMASIKINI NI CHANZO KIKUBWA CHA MATATIZO
MENGI KWA WATU.
Uchunguzi
wa afya wa mapema unaweza kuepusha madhara mengi na hata wakati mwingine vifo.
Yule kijana mama yake kutokana na kutokuwa na uwezo alihangaika na matibabu
madogomadogo mtaani mpaka pale hali ilipokuwa mbaya zaidi akiwa
ameshachelewa akampoteza mwanaye. Ukiwa
mzima huna tatizo lolote la kiafya, pigana kufa na kupona katika shughuli zako
za kiuchumi ili wakati wa majanga kama ya homa uweze kujisaidia mwenyewe kwa
matibabu ya maana.
3. MAGONJWA MENGINE HUWEZI HATA KUDHANIA
KAMA YAPO.
Ni
vigumu sana kwa mtu wa kawaida kuamini kama magonjwa hatari kama vile tetanus,
homa ya inni, glakoma na mengineyo bado ni hatari na yanaendelea kuua watu. Kwa
kuwa hayatokei mara kwa mara, mtu anapougua magojwa hayo wale
wanaomzunguka huwa hawaamini, wanabakia tu kuhangaika na kulaumu nguvu za
giza ambazo ni vigumu mtu kuzithibitisha.
4. CHELEWACHELEWA NAYO SIYO NZURI, KUNA
MAMBO MENGINE SI YA KUSUBIRI HATA MASAA.
Nilichelewa
sana kuchukua hatua za haraka jambo ambalo lingeweza kunifanya nipoteze jicho
langu au yote mawili. Nimegundua kuna magojwa mengine ambayo mtu hutakiwi
kabisa kuyachelewesha. Nilitakiwa kuchukua hatua za maana tangu siku ile ya
kwanza tu nilipoanza kuhisi maumivu ya jicho, gharama haikuwa kikwazo sana
kwangu bali ile kusema tu, ‘ngoja kwanza
nianzie hospitali ndogo’ hata hivyo ndani ya zile siku saba bado nilizembea
sana.
5. BIMA NI
MUHIMU MNO DUNIA YA SASA!
Gharama
za bima ya afya kwa mwaka huwezi ukalinganisha na gharama utakazokuja kulipa
pindi ukiugua ugojwa mkubwa na huna bima. Ifike mahali sasa watu tuone bima
kama ni kitu cha lazima katika maisha yetu.
6. KAMA VIUNGO VYA MWILI VINAVYOTEGEMEANA, MAISHA NAYO ILI YAENDE VIZURI NI LAZIMA KITU ZAIDI YA KIMOJA VIBALANSI, AFYA, UCHUMI, MAHUSIANO NA ROHO.
Pamoja na kuhangaika kutafuta maisha mazuri kiuchumi, lakini unatakiwa pia kuichunga sana afya yako ya kimwili, mahusiano yako na watu wengine yakiwemo ya kifamilia & ndoa, lakini pia mahusiano yako na Mungu(kiroho). Kila kimoja kipe nafasi yake kwani kimoja kati ya hivyo kikitetereka huwezi kufikia maisha mazuri unayoyatamani.
Pole Sana mwalimu wangu
ReplyDeleteNashukuru sana mdau na Mungu akubariki.
Delete