Ni miezi miwili tu na siku 9 zimebakia tokea
leo hii ili mwaka wa kawaida uishe, lakini ni miezi 3 kamili imebakia ili
kampeni yetu ya mwaka huu imalizike rasmi. Kampeni au kauli mbiu yetu ya mwaka
2018 ilikuwa inasema hivi, MZUNGUKO MZURI WA FEDHA NDIYO NJIA BORA ZAIDI YAKUFIKIA MALENGO YAKO MWAKA 2018 na ilikuwa ikitekelezwa kupitia blogu ya
jifunzeujasiriamali, Group la whatsapp la Michanganuo-online na katika mitandao
mingine ya kijamii mbalimbali. Tulianza rasmi tarehe 19/1/2018.
Muda huu mfupi uliobakia tutamalizia baadhi
ya malengo tuliyojiwekea huku tukifanya tathmini ya yale tuliyokwishatimiza
kama ilivyokuwa kwa kampeni nyingine zote zilizopita huko nyuma. Kumbuka
tuliwahi kuwa na kampeni nyingine mbili miaka iliyopita, ile ya "Kuelekea
utajiri" na nyingine ilikuwa ikiitwa, "Kujirudishia ukuu wako tena"au “Make yourself
Great Again”.
Malengo yetu makuu kwa mwaka huu yalikuwa ni
haya yafutayo;
1. Kutoa
masomo kila siku yanayohusu mzunguko chanya wa fedha katika biashara na mtu binafsi.
2. Kuandika
Hatua kwa hatua mipango ya biashara 12. Hii ni michanganuo bunifu ya biashara
zile zenye uwezo mkubwa wa kuzalisha faida haraka.
Utekelezaji
wake.
Mpaka sasa lengo la 1 tumelitimiza kwa zaidi ya asilimia
95, wale waliojiunga na group la wasap la Michanganuo-online ni mashahidi.
Tumetoa masomo mbalimbali ambayo mkusanyiko wake tumetengeneza vitabu 2 vyenye
kurasa zipatazo 100 kila kimoja. Masomo hayo ni ya hali ya juu yanayolenga
kumfanya mtu aweze kuboresha mzunguko wake wa fedha katika biashara yake na pia
mfukoni mwake. Ni furaha yangu kubwa kuwa wewe rafiki na mdau wangu
muhimu kabisa hautakosa kuvisoma vitabu hivi 3 vilivyokusanya madini mengi ya mwaka mzima.
Katika lengo letu la pili tumeweza kulitimiza kwa
asilimia 35 mpaka sasa hivi na tumechanganua hatua kwa hatua michanganuo ya
biashara nne 4, mitatu ya ufugaji wa kuku wa aina zote na mmoja kilimo cha
matikiti maji. Michanganuo hiyo yote tuliandika hatua kwa hatua huku kila
mshiriki akijifunza jinsi michanganuo ya biashara hizo inavyoandikwa kuanzia
mwanzo hadi mwisho na kisha kila mtu kupata kopi yake ya mchanganuo
uliokamilika kila kitu.
Muda
uliobakia wa miezi 3
Tutafanyia kazi lengo letu hili la pili ambalo
halijakamilika bado tumalizie asilimia 65% zilizobakia . Tutaanza tarehe 3/11/2018 tukiandika
hatua kwa hatua mpango wa biashara ya Mgahawa wa chakula. Chakula ni moja kati ya
biashara zinazolipa sana ukiifanya kwa ubunifu, hivyo tutaanza nayo na kila
baada ya wiki moja tena tutaendelea kuchanganua biashara nyingine zilizobakia
mpaka zitimie zote 12 ifikapo Januari 19 2019 tutakapohitimisha rasmi kampeni
yetu hii na kuanza tena nyingine mpya.
SOMA: Usiogope mabadiliko kwenye maisha kwani ni kama plasta, ikishabanduka kidonda hupona chenyewe.
Wito
wangu kwako na zawadi ya vitabu 3
Ikiwa bado hukuwa umejiunga na kampeni yetu hii, nafasi
bado ipo na utaweza kupata kila kitu walichopata wale waliotangulia. Masomo
yote ya mtiririko wa fedha tumeyakusanya(compile) katika vitabu vikubwa 2 na
yale yahusuyo kuandika Michanganuo hatua kwa hatua tumeyakusanya pia katika
kitabu kimoja kikubwa chenye kurasa 100. Isitoshe kuna vitu vingine unapata
kama kile kitabu cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali, vitabu vingine na
masomo mbalimbali ambayo hayapo katika vitabu hivyo. Orodha kamili ya vitu
vyote unavyopata baada ya kujiunga ni hivi hapa chini;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu
kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu
kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu
kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.
5. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA:
Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo
wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
9. Vielezo(Templates)
za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
10. Mfumo
mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM)
unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake
pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
11. Somo
muhimu sana la mzunguko wa fedha.
12. Ukurasa
mmoja wa mchanganuo.
Mwisho wa offa na vitabu hivi ni Januari 19, 2019 lakini
pia itategemea muda group hili la Michanganuo litakapojaa watu 250, iwapo
litajaa kabla ya tarehe hiyo jambo ambalo nategemea litatokea kwani sasa group
lina zaidi ya watu 100, basi na nafasi nazo zitakuwa zimejaa.
Baada ya hapo
tena vitu vyote hivyo vitakuwa kila kimoja kikiuzwa peke yake kwa bei tofauti.
Hivyo ni bora mtu ukawahi mapema kusudi uweze kupata kila kitu kwa shilingi elfu
10 tu. Ni punguzo kubwa ambalo halitakaa litokee tena na halijawahi kutokea
popote. Ukisema uje ununue kila kimoja peke yake, vyote utalazimika kulipa zaidi ya shilingi laki moja.
SOMA: Hebu sikiliza hapa, Kwanini semina hii ni ya kipekee na haijawahi kutokea mahali pengine popote?
Ikiwa unapenda kujiunga na group la Michanganuo-online
uweze kushiriki semina zinazoanza tarehe 3, Novemba pamoja na kupata vitabu
hivyo vipya 3 na offa nyingine zilizotajwa hapo juu zote, lipa kiingilio chako
ambacho ni shilingi elfu 10 kupitia namba zetu za simu, 0712202244 au
0765553030, jina ni Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe wa whatsapp au wa kawaida usemao, “NIUNGANISHE NA
GROUP LA MICHANGANUO” Namba ya whatsapp ni 0765553030. Baada ya hapo
utaunganishwa muda huohuo na kutumiwa kila kitu.
Kama hutumii whatsapp, masomo haya na kila kitu tunatuma
kupitia email na blogu ya private hivyo utatutumia tu anuani yako ya gmail
unayotumia.
Ufuatao ni muonekano wa vitabu vyako vipya vitatu;
Kitabu
cha 1
Kitabu cha 2
Kitabu cha 3
0 Response to "IKIWA IMEBAKIA MIEZI 3 KAMILI MWAKA UISHE, POKEA ZAWADI HII YA VITABU 3"
Post a Comment