Siku zilizopita niliwahi kuandika makala moja nikasema
hivi, Huna mtaji wa kutosha, hukopesheki?Jaribu njia hii ya kufunga mkanda(Bootstrapping). Katika makala hiyo
nilieleza jinsi mjasiriamali mdogo asiye na mtaji mkubwa anavyoweza kutumia
rasilimali kidogo alizokuwa nazo kuendesha biashara yake pasipo kutafuta msaada
kutoka nje.
Sasa leo tena nimekuja na mikakati mingine 11 tofauti
ambayo yeyote yule mwenye biashara inayoanza au iliyozorota anaweza akaitumia
katika kukabiliana na changamoto kubwa ya mtaji. Mbinu hzi za kujikwamua au
kufunga mkanda zimetumiwa na watu wengi zikiwemo hata na taasisi na nchi
mbalimbali kama nilivyoeleza kwenye makala hiyo iliyopita. Mbinu za leo 11 ni
hizi zifuatazo;
1.Kasi
na viwango.
Unapokuwa ukiendesha biashara yako tambua kuwa gharama
muda wote zipo palepale uwe umeuza ama haujauza kabisa. Lakini kwa upande wa
mapato yanajiamulia yenyewe ni mda gani yaingie kwa mfano mapato yataingia tu
pale utakapouza, usipouza hamna kitu! Kwahiyo piga ua kama mjasiriamali, kila
kitu kinakutegemea wewe na unapaswa kuhakikisha unajitosheleza muda wote ili
mambo yasiende mrama.
Kitu utakachotakiwa kukifanya ili kulitimiza hilo kwa
kuwa mfukoni hauna pesa cash za kutosha ni KUONGEZA KASI YAKO YA MAUZO pamoja
na kuwa mtu wa VIWANGO. Unapaswa kuwa ni mtu wa kufanya majaribio(utafiti)
haraka sana kujifunza haraka na pia kuingiza pesa haraka! Vinginevyo utajikuta
umeishiwa kabisa fedha kidogo ulizokuwa nazo na kusababisha biashara kufa au
kuanguka vibaya.
2.Anza
kidogo.
Kidogokidogo hujaza kibaba na kuna dhana moja inayotumiwa
sana katika mabenki na taasisi za fedha, “Compound
Interest” ambayo maana yake ni hii, kitu kidogo kinapojiongeza chenyewe
halafu kile kilichoongezeka nacho kikawa kinajiongeza sambamba na kile cha
mwanzo mfano, riba katika mikopo inapoongezeka huku riba nayo ikizaa riba pia,
matokeo yake ni ya kushangaza sana!
Kitu hicho hatimaye huongezeka haraka na kufikia ukubwa
wa kushangaza. Na biashara nayo unapoanza kidogo tu lakini huku ukiirudisha
faida ile inayopatikana katika mtaji wa awali faida itaongezeka haraka sana na
biashara kuwa kubwa ndani ya muda mfupi.
3.Tekeleza
kwanza ndipo upange.
Hapa inaweza kuonekana nakinzana na dhana nzima ya mpango
wa biashara(business planning) lakini hapana nitafafanua. Moja ya tatizo kubwa
la wajasiriamali wanaoanza kushindwa kutoka
pale walipo na kupiga hatua zaidi ni kupanga kupita kiasi. Mipango
haiepukiki lakini kuna kiwango anachotakiwa mfanyabiashara mdogo anayeanza
kupanga tofauti na wafanyabiashara wakubwa au makampuni.
SOMA: Huna muda wa kutosha kuandika mpango wa biashara? tumia njia hizi 3 rahisi.
SOMA: Huna muda wa kutosha kuandika mpango wa biashara? tumia njia hizi 3 rahisi.
Ndio maana kwa mfano katika darasa letu la wasap la
michanganuo-online tumeweka machaguo(options) mbalimbali kama vile, tuna kitu
kinachoitwa “Ukurasa mmoja wa mchanganuo” hiki ni kielezo(template) inayompa
mjasiriamali mdogo anayefunga mkanda fursa ya kutengeneza mchanganuo wake mfupi
kwa muda mchache sana huku akiendelea na mambo yake mengine ya biashara haraka.
Kuna Advanced
Business Plan Template ya kawaida sasa ambayo hutumika kutengeneza mpango
kamili wa biashara, na huu sasa kama unataka kuanzisha biashara kubwa au ya
kati, pengine unataka kuanzisha kiwanda chako cha kutengeneza juisi, sabuni,
mikate huku ukiwa na mtaji wako wa milioni kadhaa, huwezi kukwepa kutengeneza
mpango kamili wa biashara.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.
Pointi yangu hapa ni kwamba unapokuwa katika ngazi hii ya
ufungaji mkanda mipango iwepo lakini utekelezaji uwe mkubwa na wa haraka zaidi,
hii itakusaidia kuepukana na kuja kutekeleza mawazo ambayo tayari yameshapitwa
na wakati. Ukiendelea kupanga tu pasipo utekelezaji wa haraka utaishia kubakia
na ndoto kichwani zisizotekelezeka. Na hii hutokana hasa na sababu kwamba
biashara ndogo zina rasilimali chache mno zisizoruhusu muda upotee.
4.Wewe
ndio kila kitu kwenye biashara.
Kwa kimombo wanasema hivi,
CEO = Chief Everything Officer.
Usipoiamini kanuni hiyo hapo juu basi na wala usifikirie
hata kidogo wazo la kuanzisha biashara yako mwenyewe, na sahau kabisa habari ya
kufunga mkanda. Wewe ndiye utakayefanya kila kitu katika biashara yako kuanzia
kufanya usafi kama ni ofisi, kuingia mikataba na wateja, kuuza, kutunza
mahesabu, kutafuta soko mpaka kurekebisha holder ya taa na kuinstall program
mpya kwenye laptop yako.
SOMA: Jinsi ya kusimamia biashara yako ndogo unayomwachia mfanyakazi.
SOMA: Jinsi ya kusimamia biashara yako ndogo unayomwachia mfanyakazi.
5.Kuuza
kwa kubadilishana bidhaa au huduma na mteja(Barter Trade)
Unaweza usiamini kama inawezekana kupata kitu fulani au
huduma bila ya kulipa fedha taslimu kwa kubadilishana na mtu mwingine huduma au
bidhaa unazouza wewe yeye akakupatia pia huduma au bidhaa anazouza tena kwa
gharama nafuu kuliko ungezilipia taslimu. Njia hii licha ya kupunguza gharama
pia huweza kukujengea mahusiano imara na wajasiriamali au wafanyabiashara
wengine kama wewe. Chunguza wateja wako mbalimbali wanaokuletea bidhaa au
huduma kama na wao wanaweza kuhitaji kile unachouza kisha mnabadilishana.
Mtindo huu wa kubadilishana bidhaa/huduma unaweza usiwe
sawasawa na ule uliokuwa ukitumika zama zile za kale za mawe lakini unachopaswa
tu kufanya ni kuhakikisha unapata punguzo tofauti na vile ambavyo ungelinunua
kwa fedha taslimu. Inaweza kuwa vigumu kubadilishana kitu na wafanyabishara
waliopiga hatua, tafuta wale mlio katika ngazi(levo) moja.
6.Fanya majadiliano ya bei ili kupata bei
nzuri zaidi.
Hakikisha bei unayouza ina maslahi kwako, unaweza ukaanza
kutaja kiasi cha juu kidogo mwishowe mkafikia muafaka kwenye bei itakayokuwa
nzuri kwako.
7.Wekeza
kwenye teknolojia.
Teknolojia ikitumika vizuri inaweza ikaokoa fedha nyingi
sana na kuongeza ufanisi katika biashara. Tumia muda kutafiti teknolojia
zinazoweza kukupunguzia gharama na kuboresha mawasiliano. Teknolojia haitakiwi
kuwa ni ya gharama ya juu sana, kwa mfano badala ya kununua programu za
kompyuta kwa hela nyingi unaweza ukatumia zile zinazopatikana bure mtandaoni
ilimradi zikidhi shida unayotaka kuitatua.
SOMA: Mawazo ya biashara zitakazovuma miaka ijayo 2018 na kuendelea mpaka 2020
SOMA: Mawazo ya biashara zitakazovuma miaka ijayo 2018 na kuendelea mpaka 2020
8.Mapato
ya ziada ya biashara.
Kuna mazingira mengine biashara inaweza ikatengeneza
fedha kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja kama vile;
· Kukodisha
sehemu ya eneo/chumba chako cha biashara au kualika watu wengine kuja kushea na
wewe ofisi na kisha mnashirikiana pia kulipa pango kwa mwezi.
· Kuuza
vifaa ambavyo huvitumii tena ofisini kwa mfano kompyuta ya zamani nk.
9.Kuhakikisha
hesabu za biashara yako zipo sawasawa.
Unapotaja hesabu za biashara mtu moja kwa moja anaweza
akaanza kufikiria kumuajiri mhasibu au mtu aliyesomea utunzaji wa fedha lakini
hilo si muhimu kwa mjasiriamali anayefunga mkanda. Kujifunza wewe mwenyewe ABC
za mahesabu ya biashara siyo lazima uingie darasani. Vitabu na semina vinaweza
vikatosha kukidhi haja hiyo.
Kwa mfano kitabu kama kile cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA
UJASIRIAMALI tumejitahidi sana kuweka ABC zote za hesabu za biashara kwa mtu wa
kawaida kabisa ambaye hata kama hajawahi kusoma masomo ya book keeping anaweza
kushika na kuelewa. Vitu kama vile Mapato, gharama, matumizi, Faida na hasara,
Mizania ya biashara, mzunguko wa fedha na uwiano wa sehemu za biashara ni vitu
vya msingi kufahamu ikiwa kweli utapenda uwe na uwezo kamili wa kuidhibiti
biashara yako.
10.Uza
bila gharama za matangazo.
Kuna njia nyingi mtu unaweza ukazitumia kutangaza na
kuuza biashara yako pasipo kutumia gharama kubwa kwenye matangazo ya biashara.
Kila biashara inaweza kutumia njia tofauti lakini njia zilizozoeleka zaidi ni
hizi hapa chini,
· Mitandao
ya kijamii
· Kutengeneza
mtandao wa watu mnaojuana.
· Matangazo
ya mdomo kwa mdomo
· Mahusiano
mazuri kwa umma
Njia hizi zina gharama kidogo sana na wakati mwingine hazina
kabisa, pia zina uwezo mkubwa wa kukuletea wateja watiifu wakudumu.
11. Zingatia kipaji
unapoajiri kisha pima utendaji.
Utakapoamua sasa unataka kuajiri mtu akusaidie shughuli zako,
usiangalie cheti wala ana digirii ngapi ingawa navyo pia ni muhimu, cha msingi
zaidi pamoja na elimu yake lakini ni lazima afikie vigezo hivyo 2, kipaji na
uwezo wa kufanya kazi unayotaka aifanye. Tafuta muda wa kuwaendeleza
wafanyakazi wako na kuwajenga waendane na malengo ya biashara yako kisha pima
utendaji wao wa kazi na kutoa mrejesho. Ikiwa utaajiri watu/mtu asiyekuwa
sahihi hataruhusu biashara yako ikue na mwishowe ataua kabisa dhana nzima ya
kufunga mkanda.
………………………………………
Ni matumaini yangu kuwa njia nilizozitaja hapo juu, muendelezo wa
mbinu za kufunga mkanda ili mtaji uweze kukua pasipo kuingia madeni zinaweza
zikasaidia kuikwamua biashara ndogo inayoanza au iliyozorota. Kwa makala zaidi
karibu katika group letu la watsap la MICHANGANUO-ONLINE pia unaweza ukajipatia
vitabu vyetu mbalimbali, bonyeza hapa kwenye duka la vitabu mtandaoni kuviona.
Mimi na mtj wa laki nne
ReplyDelete