Ukiachilia mbali ufugaji wa kuku ule wa mazoea wa kujenga
afya ambao mtu huokota yai moja, mawili au matatu kwa siku na kuchinja jogoo
siku ya sikukuu za Iddi, Pasaka au Krismasi peke yake, wale wanaoamua kufanya
biashara ya kufuga kuku kwa dhati, wawe ni kuku wa kienyeji, kuku wa mayai wa
kisasa, kuku wa nyama(broiler) au hata kuku chotara kama vile kroiler hutumia
njia na mbinu mbalimbali nyingine zikiwa ni za kitaalamu na nyingine hata za
kienyeji lakini zenye uwezo wa kuleta faida.
Ufugaji wa kuku
tangu vifaranga wa siku moja mpaka wanataga au kuuzwa kwa ajili ya nyama
una gharama mbalimbali lakini gharama iliyokuwa kubwa kuliko nyingine zote ni ile
ya chakula. Gharama za chakula cha kuku huchukua asilimia 70% mpaka asilimia
75% ya gharama zote. Hivyo unapozungumzia upunguzaji wa gharama za utunzaji wa
kuku ni lazima uanze na gharama kwa upande wa chakula. Fursa au njia
nitakazozitaja hapa chini mtu anaweza akachagua kutumia zile atakazoona zinafaa
kulingana na mazingira yake anayofugia kuku na wala siyo lazima mtu azitumie
zote.
1.Kujitengenezea
chakula cha kuku mwenyewe.
Unapoamua kuchanganya chakula cha kuku mwenyewe nyumbani,
ni lazima kwanza ufahamu uwiano
sahihi(ratio) wa viambato(malighafi) mbalimbali zikiwemo nafaka
zinazotumika kutengenezea mchanganyiko huo wa chakula cha kuku. Kanuni ya
kuchanganya vyakula vya kuku siyo hesabu ngumu sana na mtu yeyote yule anaweza
akaitumia ikiwa atapata maelekezo vizuri.
Kwa kawaida kuku kama walivyokuwa viumbe hai wengine
kiafya wanahitaji makundi yote muhimu ya vyakula, wanahitaji wanga na mafuta
kwa ajili ya kutia joto na nguvu, Protini kwa ajili ya kujenga miili yao na
Vitamini na Madini kwa ajili ya kuwalinda na magojwa.Vile vile wanahitaji maji
safi ya kunywa. Kwa hiyo unapofahamu uwiano wa vitu hivi na ukachanganya
chakula chako katika hali ya usafi unaotakiwa utajikuta ukipunguza gharama za
ulishaji kuku wako kwa zaidi ya asilimia 50% ya bei ya vyakula kama hivyo
madukani.
Kuna teknolojia moja rahisi sana na yenye faida kubwa
ambayo mbegu za nafaka huoteshwa kwa kutumia maji bila udongo kabisa na baada ya
siku nne zinapokua zimemea zinakuwa zinaongezeka uzito karibu mara 7 ya uzito
wake wa awali. Majani haya ni chakula kizuri sana cha kuku na hata ndege aina
nyingine na mifugo kama vile ng’ombe, mbuzi na kondoo.
3.Uzalishaji
wa minyoo, funza, mchwa na azola.
Wadudu hawa na aina ya mimea iitwayo Azola huweza
kuzalishwa kwa wingi kwa kutumia teknolojia rahisi sana mfano kama funza
unaweza ukatumia damu ya wanyama kama vile ng’ombe, ukaiozesha katika chombo
kama ndoo kwa siku chache mpaka funza watakapozaana na kukua kisha unawasuuza
kwa maji safi tayari kwa ajili ya kuwalisha kuku wako. Mchwa nao ni hivyohivyo
unategesha kivutio cha mchwa karibu na eneo wanakopenda kupita, wakishajaa pale
unatifua na kulisha kuku wako.
4.Kulisha
kuku mabaki ya vyakula.
Unaweza kutumia mabaki ya vyakula nyumbani kwako lakini
pia kama kuna sehemu nyingine mfano mashule, mahospitali, mahoteli au taasisi
yeyote ile wanakopika vyakula vingi kila siku unaweza ukajenga nao ukaribu wakawa wanakupa mabaki ya vyakula. Lakini
vyakula hivyo hakikisha vinakuwa havijaanza kuharibika au kutengeneza kuvu
kwani vinaweza kuwadhuru kuku wako kutokana na sumu au magonjwa.
5.Lisha
kuku wako huria.
Kana unalo eneo la kutosha na ambalo unaweza kuweka uzio
wa kuzuia wanyama na wadudu hatari wanaokula kuku, unaweza kuwaachia kuku wako
wakajitafutia chakula wenyewe katika eneo la wazi kama wafanyavyo wafugaji
wengi wa kuku wa kienyeji.
6.Lima
mazao ya nafaka, mbogamboga na matunda
Pia hii ni kama unalo eneo au unaishi maeneo ya kijijini.Ukilima
mwenyewe vyakula hivi utakuta gharama ya kuwalisha kuku wako inakuwa chini sana
na faida inapanda juu. Kwa mfano ufugaji wa kuku wa mayai, ufugaji wa kuku wa
nyama na ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa mfugaji anayetumia majani mabichi
kulisha kuku wake kama chalula cha ziada anaweza kupata faida nyingi hasa
katika upande wa gharama za madawa kwani kuku hawaugui ovyoovyo na mayai huwa
na kiini cha njano jambo linalovutia wateja wengi kuyanunua.
7.Chagua
aina ya kuku wanaokula chakula kidogo na usilishe kuku wako kupita kiasi.
Waatu wengi hudhani kwamba kuku wanatakiwa wale mpaka
wasaze, hii siyo sahihi. Ukishawapa kuku kiasi kile cha chakula wanachostahili
kupewa kwa siku basi usiongeze zaidi ya hapo. Vile vile punguza kuku waliozeeka
na ambao utagaji wao ni hafifu.
Njia nilizozitaja na nyinginezo ambazo pengine unaweza
kuwa unazijua ndizo wale wote unaowaona wakifuga kuku bila kuacha huzitumia kila siku na kushangaa wanapatajepataje faida na wala
hakuna muujiza mwingine wowote ule.
……………………………………
Ndugu msomaji, karibu ujiunge na group letu la whatsap,
mle tunajifunza kila siku masomo mbalimbali ya ujasiriamali na mzunguko wa
fedha ikiwemo michanganuo ya biashara mbalimbali kama vile michanganuo ya kuku
aina zote.
Kiingilio ni shilingi elfu 10, na unapata, kifurushi cha
michanganuo ya kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACK), na vitu vingine vingi kama
kitabu cha Michanganuo na Ujasiriamali na semina za mara kwa mara. Unakuwa pia
mwanachama wa kudumu bila kulipa zaidi.
Namba za kulipia ni 0712202244 au 0765553030 na baada ya malipo tuma ujumbe
wa kawaida au wasap kwa namba 0765553030 usemao; “NIUNGANISHE NA GROUP LA
MICHANGANUO”
Somo
la leo tarehe 10 October usiku saa 3 ni hili lifuatalo;
“RASILIMALI
2 ADIMU ZAIDI DUNIANI KULIKO DHAHABU NA ALMASI NA JINSI YA KUZIPATA”
Usikose somo hili muhimu.
0 Response to "Kupata faida kwenye ufugaji wa kuku wa kienyeji au wa kisasa mfugaji mjanja hutumia mbinu hizi."
Post a Comment