Unatumia kanuni ipi ya ushindi inayokuwezesha kufanikiwa
katika jambo lolote lile unaloamua kufanyia kazi? Jambo hilo linaweza likawa ni
biashara, kazi, masomo au shughuli nyingine yeyote ile ambayo ungependa
kuifanya kwa ukamilifu.
Unapowauliza watu wengi wakiwemo wataalamu wa masuala ya
ya elimu ya mafanikio na washauri wa biashara
juu ya ni nini cha kufanya ili mtu aweze kufanikiwa katika jambo lolote,
wengi watakujibu kuwa ni, JUHUDI au SHAUKU KUBWA kwenye jambo unalofanya, kwa
lugha ya kigeni unaweza ukasema, ‘PASSION’.
Ikiwa kwa mfano wewe unafanya kazi, umeajiriwa mahala
fulani na ungependa siku moja uone unapandishwa cheo kazini, kitu kikubwa
ambacho unapaswa kukionyesha ni Juhudi zako na Shauku kubwa kwenye utekelezaji
wa majukumu yako mbalimbali ya kila siku pale kazini uliyopangiwa kuyafanya na
bosi wako. Kisha bosi wako huyo naye bila shaka yeyote ile atakapogundua
mwenendo wako huo mzuri wa uchapaji kazi kwa nia, hatakuwa na sababu yeyote ile
wala kipingamizi cha kukupendekeza wewe upandishwe cheo kazini.
Hali ni hivyohivyo kwa upande wa ajira binafsi, ikiwa
labda unamiliki mradi wa ujasiriamali au tuseme biashara yako mwenyewe,
ukitengeneza au kuuza bidhaa na huduma bora na za hali ya juu kabisa zenye
uwezo wa kutoa thamani kwa yule atakayezitumia, unao uhakika asilimia kubwa ya
kuweza kupata wateja wengi watakaonunua bidhaa na huduma zako muda wote.
Hivyo hayo yote yaliyotajwa hapo juu yanahusisha mtu kuwa
na JUHUDI au SHAUKU KUBWA katika jambo lolote lile analolifanya liwe ni
biashara, kazi, masomo au kingine chochote kile kinachohusiana na majukumu yale
binadamu anayopaswa kuyatimiza ili maisha yaweze kusonga mbele kwa urahisi.
Kumbuka kwamba,
Mtu
mmoja tu aliye na Juhudi na Shauku kubwa katika kukifanya kile anachopaswa
kufanya, mtu huyo huweza kuwazidi watu wengine zaidi ya 50 wanaofanya kazi kwa
mazoea tu.
Pamoja na juhudi na shauku kubwa lakini nimeahidi pale
mwanzoni kuwa nitakupa njia nyingine mbili (2) za kukuwezesha kushinda
changamoto yeyote ile ya kimaisha iwe ni katika kutafuta kazi, mafanikio katika
biashara au hata mafanikio kwenye masomo. Mbinu hizi kama nilivyotangulia
kusema katika kichwa cha makala hii, siyo rasmi na wala huwezi ukakutana nazo
rasmi katika mfumo wa kawaida wa elimu na madarasa ya ujasiriamali.
Njia au mbinu hizi unaweza ukazihusisha na imani au dini
lakini pia nikuambie tu kwamba wala hazifungamani na imani ya mtu yeyote ile,
ni ‘Universal’ inakata kotekote, haina mwenyewe, aliye na imani na asiyeamini
wote zinawahusu. Mbinu hizo 2 si nyingine bali ni hizi hapa chini;
1.MSAMAHA.
Wasamehe kila mtu aliyewahi kukutendea jambo baya (Hata
kwa mfano kama uliwahi kutekwa na watu wasiojulikana kama Mohamed Dewji, MO)
wewe wasamehe tu watekaji wako. Iwe uliwahi kusalitiwa na mpenzi wako, rafiki
wa kiume(boy friend) au rafiki wa kike(girlfriend), mke, mume, rafiki wa
karibu, wewe samehe tu.
Kuna watu wengine waliwahi kukimbiwa na watu wao wa
karibu pale walipopatwa na mitihani mikubwa ya kimaisha, wewe samehe wala
usiweke kinyongo moyoni. Wenzako shuleni wanapiga makelele wewe ukijisomea huku
wakikuzodoa na kusema, ‘unasoma kama vile
umetumwa na kijiji’, wewe wasamehe bure.
Ulienda ofisi fulani kuomba kazi ukaombwa rushwa ya ngono
na kazi yenyewe wala usiipate, wewe samehe wala usiweke moyoni tena. Ulifukuzwa
kazi kwa majungu, ubaguzi na chuki tu, wewe wasamehe wabaya wako tena bila
sharti lolote lile.
Je,
wajua kwanini nakuambia Usamehe tu?
KUSAMEHE kunaondoa kabisa kwenye moyo wako na akili
hasira, kuchanganyikiwa na kukata tamaa jambo litakalokupa ahueni kubwa. Akili
yako na mwili vyote vitapata nafuu kutokana na majeraha yote uliyoyapata,
vitafunguka na kuwa tena vyepesi mithili ya vile ulivyokuwa wakati ulipokuwa
mtoto mdogo, unakumbuka ulivyokuwa mtoto ulivyokuwa kila wakati unajisikia
raha? Muda wote ukiwaza mambo mazuri utakayofanya ukiwa mkubwa? Utanunua
gari…utaoa…utakuwa profesa…nk?
Ukishafunguka hivyo sasa akili yako itakuwa na uwezo mpya
wa kuanza tena kufikiria malengo yako makubwa maishani kwa urahisi zaidi. Mbinu
hii ni ya kidhahania zaidi(kimawazo) na ingawa inaweza ikawa vigumu kuikubali
na kuitia katika vitendo lakini ukifanikiwa japo kuitumia hata kwa asilimia
chache tu utaanza mara moja kujisikia tofauti kubwa.
2.SHUKRANI.
Toa shukrani kwa kila mtu anayekuzunguka, taasisi
mbalimbali zilizochangia mafanikio yako kama vile, shule, chuo, kanisa,
msikiti, wazazi wako, walezi pamoja na wateja wako wote wanaonunua bidhaa na
huduma unazotoa na mfano hai hapa hapa nitakaokupa ni mimi binafsi, “Ninavyokushukuru
sana wewe kwa kuendelea kusoma makala na vitabu vyangu”
Hitimisho.
Mwisho ningepenga kuhitimisha makala hiii ya leo kwa
kukukumbusha kitu kimoja kwamba, hata kama utasahau kila kitu nilichoandika
tokea mwanzo wa makala hii lakini chondechonde shika mistari michache tu ya hii
aya ya mwisho ifuatayo;
Sisi
binadamu bila ya kujali hatua ile tulipo sasa, tunao uwezo mkubwa uliojificha
ndani yetu wa kufanikisha mambo makubwa ya kushangaza. JIAMINI na ufanye kile
unachotaka kukifanya kwa JUHUDI na SHAUKU KUBWA, SAMEHE wote waliokukwaza,
MSHUKURU kila mtu na matokeo yake yatakushangaza hata wewe mwenyewe.
…………………………………
Ndugu mdau na rafiki yangu katika blogu hii, kwa mwaka
huu mzima nimekua nikiandika makala za kuelimisha hapa katika blogu yako ya
jifunzeujasiriamali na katika list ya email. Naamini na wewe pia umekuwa
ukizifurahia, lakini ningependa uweze kupata na kunufaika na makala zaidi ya
hizi ninazotuma hapa(The best of my
works 2018).
Juzi nilikujulisha juu ya vitabu vipya 3, viwili
kuhusiana na masomo ya mzunguko wa pesa niliyokuwa nikiyatoa katika group la
whatsapp la Michanganuo-online, na kimoja kuhusiana na Kuandika hatua kwa hatua
michanganuo ya biashara mbalimbali zenye fursa kubwa ya kuzalisha faida.
Unaweza ukafikiria vitabu hivi vimebeba masomo ya kawaida
tu, lakini ningependa kukuhakikishia kuwa, hizi ni moja ya kazi zangu kubwa
zaidi kuzifanya mwaka huu wa 2018, ni masomo ya fedha yaliyo na msisimko wa
kipekee(The most Insirational Money
Topics of the Year 2018) Kwa kweli nisingejisikia vizuri kabisa wewe kama
mdau mdau wangu muhimu kukosa masomo haya.
Ada ya shilingi elfu 10 sikumaanisha kabisa kufanya
biashara bali ni kwa ajili tu ya kusaidia katika gharama za kuendeleza group na
kampeni hii kwa ujumla. Ndio maana ukiangalia vitu vyote mtu anavyopata hapo
chini kisha ukalinganisha na kiasi hicho cha ada, unaweza ukajisemea, “Peter Unacheza” Lakini yote ni kwa ajili ya kutengeneza timu
nzuri na imara kwani naamini katika Ushirikiano(Mastermindgroup) ndipo watu
hufanikiwa, siyo pesa peke yake.
Group letu la Michanganuo-online ambalo sasa tumezidi
watu 100, lengo letu ni kufikisha watu 250 tu mpaka mwishoni mwa mwaka huu,
tutakapoanza kampeni mpya. Nakusihi njoo ujiunge.
Kwanza kabisa ni ili uweze;
· Kuwahi
nafasi yako kabla hazijaisha,
· Pili,
uweze kunufaika na masomo yote tuliyokwishajifunza siku zilizopita kwenye group.
· Uweze
kushiriki semina za kuandika michanganuo zinazoanza tarehe 3 Novemba 2018.
· Uweze
kupata vitabu kikiwemo kitabu maarufu cha ‘MICHANGANUO YA BIASHARA NA
UJASIRIAMALI’
· Uweze
kuwa mwanachama wa kudumu wa kundi hili la kushauriana(Mastermindgroup) la
michanganuo-online
Vitu vyote utakavyotumiwa mara tu baada ya kulipia ada na kujiunga katika group ni hivi vifuatavyo;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu
kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu
kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu
kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.
5. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA:
Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo
wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
9. Vielezo(Templates)
za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
10. Mfumo
mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM)
unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake
pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
11. Somo
muhimu sana la mzunguko wa fedha.
12. Ukurasa
mmoja wa mchanganuo.
*Ikiwa
hutumii Whatsapp, hamna shida kwani masomo haya na semina vyote utatumiwa kwa
njia ya e-mail.
Namba
za kulipia ni;
0765553030
0712202244
Wasap:
0765553030
Jina
ni: Peter Augustino Tarimo
Ukishalipia,
tuma ujumbe usemao, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE”
0 Response to "MBINU 2 ZA USHINDI ZA KUFANIKIWA JAMBO LOLOTE, HAZIFUNDISHWI SHULENI, VYUONI WALA MADARASA YA UJASIRIAMALI"
Post a Comment