Kuna mashaka kidogo ikiwa yapo kwamba Henry Ford alikuwa ni mmoja kati ya watu waliokuwa wajuzi zaidi katika dunia ya biashara na viwanda. Suala la utajiri wake halihitaji mjadala. Chunguza marafiki wa karibu wa Bwana Ford ambao baadhi yao tayari wamekwishatajwa na utakuwa tayari kuelewa kanuni ifuatayo: Watu huchukua asili na tabia na NGUVU YA MAWAZO ya wale ambao wanashirikiana nao katika roho ya upole na masikilizano.
Henry Ford aliushinda
umasikini, kutokuwa na elimu na ujinga kwa kushirikiana mwenyewe na watu wenye
akili nyingi ambao mitetemo yao ya fikra aliivyonza katika akili yake mwenyewe.
Kupitia ushirikiano wake na Edison, Burbank, Burroughs na Firestone, Bwana Ford
aliongeza kwenye nguvu ya ubongo wake mwenyewe jumla ya akili, uzoefu, maarifa
na nguvu za kiroho za watu hawa wanne. Zaidi alijipatia na kutumia kanuni ya ushirikiano kupitia njia
zilizoelezwa katika kitabu hiki.
Kanuni hii ni kwa
ajili yako!
Raisi Franklin
Roosevelt alileta Washington watu wenye
akili zaidi nchini kuunda kundi la kushauriana aliloliita “Akili za kutegemewa”(Brain
Trust) Wakati na baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia, makundi ya kushauriana yaliyojulikana
kama “Think tank” mara kwa mara yaliitwa na na viongozi wa serikali na viwanda
kusaidia kukabiliana na matatizo magumu.
Tayari tumemtaja
Mahatma Gandhi. Pengine wengi wa wale ambao wamewahi kumsikia Gandhi humtizama
tu kama mtu mdogo mwenye tabia isiyokuwa ya kawaida aliyezunguka bila mavazi
rasmi na kusababisha usumbufu kwa serikali ya Uingereza.
Ukweli Gandhi hakuwa
mtu mwenye tabia za ajabu bali alikuwa
mtu mwenye nguvu zaidi katika zama zake(inakisiwa hivyo kutokana na idadi
ya wafuasi wake na imani yao kwa kiongozi wao). Zaidi alikuwa bila shaka mtu
mwenye nguvu zaidi aliyewahi kuishi. Nguvu zake zilikuwa ni za kimyakimya
lakini zilikuwa ni za ukweli.
Hebu tujifunze njia
aliyotumia kupata nguvu zake kubwa.
Inawezekana ikaelezwa kwa maneno machache. Aliingia madarakani kupitia
kuwashawishi watu zaidi ya milioni 200 kuungana kwa akili na mwili katika roho
ya masikilizano kwa ajili ya lengo kamili.
Kwa kifupi Gandhi
alikamilisha maajabu, ni maajabu kwa
sababu watu milioni 200 wanaweza wakashawishiwa – siyo kulazimishwa kuungana
katika roho ya masikilizano, katika muda usiokuwa na mipaka. Ikiwa kama una
shaka kama haya ni maajabu, jaribu kushawishi watu wowote wale wawili kushirikiana katika roho ya masikilizano katika kipindi
cha muda wowote ule. Kila mtu anayeendesha biashara anafahamu ni jambo gumu
kiasi gani kuwafanya wafanyakazi wafanye kazi pamoja hata katika roho
inayofanana na masikilizano kwa mbali.
Orodha ya vyanzo
vikuu ambavyo kutokana navyo nguvu inaweza kupatikana ni kama ulivyoona,
huongozwa na nguvu kuu. Watu wawili
au zaidi wanaposhirikiana katika roho ya masikilizano
na kufanya kazi kuelekea lengo kamili,
wanajiweka wenyewe katika nafasi, kupitia huo ushirikiano, kufyonza nguvu moja
kwa moja kutoka ghala kubwa la nguvu kuu kuliko zote. Hiki ni chanzo kikubwa
kuliko vyote cha nguvu. Ni chanzo ambacho ndio wale walio na akili nyingi
hugeukia. Ni chanzo ambacho kila kiongozi mkubwa hugeukia(iwe anatambua ukweli
huo au hatambui)
Vyanzo vingine viwili
vikubwa ambavyo maarifa yanayohitajika
kwa ajili ya ukusanyaji wa nguvu yanaweza kupatikana haviwezi vikategemewa
zaidi kuliko milango yetu mitano ya fahamu. Milango ya fahamu siyo mara zote inaweza
ikategemewa. Nguvu kuu kuliko zote huwa haikosei.
Itaendelea tena wiki ijayo.
0 Response to "Njia aliyotumia kiongozi mwenye nguvu zaidi kuwahi kuishi duniani kuunganisha watu wake"
Post a Comment