Soma, fikiri na
tafakari kadiri utakavyokuwa ukisoma. Mara moja somo zima litajifunua na
utaliaona kwa mapana. Sasa utaona undani wa sura mojamoja.
Pesa zina aibu na ni
zenye hila, ni lazima zibembelezwe na kupatikana kwa njia ambazo siyo tofauti
na zile zinazotumika na mpenzi aliyedhamiria kumtafuta mwenza. Na kwa kadiri
vinavyofanana, nguvu inayotumika katika kubembeleza(kutongoza) pesa haina
tofauti kubwa na ile inayotumika katika kumtongoza mpenzi. Nguvu hiyo inapotumika vizuri katika kutafuta pesa, ni
lazima ichanganywe na Imani. Ni lazima ichanganywe na Shauku.
Ni lazima ichanganywe na Msimamo. Ni lazima itumiwe katika
mpango, na mpango huo ni lazima uwekwe kwenye vitendo.
Pesa zinapokuja kwa
kiasi kikubwa zinazojulikana kama ‘Pesa nyingi’ hutiririka kwa yule
anayezikusanya kwa urahisi kama vile maji yatiririkavyo chini ya mlima. Upo
mfereji mkubwa wa nguvu isiyoonekana ambao unaweza kulinganishwa na mto,
isipokuwa kwamba unatiririka kuelekea pande mbili. Upande mmoja hubeba wale
wote wanaoingia katika upande huo wa mfereji kwenda mbele na juu kuelekea utajiri na upande mwingine hutiririka
upande mkabala ukibeba wale wote walio na bahati mbaya kuingia humo(na hawawezi
kujinasua wenyewe kutoka humo) kuelekea chini katika taabu na umasikini.
Kila mtu
aliyejikusanyia utajiri mkubwa anatambua uwepo wa mfereji huu wa maisha. Ndani
una mchakato wa mtu kufikiri. Mihemko
chanya ya fikra hutengeneza upande wa mfereji ule unaompeleka mtu kwenye
utajiri. Mihemko hasi hutengeneza upande ule unaompeleka mtu chini kwenye
umasikini.
Hili hubeba wazo
lenye umuhimu mkubwa kwa mtu anayefuatilia kitabu hiki kwa lengo la kujipatia
utajiri. Ikiwa kama upo katika upande wa mfereji wa nguvu unaolekea kwenye
umasikini, hii inaweza kuwa kama makasia ambayo unaweza ukaitumia kujisogeza
mbele mwenyewe kuingia ndani upande mwingine wa mfereji. Inaweza kukusaidia tu
ikiwa utaiweka katika matumizi na kuitumia. Kuisoma tu peke yake na kujadili
aidha kwa njia moja au nyingine haitakunufaisha kwa njia yeyote ile.
Baadhi ya watu
hupitia uzoefu wa kupokezana kati ya upande chanya na upande hasi wa mfereji,
wakati mmoja kuwa katika upande chanya na wakati mwingine upande hasi. Anguko
kubwa la soko la hisa Marekani(The wall street crash ’29) lilifyagia mamilioni
ya watu kutoka upande chanya kwenda upande hasi wa mfereji. Mamilioni hao
walipambana –baadhi yao katika hali ya kukata tamaa na woga-kurudi tena katika
upande chanya wa mfereji. Kitabu hiki kiliandikwa mahsusi kwa ajili ya hao
mamilioni.
Umasikini na utajiri
mara nyingi hubadilisha nafasi. Umasikini unaweza na kwa ujumla unaweza kwa
hiyari kuchukua nafasi ya utajiri. Utajiri unapochukua nafasi ya umasikini,
mabadiliko kwa kawaida huletwa kupitia mipango iliyopangwa vizuri na
kutekelezwa kwa uangalifu. Umasikini hauhitaji mipango. Hauhitaji mtu kuuongoza
kwasababu ni shupavu na katili. Utajiri ni wenye aibu na woga. Ni lazima
‘uuvute’
Mtu yeyote anaweza akatamani
utajiri, na watu wengi hufanya hivyo, lakini ni wachache tu wanafahamu kwamba
mpango kamili pamoja na Shauku kali kwa ajili ya kupata
utajiri ndiyo njia pekee za uhakika za kuupata.
...............................................................
Tumefika mwisho wa Sura hii ya 10 wiki ijayo tutaanza Sura mpya ya 11, "MAAJABU YA KUBADILI FIKRA ZA KIMAPENZI"
Usikose Semina ya kuandika mpango wa biashara ya mgahawa wa chakula siku ya Jumamosi tarehe 3 Novemba 2018 itakayofanyika kupitia watsap, kujiunga lipia kiingilio sh. elfu 10 kupitia namba za simu, 0712202244 au 0765553030.
0 Response to "Utajiri ni wenye aibu na woga, umasikini ni shupavu katili na hauhitaji mipango"
Post a Comment