WATU WALIOFANIKIWA KIFEDHA WAMEWEZA KUWASHINDA MAADUI HAWA 5 WALIOJIFICHA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WATU WALIOFANIKIWA KIFEDHA WAMEWEZA KUWASHINDA MAADUI HAWA 5 WALIOJIFICHA

Elon Musk na Moo
Masuala ya pesa wakati mwingine ni tata sana na kuna mambo mengi mno ya kujifunza kuhusiana na pesa zaidi ya kujua tu kutunza vitabu vya fedha na kumbukumbu. Kwa bahati njema pia kuna ushauri mwingi kuhusiana na pesa kutoka sehemu nyingi mbalimbali kuanzia kwa wataalamu wa mambo ya fedha, vitabu, majarida, mitandaoni na hata kutoka kwa mamentor(wale tunaoiga mifano yao). 

Leo hii nimeleta somo hili linalohusu matatizo makubwa matano (5) ya kitabia ambayo asilimia kubwa ya watu hasa wale ambao hawajafikia ngazi(levo) kubwa za mafanikio  wanayo lakini wala hawana habari kama wanayo na yanawazuia kupiga hatua za mafanikio kuelekea uhuru wao kamili wa kifedha. 
Kuzifahamu tabia hizo na jinsi ya kubadilika inaweza hatimaye kukuwezesha wewe kufanikiwa kifedha na kubadilisha kabisa namna unavyofikiria kuhusiana na fedha na jinsi utakavyochagua kuingiza pesa, kutumia pesa, na kuweka akiba pesa zako.

Matatizo hayo 5 ya kitabia ni haya hapa chini;


1.Lugha tunayotumia inaweza ikawa ni tatizo linalotuvuta nyuma kila siku tusiweze kufanikiwa.
Kwa mfano unapozungumzia kuweka akiba ukatumia wakati uliopo sasa hata ikiwa unamaanisha wakati ujao huwa inasaidia zaidi kiutekelezaji. Sema “naweka akiba kesho” badala ya “Nitaweka akiba kesho”. Wakati ujao unapoonekana kuwa mbali mno kutoka wakati uliopo sasa hupunguza ule morali wa kuweka akiba. Kitendo cha kuweka akiba ukisha sema “Nita..” hakina maana tena kwani ule muda ujao nao unategemea akiba iliyowekwa muda uliopo sasa. Kwahiyo akiba haiwezekani kuwekwa muda ujao bali huwekwa muda huu uliopo sasa.
Binadamu tuna nafsi mbili, nafsi ya kwanza ni nafsi iliyopo(wakati huu sasa) na nafsi ya pili ni nafsi ijayo(wakati ujao). Nafsi iliyopo huwa haipendi kabisa kuweka akiba, inapenda tu kutumia sasa, wakati nafsi ijayo  yenyewe huwa inategemea nafsi iliyopo kuiwekea akiba. Kwahiyo tunapaswa kuanza kuijali nafsi ijayo kwa kuiwekea akiba jambo litakalotuletea mafanikio makubwa kifedha siku za baadae.

2.Fedha haiwezi kununua furaha, na Heri ngamia kupenye katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia peponi.
Maneno haya japo yana kaharufu ka imani wakati mwingine huchangia sana kumfanya mtu asione umuhimu wa ‘kufight’ ili aweze kujinasua kiuchumi. Tunahisi kama vile kupata pesa nyingi ni hatia na tunaishia tu kuridhika na vijisenti vya mboga, likiibuka tatizo kubwa tunaanza kuhaha huku na kule wakati huo watu wakitucheka na kutuita kila majina, “..ooo..yule mzembe bwana!: “mvivu” “shauri lake, mwache ajibebe mwenyewe?” nk.
Dhana hizi kwa kiasi kikubwa siyo sahihi kabisa na ikiwa unafikiria kama ni sahihi kwamba pesa haina uwezo wa kumletea mtu furaha, basi jua yakwamba wewe pesa unazitumia vibaya. Mara nyingi pesa hutufanya watu kuwa wachoyo na wabinafsi. Sababu kubwa pesa hazitupi furaha ni kwamba tunazitumia katika mambo ambayo siyo sahihi kabisa kwetu.
Kwa mfano utafiti mmoja uliowahi kufanyika huko Ulaya, lilichunguzwa kundi moja la watu waliokuwa wakitumia fedha zao wenyewe bila kumsaidia wala kumpa mtu mwingine yeyote yule, halafu tena kundi jingine la watu waliokuwa wakitumia fedha zao lakini pia wakitoa misaada kwa jamii na watu wenye uhitaji. Kisha wataalamu hao walipima viwango vya furaha vya watu katika makundi yote mawili na kushangaa kukuta kwamba, kundi lililokuwa likitoa misaada kwa jamii si tu waliwanufaisha wanajamii wengine bali pia walipata manufaa makubwa wao wenyewe na katika kazi zao kwa ujumla.

3.Hatuwafunzi watoto wetu roho ya kuwa matajiri(Ujasiriamali)
Tumekuwa tukiwadanganya watoto wetu vitu ambavyo kiuhalisia wanakuja kukuta ni tofauti ukubwani. Tunapaswa kuwafunza ujasiriamali na wala siyo kukazania kuwafunza waje washike taaluma mbalimbali. Nielewe vizuri hapo, sijasema watoto wasichague fani wanazopenda wajikite kwenye ujasiriamali hapana, bali ikiwa mtoto wako unataka aje awe mwalimu, mwanasheria au daktari mzuri basi hakikisha atakuwa mwalimi au mwanasheria mjasiriamali na siyo tu mwalimu au mwanasheria ambaye akija kustaafu anabakia na maisha yaleyale aliyokuwa akiishi babu/bibi yake na......................................... .....................................................................,..............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................
Somo hili zima litatolewa leo usiku  saa 3 Tarehe  2/6/2023 katika Mastermind group la Michanganuo-online. Unapata na masomo mengine yote yaliyopita tangu group lianze, kupata vitu vyote hivi jiunge na group hili kwa kulipa ada sh. elfu 10 tu ambayo ni ya mwaka mzima

Masomo ni kila siku saa 3 - saa 4  na tunakuwa na semina pia mara kwa mara za jinsi ya kuandika michanganuo ya Biashara zenye fursa kubwa ya kutengeneza faida  haraka.

Ukilipa nakutumia pia OFFA ya e-books na Michanganuo jumla vitu 12 muda huohuo.

Kujiunga lipa kiingilio chako sh. 10,000/= kupitia namba zetu, 0765553030  au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo. Ukifuatia na ujumbe wa, "NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO & OFFA YA VITU 12"

Ikiwa hutumii wasap unaweza kututumia anuani yako ya E-mail na kila kitu tukakutumia kwa email. 


NA HII HAPA NDIYO OFFA YA VITU 12 ;

 

                 1.      COURSE/SEMINA: (compiled complete course) ya Jinsi ya kuandika Mchanganuo wa biashara –(Ukishindwa kuandika mchanganuo wako mwenyewe utarudishiwa pesa zako) - kwa kiswahili

                 2.       KITABUMichanganuo ya Biashara na Ujasiriamali chenye course zote muhimu za BIASHARA, jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara na sample za michanganuo mbalimbali 10 iliyokamilika kila kitu. – kwa kiswahili

                 3.      KITABU: Mifereji 7 ya Pesa na Siri Matajiri wasiyopenda kuitoa -kiswahili

                 4.      KITABU: Siri za upishi wa chapati laini-UPENDO CAFE pamoja na Mchanganuo wake kamili.-kwa kiswahili

                 5.       KITABUNjia rahisi ya kuandika mpango wa biashara-dakika 30 - kwa kiswahili

                 6.       KITABU: HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ni maarufu sana duniani na ndio hutumika vyuo vikuu vingi.-kwa kiingereza

                 7.       MCHANGANUO: Kuku wa nyama -Tumaini Broilers - kwa kiswahili

                 8.      MCHANGANUO: Kuku wa nyama –kwa kiingereza

                 9.      MCHANGANUO: Ufyatuaji tofali za saruji- kwa kiswahili

              10.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa Kiswahili

              11.    MCHANGANUO: Mgahawa wa chakula-Jane Restaurant –kwa kiingereza

              12.    MCHANGANUO: Kiwanda cha usagishaji Dona (Usado millingkwa Kiswahili

              13.    Kuunganishwa Group la masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo mwaka mzima ukitaka. (Mentorship group) (Ni hiyari yako lakini, usipotaka hatukuunganishi)

 

Karibu tukutane darasani leo usiku saa 3 tarehe 2/06/2023

Kwa vitabu, michanganuo na semina mbalimbali tembelea duka letu la vitabu SMARTBOOKSTZ

 

Somo hili limeandaliwa na:

Peter Augustino Tarimo

Mtaalamu wa Michanganuo ya biashara aina zote

Phone/Watsap: 0765553030 au 0712202244



SOMA NA HIZI HAPA PIA;

1. Tabia 9 zitakazobadilisha maisha yako kifedha

2. Mwaka huu ishi kama Tai usiishi tena kama kunguru

3. Je, ipo kanuni ya mafanikio ya kifedha?

4. Biashara ya mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado


0 Response to "WATU WALIOFANIKIWA KIFEDHA WAMEWEZA KUWASHINDA MAADUI HAWA 5 WALIOJIFICHA"

Post a Comment