JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA YA MGAHAWA WA CHAKULA HATUA KWA HATUA (JANE RESTAURANT): SEMINA TAYARI IMEANZA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA YA MGAHAWA WA CHAKULA HATUA KWA HATUA (JANE RESTAURANT): SEMINA TAYARI IMEANZA


Kabla ya kesho na keshokutwa hatujakwenda kuandika mpango wa biashara ya mgahawa, JANE RESTAURAN katika lugha zote 2, kiingereza na Kiswahili, leo hii hebu tuone kwanza kwa ufupi umuhimu wa kuandaa mpango wa biashara au mchanganuo kabla hujaifungua rasmi biashara yako ya mgahawa wa chakula.

Pia tutakwenda kuona ni vitu gani muhimu mtu utakavyohitaji ili kuweza kuandika mpango wa biashara yako ya mgahawa.


Kesho na keshokutwa tutakwenda kuona mchanganuo wenyewe halisi, hesabu zake, chati na majedwali mbalimbali yanayotakiwa kuwepo.

KARIBU SANA!

(UMUHIMU WA MPANGO WA BIASHARA)
Mpango wa biashara yako ya mgahawa ni ramani itakayokuongoza katika safari yako ijayo kibiashara na ni hatua gani uchukue kufika huko. Haukupi tu muongozo bali pia unakutaka kuzingatia fursa na hatari zote zinazoweza kuja kujitokeza mbele ya safari katika mradi wako tarajiwa wa mgahawa.

Ni andiko linaloelezea namna mgahawa wako utakavyokuwa. Unaweza kuutumia katika kutafuta mtaji kwa ajili ya uendeshaji kutoka kwa wabia, wafadhili, benki au hata kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki. Kwa ujumla ili wazo lako la kuanzisha mgahawa liweze kugeuka kuwa kitu halisi unahitaji kuwa na mpango wa biashara ulioandikwa au hata ambao hujauandika mahali popote, upo kichwani tu.


Watu wengi wanaofungua migahawa bila kuandaa mpango wa biashara huamua kufanya vile ili kuhakikisha mambo yanaenda haraka haraka lakini kumbe hawafahamu kuwa wanaharakisha kuja kuanguka katika biashara ya mgahawa. Wapo pia wanaoandaa mipango ya biashara za migahawa yao kwa lengo tu la kupata mkopo(pesa) au ufadhili na wakishamaliza shughuli hiyo hawana tena habari nayo. Lakini wanasahau kitu muhimu sana,”kufikiri kwa kina(brainstorming)  wakati wa matayarisho ya mpango wa biashara za migahawa yao”.

Nia na shauku ya kufanikiwa, jengo zuri na chakula kizuri peke yake havitoshi, unahitaji pia mafunzo kwa wafanyakazi, taratibu za uendeshaji zinazoeleweka na mipangilio mizuri ya soko lako kabla hujafungua mgahawa wako. Vitu hivyo ni muhimu kushinda hata viti na meza nzuri, mandhari ya mgahawa ya kuvutia au majiko na oven za kisasa.


UANZIE WAPI UNAPOTAKA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA YAKO YA MGAHAWA?
Kama ilivyokuwa kwa biashara nyingine yeyote ile, unapotaka kuandika mpango wa biashara ya mgahawa kitu kikubwa zaidi cha kufanya mwanzoni kabisa kabla ya vitu vingine vyote ni..........

Huo ni utangulizi wa semina hii iliyoanza leo hii saa 4 asubuhi na itaendelea hadi siku ya Jumatatu.

Kujiunga wasiliana nasi kwa namba zifuatazo, 0712202244 au wasap 0765553030. 

0 Response to "JINSI YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA YA MGAHAWA WA CHAKULA HATUA KWA HATUA (JANE RESTAURANT): SEMINA TAYARI IMEANZA"

Post a Comment