Elimu ya fedha ni uwezo wa kuelewa jinsi fedha
zinavyofanya kazi, jinsi mtu anavyoweza kupata pesa, jinsi ya kusimamia na kutunza fedha, jinsi
ya kuwekeza fedha na jinsi ya kutumia fedha. Kila mtu anapaswa kufahamu kwa
undani elimu hii ya pesa namna pesa inavyofanya kazi na jinsi pesa inavyoweza
kumfanyia kazi hata ikiwa amelala usiku kwa njia ya kuiwekeza katika miradi
inayoweza kumzalishia faida mfano katika masoko ya hisa, masoko ya mitaji au
hata kwenye miradi na biashara nyingine kama za ardhi na majengo.
Ili kuielewa vizuri pesa na namna inavyofanya kazi ni vyema mtu akafahamu kwanza kanuni zile za msingi za fedha kama vile; Malengo ya kifedha, Bajeti, Uwekezaji, Mafao ya uzeeni, Mikataba na mifumo ya ajira.
SOMA: Kama fedha haijawahi kuwa rahisi kupatikana, kwanini uchezee pesa?
Tafiti mbalimbali zilizowahi kufanyika kuhusiana na
uelewa wa watu wa pesa zimeonyesha
kwamba watu wengi wakiwemo Wajasiriamali na Waajiriwa hawana elimu ya msingi ya fedha wala uelewa wa dhana
mbalimbali zinazohusiana na pesa hata zile za kawaida kabisa kama vile mikopo,
riba na uwekaji wa akiba, hii huwafanya wengi wao kuogopa mno kukopa kwa ajili
ya kuwekeza katika miradi jambo linalowafanya wengi kufa masikini.
Aidha kwa upande wa watumiaji wa bidhaa mbalimbali za
kifedha kama vile mikopo na mifuko ya mbalimbali ya hifadhi ya kijamii huwa hawajishughulishi
na kutafuta taarifa za kifedha kabla hawajafanya maamuzi yao mbalimbali ya
kifedha, huishia kukosa uwezo wa kuchagua na kusimamia mikopo au mafao yao
kikamilifu, kutokuweza kupanga biashara zao au kushindwa kupanga maisha yao
baada ya kustaafu. Wastaafu wengi hukosa taarifa kuhusiana na akiba na
uwekezaji kwa ajili ya kustaafu, wanashindwa kupanga kabla na kuamua kuchukua hatari za kifedha pasipo kujua.
SOMA: Je, kukopa ili ukalipe deni la zamani kunawezaje kuboresha mzunguko wa fedha kwenye biashara yako?
SOMA: Je, kukopa ili ukalipe deni la zamani kunawezaje kuboresha mzunguko wa fedha kwenye biashara yako?
Tatizo la madeni ni kubwa kwa watu wengi kwasababu ya
kutokuwa na elimu ya fedha na kundi linalokabiliwa na tatizo hili ni vijana
zaidi kuliko wale walio ana umri wa makamo au wazee. Elimu ya kutunza fedha inaweza
kuwanufaisha makundi ya watu wa rika zote na vipato. Kwa vijana ambao ndio
kwanza wanaanza maisha inaweza kuwapa uwezo wa kubajeti na kujiwekea akiba itakayowawezesha
kudhibiti matumizi yao na madeni.
Maarifa ya msingi ya fedha pia yanaweza kuzisaidia familia kuwa na
nidhamu ya fedha itakayowawezesha kujiwekea akiba kwa ajili ya elimu ya watoto
wao au maendeleo mengine ya familia. Inaweza kuwasaidia wafanyakazi wazee
kuhakikisha kwamba wanakuwa na akiba ya kutosha kwa ajili ya kustaafu raha
mustarehe pasipo kuhofia kikokotoo hatimaye kuchanganyikiwa bure kunakoweza
kuwapa magonjwa ya moyo na kiharusi kwa kuwapa mbinu na taarifa
zitakazowawezesha kuchagua uwekezaji unaofaa katika pensheni na mipango mingine
ya akiba.
SOMA: Njia 6 za kuondoa woga na stress za fedha katika maisha yako.
SOMA: Njia 6 za kuondoa woga na stress za fedha katika maisha yako.
Elimu ya fedha inaweza ikawasaidia watu wa kipato cha
chini kufanya kila linalowezekana katika kujiwekea akiba itakayowasaidia
kuepukana na mikopo yenye riba kubwa inayotolewa na taasisi au watu binafsi nje
ya mifumo rasmi ya kibenki.
Kiwango cha mtu cha Elimu yake kifedha huathiri kwa kiasi
kikubwa ubora wa maisha yake. Huathiri uwezo wake wa kujipatia mahitaji yake lakini
na ya familia yake pia, mwelekeo wake kwenye pesa na uwekezaji pamoja na
mchango wake kwa ujumla kwenye jamii nzima inayomzunguka, hivyo kuipata elimu hiyo ni sawa na hazina itakayodumu daima na haiwezi kuharibiwa kirahisi.
SOMA: Download(pakua) kitabu hiki cha elimu ya pesa na mafanikio bure mtandaoni.
SOMA: Download(pakua) kitabu hiki cha elimu ya pesa na mafanikio bure mtandaoni.
Uelewa wa pesa humfanya mtu afahamu ni kitu gani
kinachohitajika kufanyika ili kufikia maisha endelevu yenye maadili,
uwajibikaji na uhuru wa kifedha. Humsaidia mjasiriamali pia kutumia fedha za
watu wengine kama nyenzo ya biashara ya kutengeneza MAUZO na FAIDA.
2019
Njoo Tuhamishe Milima!
Siri hii sikupenda kabisa kuitoa kiholela kwa kila mtu
kwani nahofia sana washindani wangu kibiashara kuikopi na kuitumia, makundi
mengine ya wasap na hata yale ya facebook. Si unajua tena huku mitandaoni,
huwezi kuwa na hatimiliki ya mbinu uliyobuni kirahisi inayotekelezeka
kivitendo. Siri hiyo ni mfumo tunaoutumia katika uendeshaji wa GROUP letu la
masomo ya kila siku, mijadala na Seminars za mara kwa mara, MICHANGANUO-ONLINE.
SOMA: Semina 12 za kuandika michanganuo ya biashara za kipekee zenye fursa kubwa ya kutengeneza faida.
SOMA: Semina 12 za kuandika michanganuo ya biashara za kipekee zenye fursa kubwa ya kutengeneza faida.
Tumeamua kutumia mtindo uliowahi kutumika na Mabilionea
wakubwa wengi duniani(MASTERMIND GROUP), ni vigumu kukuelezea jinsi mfumo huu
unavyofanya kazi kwa maneno matupu ukaelewa labda tu kama unajiunga ndiyo utaweza
kunielewa kikamilifu. Ni hivi, Kwanza hatuna kocha, kiranja wala mentor yeyote
ndani ya group letu, admini yupo tu kwa ajili ya kuwezesha (kufacilitate) wanaoingia na
wanaotoka au wanaotaka kubadilisha namba zao. Kila mtu ana nafasi sawa ya
kumuelimisha na kumshauri mwenzake.
Tunaishi kistaarabu kupita kiasi, hakuna matusi isipokuwa
utani na vichekesho havizuiwi, kazi kubwa ni moja tu, kujifunza elimu ya fedha,
uwekezaji, Business plans na ujasiriamali kwa ujumla. Tunashea vitu vingi vya
thamani ambavyo mtu peke yako ingelikugharimu muda mwingi na hata fedha
kuvipata, documents na hata vitabu mbalimbali vizuri. Wadau ni watu kutoka
tasnia mbalimbali wengine wamebobea katika fani zao na hukubali kushea mambo
bila uchoyo.
Maajabu haya ya kundi kushirikiana kwa kufuata kanuni
nilizozitaja na nyingine ambazo siwezi kuziweka wazi kwa sababu za kibiashara, ndizo zinazotufanya kuwa group la kipekee zaidi nchini Tanzania
linalooperate si tu kwenye wasap bali pia kupitia email kwani si kila mtu
hutumia wasap na wote hupata masomo yote na semina tunazofanya.
SOMA: Kwanini kundi la kushauriana(Master mind group) ni muhimu kwa kila anyetafuta mafanikio?
SOMA: Kwanini kundi la kushauriana(Master mind group) ni muhimu kwa kila anyetafuta mafanikio?
Kushirikiana kuna faida nyingi siyo katika group kama
hili tu, hebu tazama Mataifa makubwa mfano Marekani, Umoja wa Ulaya na hata
Urusi kabla ya kusambaratika(Soviet Union). Marekani kwa mfano jeuri yake yote
inatokana na muunganiko wa nchi zaidi ya 50(States). Tumeona Ulaya jinsi
Uingereza na kiburi chake inavyoanza kutaharuki hata kabla ya BREXIT yenyewe.
Unaikumbuka Usovieti? Superpower pekee iliyoweza kuitikisa Marekani ikashika
adabu, zilikuwa nchi 15. Hatujui pengine kama Putin anaweza akarudisha
Soviet nyingne kwa kuamua kuungana na Iran, Uchina na Baadhi ya mataifa mengine
ya Mashariki, hatujui, muda ndio utakaoamua.
SOMA: Mafanikio makubwa ya Henry Ford yalianza pale alipoanza ushirikiano na matajiri wengine.
SOMA: Mafanikio makubwa ya Henry Ford yalianza pale alipoanza ushirikiano na matajiri wengine.
Nimeeleza hayo yote ili kuonyesha jinsi ambavyo
ushirikiano ulivyokuwa na nguvu ya ajabu, kidole kimoja hakivunji chawa,
Mnapokuwa wengi mnaweza kufanya mambo makubwa yanayoweza yakalinganishwa na
mlima, hebu jaribu kufikiria jinsi mlima ulivyo, halafu uambiwe mlima huo
uuhamishe ukiwa peke yako, je utaweza? itakuchukua miaka mingapi? Lakini mkiwa wengi sina shaka utahama, tena ndani ya kipindi kifupi tu.
2019 NJOO JIUNGE NASI KATIKA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE NA KWA PAMOJA
TUTAHAMISHA MILIMA!
Ujumbe wangu wa mwisho kwako(ikiwa hujajiunga lakini)
katika mwaka huu wa 2018 nataka nikuambie hivi;
“Ukitaka
mahali sahihi zaidi utakapoweza kupata elimu ya pesa mtaani(nje ya mfumo rasmi
wa shule) kwa gharama rafiki zaidi kuliko sehemu nyingine yeyote usihangaike, bali njoo
Michanganuo-online, nakuhakikishia utapata kila kitu unachohitaji katika
kutengeneza maisha yako upya kifedha”
Kujiunga Lipa ada yako sh. Elfu 10 kupitia namba 0765553030 au 0712202244, jina ni Peter Augustino
Tarimo.
Baada ya malipo, tuma ujumbe wasap au sms usemao, “NIUNGANISHE
NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE”
Wasap: 0765553030
Ikiwa hutumii wasap hamna shida, tuma anuani yako ya
email tutakayokutumia masomo na semina zote pamoja na updates kila zikitokea.
0 Response to "ELIMU YA FEDHA NA UMUHIMU WAKE 2019 NJOO TUUNGANISHE NGUVU TUHAMISHE MILIMA!"
Post a Comment