HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA WENYE MAFANIKIO TELE, 2019 ISHI KAMA MBAYUWAYU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA WENYE MAFANIKIO TELE, 2019 ISHI KAMA MBAYUWAYU

Mbayuwayu, akili ya kuambiwa changanya na ya kwako

Habari mpendwa msomaji wa makala hii,
Ikiwa bado harufu ya Krismasi bado haijatoweka kwa wale wanaosherekea sikukuu hiyo, Mwaka mpya nao unanukia, zimebakia siku mbili tu! Mimi pamoja na timu yangu nzima kutoka Self Help Books Tanzania, Blogu ya jifunzeujasiriamali na Group la masomo (Master mind group) la Michanganuo-Online tunakutakia wewe pamoja na familia yako nzima, sikukuu njema, heri na baraka tele. Ni matumaini yetu kuwa unafurahia na kusherehekea sikukuu hizi kwa namna moja au nyingine.

Katika ujumbe wangu wa leo na pengine wa mwisho kwa mwaka huu, nisingependa nikuchoshe kwa maneno meengi sana ingawa katika makala zilizopita kwa mwezi huu niliahidi kukukumbusha mara kwa mara juu ya umuhimu wa kujiunga na Group la masomo na mijadala ya kila siku, masomo spesho 30 ya mwezi Desemba, pamoja na masomo mengine na semina za mwaka mzima wa 2018 yaliyotolewa kupitia wasap na email. Hata hivyo sikutimiza hili kwa kiasi kikubwa ingawa programu hiyo ilikuwa ikiendelea na inaendelea mpaka sasa hivi hadi pale itakapofika mwisho wake tarehe 30 mwezi huu.

SOMA: Salamu zangu 2018 kukutakia heri na mafanikio ya kweli.

Madhumuni hasa ya ujumbe wangu wa leo pamoja na kukutakia sikukuu njema za mwisho wa mwaka pia ni kukuelezea mipango na malengo yetu ya mwaka huu mpya unaoanza wa 2019, taarifa za mpango unaomalizika wa mwaka 2018 pamoja na ushauri mwingine wa hapa na pale tu.


Taarifa ya Kampeni yetu inayomalizika ya mwaka 2018

Mwaka unaomalizika wa 2018 Kaulimbiu yetu kuu ilikuwa inasema hivi; “MZUNGUKO MZURI WA FEDHA NDIYO NJIA BORA ZAIDI YA KUTIMIZA MALENGO YAKO MWAKA 2018”. Nakumbuka tuliweka malengo kadhaa ya kutimiza kwa upande wa blogu ya jifunzeujasiriamali, Group la Michanganuo-Online pamoja na masomo tunayotuma kwa njia ya email. Kusema ule ukweli asilimia kubwa ya malengo hayo tuliyatimiza kwa mfano masomo ya kila siku ya fedha ndani ya group tulijitahidi kwa asilimia zaidi ya 90% kuyatimiza.

SOMA: Ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena(Make your self Great again)

Lengo jingine lilikuwa ni kuandika hatua kwa hatua Michanganuo 12 ya biashara bunifu zenye uwezo mkubwa wa kulipa haraka na tulitimiza lengo hilo kwa zaidi ya asilimia 50%. Lengo la tatu la kutoa masomo maalumu 30  ya fedha mwezi huu wa Desemba mpaka leo hii tumetimiza kwa karibu asilimia 60% na kwa Uwezo wa Mwenyezi Mungu ifikapo tarehe 30 tunaamini tutakuwa tumelitimiza kwa asilimia 100%

Kitu ninachotaka kukueleza hapa ni kwamba, kutimiza malengo ya mwaka  unayojiwekea kwa asilimia 100% ni jambo linalowezekana kabisa lakini ni watu wachache utakuta wanaweza kutimiza hilo. Lakini hili lisikukatishe tamaa ikiwa na wewe ni mmoja wa wale ambao hawakuweza kutimiza malengo yao kwa asilimia 100% kama walivyokuwa wamejipangia mwaka ulipokuwa ukianza.

SOMA: Ni robo ya mwaka sasa, bado upo kwenye mstari wa malengo uliyojiwekea Januari? 

Nakuambia hivi kwani haupo peke yako, tupo wengi. Nchi, Taasisi kubwa kubwa na hata Umoja wa Mataifa wenyewe(UN) kuna malengo hawawezi kuyatimiza kila mwaka ingawa huyapanga vizuri tu wanapokuwa wakiuanza mwaka sembuse ije kuwa wewe na mimi?

Kikubwa na muhimu cha kufanya ni kuangalia ni wapi ulishindwa na ni sababu zipi zilipelekea wewe kushindwa. 2019 hii hapa inakuja, jipange tena upya kama bado unaishi. Huwezi kujinyonga kisa eti hukuweza kutimiza malengo yako yote wala huwezi kula sumu bali unachopaswa kukifanya ni kujikagua na kuangalia ni wapi kuna MPENYO mwingine mpya wa kupita na kujitahidi kujipinda kadiri ya uwezo wako wote ili hatimaye uweze kupenya.

Mbona tundu hata liwe dogo vipi panya hupenye tu na kutokeza upande wa pili anapokabiliwa na hatari?  Uchukulie umasikini kama HATARI kubwa kwenye maisha yako. Wakati ukiweka tena upya malengo yako au kuboresha yale uliyoshindwa kuyatimiza mwaka uliopita usisahau kuzingatia kanuni hii isemayo, jinsi ya kupanga malengo mazuri ya biashara au maisha yanayotimizika kwa ufanisi.


2019 ishi kama mbayuwayu, huu ndio ushauri wangu mkubwa kwako leo.

Ushauri wangu kwako kwa mwaka huu wa 2019 ni kwamba pamoja na kusikiliza ushauri toka kwa watu mbalimbali nikiwemo hata na mimi mwenyewe, hebu kuwa kama ndege Mbayuwayu, usikubali tena kuishi maisha ya watu wengine wala usifanye vitu ili kuwafurahisha watu bali simama wewe kama wewe mwenyewe. Sijasema usishirikiane na watu la hasha hebu ninukuu vizuri. Watu wengi watajaribu kujifanya wanakuonea huruma na kukupa ushauri wa hapa na pale, kama vile, ..oo..unajua…unashindwa kufanikiwa malengo yako kwa sababu ya hili, lile na blaa..blaa…kibao, laini mustakabali wa maisha  yako upo mikononi mwako wewe mwenyewe na wala siyo kwa mtu mwingine yeyote yule.

SOMA: Uamuzi mgumu na muhimu wa kuchukua ili biashara yako iendelee kukupa faida mwaka huu.

Ridhika na kufurahia kile unachoweza kupata wewe na watu wako wa karibu zaidi(familia yako) hata kama ikiwa ni kidogo, achana na marafiki wanafiki na wa uwongo wanaojifanya marafiki wa karibu pale tu wanapokuwa wanahitaji kitu fulani kutoka kwako lakini ukifulia wanakukwepa utadhani una ukoma vile. Familia yako ni nadra sana kukutupa mpaka mwisho. Ukilazimika kuwa karibu na mtu/watu ambao siyo wanafamilia siyo vibaya pia kwani kuna marafiki, wanajumuia mbalimbali nk. lakini hakikisha unachukua tahadhari zote ikiwa ni pamoja na hiyo ya kuishi kama mbayuwayu.

SOMA: Punde kabla hujakata tamaa ya maisha fanya vitu hivi 4 utabadili nia.

Falsafa  maarufu sana ya ishi kama Mbayuwayu au “AKILI YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YA KWAKO” inamhusu ndege aitwae Mbayuwayu na umaarufu wake ulizidi pale Rais msaafu wa awamu ya nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete alipoitoa akihutubia, inawahusu ndege wawili Gong’ota na Mbayuwayu, Gongota baada ya kumhadaa Mbayuwayu kuwa mdomo wake ungelikuwa imara na mgumu kama wa kwake ikiwa angejirusha juu angani kisha kudondokea juu ya jiwe akitanguliza mdomo wake, yeye badala yake alifanya kinyume chake kwani angelifanya kama alivyoshauriwa ingelikuwa ndio mwisho wa maisha yake.  


Mipango na malengo yetu makubwa 3 kwa mwaka 2019

Baada ya ushauri huo kidogo sasa nikupe rasmi mipango na malengo yetu makubwa kwa mwaka 2019 katika blogu ya jifunzeujasiriamali, Group la Michanganuo-online na katika masomo kwa email.

1.  Kwanza tutahakikisha tunamalizia baadhi ya malengo ambayo hatukuweza kuyakamilisha mwaka unaoisha wa 2018 na tuliahidi kuyafanya.

2.  Kaulimbiu yetu rasmi ya mwaka 2019 inaitwa; “KIWANDA NI UTAJIRI, TUACHE MANENO TUANZISHE VIWANDA KWA VITENDO”. Shughuli zetu nyingi zitalenga kwenye kauli mbiu hii. Tutaandika hatua kwa hatua michanganuo kwa ajili ya kuanzisha viwanda 4 vya uhakika ambavyo kila mtu ataweza kuanzisha cha kwake, sipendi kuweka malengo ya viwanda vingi, hivi 4 vitakuwa kama mfano na mtu ataweza kufuatisha mifano hiyo kuanzisha idadi na aina yeyote ya viwanda atakavyo.

3.  Tutafanya kazi kama timu zaidi kupitia kundi letu la kushauriana(MASTERMIND GROUP) la Michanganuo-online lakini pia hatutawaacha nyuma wale waliojiunga nasi kwa njia ya email kwani tunatarajiwa kuwa wengi wao wanatarajia kujiunga nasi siku moja kwenye group letu.

Ada kidogo ya kujiunga na Group shilingi elfu 10 au 20 endapo itapanda lengo lake ni ili kuweza kuendesha shughuli hizi tu na si faida, faida kubwa tunategemea zaidi maarifa tunayoshea kama group, watu wengi hawajui faida kubwa iliyopo katika ushirika wa namna hii, ni mpaka wamejiunga ndipo hutambua. Matajiri wengi wakubwa duniani wakiwemo kina Henry Ford, Andrew Carnegie,  John Rockefeller, Bill Gates, Steve Jobs na wengineo wengi ukisoma shuhuda zao katika vitabu mbalimbali utaelewa ni kitu gani ninachomaanisha ninapozungumzia juu ya MASTERMIND GROUPS.

Kwenye makundi ya namna hii tofauti na makundi mengine yaliyozoeleka hakuna Kocha wala Mentor, kila mtu ni mwalimu wa mwingine, mnatengeneza ushirikiano na uhusiano wa watu mnaoshea mambo yanayofanana huku mkishauriana kwa faida ya kila mmoja na kama ujuavyo palipo na wengi kamwe hapaharibiki kitu.

Wakati nikiandika malengo hayo matatu, mmoja wa wanagrop la Michanganuo-online alitoa wazo moja ambalo nimeona si vibaya likawa miongoni mwa malengo yetu ya mwaka huu hata kama hatutaweza kulikamilisha ndani ya mwaka. Wazo hilo lililoungwa mkono  na wadau wengine wengi ni la Group kwenda mbali zaidi kwa kuanzisha mradi wa pamoja. Kwanza tutakutana wote na kufahamiana zaidi kisha kuona ni mradi gani tutakaoweza kuanzisha kwa ushirikiano. Wazo hilo hata mimi nimeona ni zuri na linaweza likatekelezeka.

Kila mtu huwa ana malengo yake binafsi, binafsi mimi kwa mwaka huu pia ninayo malengo yangu ingawa si muhimu kuyataja hapa lakini walao nitataja moja nalo ni kuanzisha viwanda 2 vidogo, kimoja cha uzalishaji bidhaa zinazohusiana na kilimo au ufugaji na cha pili ni kiwanda cha kuzalisha bidhaa(mashine) itakayowarahisishia kazi kina mama majumbani.

SOMA: Tayari malengo yako kiuchumi umeshayaandika mahali?

Siwezi kuitaja ni mashine ya nini kwa sasa lakini nategemea nitashea uzoefu wangu katika vitu hivyo 2 kwenye group na Wanamastermind wenzangu pale Michanganuo-online.

Viwanda vyote 2 naamini soko lake ni la uhakika, si unajua tena kila mtu anakula, na vipi kuhusu kinamama wa majumbani…, ndio kila kitu kwani ukifanikiwa kuwavutia na bidhaa yako yeyote huwezi kufa njaa, kazi zao ndiyo injini ya uchumi wa familia nyingi hasa zile za kipato cha chini na cha wastani ambao bila shaka ndio walio wengi katika jamii yetu.

SOMA: Njia 10 za kuhamasika na kuendelea kubakia na hamasa hiyo kwa muda mrefu ujao.

Hebu niambie mpaka hapo kama lengo litatimia sijawini tu? Njoo kundini ujionee maajabu nitakayokwenda kufanya 2019 hii. Siwezi kukupa uhondo wote acha niishie hapa tu kwa leo kwani 2019 nimeazimia unaenda kuwa mwaka wangu wa viwanda, nimechoka kuwa msindikizaji wa Wachina.

Mwisho kabisa nakuomba usiache mwaka uishe hivihivi kabla hujathibitisha kazi tulizofanya mwaka mzima wa 2019 tukiwa kama kundi la kushauriana(MASTERMIND GROUP) la Michanganuo-online. Na njia pekee ya kuthibitisha ninayoyasema ni kwa wewe kujiunga na group hili sasa kwa kiingilio cha Tsh. Elfu 10 kabla ya siku ya tarehe 30 ambayo kutakuwa na mabadiliko ya bei.

Hii ni offa kwani unapata kila kitu kwa sh. Elfu 10 tu kuanzia masomo yote ya mwaka mzima, michanganuo ya biashara bunifu zinazolipa na semina za mwaka mzima pamoja na fursa ya kuwa Mwanamastermind wa kudumu.

Lipia ada yako sh. 10,000/= kupitia namba 0765553030  au 0712202244 na jina hutokea, Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe usemao, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE”. Mara moja nitakuunganisha na kukutumia kila kitu kupitia wasap au email yako.

SOMA: Je wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya 4 madogomadogo?

Ikiwa hutumii Wasap, usihofu kwani email inatosha, nitakutumia kila kitu kwa nia ya email na updates za masomo ya kila siku pia nitakuwa nakutumia kila siku.

Nikutakie kwa mara nyingine tena Mwaka mpya wenye amani na mafanikio yaliyojaa tele karibu kumwagika! Lakini chondechonde usije ukasahau kuishi kijanja kama,
MBAYUWAYU.

Peter A. Tarimo
self help books Tanzania

0 Response to "HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA WENYE MAFANIKIO TELE, 2019 ISHI KAMA MBAYUWAYU"

Post a Comment