Watu tuna masaa mengi mchana ambayo huwa hatuyatumii
kikamilifu inavyotakiwa. Kuna vitu vingi huwezi kuamini vinakula muda wetu
wakiwemo wezi maarufu 3 wa muda na kusababisha tusiweze kupata pesa kama vile
ambavyo tungependa tupate. Hebu fikiria kila siku unatamani kufungua biashara
au mradi wako wa pembeni ili uboreshe zaidi kipato chako badala ya kutegemea tu
mshahara au faida ya biashara yako kuu.
Unajitahidi uwe na kipato nje ya hicho lakini kila
unapojaribu kuanza unaishia njiani. Hupati matokeo mazuri na majukumu unayaona
yanaingiliana. Muda unaoutumia katika biashara yako hiyo ya pembeni unakuta
hautoshi na unalazimika kuingiliana na ule wa kazi yako ya msingi au biashara
mama.
Ili mtu kuwa na akili iliyohamasika muda wote na uweze
kutimiza majukumu yako kwa ufanisi wa kiwango cha hali ya juu, inategemea sana
ni jinsi gani unavyokamilisha ratiba zako . Usitegemee baada ya kutoka kazini
kwako utakuwa na hamasa ya kutosha ya kufanya kazi za kukuingizia kipato cha
ziada kama huko kazini umeacha viporo vya kazi zinazokusubiri uje uzikamilishe
siku ya pili au kuna kazi hukuzifanya kwa ufanisi na bosi wako amekasirika na
kukufokea.
Hata kwa yule anayefanya biashara yake binafsi kuna kiasi
kikubwa cha pesa anachokikosa kutokana na kutojipanga sawasawa kwenye eneo la
muda, vitu mbalimbali anavyofanya na vipaumbele vyake kwa ujumla. Ikiwa mtu wa namna hii atajipanga
vizuri na kuwaepuka matapeli wa muda anaweza kupata muda zaidi wa kutosha
akajenga jina la biashara yake na bila shaka yeyote kutengeneza pesa nyingi
zaidi ya vile alivyokuwa akipata zamani.
Lakini wezi hawa wa muda wako ni kina nani?
........................................................
Mpenzi msomaji wa makala hii, fuatana nami kwenye group la masomo ya kila siku la MICHANGANUO-ONLINE, hili ni somo la 5 leo katika mfululizo wa masomo 30 kwa mwezi huu wa 12
Karibu ulipie kiingilio chako sh. elfu 10 upate na offa ya masomo mengine yote toka mwezi Januari, semina, vitabu na michanganuo mbalimbali ya biashara bunifu zinazolipa. offa hii mwisho wake ni tarehe 30 Desemba 2018.
Namba za malipo ni, 0765553030 au 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo. Ukishalipia tuma ujumbe wa wasap au wa kawaida usemao, 'NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO'
Siyo lazima uwe unatumia wasap ndipo uweze kupokea masomo haya, tunatuma pia kwenye email kila kitu sawa na tunavyofanya katika wasap.
0 Response to "KAMATA, PELEKA JELA WEZI HAWA 3 WANAOKUIBIA MUDA WAKO USIPATE PESA NYINGI"
Post a Comment