*Kama mtafiti wa maswala mbalimbali ya kijamii, makala/Mjadala huu ulio na maudhui ya kidini nimeandika kwa lengo la kuhabarisha na wala siyo ushabiki, ikiwa kwa namna yeyote ile utakwazika na yaliyoandikwa humo basi natanguliza samahani halikuwa lengo langu kukwaza mtu yeyote.
Sikukuu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Yesu
Kristo mtu anayeaminika na waumini wa
dini ya Kikristo kuwa ndiye mwokozi wao imekuwa ikiadhimishwa kwa karne nyingi
lakini sikukuu hii historia yake inaaminika kuanzia karne ya 3 baada ya Yesu
mwenyewe kuishi hapa duniani na hakuna kumbukumbu yeyote rasmi katika kitabu
kitakatifu cha Biblia kwamba iliwahi kuadhimishwa na Wakristo wa mwanzo isipokuwa
tu Biblia inachotamka ni tukio lenyewe la kuzaliwa, haitaji siku, mwezi wala
tarehe ya tukio hilo.
SOMA: Nyimbo nzuri za Krismasi zinazopendwa zaidi na siri kubwa 2 zilizojificha ndani yake.
SOMA: Nyimbo nzuri za Krismasi zinazopendwa zaidi na siri kubwa 2 zilizojificha ndani yake.
Historia ya vikundi na Madhehebu ya Kikristo
duniani haiwezi kukamilika pasipo kutaja pande kuu tatu, Ukristo wa
Magharibi(Wakatoliki), Ukristo wa Mashariki(Waorthodox) na Waprotestant(Wale
wote waliopingana na matawi hayo makuu mawili). Baada ya Yesu kuondoka duniani
pamoja na Wanafunzi wake(Mitume 12) wale waliobakia kuuendeleza Ukristo kwa nyakati
tofauti walitofautiana kama ilivyokuwa kwa dini na imani nyinginezo zozote zile
duniani anapokuwa ameondoka yule aliyeanzisha.
Upande
wa wale wanaosherekea Krismasi.
Krismasi chimbuko lake ni katika Ukristo wa
Magharibi na Mashariki huko Ulaya na ndio maana utakuta siku hizi wote
Wakatoliki na Waorthodox wanaadhimisha Sikukuu ya Krismasi ingawa pia
wanatofautiana kidogo tarehe na mwezi, wakati Wakatoliki na baadhi ya Wakristo
wengine wa Magharibi wakiadhimisha Krismasi tarehe 25 Desemba Waorthodox wa
Mashariki wao huiadhimisha Mwezi January tarehe 7. Tofauti hii hutokana na
Magharibi kutumia kalenda ya Kigregori(Gregorian calendar) wakati Mashariki wao
hutumia kalenda ya Kijuliani (Julian calendar)
SOMA: Heri ya siku ya kuzaliwa mr. Peter Augustino Tarimo
SOMA: Heri ya siku ya kuzaliwa mr. Peter Augustino Tarimo
Sababu kubwa inayotolewa na makundi haya
yanayoadhimisha Krismasi pamoja na kwamba Biblia imekaa kimya juu ya sikukuu
hiyo ni kuwa, tukio hili wao hasa wanachozingatia zaidi ni maudhui au maana ya
tukio lenyewe lililotokea kweli na wala siyo siku wala tarehe yenyewe. Wanadai
hata kama biblia haitamki wazi Yesu Kristo alizaliwa siku gani lakini hiyo
haiwezi kufuta ukweli kwamba Yesu Kristo alizaliwa kweli huko Bethlehemu ya
Uyahudi. Suala la kukumbuka jambo mtu unaweza ukakumbu siku yeyote ile na wala
si lazima iwe ni tarehe ileile tukio lilipotokea. Wangeweza hata kukumbuka
katika tarehe nyingine yeyote ile au mwezi wala isingelikuwa tatizo.
Sasa
basi kwanini waadhimishe siku inayodaiwa kuwa ilikuwa ni sikukuu ya kipagani ya
kuzaliwa kwa Mungu jua?
Huko Ulaya hasa Ulaya ya Magharibi enzi
Ukristo unaingia huko watu walikuwa na dini zao za asili kama tu ilivyokuwa
huku Afrika Wakoloni walipoingia na ilikuwa vigumu sana kuwabadilisha watu
waamini Ukristo na moja ya mbinu zilizotumika ni pamoja na kubadilisha matukio
ya kipagani kuwa ya Kikristo.
Kuna ubaya gani ikiwa siku watu waliyokuwa
wakiamini Mungu wa uwongo badala yake ikafanywa kuwa siku ya kumuamini Mungu wa
kweli?. Hivi ndivyo ilivyokuwa watu badala ya kuendelea kuamini siku ya
kuzaliwa Mungu Jua wa uwongo wakafundishwa waamini kuzaliwa kwa Yesu Kristo
aliyetumwa na Mungu Kuwaokoa. Hivyo pamoja na dhamira hiyo nzuri lakini bado
watu hawakuweza kuacha moja kwa moja desturi walizokuwa nazo wakati wa hizo
sherehe za kipagani mfano kupeana zawadi, miti ya krismasi nk. ndio maana mpaka
sasa hivi desturi hizo zimeendelea kuwepo.
SOMA: Mji wa kale Ukristo ulipoanzia washambuliwa vikali.
SOMA: Mji wa kale Ukristo ulipoanzia washambuliwa vikali.
Kwa sababu hizo Wakristo wa madhehebu ya
Kikatoliki, Waorthodox na hata wengi wa madhehebu ya Kiprotestant mfano
Waanglikana, Walutheri, na makundi mbalimbali ya kilokole wameendelea kuona
hakuna sababu ya msingi ya kuipinga Krismasi ilimradi tu dhamira yake kuu ni
kukumbuka tukio kuu la Imani yao la kuzaliwa Yesu Kristo kama biblia inavyosema
ingawa tarehe siyo muhimu.
Wanajitetea dhidi ya wale wanaopinga kuwa wako
sahihi kwani hata kama Yesu mwenyewe angekuja leo asingeliweza kukasirika kwa
watu kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ilimradi tu wana nia safi. Wanaendelea
kujitetea kwa kusema kuwa hata hao wanaopinga ni wanafiki kwani suala la
mapokeo katika imani yeyote ile haliwezi kuepukika wakitolea mfano kwamba hata
Biblia yenyewe Kitabu kitakatifu nyakati za kanisa la mwanzo hakikuwa kama
kilivyokuwa sasa, maandishi yalikuwa yamechapwa katika magome ya miti na ngozi
za wanyama.
SOMA: Vitabu chanzo cha maendeleo na mafanikio makubwa ya binadamu Duniani.
SOMA: Vitabu chanzo cha maendeleo na mafanikio makubwa ya binadamu Duniani.
Mbona sasa hao wanaojidai kupinga mapokeo ya
aina yeyote ile mbali na yaliyoandikwa kwenye biblia wasikatae na kutumia
biblia iliyochapishwa kwenye karatasi na kurudia kuendelea kutumia biblia
zilezile zilizokuwa zimechapwa kwa ngozi, magome ya miti na katika miamba?
Hawaoni kuwa ni mapokeo kutumia kitu tofauti na walichotumia wakristo wa
mwazo?.
Si hivyo tu, Teknolojia nyingi ni mapokeo
kutoka kwa watu mbalimbali na wengine walioziasizi hata hawako katika imani ya
kikristo, ingetegemewa basi hata na vitu kama intaneti, kompyuta, simu na hata
magari yanayotumia injini kuwa haramu kabisa kwa watu hao wapinzani kwani enzi
zile za kanisa la mwanzo vitu hivyo havikuwepo na wala hamna mahali kwenye
biblia palipoandikwa habari za intaneti na simu zije kutumiwa kueneza injili.
Iweje sasa leo wajiongeze kuvitumia vitu hivyo katika kueneza imani yao, haya
si mapokeo? Au ni kutaka tu kutafuta uhalali na sababu ya kujitofautisha na
makundi wanayoyahama? Kwanini wasitumie ngamia, punda na miguu kuzunguka dunia
nzima kama walivyofanya mitume 12 wa Yesu?
SOMA: Mbinu mpya za kufanya mambo Dunia, biashara ,ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu.
SOMA: Mbinu mpya za kufanya mambo Dunia, biashara ,ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu.
Wanaenda mbali zaidi kwa kusema hata wale
Mitume walioandika Injili ya Yesu wenyewe hawakuweza kuandika neno kwa neno
kila kitu kama Yesu alivyotenda sembuse ije kuwa mambo madogo kama kukumbuka
kuzaliwa kwa Yesu, wanatolea mfano kwamba Injili za Luka Mathayo na Marko
ingawa maudhui ni yaleyale lakini kuna tofauti kubwa katika lugha na maneno
waliyotumia kuwasilisha ujumbe hivyo siyo kweli kwamba mapokeo hayawezi kabisa
kukubalika katika kanisa lenye umri zaidi ya miaka 2000 linalopitia mabadiliko
makubwa Kijamii, Kiteknolojia, kimuundo, kimtazamo na hata Kiuchumi.
Orodha
kamili ya Madhehebu yanayosheherekea sikukuu ya Krismasi.
· Wakatoliki
· Waordhodox
· Waanglikana
· Waprotestant
wengi wakiwemo wa makanisa ya Kiinjili ya Kilutheri, Wapentekoste, Moravian,
Menonite nk.
Upande
wa wale wanaopinga kusherekea sikukuu ya Krismasi.
Katika makundi 3 niliyoyataja ya Wakristo ni asilimia
ndogo sana wanaopinga Krismasi. Na wengi wao wanatokea katika kundi la
Kiprotestant wale wapinzani wakubwa wa Ukatoliki na Uorthodox. Taratibu na
desturi nyingi za Wakatoliki na Waordhodox karibu ni sawa isipokuwa tu
wanatofautiana kwenye Uongozi mkuu wa Kanisa kila mmoja akiwa na kiongozi wake
mkuu(Papa). Waprotestant wanatofautiana na hao 2 kuanzia Uongozi mpaka
mafundisho makuu ya kanisa hata na mafundisho mengine yaliyokuwa na msingi wake
katika Kitabu Kitakatifu cha Biblia.
Vikundi vya Kiprotestanti ukiacha vile
vikubwa kama Walutherani na Wapentekoste vipo vingi sana ingawa idadi ya kila
kikundi ni ndogo, wingi huu unatokana na kila siku kuibuka tofauti ndogondogo
za kimafundisho, mtu akitofautiana kidogo tu na kanisa alilopo huhama na kwenda
kuanzisha kikundi chake. Sababu hizi ndizo zilizosababisha baadhi yao kutokusherekea
Krismasi.
SOMA: Alichofanya mwimbaji huyu wa Injili unakijua?
SOMA: Alichofanya mwimbaji huyu wa Injili unakijua?
Unaweza kukuta vikundi vingine wao kujimega
kutoka madhehebu yao ya mwanzo sababu kubwa ilikiwa ni Krismasi tu, wengine ni
Kuabudu siku ya Jumapili tu nk. Tofauti ziko nyingi kulingana na jinsi kila mtu
anavyoweza kuisoma na kuielewa Biblia kivyake, na wote wanaojimega hawawezi
kukosa kifungu kwenye Biblia kinachotetea madai yao kama tu ilivyo kwa upande
wa pili nao usivyoweza kukosa kifungu cha kutetea msimamo wao katika Biblia
hiyohiyo. Vikundi vingi vinavyopinga Krismasi havikuanza siku nyingi, vingi ni
kuanzia Karne ya 18
Madai
yao makubwa.
Madai makubwa ya wanaopinga Krismasi ni
kwamba, Kwanza Krismasi haipo mahali popote pale katika Biblia bali ni mapokeo
tu ya imani za kipagani, tarehe kamili ya Krismasi siyo 25 Desemba kwani biblia
iliandika kwamba Bikira Mariamu alipopewa habari za kumzaa Yesu ulikuwa ni
mwezi wa 6 na hivyo isingewezekana mimba kukaa miezi 6 pekee mpaka kujifungua
na hata majira yanayotajwa kwenye biblia kuwa ilikuwa ni kiangazi ni tofauti
kabisa kwani mwezi Desemba Bethlehemu kuna baridi na theluji kali.
SOMA: Mungu hutenda kwa namna ya ajabu sana.
SOMA: Mungu hutenda kwa namna ya ajabu sana.
Sababu nyingine ni Watu kufanya ibada za
kipagani na matendo yasiyompendeza Mungu wanaposherekea sikukuu ya Krismasi
mfano kulewa, ulafi, starehe za kila aina, kupeana zawadi, kuabudu sanamu kwa kutengeneza
vijumba mfano wa hori la mifugo alimozaliwa Yesu Kristo.
Madai yao makubwa ni kwamba ikiwa Yesu Kristo
angelishuka leo hii angekasirika sana kukuta watu wakiabudu vitu ambavyo
hakuamuru viandikwe kwenye kitabu chake Kitakatifu tena kwa namna inayomchukiza
mno baba yake, ulevi na matendo mengi maovu. Tena wanaenda mbali zaidi kwa
kutaja vifungu mbalimbali kwenye biblia vinavyokataza kuabudu Miungu na sanamu
za kujichongea. Wanakataa kata kata mapokeo ya aina yeyote yale yanayoenda
kinyume na yale yaliyoandikwa katika kitabu Kitakatifu cha Biblia. Wanadai
Mkristo ni lazima aishi kulingana na muongozo wa Biblia Takatifu neno kwa neno
na haitakiwi kabisa kutenda jambo hata moja lililokuwa nje ya kitabu hicho.
Vikundi hivi vingine hata vimefikia hatua ya
kukataa kutambua sherehe au sikukuu za aina yeyote ile nyingine zaidi ya ile ya
kufa kwa Yesu(Ijumaa Kuu), wanapinga kuanzia sikukuu za kuzaliwa(Birthdays),
sikukuu za kiserikali na sherehe nyingine zote za kidini na kitaifa wakidai
kufanya hivyo ni kuabudu Miungu na sanamu.
Vikundi
na Madhehebu ya Kikristo yanayopinga kusherekea sikukuu ya Christmas
· Mashahidi
wa Yehova
· Waadventist
Wasabato
· Union
Church of God (UCG)
· Kanisa
la Kibaptist la Magharibi(Westboro)
· Baadhi
ya Makanisa mengine mengi madogomadogo yenye watu kuanzia 1 na kuendelea.
Mpendwa msomaji wangu kama ulivyoona katika
mjadala huu mimi sina upande wowote, nimejitahidi kwa kadiri ya uwezo wangu
kuwasilisha tu ukweli ulivyo kulingana na taarifa kutoka vyanzo mbalimbali,
nisingelipenda unihusishe na upande wowote ule. Ikiwa wewe ni mshabiki wa upande
fulani ni uamuzi wako mwenyewe. Kikubwa hapa kwa mujibu wa jukumu langu mimi
ilikuwa ni kutoa tu taarifa(kuelimisha jinsi mambo yalivyo) kulingana na msimu
wenyewe kuwa wa Krismasi.
................................................................
Karibu katika Group letu la masomo la Michanganuo-online kwa masomo kila siku ya fedha na michanganuo ya biashara kwa kiingilio cha shilingi elfu 10 tu unakuwa mwanachama wa kudumu. Mawasiliano ni, Wasap 0765553030 au simu 0712202244
Unaweza pia kujipatia vitabu vyetu hapa; Smartbookstz
0 Response to "MADHEHEBU YA KIKRISTO WASIOSHEREKEA SIKUKUU YA KRISMASI NA SABABU KUBWA YA KUTOADHIMISHA"
Post a Comment