Mwanzo wa mahusiano mengi ya kimapenzi uwe ni uhusiano wa
kawaida tu au hata uchumba, mara nyingi sana utakuta mvulana au mwanaume ndiye
hujishughulisha zaidi kuandaa maneno mazuri ya kumwambia mpenzi wake wa kike.
Na msichana au mwanamke kwa upande wake mwanzoni atazungumza maneno kwa
tahadhari kubwa kuhakikisha kwamba anajilinda asije akaharibu kwa kuongea vitu
vitakavyompunguzia credit au hadhi.
Wawili hawa kulingana na malengo ya uhusiano wao hakuna
njia nyingine ya kila mmoja kumfahamu mwenzake vizuri zaidi ya njia ya
mazungumzo, hivyo katika kila hatua watakuwa wakijadiliana mambo mbalimbali
yatakayoathiri mahusiano yao sasa na katika muda ujao ikiwa wataamua uhusiano
wao udumu au kuoana. Miongoni mwa vitu watakavyojadili ni masuala yanayohusu
pesa
Kwahiyo leo hii tutakwenda kuona masuala ya pesa, ni yapi
mtu anaweza akayazungumza na ni yapi hayastahili kabisa kuzungumzwa na kila
upande. Kuna watu wengi wamewahi kujikuta maamuzi yao waliyowahi kufanya ya
kuanika vitu ambavyo hawakustahili kabisa kuvisema na vilevile wapo pia wengine
waliojutia uamuzi wa kutokuweka bayana mapema baadhi ya maswala, wakafichaficha
wakijua ndio itawafanya kuwa salama zaidi
kumbe ni kinyume chake.
Wapo wengine hata waliishia kuwakosa wapenzi wao hivihivi
katika dakika za mwisho kisa tu midomo yao kutokujua waongee kitu gani. Hivyo
somo hili ni muhimu sana hasa kwa ‘mateenager’ na wale wote ambao wanatarajia
kuingia katika mahusiano hususani yale ya uchumba. Watu wengine hudhani eti wasichana
hawana maswali ya kuwauliza wavulana katika sekta ya pesa na jukumu lao ni
kuitikia tu na wakizungumza basi wanabembeleza au kudeka lakini siyo hivyo, mahusiano
ni mkataba baina ya watu wawili na tena ikiwa ni ndoa basi mkataba huo ni wa
kisheria hasa, hivyo basi pande zote mbili yafaa ziwajibike kwa kila mmoja
kuzungumza.
Wanaume huongoza kuwa wasiri wa hali zao kifedha mfano mwanamke haambiwi chochote kuhusu mipango ya ujenzi wa nyumba anashitukia tu siku anaambiwa, "mama fungasha twende" "tuende wapi mme wangu", anaambiwa wewe twende gari ipo nje inatusubiri. Mwanamke anashitukia wakiingia nyumba mpya(kwao) bila kudokezewa chochote kabla, vipi hii ni sawa?

Swala hapa ni mazungumzo ya aina gani na kwa wakati gani.
Yote haya ni leo katika mfululizo wa masomo yetu 30 ya fedha kwenye group la watu makini watsap la Michanganuo-online. Leo ni somo la 4 bado masomo mengine 26. Karibu sana wewe ambaye bado hujajiunga. Lipia kiingilio chako sh. Elfu 10 nikuunganishe muda huohuo pamoja na kukutumia masomo, vitabu, michanganuo na semina zote tangu mwezi January

Namba zetu ni, 0765553030 au 0712202244
Wasap: 0765553030
0 Response to "MASWALA YA PESA USIYOTAKIWA KUMWAMBIA MPENZI WAKO MNAPOANZA MAHUSIANO"
Post a Comment