Leo tutazungumzia juu ya hatari ya
utegemezi katika mshahara au kipato kimoja tu, mtu hapaswi kuwa kama samaki
kwamba akitolewa kwenye maji tu na huo unakuwa ndio mwisho wa maisha yake.
Yafaa tufanane na kiboko, kwenye nchi kavu anadunda na majini pia anadunda bila
wasiwasi wowote.
………………................
Siyo kila mtu unayemuona anafanya kazi ya
kulipwa mshahara mwisho wa mwezi basi ni tegemezi kwa mshahara anaolipwa
hapana, kuna baadhi ya watu wengine ingawa ni wachache hufanya kazi kwasababu
tu wanaipenda na wanataka kukidhi hamu yao ya kuifanya hiyo kazi, wanafanya
kazi ili waishi kwa furaha. Watu hawa kwa maneno mengine tunaweza kuwaita watu
walio huru kifedha.
Lakini kwa upande mwingine asilimia kubwa ya
watu walioajiriwa zaidi ya asilimia 95% au wale wanaofanya biashara
inayowaingizia kipato kimoja tu hawawezi kuishi bila kipato hicho, maana yake
ni kwamba ikiwa kipato chao cha mwezi kitasita siku moja hawana tofauti na
samaki aliyetolewa nje ya maji. Kwa upande wa waliojiajiri lakini wanategemea
chanzo kimoja tu cha mapato mfano biashara moja tu nao hawana tofauti na wale
walioajiriwa wakitegemea mshahara wa mwezi peke yake kwani hawana njia nyingine
mbadala inayoweza kuwaingizia kipato. Hata hivyo makala hii imekazia zaidi
ajira.
Kwanini
watu wanakuwa tegemezi kwa mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha mapato?
Sababu kubwa ya utegemezi kwenye mshahara wa
mwezi ni kwamba kipato kinachotokana na mshahara ndiyo kipato kinachoweza
kutabirika kwa urahisi kuliko vipato vya aina nyingine zote lakini ubaya wake
ni kwamba huwafanya watu kuridhika kupita kiasi(kubweteka) kuhusiana na hali yao ya kifedha.
Kipato cha mshahara ni cha uhakika tu pale
mtu anapokuwa akifanya kazi, ikiwa atasitisha kazi leo na mshahara nao utakoma
siku inayofuata. Watu hujihisi salama zaidi wawapo na ajira na hivyo kuchukulia
utegemezi kwenye ajira kuwa ni jambo la kawaida tu. Lakini hali hii hubadilika
ghafla kipindi usalama wa ajira unapokuwa hatarini. Kipindi hiki ndicho mtu
hutambua hasara za kuwa tegemezi kwenye mshahara wa mwisho wa mwezi.
SOMA: Kwanini kama huipendi ajira yako bado unaendelea kuifanya?
SOMA: Kwanini kama huipendi ajira yako bado unaendelea kuifanya?
Watu wengine hata inakuwa vigumu kukubali
ukweli kwamba maisha ya kutegemea mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha
mapato ni jambo baya na la hatari. Watu tokea utotoni tumeaminishwa aina hizi
za fikra na yeyote yule anayejaribu kuhoji kasumba hizi hukumbana na upinzani
mkali na kukosolewa.
Kuishi ukitegemea mshahara peke yake au
chanzo kimoja tu cha mapato ni hatari iliyokuwa wazi kabisa, hebu fikiria labda
umepoteza kazi yako leo kwa sababu yeyote ile, inamaana kwamba mwezi unaofuata
huwezi tena kuwalipia watoto wako tuisheni wala kuwapatia hela ya matumizi
shuleni. Hata chakula na matumizi mengine ya msingi nyumbani hutaweza tena
kuyanunua, huwezi kuwanunulia mlo mzuri kama nyama, samaki nk wataishia tu kula
mchicha na maharage ya kubangaiza na
kila kitu kitakuwa kigumu kwako.
Mtu
atapunguza au kuondokana vipi na utegemezi katika mshahara wa mwezi au chanzo kimoja
cha mapato?
Kabla hatujakwenda kuona njia ya kupunguza au
kuondoa kabisa utegemezi katika mshahara wa mwezi, hebu kwanza tuone kwa undani
nini maana ya kutegemea mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha mapato(Kuishi
ukitegemea mshahara wa mwezi hadi mwezi au paycheck to paycheck). Unaweza
kudhani kuwa watumwa wa mshahara wa mwezi ni watu wale wa hali ya chini tu
wanaolipwa mshahara mdogo lakini utakuwa umekosea sana.
SOMA: Wafanyakazi kwenye kazi za ajira wengi hawana fura, upo ukweli wowote au ni uzushi mtupu?
Hata mtu anayelipwa mamilioni ya fedha ikiwa hana kipato cha ziada na nidhamu nzuri ya matumizi ya fedha hizo za mshahara hatakuwa na tofauti yeyote na mtu yule anayelipwa mshahara wa kima cha chini kabisa ambaye naye hana nidhamu na mshahara huo wala chanzo kingine cha mapato.
SOMA: Wafanyakazi kwenye kazi za ajira wengi hawana fura, upo ukweli wowote au ni uzushi mtupu?
Hata mtu anayelipwa mamilioni ya fedha ikiwa hana kipato cha ziada na nidhamu nzuri ya matumizi ya fedha hizo za mshahara hatakuwa na tofauti yeyote na mtu yule anayelipwa mshahara wa kima cha chini kabisa ambaye naye hana nidhamu na mshahara huo wala chanzo kingine cha mapato.
Kuna
vitu hivi vikubwa viwili,
1. Chanzo
cha fedha
2. Mahitaji
au matumizi
Ikiwa wewe chanzo chako cha fedha ni mshahara
peke yake na matumizi yako asilimia kubwa zaidi ya 95% unategemea mshahara huo
basi jua kabisa kwamba upo miongoi mwa watumwa wa mshahara wa mwezi. Mtu yeyote
ambaye mapato yake ni kidogo kuliko matumizi hayupo huru, ni tegemezi kwa
kipato anachopata iwe ni mshahara wa kila mwezi au hata au hata faida kwenye
biashara. Mtu wa aina hii hawezi kabisa kujiwekea akiba wala kuishi bila ya
kipato chake hicho hata kwa miezi 2 au 3 mbele.
SOMA: Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi?
SOMA: Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri binafsi?
Ikiwa upo miongoni mwa watu wengi
waliotegemezi kwa mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha mapato usiogope kuna
habari njema kwako, unaweza kuchukua hatu za kubadili muelekeo na kuwa huru
zaidi kifedha.
KIVIPI?
Ni kwa njia moja tu ya kuweka akiba wakati huohuo ukitumia akiba hiyo
kujijengea/kujinunulia rasilimali(assets) zinazoweza kuzalisha mapato zaidi.
Hii ndiyo njia ya uhakika zaidi ya kupunguza na hatimaye kumaliza kabisa
utegemezi kwenye mshahara au kipato kimoja tu. Huu ni mchakato unaopaswa kwenda
taratibu na kwa uvumilivu mkubwa, hakuna njia ya mkato hapa.
SOMA: Ajira siyo laana bali ni mtaji wa uhakika kuliko aina nyingine zote za mitaji.
SOMA: Ajira siyo laana bali ni mtaji wa uhakika kuliko aina nyingine zote za mitaji.
Kitu cha kwanza na muhimu zaidi kwako ni
kutambua kwamba kutegemea mshahara wa mwezi au chanzo kimoja tu cha mapato
maishani ni jambo baya na la hatari sana kwako. Halafu sasa anza kujinunulia
asseti/rasilimali zenye uwezo wa kukuingizia kipato cha ziada. Kipato cha ziada
hapa ninamaanisha kile kipato ambacho wewe hulazimiki kufanya kazi ndipo kiweze
kuingia, huingia tu hata kama umelala au unaumwa.
Unaweza ukauliza swali hili, ikiwa kipato
chako cha mwezi hakitoshelezi mahitaji yako yote utaweka akiba na nini kusudi
uweze kuja kujinunulia rasilimali? Majibu ni haya yafuatayo;
1.Jifunze
kujinyima kusudi uweze kuweka akiba zaidi.
Kuna vitu ukijinyima au ukaahirisha kuvinunua
huwezi kufa, kwa mfano vitu vyote tunavyotumia ili kuridhisha tu nafsi zetu tunaweza kuachana navyo kabisa
bila madhara yeyote mfano mmojawapo ni kula mlo wa gharama ya juu kama chipsi
kuku nk. wakati kuna vyakula vya gharama ndogo tu kama ugali, wali na mihogo.
Kadiri utakavyoweka akiba zaidi huku ukijinunulia rasilimali ndivyo na nafasi
yako ya kuondokana na utegemezi kwenye mshahara nayo itakavyoongezeka.
SOMA: Huna mtaji wa kutosha na hukopesheki? Jaribu njiia hii ya kufunga mkanda (bootstrapping)
SOMA: Huna mtaji wa kutosha na hukopesheki? Jaribu njiia hii ya kufunga mkanda (bootstrapping)
Jitahidi kuwa mvumilivu kabla hujataka kitu
au kufanya jambo linalotoa fedha mfukoni kwako. Inawezekana ni mahai pa
kutembea tu kwa miguu, wewe bajaji au bodaboda ni ya nini? Ishi leo kama
masikini lakini kesho uje uishi kama mfalme. Ndugu yako anayetaka leo umpe
msaada wa fedha kwa mambo madogomadogo yasiyokuwa na umuhimu mkubwa kwanini
usimnyime ukijua ukijakufanikiwa utampa msaada mkubwa zaidi kama kumsomeshea
mwanae, hela za matibabu nk.?
2.Jijengee
taswira ya uhuru wa kifedha kwenye akili yako.
Oanisha na kuzizoea akilini dhana mbalimbali zinazohusiana
na uhuru wa kifedha kabla hata hujaufikia uhuru wenyewe kifedha kwa mfano;
1. Kipato
cha mshahara
2. Kuweka
akiba
3. Kujilimbikizia
rasilimali(asseti) zinazowezaweza kukuzalishia kipato cha ziada
4. Kipato
cha ziada mbali na ajira
5. Gharama/matumizi
yako yote ya kila mwezi
6. Fedha
za dharura
7. Kuwa
huru na madeni
8. Jinsi
ya kuweka akiba
9. Jinsi
ya kujijengea rasilimali zinazozalisha faida. Nk.
Hakikisha unakuwa na uelewa na dhana hizi mbalimbali, kujua maana yake na jinsi unavyoweza kuzitumia katika harakati zako mbalimbali za kusaka pesa.
SOMA: Kama una biashara ndogo ya mtaji kidogo, hizi hapa njia 11 za kiboost
Hakuna kitu kinachoweza kuizidi tabia njema ya kujiwekea akiba linapohusika suala zia la Uhuru wa mtu wa kifedha au kwa maneno mengine mafanikio kifedha. Kuweka akiba ndio mwanzo wa kila kitu pale mtu anapotaka kuanza kununua rasilimali yake ya kwanza(asset). Lakini kuweka tu akiba hakuwezi kutosha, unatakiwa pia ununue rasilimali zitakazokuingizia kipato kama hizi hapa chini;
· Hisa
· Akaunti
ya kudumu ya benki(fixed bank account)
· Hata
tu kununua chupa ya chai(thermos) kwa ajili ya kuuzia chai nayo ni asseti,
mashine mbalimnali mfano za kufyatulia tofali, kukamulia juisi ya matunda kama
miwa, chungwa, embe nk. Kununua kipande cha ardhi au nyumba ingawa vitu hivi
unaweza kuhitajika ushiriki wako pale kwa namna moja au nyingine siyo kama
ilivyo kwa hisa au akaunti ya kudumu ya benki. Kumbuka biashara inahitaji rasilimali ili iweze kufanyika.
SOMA: Kwanini kila mwanamke anastahili kumiliki vyanzo vingi vya mapato?
Tunaweza kuondokana kabisa na utegemezi kwenye mishahara yetu ya kila mwezi au kipato kimoja tu kwa kujijengea au kujinunulia rasilimali(assets) zenye uwezo wa kuzalisha kipato cha ziada cha kutosha kukabiliana na matumizi yetu yote ya mwezi mzima bila ya kugusa mshahara wenyewe. Jambo hili linatakiwa kuwa ndio LENGO kuu la kila mtu maishani katika kuhakikisha maisha bora yaliyojaa furaha tele. Ingawaje fedha tu peke yake haiwezi kuwa ndio nyenzo kuu ya kukuletea furaha lakini ina mchango mkubwa katika kumfanya mtu aishi maisha ya UHURU.
Tunaweza kuondokana kabisa na utegemezi kwenye mishahara yetu ya kila mwezi au kipato kimoja tu kwa kujijengea au kujinunulia rasilimali(assets) zenye uwezo wa kuzalisha kipato cha ziada cha kutosha kukabiliana na matumizi yetu yote ya mwezi mzima bila ya kugusa mshahara wenyewe. Jambo hili linatakiwa kuwa ndio LENGO kuu la kila mtu maishani katika kuhakikisha maisha bora yaliyojaa furaha tele. Ingawaje fedha tu peke yake haiwezi kuwa ndio nyenzo kuu ya kukuletea furaha lakini ina mchango mkubwa katika kumfanya mtu aishi maisha ya UHURU.
Xxxxxxxxxxx Mwisho wa mkala hii. Xxxxxxxxx
Ndugu msomaji wa makala hii, huu ni mwezi wa 2
tangu mwaka huu uanze na katika email yangu ya mwisho kwako nilikuahidi moja ya
malengo ya kampeni yetu ya mwaka huu tutashughulika zaidi na VIWANDA , nilisema kwamba michanganuo
mingi tutakayoandika itahusiana na viwanda mbalimbali vidogo na vya kati ambapo
mtu anaweza kuanzisha cha kwake kwa urahisi.
Baada ya mwezi mzima wa
kwanza kumalizika ambao ndio uliokuwa mwezi wa likizo kwa upande wetu(kumbuka
Desemba tulifanya kazi mwezi mzima bila ya kupumzika) sasa kampeni zetu za
mwaka huu wa 2019 ndio zimeanza rasmi Februari hii. Kwa kuanzia nimegundua watu
wengi katika kuandika michanganuo ya biashara tatizo kubwa lipo kwenye NAMBA au
MAHESABU. Kimsingi hesabu hizi hazipaswi kuwa ngumu ikiwa utafuata kanuni inayotakiwa.
Ndio maana kabla hatujaanza
rasmi Michanganuo ya viwanda mbalimbali tumeona ni vizuri kufanya semina kubwa
ya jinsi ya kuandaa hesabu za mpango wa biashara. Semia hiyo itaanza tarehe 12
Februari siku ya Jumnne mpaka tarehe 15 Feb. siku ya ijumaa. Ni semina ya siku
4(Intensively) na tutahakikisha yule aliye na nia ya dhati ya kufahamu kuandaa
makadirio ya hesabu za biashara anafahamu kwa uhakika kabisa.
Semina itaendeshwa kupitia
group la whatsap la MICHANGANUO ONLINE,
Kiingilio cha semina hii ni shilingi elfu kumi,
10,000/= na mwisho wa kulipia ni Jumatatu ya tarehe 11. Undani wa semina
yenyewe tutajulishana kila siku kabla ya siku yenyewe kufika hapa katika blog
na kwa njia ya email.
Vile vile masomo yetu ya
kila siku katika group la WASAP la Michanganuo online yanaendelea kama kawaida
kwa wale waliokwishajiunga tayari. Wale wanachama wa zamani hawatalipia tena
semina hii ya Mahesabu ya mpango wa biashara, wataingia free.
Nafasi zinaweza kujaa muda
wowote kuanzia sasa kutokana na idadi ya group kukaribia kufika watu 250, idadi
ya mwisho, hivyo ni vizuri kama unapenda kuwa miongoni mwa group hili makini(SUPER MASTERMIND GROUP 2019) kwa mwaka
mzima huu wa 2019 basi uwahi siti yako mapema kabla group halijajaa, hatutakuwa
na uwezo wa kuendesha magroup mawili kwa wakati mmoja.
ASANTE
SANA
Peter Augustino Tarimo
self help books Tanzania ltd
Wasap: 0765553030
Simu: 0712202244
0 Response to "Unategemea mshahara wa mwezi au kipato kimoja? Hizi hapa mbinu za kujinasua na kuishi maisha mazuri unayotamani."
Post a Comment