Kuna msemo mmoja maarufu watu hupenda sana
kuutumia kwa watu wanaofanikiwa kuwavutia kwa haraka zaidi watu wengine iwe ni
katika nyanja ya mapenzi, biashara kuvutia wateja na hata wale wanaopendwa
zaidi na ndugu, jamaa zao au marafiki. Msemo huo watu husema hivi, “Fulani
bwana si bure, yule ana kamzizi” wakimaanisha kuwa fulani ana dawa ya kienyeji
inayomwezesha kuwa na ushawishi mkubwa kiasi hicho cha watu kumpenda haraka
mithili ya sumaku.
Ushahidi kutokana na tafiti mbalimbali za
kisayansi unaonyesha kwamba humchukua binadamu chini ya sekunde 30 kuamua ikiwa
amempenda mtu au la. Hii ni silika ya binadamu iliyojengeka taratibu ndani ya
vinasaba vyake mamilioni ya miaka yaliyopita wakati binadamu wa kale kabisa
alipotaka au kuamua kujenga urafiki na wanadamu wenzake.
SOMA: Jinsi ya kupata marafiki na kuwa na ushawishi kwa watu wengine(How to win friends and and influence people)
SOMA: Jinsi ya kupata marafiki na kuwa na ushawishi kwa watu wengine(How to win friends and and influence people)
Silika au tabia hii katika nyakati tunazoishi
leo hii ndio huathiri kwa kiasi kikubwa sana mahusiano yetu binafsi baina ya
mtu na mtu na hata yale ya kibiashara au ya kikazi. Maaamuzi karibu yote mtu anayoyafanya
kibiashara kuanzia kile kinachomkusukuma anunue bidhaa au huduma fulani kutoka
kwa mtu mwingine mpaka kufanya mkataba na mtu wa kibiashara au kazi yanategemea
ni kwa kiasi gani watu hao anaofanya nao biashara/mkataba wanavyompenda au
kumuamini.
Halikadhalika huwezi ukamtongoza mpenzi awe
ni mwanamke au mwanaume akakukubalia hivihivi tu pasipo kwanza kukupenda na
kukuamini, kwa hiyo ni lazima kwanza uhakikishe unajenga hiyo hali ya kupendwa
na kuaminiwa kabla ya kupendwa kwenyewe. Kwa upande wa biashara ndio hivyo
hivyo, haiwezekani mteja atoke huko tu kusikojulikana pap! na kuanza kununua
bidhaa/huduma unazozitoa pasipo kwanza kukufahamu na kuifahamu vizuri bidhaa yako,
aipende na ajiridhishe kweli inaaminika.
SOMA: Je wajua kitu binadamu anachopenda zaidi kuliko vyote duniani?
SOMA: Je wajua kitu binadamu anachopenda zaidi kuliko vyote duniani?
Sasa wataalamu wamegundua kwamba ili mtu
uweze kupendwa na kuaminiwa haraka zaidi na watu wengine bila kujali ni katika
mazingira yapi, mapenzi biashara au kazi, kuna vitu au vitendo ambavyo unaweza
kuvifanya ili kutengeneza huo mvuto wa ajabu. Mbinu hizo ni hizi hapa chini;
1.TABASAMU:
Unaweza kufikiria kwamba hili nitendo la
kawaida tu lakini hebu kumbuka kwanza siku uliyowahi kuhudhuria mkutano wowote
ule wa kibiashara, maonyesho ya biashara au tamasha, unakumbuka jinsi washiriki
mbalimbali walivyoonekana siku hiyo? Je walikuwa wamenuna au wametabasamu? Na
kama walikuwa wametabasamu walifanya hivyo kwa bahati na sibu au ni kitendo cha
kupangwa?
SOMA: Sababu nne kwanini matangazo yako ya biashara hayaleti wateja kama unavyotaka.
SOMA: Sababu nne kwanini matangazo yako ya biashara hayaleti wateja kama unavyotaka.
Kiukweli suala la kutabasamu wataalamu husema
huwa halitokei tu hivihivi kwa bahati, bali ni kitendo cha kukusudia, mtu
hutabasamu akiwa na malengo fulani. Kuna watu wengine hudhani labda ili waweze
kuonekana ni weledi wenye kuheshimika basi wanatakiwa kuwa wakimya sana(serious)
lakini ukweli wa mambo ni kwamba tabasamu dogo tu usoni huweza kukupa kila
kitu, heshima, kupendwa na pia watu wavutiwe zaidi kuwa na wewe karibu.
2.KUKUTANISHA
MACHO.
Kukutanisha macho yako nay a mtu mwingine
maana yake ni kwamba unaaminika na huna chochote kile cha kuficha. Hakikisha
lakini hufanyi hivyo kwa kujifanyisha bali inakuwa ni tabia yako uliyoizoea
kula siku na muda mzuri wa kukutanisha macho yako na mtu ni pale mtu huyo
anapokuwa akizungumza huku ukionyesha shauku ya kweli. Pia kutanisha macho yako
nay a mtu mwingine wakati mnapokuwa mkizungumza pointi muhimu au ukisisitiza
maoni yako.
SOMA: Hivi unajua ni nani anayeyadhibiti maisha yako?
SOMA: Hivi unajua ni nani anayeyadhibiti maisha yako?
3.AKISI
YULE UNAYEZUNGUMZA NAE
Kuiga mkao au pozi za yule unayezungumza naye
kisaikolojia kutamfanya ahisi unakubaliana nae na kupekea kile anachokisema.
Kama amesimama mikono kaweka mfukoni na wewe fanya hivyohivyo. Ukikuta kaka chini
na wewe fanya hivyo pia ila usionyeshe
kufanya kwa kujilazimisha, fanya kama ni kawaida yako.
4.ONYESHA
SHAUKU
Kawaida ya watu hupendelea zaidi kuzungumzia
mambo yale yanayowahusu wao tu, kwahiyo wewe mwache azungumze kwanza. Siyo tu
itamfanya ajisikie vizuri bali pia itakupa wewe uelewa wa ni kitu gani hasa
anachokifikiria akilini mwake. Na unaweza pia kumuuliza maswali yasiyokuwa na
majibu ya ndiyo au hapana, kusudi aweze kufunguka zaidi kwako.
SOMA: Siri 2 za ushindi za kufanikiwa jambo lolote lile, hazifundishwi shuleni, vyuoni wala madarasa ya ujasiriamali.
SOMA: Siri 2 za ushindi za kufanikiwa jambo lolote lile, hazifundishwi shuleni, vyuoni wala madarasa ya ujasiriamali.
5.ONYESHA
SHUKRANI
Kila mtu yupo bize ana shughuli nyingi za
kufanya kuliko muda aliokuwa nao, mshukuru kwa muda wake, mshukuru pia kwa
kukushirikisha mawazo na maneno yake bila kusahau kumshukuru kwa kufanya
biashara na wewe. Watu hupenda sana kushukuriwa, kuthaminiwa na mara zote
huvutiwa na wale watu wanaoweza kuwafanya wajisikie hivyo.
……………………………………..
Ndugu msomaji, masomo yetu mengine ya Pesa
yanaendelea katika lile Group la MICHANGANUO-ONLINE kila siku, Jana tarehe 27
tulikuwa na somo lisemalo,
Somo letu la leo tarehe 27 usiku ni hili hapa
chini;
“KANUNI
8 ZA KUVUTIA PESA ZIJE KWAKO MITHILI YA SUMAKU”
Baada ya masomo ya ile semina ya Hesabu za
michanganuo kupotea na kompyuta tunayaandaa tena upya na siku ya semina
itatangazwa hivi karibuni, semina hii ni moja kati ya semina kubwa sana kuwahi
kufanyika katika group hili kutokana na umuhimu wa mada yenyewe. Kumbuka sehemu
inayodhaniwa kuwa ngumu kuliko nyingine zote katika mpango wa biashara ni
sehemu hii ya fedha. Na kama utakumbuka kwenye malengo yetu kwa mwaka huu
tulisema tutakuwa na Michanganuo mikubwa 4 kuhusiana na Uanzishaji wa viwanda.
Kabla ya michanganuo hiyo tunapenda mtu ajifunze kwanza somo hili la fedha ili
michanganuo hiyo iwe rahisi zaidi kwake.
Unapojiunga katika group hili moja kwa moja
unakuwa na sifa ya kushiriki kila kitu kwa mwaka mzima huu wa 2019. Pia
tunakupatia masomo na vitu vyote tulivyojifunza mwaka uliopita kama ifuatavyo.
1. Kitabu cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua
kwa hatua.
5. Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN
kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI
CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili
na kiigereza
9. Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
10. Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha
kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
11. Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE
MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati
kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
12. Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.
13. Ukurasa mmoja wa mchanganuo.
Nafasi ya kujiunga bado ipo lakini inazidi
kuwa finyu kadiri siku zinavyokwenda, group lina ukomo wa idadi ya watu na
itakapotimia ni basi hatutapokea tena washiriki kwa mwaka huu hivyo kama
utapenda kuwa nasi 2019 nakusihi sana ujiunge mapemba.
Ukishalipa kiingilio sh. Elfu 10 kupitia
namba 0765553030 au 0712202244 tuma ujumbe wa wasap au sms usemao, ‘NIUNGANISHE
NA GROUP LA MASOMO’ na nitakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia kila
kitu kama vilivyoorodheshwa hapo juu.
Wooow..! Nice
ReplyDeleteThank you!
Delete