Habari ndugu msomaji na mdau wa blogu hii, natumaini hujambo na unaendelea na majukumu
yako vyema.
Kwa upande wangu mimi ni mzima ila leo hii alfajiri
nilikumbwa na mkasa wa kuibiwa vifaa vyangu muhimu ikiwemo simu pamoja na
laptop. Vifaa hivi ndio huniwezesha kuandika na kuposti makala katika blogu ,
wasap na hata katika mitandao mingine ya kijamii.
Kusudio langu la kutoa taarifa hii ni ili kuwajulisha
wadau hasa wale waliokuwa katika group la wasap kwamba wanaweza kuona post
yeyote pengine inayoweza kutumwa na wezi hao kwa namba au account yangu katika
kipindi hiki kuanzia siku ya Jumamosi alfajiri mpaka siku ya Jumatatu, watambue
kuwa siyo mimi niliyetuma. Nasema hivyo kwani process za ‘kurenew’ line siku za
weekend polisi huwa hamna huduma ya kutoa ‘loss report’ kwa hiyo nalazimika
kusubiri hadi jumatatu asubuhi ili kuipata tena laini yangu ya 0765553030.
Aidha pia nawaomba wadau wasitishe mijadala katika group
la MICHANGANUO-ONLINE mpaka pale mambo yatakaporekebishwa. Kwa upande wa ile
semina yetu ya tarehe 12 siku ya Jumanne inayohusu, JINSI YA KUANDAA HESABU ZA
MPANGO WA BIASHARA nayo nawaomba pia tuisogeze mbele kidogo mpaka tarehe
nyingine tutakayopanga baadae kidogo . Kwa waliokwishalipia tayari nawaomba
wasiwe na wasiwasi kwani rekodi zao zitakuwa salama katika email.
Nakutakia majukumu mema,
Peter Augustino Tarimo
Self Help Books Tanzania.
0 Response to "TAARIFA MUHIMU KWA WADAU WOTE WA BLOGU YA JIFUNZEUJASIRIAMALI NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE"
Post a Comment