Nakukaribisha kusoma makala hii
inayohusiana na utimizaji wa malengo, mengi utayakuta ndani yake karibu sana! Usisahau
pia kuwahi nafasi yako kwenye ile semina yetu iliyoahirishwa mwezi uliopita ya
JINSI YA KUANDAA HESABU KATIKA MPANGO WA BIASHARA. Sasa itafanyika 20/3/2019
1.Usisubiri
ruksa wala kibali
Acha kuwa kama wanariadha au wacheza soka
kusubiri kipenga(filimbi) ilie ndipo
uanze kucheza mechi. Watu wengi linapokuja suala la kutimiza ndoto zao hawana
tofauti na mwanamichezo anayesubiri filimbi au kengele ilie ndipo aanze jambo.
Ulimwengu wa namna hiyo wanaishi watoto. Hebu
kumbuka ulipokuwa mtoto unasoma tangu chekechea mpaka chuo kikuu au ngazi
nyingine yeyote ile. Katika kipindi hicho ulizoea kuishi kwa kufuata ratiba
matukio karibu yote, mfano ulizoea shule kufunguliwa January na kufungwa June,
somo la hesabu kuanza saa 4 na kumalizika saa 5 kisha unaenda mapumziko au
kupata kikombe cha uji nk.
SOMA: Mbinu 2 za ushindi za kufanikiwa jambo lolote, hazifundishwi shuleni, vyuoni wala katika masarasa ya ujasiriamali.
SOMA: Mbinu 2 za ushindi za kufanikiwa jambo lolote, hazifundishwi shuleni, vyuoni wala katika masarasa ya ujasiriamali.
Mtindo huo jinsi akili ya binadamu
ilivyoumbwa, hushika vitu kulingana na ratiba na hujizoesha yenyewe kutegemea
ratiba. Kwahiyo mtu anapokuja kuwa mtu mzima na kuingia mtaani katika maisha ya
kawaida hushtuka baada ya kukuta dunia tofauti kabisa na ile aliyoizoea
shuleni, hukuta hamna ratiba tena, kipenga wala kengele kila anapotaka kuanza
jambo.
Katika maisha hupaswi kusubiri wingu
lipungue, mvua wala wimbi litulie ndipo eti uanze safari, wewe anza hivyohivyo,
ikiwa utasema usubiri basi utasubiri hapo milele.
SOMA: Ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena(make yourself great again)
SOMA: Ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako tena(make yourself great again)
2.Usisubiri
zamu yako.
Kuna dhana moja watu husema hivi; “Ili ufanikiwe inakubidi uwe na roho mbaya”
Unajua ni kwanini wenye roho mbaya hufanikiwa haraka? Ukweli ni kwamba hawafanikiwi kwa sababu wana
roho mbaya hapana, bali kinachowafanya watu wabaya wafanikiwe ni kule
kutokufuata utaratibu wa kawaida kama wa kukaa foleni na kusubiri jambo, wapo
radhi hata kuhonga au kutumia nguvu na kumpita mtu aliye hoi mstarini akisubiri
ilimradi tu yeye awahi kupata huduma, hamwogopi mtu na hivyo kufanikiwa haraka.
Tabia hii pia wanayo watu wazuri wanaofanikiwa lakini wao hawatumii njia haramu
kutimiza ndoto zao.
3.
Jitoe ndani ya ukanda wako wa faraja
Sawa sawa na kama tulivyoona kwenye mbinu ile
ya kwanza, baadhi ya wasomi, sio wote
lakini, hata wanaotoka vyuo vikuu hujikuta wanashindwa kuendana na mazingira ya
nje ya mfumo wa vyuo na kutafsiri maarifa waliyoyapata kwa vitendo kwasababu
wamezoea maisha ya kufanya kila kitu kwa maelekezo kutoka kwa maprofesa,
wakufunzi, serikali na mfumo mzima wa chuo kwani kila upande unataka mwanafuzi
huyo afanikiwe.
Lakini katika maisha halisi kwenye uwanja wa
mapambano goli halitulii sehemu moja tena ili iwe rahisi kwako kufunga bao,
linazunguka kusini, kaskazini, mashariki na magharibi. Uwanja muda wote umejaa
ukungu na tope, siyo shwari tena kama ilivyokuwa chuoni, tena hamna refarii
wala mshika kibendera, na hata ukivunjika mguu hamna yeyote anayejali na mpira
utaendelea kama kawa.
SOMA; Je upo kwenye fani au kazi uliyotamani kuwa tangu ulipokuwa mtoto mdogo?
SOMA; Je upo kwenye fani au kazi uliyotamani kuwa tangu ulipokuwa mtoto mdogo?
4. Kuwa
makini na wale wanaokuzunguka.
Pingu nyingine inayoweza kukuzuia usisonge
mbele kabisa kutimiza ndoto zako ni aina ya watu wanaokuzunguka wewe mwenyewe.
Nakushauri
kafanye jaribio lifuatalo;
Buni kitu chako na kitu hicho chaweza kuwa ni
biashara, kazi ya sanaa kama vile wimbo, igizo, hadithi, shairi au chochote
kile na kisha wafuate marafiki zako unaopenda kupiga nao stori waonyeshe hiyo
kazi kisha waombe wakupe maoni yao kukukosoa.
Ikiwa marafiki hao mrejesho wao wa awali
kabisa utaonyesha ukosoaji unaolenga kukusahihisha ili kazi yako iweze kuwa
bora zaidi, basi ujue unao marafiki wazuri. Lakini ukiwaona wanabeza na kukukatisha
tamaa kwa kusema wao wangeweza kubuni kitu kizuri kushinda hicho cha kwako,
basi ujue kabisa marafiki zako hao hawakufai na tambua hilo siyo tatizo lako
bali lakwao hivyo fikiria mara mbilimbili kupoteza muda wako mwingi ukiwa nao.
Unahitaji marafiki watakaokuokoa na wala siyo kukuzamisha zaidi majini
uangamie. Chagua kuwa nao au kukaa nao mbali lakini ndoto zako zitimie.
5.
Muda mzuri wa kuanza ni sasa.
Pengine unatamani sana kufanya kazi fulani
lakini kazi hiyo inahitaji kwanza mtu upate shahada(digirii). Ina maana kwamba
utahitaji miaka 3-4 ili uweze kuwa na sifa za kupata kazi hiyo. Ikiwa una umri
wa miaka 20 sasa ina maana utamaliza shahada yako ukiwa na miaka 25 au 26. Sasa
unaweza kuona kama ni muda mrefu lakini hebu fikiria kama utaamua kuja kuanza
ukiwa na miaka 30 au 40 utamaliza ukiwa na umri gani na kazi hiyo utaifanya lini? Itakuchukua muda mwingi
sana ukijutia kutokuanza mapema. Kadiri utakavyoanza mapema ndivyo pia utakavyo
timiza ndoto zako mapema.
SOMA: Njia 10 za kuhamasika na kuendelea kubakia na hamasa hiyo kwa muda mrefu ujao.
SOMA: Njia 10 za kuhamasika na kuendelea kubakia na hamasa hiyo kwa muda mrefu ujao.
6.Ondoa
woga
Woga mkubwa watu wanaokuwa nao wanapotaka
kutimiza ndoto zao ni woga wa kushindwa. Hebu
jaribu kuwafikiria wanamichezo tena. Wachezaji hufanya makosa mengi sana
wakati wa mazoezi wanapokuwa wakijiandaa na michuano. Lakini pia hata siku
yenyewe ya mashindano(fainali) bado hufanya makosa na hata kushindwa au
kufungwa magoli. Lakini hiyo haiwezi kuwafanya wasicheze tena michezo kwani
kushindwa ni sehemu ya kujifunza ili wafanye vizuri zaidi hapo baadae.
7.
Kuwa na Mshauri/mtu wako wa mfano
Umewahi kuwaona wapanda milima? Kwanini
wanakuwa na waongozaji(Guids)? Mshauri si lazima awe ni yule uliyemtafuta
mwenyewe hapana, wengine hujitokeza wenyewe tu kulingana na jinsi mwenyewe
unavyoonyesha juhudi zako kwa watu na jamii. Mshauri anaweza kuibuka miongoni
mwa watazamaji, wale wanaoshuhudia kile ufanyacho sawa na ilivyo kwa wachezaji
chipukizi wazuri wa mpira wanaochaguliwa na kocha katika mechi za majaribio
mchangani. Wachezaji wakati mwingine wala hawajui kama miongoni mwa watazamaji
wapo makocha wanaofuatilia, hivyo usifichefiche tena kile unachokifanya.
Hitimisho
Sasa umepta mwangaza kuwa hakuna chohchote
kile kinachoweza kukuzuia usitimize ndoto zako, amua ni nini unachohitaji
kukamilisha ndoto zako kisha unaweza kuweka katika vitendo mbinu nilizokueleza
hapo juu. Anza hata kama ni kidogo usiogope kama utashindwa wala usisubiri
ruksa na kibali kutoka kwa mtu yeyote.
…………………………………………………..
TAARIFA HII NI KWA YULE TU AMBAYE BADO HAJAJIUNGA NA SEMINA ZETU.
· Napenda
kukujulisha kwamba ile semina yetu kubwa na iliyokuwa muhimu zaidi kuliko
semina zote tulizowahi kufanya ya JINSI YA KUANDAA MAHESABU KATIKA MCHANGANUO
WA BIASHARA itafanyika kuanzia siku ya tarehe 20/3/2019 kupitia group la wasap
na kwenye email.
· Mshiriki
wa semina hii ni mtu yeyote aliyekwishajiunga na group letu la masomo ya pesa
ya kila siku la whatsapp liitwalo Michanganuo-online au yeyote yule anayelipa
kiingilio ambacho ni sh. Elfu 10.
· Lengo
kubwa la semina hii ni kuwaandaa washiriki kwa ajili ya uandaaji wa michanganuo
ya uanzishaji wa viwanda ambalo ndio lengo letu la mwaka huu. Tumepanga kuandaa
michanganuo 4 ya viwanda vidogo na vya kati vinavyolipa na ambavyo vitampa mtu
uzoefu mkubwa wa kuandaa mpango wa kiwanda cha aina yeyote ile kikubwa au
kidogo.
· Kwakuwa
mwaka jana tulibaini changamoto kubwa ya watu katika michanganuo ipo katika
hesabu na namba ndio maana tukaona eneo hilo tulifanyie semina maalumu.
· Ili
kukamilisha idadi ya watu darasa linatakiwa kuwa na watu 250 tu ambao bado
kidogo sana idadi hiyo itimie. Kwahiyo ikiwa unahitaji hizi semina nakusihi
usichelewe wahi nafasi yako. Sina hakika kama tarehe 20 itafika kabla idadi
hiyo haijatimia.
· Inawezekana
hupendi kujiunga na magroup ya wasap, hilo lisikusumbue kwani natuma semina
nzima kwa email pia.
· Ada
ya sh. Elfu 10 ni ya mwaka mzima, utapata semina zote zijazo na masomo katika
group. Usisahau pia kwamba nitakutumia masomo na semina zilizopita, vitabu na michanganuo mbalimbali na baadhi yake ni hivi hapa chini;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu
kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu
kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu
kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.
5. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA:
Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza
9. Mchanganuo
wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
10.
Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara
inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
11.
Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2
IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja
au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
12.
Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.
Ukihitaji
kujiunga na Semina hii, tuma kiingilio chako sh. Elfu 10 kupitia namba 0765553030 au 0712202244 jina hutokea Peter Augustino
Tarimo, kisha tuma ujumbe wa, “NIUNGANISHE NA SEMINA”
Ikiwa
hutapenda kuingia kwenye group la whatsapp, nijulishe lakini pia nitumie na
anuani yako ya email kwa ajili ya kukutumia masomo ya semina na vitu
vilivyotajwa pale juu.
ASANTE
SANA
Peter
Augustino Tarimo
0765553030
0712202244
0 Response to "BADO UNASUBIRI KIBALI KUTIMIZA NDOTO ZAKO? TUMIA NJIA HIZI 7 UFANIKISHE MWENYEWE"
Post a Comment