Wakati redio ya Clouds fm inaanza mwishoni
mwa miaka ya 90 kuelekea mwanzoni mwa miaka ya 2000 mtu angekuambia kwamba
nyuma yake kulikuwa na kichwa cha “bwana mdogo” Ruge Mutahaba aliyekuwa katika
miaka yake ya 20 usingeliweza kuamini kirahisi. Redio hii siri yake kubwa ya
mafanikio ilikuwa ni mkakati kabambe waliokuja nao Ruge na mwenzake Joseph
Kusaga wa kuliteka soko kubwa la vijana katika biashara ya burudani na habari
kwa ujumla.
Joseph Kusaga akisimulia jinsi walivyokutana
yeye na Ruge Mutahaba kabla hawajaanzisha Clouds aliwahi kusema hivi; “Ruge
nimekutana nae miaka 22 or 23 iliyopita wakati huo ndiyo tulikuwa tunapiga
disko na Ruge alikuwa wale watu wasiolala mpenda raha. Yeye alikuwa na mapenzi
ya muziki na alikuwa mtoto wa kishua akija lazima umuweke pembeni umchunge ili
wahuni wasimzingue….”
SOMA: Utoke vipi kimaisha? Ruge anakupa fursa muhimu 10 hizi hapa.
Nakumbuka kipindi hicho hata kama ulikuwa mpenzi wa redio nyingine za wakati huo, ilikuwa vigumu sana kujizuia kusikiliza Clouds fm kwa vionjo vyake vilivyokuwa na msisimko wa hali ya juu. Ujio wa redio hii ukawa ndio mwanzo pia wa mlipuko mkubwa wa muziki wa Bongo fleva, matamasha ya muziki na hata mashindano mbalimbali ya vipaji vya kuimba yaliyoratibiwa na clouds chini ya Ruge.
Nakumbuka kipindi hicho hata kama ulikuwa mpenzi wa redio nyingine za wakati huo, ilikuwa vigumu sana kujizuia kusikiliza Clouds fm kwa vionjo vyake vilivyokuwa na msisimko wa hali ya juu. Ujio wa redio hii ukawa ndio mwanzo pia wa mlipuko mkubwa wa muziki wa Bongo fleva, matamasha ya muziki na hata mashindano mbalimbali ya vipaji vya kuimba yaliyoratibiwa na clouds chini ya Ruge.
Binafsi kitu ambacho kamwe hakiwezi kunitoka
akilini kirahisi ni baadhi ya Jingle za redio hii na matangazo mbalimbali ya
biashara ambayo usingejua kama ni jingle au tangazo bali burudani ya aina yake.
Jingle moja kwa mfano lililosisimua kiasi natamani hata leo wangelirudisha
hewani ni lile lililosema hivi, “Sijalala
mwanangu Utauwawa bure” Jingle hili lilimhusu jamaa mmoja dizaini kama vile
alikuwa kibaka aliyemkuta mtu akisikiliza redio yake huku amelala akawa
anainyatia ili amwibie ile redio kiulaini, lakini kumbe bwana yule hakuwa
amelala usingizi aslani bali alikuwa tu
amepumzika akibembelezwa na mirindimo mwanana ya Clous fm. Ndipo alipotaka kumuua na kumwambia yule kibaka, “SIJALALA
MWANANGU UTAUWAWA BURE”
SOMA: Una ndoto ya kufanikiwa? ungana na Ruge clouds TV saa 3 usiku kipindi kipya, ndoto za kitaa.
Kulikuwa na jingle pamoja na vionjo vingi vilivyogusa nyoyo za watu ile mbaya si hivi tu, nadhani clouds wangefanya kuwe na kipindi maalumu cha kukumbuka vitu hivyo kwa kuvipiga tena. Kulikuwa pia na Jingle moja hivi, jina la clouds lilikuwa likitajwa kwa sauti ya muungurumo mkubwa uliokuwa na msisimko wa aina yake wa kuvuta, “CLOOOOOOUDS FM”
Kulikuwa na jingle pamoja na vionjo vingi vilivyogusa nyoyo za watu ile mbaya si hivi tu, nadhani clouds wangefanya kuwe na kipindi maalumu cha kukumbuka vitu hivyo kwa kuvipiga tena. Kulikuwa pia na Jingle moja hivi, jina la clouds lilikuwa likitajwa kwa sauti ya muungurumo mkubwa uliokuwa na msisimko wa aina yake wa kuvuta, “CLOOOOOOUDS FM”
![]() |
Ruge Mutahaba enzi za Uhai wake.
|
Vitu vingine vya kusisimua ninavyokumbuka ni
pamoja na kile kilichokuwa kipindi maarufu cha burudani nyakati za jioni kila
siku cha AFRICAN BAMBATAA
kilichokuwa kikirushwa hewani wakati fulani na mtangazaji Marehemu Amina
Chifupa. Yalikuwa ni mapinduzi makubwa ya burudani yaliyokonga nyoyo za wasikilizaji
kiasi kwamba kila mtu wazee kwa vijana waliupenda muziki wa Kiafrika. Ilikuwa
ikifika jioni tu hakuna mtu aliyebadilisha stesheni zaidi ya Clouds fm.
SOMA: Seth Katende mwanaume utajiitaje Bikira?
SOMA: Seth Katende mwanaume utajiitaje Bikira?
Mapinduzi haya yote kumbe nyuma yake
alikuwepo Marehemu Ruge Mutahaba kitu ambacho nimekuja kukijua siku hizi mbili
tatu tangu ameondoka Duniani mpaka kuzikwa kwake leo na nadhani si mimi tu
mwenyewe bali ni watu wengi walikuwa hawajui. Hata kama kuna watu walioandaa
burudani na shughuli zote hizo kama vile wasanii na waigizaji mfano kina Mzee
Onyango na Mwita, lakini imebainika kuwa kumbe Ruge mutahaba ndiye aliyekuwa MASTERMIND wa kila kitu.
(Siri
kubwa 2) Ubunifu huu wa aina yake Ruge aliutoa wapi?
Watu wengi wanashindwa kujua kwamba Mafanikio
huchangiwa na vitu vingi lakini kuna baadhi ya vitu ambavyo mtu ukiwa navyo na
ukavifanyia kazi barabara mafanikio kwako litakuwa ni jambo la lazima. Lakini
pia inawezekana mtu akawa na vitu vyote nitakavyovitaja lakini ikiwa kama
hatachukua hatua yeyote hamna mafanikio yatakayotokea. Kwa hiyo hapa nitataja
baadhi ya vitu muhimu Ruge alivyokuwa navyo kisha akajitambua mapema na
kuvitendea kazi na bila shaka yeyote ile vikamfanya afike pale alipofikia
kimafanikio katika taaluma yake na tasnia nzima ya habari na Burudani.
1. FURSA:
(Kipaji
cha kutambua fursa haraka na kuitumia)
Kama watu walivyomuita mwenyewe kuwa ni mzee
wa Fursa, Ruge Mutahaba tokea utoto wake hakuwa mtu anayechezea fursa hata
sekunde moja. Kwanza fursa ya kwanza kuiona ilikuwa ni mazingira mazuri ya
kupata elimu. Mtu kukuta baba na mama yako ni watu walio na mwamko wa elimu na
pengine baba ni profesa kama ilivyokuwa kwa Mzee Gelasi Mutahaba baba yake na
Ruge si kitu kidogo. Kwa mtu unayejitambua huwezi kufanya ajizi hata kidogo.
SOMA: Fursa zipo, chagua utakacho, tengeneza mpango, tekeleza na kufuatilia kwa uvumilivu utafanikiwa.
SOMA: Fursa zipo, chagua utakacho, tengeneza mpango, tekeleza na kufuatilia kwa uvumilivu utafanikiwa.
Ni vijana wangapi hukuta wazazi wao hata ni
waalimu au wana nafasi kubwa tu lakini hujibweteka na kupuuzia kujiendeleza wao
binafsi wakitegemea kuja kurithi mali za wazazi wao? Kwa Ruge hili lilikuwa ni tofauti
kabisa na fursa yake ya kwanza kukamata ikawa ni elimu. Alisoma mpaka kupata
shahada zake za Masoko na Fedha tena ughaibuni, Marekani. Hili lilimpa ujasiri
mkubwa uliokuja kumsaidia sana baadae. Ukishakuwa na elimu kuna mambo mengi
yatawezekana ambayo yasingeliwezekana kama hukuwa nayo.
Fursa nyingine aliyoitendea haki vilivyo ni
ile ya soko lililokuwepo katika sekta ya habari na burudani wakati huo, aliweza
kutambua haraka soko linataka kitu gani kwa wakati ule na akafanya vilevile
soko lilivyokuwa linataka. Watu na hasa vijana walikuwa na kiu kubwa ya
burudani, si kama hapo kabla burudani hazikuwepo hapana, ila watu hususani
vijana walitaka mabadiliko, ubunifu zaidi siyo kitu kilekile miaka nenda rudi.
SOMA: Professa J: Historia ya muziki wa bongo Fleva, sisi ni wachonga barabara.
SOMA: Professa J: Historia ya muziki wa bongo Fleva, sisi ni wachonga barabara.
Na kwa kuwa mwenyewe alikuwa tayari
ameshasomea maswala hayo ya Masoko(Marketing) tena katika ngazi ya digirii ndio
maana tulishuhudia jingle na matangazo yaliyoenda shule kiasi kile, hivihivi tu
yangelikuwa ni ya kawaida tu. Aliamini pia katika vipaji ndio maana utaona hata
wafanyakazi wengi wa kampuni yake ni watu wenye vipaji vikubwa.
2. UTHUBUTU
NA UJASIRI
Ruge alikuwa shupavu na mwenye tabia ya
ujasiri mkubwa, ni wangapi hata leo hii wenye uthubutu wa kuunganisha nguvu na
mtu/watu wengine kuanzisha kitu, kampuni au taasisi kwa maslahi yao wote
wakavumiliana mpaka kufikia hatua ya juu kabisa? Wengi ushirikiano huvunjika
kabla hata ya kwenda BRELA kusajili kampuni au biashara yenyewe. Ruge Mutahaba
na Joseph Kusaga hili waliliweza na sasa miaka zaidi ya 20 ushirikiano wao
umekuwa wa kuigwa na vijana wengi.
Ijapokuwa binadamu huwezi kuwa mkamilifu kwa
asilimia 100% Ruge katika harakati za kutimiza ndoto yake kuna baadhi ya watu
wamemuona kama vile hakuwatendea sawa lakini kwa kweli kasoro hizo utakubaliana
nami kuwa mema mengi aliyoyafanya yanafunika hayo yote. Hakuwa mbinafsi na
alipenda kuona watu wengi zaidi wakifanikiwa kupitia vipaji vyao walivyokuwa navyo.
Tofauti na binadamu wengi, Ujasiri wa Ruge wa
kuwasaidia na kuwapa watu wengine nafasi si kitu cha kawaida. Watu wengi husita
kuwasaidia wengine au kuwaonyesha njia kwa hofu kwamba wakija nao kufanikiwa
watawafunika au hawatakuja kuwajali na kuwaheshimu. Ruge hakujali hilo yeye
aliwasaidia vijana wengi pengine kuliko kijana mwingine yeyote hapa Tanzania
aliyepata mafanikio kama yeye. Alianini katika falsafa kwamba, dunia ilivyotapakaa fursa nyingi ni sawa na lilivyokuwa anga, anga ni kubwa mno hivyo kila nyota huweza kung'ara kwa kadiri itakavyo pasipo kuzuiliwa na nyingine.
SOMA: The sky is very wide, every star can shine (Mbingu ni kubwa mno kila nyota inaweza kung'ara)
SOMA: The sky is very wide, every star can shine (Mbingu ni kubwa mno kila nyota inaweza kung'ara)
Mtu yupo radhi amsaidie mtu mwingine akiwa kesha
kufa kwa kumchangia pesa za jeneza lakini si akiwa hai, Ruge yeye badala yake
aliwasaidia watu wakiwa hai, hakusubiri wafe ndipo aje atoe rambirambi
mamilioni ya michango, na huu ni ujasiri mwingine mkubwa aliokuwa nao Ruge.
Mwisho, Ruge ana mengi vijana na hata makundi
mengine ya watu wanaweza kujifunza kutoka kwake. Ijapokuwa amekufa kimwili
lakini ataendelea kuishi nasi kwani alama aliyoiacha haiwezi kufutika kamwe.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Ruge Mutahaba mahali pema peponi Amina.
0 Response to "SIRI KUBWA 2 ZA MAFANIKIO YA RUGE MUTAHABA CLOUDS FM: WENGI HATUKUZIJUA MPAKA ANAUMWA, KUFARIKI NA KUZIKWA LEO"
Post a Comment