WANAOFANIKIWA MAISHANI WENGI HUSEMA ‘NO’(HAPANA) KWA VITU HIVI 3 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WANAOFANIKIWA MAISHANI WENGI HUSEMA ‘NO’(HAPANA) KWA VITU HIVI 3

KIJANA ALIYEFANIKIWA MAISHANI
Ni kitu watu wengi tulikuwa hatukijui au hata kama tunakijua basi tulikuwa tunakichukulia poa, kwamba wale watu wenye mafanikio makubwa maishani kumbe wana tabia moja ya kipekee sana, husema HAPANA kwa vitu vingi kuliko vile ilivyo kwa watu wa kawaida wasiokuwa na mafanikio makubwa.

Tajiri mkubwa na mbobezi katika biashara ya uwekezaji wa kununua na kuuza hisa Warren Buffet aliwahi kutamka maneno haya yafuatayo,

“Tofauti iliyopo kati ya watu waliofanikiwa  sana na wale walio  na mafanikio ya kadiri ni kwamba waliofanikiwa sana husema HAPANA kwa karibu kila kitu kinachokuja mbele yao” -Warren Buffet.

SOMA: Kanuni kuu ya mafanikio Duniani iliyo kubwa kuliko zote.

Ikiwa kama kweli mtu atataka kufanikiwa malengo yake kwa ufanisi wa kiwango cha juu kabisa basi hana budi kusema angalao hapana kwa vitu hivi vitatu 3 vifuatavyo ingawa pia kunavyo vitu vingine vingi tu mbali na hivyo mtu anaweza kusema hapana katika kusogea kutoka pale alipo na kupiga hatua ndefu zaidi ya kimafanikio;

(1) Sema HAPANA kufanya kila kitu mwenyewe(Peke yako)

Ukitaka kuendelea mbele maishani, chochote kile unachokifanya washirikishe watu werevu wa karibu yako watakaokukosoa kwa kauli chanya(si lazima lakini uwashirikishe kila kitu mpaka siri zako za ndani kabisa za kibiashara, washirikishe yale ya msingi tu).

Epuka wale wenye inda na choyo wanaopenda uanguke ili baadae waje kukucheka. Jichanganye na makundi yaliyo na tija kwenye mitandao ya kijamii kama lile group la MICHANGANUO-ONLINE na mengineyo yanayolenga kudumisha mambo mazuri ya kimaendeleo.

Pia epuka sana makundi au watu wanaokubaliana na wewe katika kila kitu utakachokisema na kukifanya hata kama si kizuri, hawakupingi hata mara moja, watu hao nao sio wazuri. Wale wanaokupa changamoto ndio wazuri kwako, ukikosea wanakuambia live bila chenga ili ujitahidi zaidi na zaidi. Sema hapana kwa vitu vyote vilivyo katika ukanda wako wa faraja(your comfort zone) unavyoona vinakinzana na ndoto zako, mfano ikiwa kama kampani yako ni watu wanaovuta vitu kama bangi au dawa za kulevya waambie byebye.  

(2) Sema HAPANA kuharakisha vitu ilimradi tu umemaliza bila ya kujali ubora wake.

Ikiwa kwa kufanya jambo haraka anautoa sadaka ubora wa hicho kitu anachokifanya, basi Mwanamafanikio yeyote wa kweli husema HAPANA, hukataa. Ni lazima kwanza mtu ufikirie kama hauwezi kufanya jambo sasa kwa ubora unaotakiwa, ni lini basi utakuja kuupata muda wa kufanya hivyo? Maana kwa kufanya harakaharaka utakuwa haujatatua tatizo la ubora bali utakuwa umeliahirisha tu.

SOMA: Kijana wa umri mdogo anaweza akaanzisha biashara ikafanikiwa?

Jifunze kusema HAPANA kwa fursa yeyote ile inayoonekana kukuharakisha uitimize na badala yake sema NDIYO kwa ubora tu. Utashangaa utakapojenga tabia hii kuona kazi zako zinawazidi kiwango wale waliokuzunguka, utaweza kuyaona malengo yanayokupa mwanga na hamasa na utajionea fahari kwa kile unachokifanya huku ukiongeza kujiamini kwako katika kila unachokifanya. Lakini kwanza ni lazima useme HAPANA!

SOMA: Jinsi ya kufanikiwa maishani, kamwe usipande mlima bila kiongozi(guide)

Tumia muda unaoupata kutokana na vile vitu ulivyosema HAPANA kwenye vile vitu muhimu zaidi maishani mwako na utajionea matokeo yaliyo bora kabisa.

(3) Sema HAPANA Kwa shinikizo lolote la kutaka ufanane na mtu mwingine ghafla bin vuu!.

Unaimba, ni mwandishi, unatangaza, unahubiri nk. acha kujifananisha na mwingine unayehisi kafanikiwa zaidi, utachekesha bure, badala yake iga kiubunifu. Wewe ni wa kipekee sana unayepaswa kuwa mkweli kwa kile unachokiamini nafsini mwako. Watu wengi waliofanikiwa kimaisha wamesimama kwenye msingi huu muhimu bila ya kutetereka mpaka pale walipozifikia ndoto zao.

SOMA: Wengi wanaofanikiwa maishani huamini vitu hivi vinne(4)

Wakati watu wa kawaida wakilenga kwenye kupata umaarufu, utukufu na anasa za kila aina, Wanamafanikio wao hujiwekea taratibu rahisi tu wanazojitahidi kuzirudiarudia kila siku kama vile, kuwahi katika shughuli zao, kutokulalamika hovyo, kutokulala kabla hawajatimiza walao sehemu ndogo ya kukamilisha ndoto zao nk.

Huwa hawajaribu kabisa kujifananisha au kutamani kuwa kama mtu fulani kwa maneno matupu, hufanya hivyo tu kwa kufuatilia kwa vitendo ni nini watu hao wanaowatamani walichokifanya mpaka wakafanikiwa na wao kufuata hatua zile zile, siyo kutafuta njia za mkato(shortcut) ili kuwa kama wao siku moja au mbili.

Huo mda wa kuigiza kuwa kama mtu fulani ni bora ukautumia kufanya kazi(HAPA KAZI TU) ili baadae uje uwe kama huyo mtu unayetamani kuwa kwa kupitia vigezo vyako utakavyovifuatilia kila siku bila kukosa.

SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.

Je na wewe ungependa kusema HAPANA(NO) kwa vitu vingi zaidi visivyokuwa na tija maishani kwako ili upate muda zaidi wa kutimiza ndoto zako maishani? Basi jiunge nasi kwa kupata Programu zetu zote zilizokwishaandaliwa tayari katika mifumo ya vitabu, PDF, Group la whatsapp na makala nzuri za kuelimisha.

Kuna njia kuu tatu(3) za kupata vitu hivyo mbalimbali.

(1). UKILIPA SHILINGI ELFU 10(10,000);
Nakutumia Kitabu maarufu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, masomo yote, semina na michanganuo tuliyowahi kujifunza katika group letu la Michanganuo-online tangu mwaka juzi. Pia ukitaka kujiunga na Group hilo unajiunga na ikiwa hupendi basi hamna shida kwani kila kitu tunakutumia kwa njia ya email yako. Vitu hiyo ni pamoja na hivi hapa chini;

1.   Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

(2). UKILIPA SHILINGI ELFU 18(18,000);
Nakutumia kila kitu tulichokuwa nacho hapo juu namba 1 lakini pia panaongezeka vitabu viwili 2 vizuri, kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA: DUKA LA REJAREJA na kingine, MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA.


(3).HII NI MAALUMU TU KWA YULE AMBAYE HAKUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI SEMINA YETU WIKI ILIYOPITA.
Tarehe 20 mpaka 22 Machi mwaka huu kwenye Group la MICHANGANUO-ONLINE tulikuwa na semina: JINSI YA KUFANYA HESABU ZA MPANGO WA BIASHARA(Advanced one).

Watu wengi zaidi ya 200 kwenye group na katika email walishiriki semina ile na ilikuwa ni ya kufana sana. Wiki hii nimepokea maombi mengi ya kurudiwa kwa semina hiyo kwa baadhi ya wale walioikosa kwa sababu mbalimbali, lakini kwa kweli nasikitika sana kusema kwamba haitawezekana, ila tumetoa fursa moja tu adimu kwa yule anayeihitaji semina hiyo kwa dhati kwa gharama ileile ya offa ya sh. Elfu 10 ambapo atapewa pia na zile fursa nyingine zilizotajwa pale juu namba (1).

FURSA hii adimu kabisa itadumu kwa muda wa siku 2 tu, Jumamosi na Jumapili (tarehe 30 machi na tarehe 1 Aprili) mwisho. Baada ya hapo Masomo haya ya hali ya juu zaidi maarufu kama Semina ya Hesabu za Fedha katika mchanganuo wa biashara(Advanced Business Plan Financials) yatakuwa yakipatikana lakini kwa gharama kubwa ya sh. Elfu 30 bila offa ya aina yeyote ile.

Kwanini iwe gharama kubwa kiasi hicho?
Unajua Kipengele cha hesabu ndio Roho yenyewe ya mpango wa biashara, hivyo ukimaster kipengele hiki basi mchanganuo wa biashara yeyote ile katika lugha yeyote hauwezi kukubabaisha tena, hivyo masomo haya muhimu yamefanyiwa utafiti wa kina mno katika mazingira halisi ya biashara za Kitanzania, hamna namna yatakavyoweza kupatikana kwa gharama nafuu kuliko hii iliyotolewa ya offa katika siku hizi 2.

Ikiwa unahitaji, Lipia leo au kesho upate na zile offa pale namba 1 zote papo hapo kwenye simu, kompyuta au Tablet yako. Namba zetu za simu ni 0712202244  au  0765553030

WASAP: 0765553030
Peter Augustino Tarimo

Self help books Tanzania.

0 Response to "WANAOFANIKIWA MAISHANI WENGI HUSEMA ‘NO’(HAPANA) KWA VITU HIVI 3"

Post a Comment