Ni takribani miaka saba 7 sasa imepita tangu niandike
kitabu changu kijulikanacho kama MIFEREJI SABA YA PESA NA SIRI MATAJIRIWASIYOPENDA KUITOA. Kitabu hiki wakati huo kiliwasisimua watu wengi sana
ukizingatia ukweli kwamba kabla ya hapo na hasa siku za nyuma kulikuwa na usiri
mkubwa juu ya maisha na hata historia za utajiri wa watu mbalimbali.
Matajiri wengi nchini Tanzania hawakupenda kabisa mambo
yao kujulikana hadharani na pengine waliogopa kufanya hivyo, si ajabu Tanzania
kwa kipindi kirefu tumekuwa na Mabilionea wengi tu bila ya kujulikana mpaka
pale jarida mashuhuri la FORBES walipoanza kuja kuwafuatilia na kuwaweka wazi
mabilionea wa mwanzo mwazno wakiwamo kina Dr. Reginald Mengi, Said salim
Bakhressa, Mohamed Dewji, Alli Mafuruki
na Rostam Azizi.
![]() |
KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA |
Inawezekana kulikuwa na sababu kadhaa zilizowafanya
matajiri wengi kutokupenda habari zao ziwe hadharani sana na kubwa ikiwa ni ile
ya nchi yetu kuwa katika mfumo wa KIJAMAA wakati ule lakini kusema ule ukweli
baadhi yao na hasa Mzee wetu Reginald Abraham Mengi yeye hakuogopa kabisa
kuweka mambo yake hadharani tokea mwanzoni kabisa na hii ndio iliyonipa motisha
mkubwa kabisa wa kukiandika kitabu hicho baada ya kuona kwamba Dr. Mengi na
baadhi ya Matajiri hao walikuwa wameshaanza kuwa na moyo ule wa kujiweka wazi.
SOMA: Vijana wanaosubiri mifumo iliyowekwa iwasaidie kujikwamua kiuchumi wataendelea kubaki kuwa watumwa wa maamuzi ya watu wengine - Dr.Mengi
SOMA: Vijana wanaosubiri mifumo iliyowekwa iwasaidie kujikwamua kiuchumi wataendelea kubaki kuwa watumwa wa maamuzi ya watu wengine - Dr.Mengi
Tokea miaka ya 90, 1992, 1993 na kuendelea Dr. Reginald
Mengi alikuwa tayari amekwishaanzisha matamasha ya kuwahamasisha watu hasa
vijana kujiunga katika vikundi na kuanzisha makampuni mbalimbali huku yeye
binafsi akiwapa kianzio cha fedha taslimu pamoja na kuwatia moyo wa hali ya juu
kabisa kama vile kuwahamasisha kwa kaulimbiu zake maarufu za, “ MSIOGOPE
KUKOPA" “KAMWE USILOGWE UKALA PESA YA MTAJI” “USIKATE TAMAA” “MSIOGOPE
CHANGAMOTO” “PENYE CHANGAMOTO NDIPO PALIPOKUWA NA FURSA” nk.
SOMA: Mengi, "Nilianza sina kitu niliona fursa nikakopa fedha, nikaanza kufanya biashara"
SOMA: Mengi, "Nilianza sina kitu niliona fursa nikakopa fedha, nikaanza kufanya biashara"
Hamasa hiyo kubwa ilinifanya hata katika Dibaji ya kitabu
changu hicho cha MIFEREJI 7 YA PESA kuamua kuandika kama ifuatavyo;
SHUKRANI
Kwa
Wazee wangu na washauri, Reginald Mengi na Said Salim Bakhresa pia na kwa
kijana mwenzangu Mohamed Dewji, kwa mioyo yao iliyojaa ukarimu, watu hawa
kusema ukweli walinifanya nipate hamasa na msukumo mkubwa katika kukiandika
kitabu hiki. Kama wangelikataa taarifa zao zisisambazwe na vyombo mbalimbali
vya habari ikiwemo Forbes, sifikiri kama ningeliweza kukiandika kitabu hiki kwa
jinsi nilivyokiandika. Mchango wao katika kuhamasisha kuukataa umasikini kwa
vijana wa Kitanzania na hata makundi mengineyo katika jamii kwa hakika ni mkubwa
kushinda hata kama ambavyo wangeliamua kuwagawia pesa mkononi.
Shukrani pia ni kwa wafanyabiashara wengine waliotajwa katika kitabu hiki, Rostam Aziz na Ali Mufuruki, na wao pia kama walivyo hao watatu niliotangulia kuwataja, wangeliamua kufanya utajiri wao kuwa siri, watu tusingeliweza kuwajua na kupata hamasa kubwa kutoka kwao, wamekuwa pia mifano ya kuigwa(mentors) kwa Watanzania wengi. Mwisho lakini kwa umuhimu ndiyo wa kwanza, ni kwa familia yangu pendwa, kwa uvumilivu wao ambao muda wote wamekuwa wakiuonyesha kwangu ninapokuwa nikifanya kazi hii ya uandishi hata pale ninapokuwa nikiifanya pasipo kuwa na uhakika wa malipo mazuri.

Na kwa kweli tangia miaka hiyo sasa tumeshuhudia Matajiri
wengi wakiweka wazi siri zao, siri hizo nilizokuwa nikimaanisha hapa si
nyingine kama wengi walivyodhania bali ilikuwa ni mbinu mbalimbali za mfafanikio.
Mtu aliyefanikiwa anapoamua kuwashika mikono watu wengine kwa hali na mali hasa
kwa kuwapa njia za wao pia kufika mbali
hata kama siyo pesa taslimu mikononi, hiyo inatosha kabisa kusema kwamba mtu
huyo amekubali kutoboa siri zake za mafanikio na kuwapa watu wengine nao
wafanikiwe kama yeye au tu hata waweze kuishi maisha yaliyokuwa na unafuu
badala ya kuishi maisha ya umasikini uliotopea.
MZEE
MENGI SIRI ZA UTAJIRI WAKE ALIMWACHIA NANI? JE NI MKEWE JACQUELINE, WANAWE,
ABDIEL NA REGINA, MAPACHA WAKE 2, AU WALINZI WAKE?
Siri za utajiri wa Dr. Reginald Mengi kusema ukweli
hajaanza kuzitoa leo, jana wala juzi, kama nilivyotangulia kusema Dr. Reginald
Mengi alikuwa ni mtu muwazi aliyeamini katika Sera za KILIBERALI, jambo
lililosababisha hata kutokueleweka vizuri wakati huo na Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere.
SOMA: Mzee Reginald Mengi hajafa, ataendelea kuishi katika mioyo yetu siku zote
SOMA: Mzee Reginald Mengi hajafa, ataendelea kuishi katika mioyo yetu siku zote
Uliberali tofauti na ulivyokuwa Ujamaa, sera zake ni za
soko huria, huna haja ya kujifichaficha ilimradi tu huvunji sheria za nchi na
wala humdhulumu mtu tofauti na vile ilivyo kwa Ujamaa ambao, unahubiri vizuri
usawa wa binadanu wote lakini nyuma ya Pazia kwa kuwa wanadamu tuna silika ya
umimi, ubinafsi na uchoyo basi dhana hiyo inakuwa ngumu kweli kutekelezeka, na
hatimaye kunaibuka wajanja wachache humohumo kwenye ujamaa wanaojinufaisha kwa
migongo ya wavujajasho walio wengi.
Hili lilikuja kujidhihirisha pale Ujamaa aliouanzisha
Mwalimu Nyerere kwa nia njema tu kuja kuanguka miaka ya 80 na Soko huria
kushika kasi yake mwanzoni mwa miaka ya 90. Hivyo nilitaka tu kuweka wazi
umuhimu wa Ukweli na Uwazi katika maswala ya kiuchumi jambo ambalo Mzee
Reginald Mengi amekuwa akilihubiri tangia miaka ya 70 mpaka hivi leo
tunapomuaga rasmi kwa safari yake ya mwisho.
SOMA: Dr. Mengi atoboa siri za biashara.
SOMA: Dr. Mengi atoboa siri za biashara.
Ukitaka kufahamu kwa kina falsafa hii ninayojaribu
kuizungumzia hapa leo, nakushauri tu kukisoma kitabu alichotuachia kama zawadi
Marehemu Mzee Reginald Mengi, I CAN, I MUST, I WILL The spirit Of Success
sehemu pekee ambamo Dr.Mengi ndimo alipoacha SIRI zake zote nzito za mafanikio.
Siri hizo hajamwachia mtu mwingine yeyote yule, si mkewe kipenzi Jacqueline
Ntuyabaliwe aliyempenda sana wala wanaye, Regina, Abdiel, mapacha wake 2, wala
si walinzi wake, wapishi wala mfanyakazi mwingine yeyote yule ndani ya kampuni lake kubwa la Industrial Projects
Promotion(IPP). Ni ndani ya I CAN, I MUST, I WILL The spirit Of Success, kitabu atakachokumbukwa nacho milele.
............................................................
Kupata vitabu vya Self Help Books Tanzania katika lugha ya kiswahili tembelea, SMART BOOKS TANZANIA
Kujiunga na MASTER MIND GROUP la MICHANGANUO-ONLINE, mahali ambapo watu makini hujifunza na kushirikishana mambo mazuri kila siku lipia kiingilio sh. elfu 10 kisha tuma ujumbe WASAP wa "NIUNGANISHE NA GROUP LA MASOMO" kwa namba, 0765553030

0 Response to "Bilionea DR. Reginald Mengi hakufa na siri yeyote moyoni, unajua siri zote alimwachia nani?"
Post a Comment