Wiki hii tumefululiza safu ya Ongea
na mshauri na lengo langu ni kuhakikisha nayajibu maswali yote ya wadau
niliyoyaweka kiporo ndani ya wiki hii. Msomaji mwingine jina lake kwa kifupi
O.S aliuliza swali lake kama ifuatavyo;
Kaka mi n mfanya biashara
ya duka la vyakula Ila c biashara yngu n ya mama angu... Ndoto yngu Ni kuwa
mfanya biashara Na kutengeneza utajiri kupitia biashara Ila tatizo nililokuwa
nalo nashindwa jinsi ya kuweka Malengo yngu binafsi Na hii biashara nnayofanya...
Naomba msaada wako kwenye hili kaka
Hellow Mr. O.S,
Mahali popote pale unaweza ukajiwekea malengo bila kujali ni
biashara ya kwako, ya mtu baki au ya ndugu wa karibu kama mama yako. Nadhani
tatizo kubwa hapo unahisi kwa vile biashara ni ya mama, basi huwezi ukajiwekea
malengo, ni kama vile anakubana hivi nk. Lakini nikuambie haipaswi kuwa
hivyo.
SOMA: Biashara ya mitindo ya nguo za kiume na viatu inavyoweza kukutajirisha.
SOMA: Biashara ya mitindo ya nguo za kiume na viatu inavyoweza kukutajirisha.
Wewe kaa na mama yako mwelezo malengo yako ni yapi, kisha
mpange mkiwa wawili unataka baadae ufanye nini nk. Weka muda maalumu utakaokaa
katika biashara hiyo pamoja na malipo unayotaka biashara hiyo ikulipe. Ukweli
kwamba biashara ni ya mama yako hauwezi kukufanya usidai malipo kama mtu baki
ilimradi tu yaendane na uhalisia wa biashara yenyewe, ule ukaribu wako na mama
usikubali ufanye kazi bila malipo, biashara na undugu ni vitu 2 tofauti kabisa.
Hebu tengeneza mazingira kama vile unafanya biashara na mtu baki kabisa na siyo
mama yako.
Na hii itasaidia biashara hiyo pia kukua kwani utakuwa na
nidhamu huku ukijua unalipwa kama mtu mwingine yeyote yule baki. Ni kwa njia
hiyo tu utaweza ukajiwekea malengo na si vinginevyo huku pia malengo ya mama
yako katika hiyo biashara nayo yakitimia bila kuathiriwa kwa namna yeyote ile.
SOMA: Je,unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara mbili ya mtaji utakaowekeza?
SOMA: Je,unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara mbili ya mtaji utakaowekeza?
Malengo yeyote yale yanahitaji pesa(fund) sasa utatimizaje malengo yako pasipo kuwa na fedha?
Ukiisimamia vizuri hii biashara ya mama yako nayo ikakulipa vizuri hatimaye
utaweza ukaja kutimiza malengo yako mengine ya kimaisha baadae kwa urahisi
zaidi kwani utakuwa na fedha za kufanya hivyo.
Bila shaka yeyote ile mama yako ndiyo mtu wa kwanza kabisa
katika maisha yako anayependa ufanikiwe, hivyo na wewe usikubali kumwangusha,
akijua una malengo ya kufika mbali sidhani kama atapenda usiyatimize, lakini ni
kwa njia ya kuiboresha biashara hiyo kwanza ndipo mambo mengine yataweza kunyooka
na siyo vinginevyo.
Hata ikiwa kwa mfano duka hilo halitaleta fedha za kutosha
kugharamia mipango yako mingine kama utakavyotaka, lakini angalau fanya kwa
uaminifu na kwa kujituma kwanza, muda ndio utakaosema wenyewe kwani itafika
mahali kama hakieleweki utamwambia mama "Mother, mimi naona bwana nikahangaike kwingine, tutafute utaratibu
mwingine wa kusimamia hili duka" Hapo mama atakuelewa na atakupa baraka
zake zote na hata kusapoti chochote kile utakachokwenda kukifanya mbele ya
safari yako.
SOMA: Biashara ya urembo inalipa, ni ya pili kutoka haraka baada ya chakula, ni fursa kubwa!
SOMA: Biashara ya urembo inalipa, ni ya pili kutoka haraka baada ya chakula, ni fursa kubwa!
Inawezekana wewe ndoto yako si kuuza duka la vyakula la rejareja, labda
ndoto yako ni kufanya biashara ya duka la nguo za mitumba na spesheli au
umejiwekea malengo ya kwenda kufanya biashara ya urembo, tena uimiliki
mwenyewe. Au hata umepanga kujiendeleza zaidi kimasomo nk. Malengo haya yote
utaweza kuyatimiza tu endapo utakuwa na subira na uvumilivu wa kutosha, kumbuka
duniani hakuna biashara yenye faida ya haraka haraka bila kwanza kuweka misingi
imara.
Asante, natumaini majibu haya yatasaidia.
............................................................
Kwa vitabu vyako Bora kabisa kutoka self help books Tanzania tembelea, SMARTBOOKSTZ
Kupata masomo ya fedha na michanganuo kila siku Whatsapp, karibu ujiunge na group la Michanganuo -online, 0765553030 kwa kiingilio cha sh. 10,000/= mwaka mzima.
............................................................
Kwa vitabu vyako Bora kabisa kutoka self help books Tanzania tembelea, SMARTBOOKSTZ
Mimi natamani sana kufanya biashara lakin sina mtaji nisaidieni wenye mitaji mikubwa hata Mimi natamani niwe mfanya biashara mkubwa,napenda sana lakin mtaji sina.Muwezeshe mwanamke kwa ukombozi wa jamii nzima
ReplyDeleteMimi natamani sana kufanya biashara lakin sina mtaji nisaidieni wenye mitaji mikubwa hata Mimi natamani niwe mfanya biashara mkubwa,napenda sana lakin mtaji sina.Muwezeshe mwanamke kwa ukombozi wa jamii nzima
ReplyDelete