Huwa najibu maswali mafupi mafupi toka kwa wasomaji wa
blogu hii na wafanyabiashara ndogondogo za mtaji mdogo au wale wa kati. Ni kawaida
swali likitumwa kwetu huwa hatubadilishi chochote hata speling na tunaliweka hapa kama lilivyoulizwa isipokuwa tu hatuwezi
kutaja utambulisho kamili wa muulizaji pasipo kuwa na idhini yake. Leo katika swali lililotufikia mezani ni hili
lifuatalo, Nataka kuacha kazi nianzishe
biashara kwa mtaji wa milion 5 hadi10: nishauri nianze biashara ipi?
Kwa kirefu swali hilo linasomeka
hivi;
SWALI.
Kiukweli mim kwa umri niliofikia hadi kukua
kwangu sijawahi kuuza hata pipi kwahyo sina idea ya biashara wala uzoefu wowote
kuhusu biashara na Nina mpango niachane na kazi ninayoifanya nianzishe biashara
kwa mtaji wa wastani wa chini ya million 5 au zaid ya hiyo lakin haitazid 10,
lakin hadi saiv kila nikuliza watu biashara ambazo zinaweza zikalipa wananambia
biashara tofauti tofauti wengine mazao wengine duka wengine grocery sasa kwa
ushauri wako kwa mtu ambae hana uzoefu kabisa na biashara unampa mwongozo gani?
MAJIBU.
Kwanza ni vizuri
usichukue ghafla uamuzi wa kuachana na kazi unayoifanya kabla hujawa na uhakika
na biashara utakayoifanya.
SOMA: Je, ajira ni jambo baya, utumwa na kukosa malengo?
SOMA: Je, ajira ni jambo baya, utumwa na kukosa malengo?
Cha pili ni kwamba
biashara ya kuanza pamoja na kupokea maoni, ushauri na maelezo toka kwa watu
mbalimbali nikiwemo na mimi, lakini uamuzi wa mwisho utoke moyoni mwako.(Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako) Hapo ninamaanisha kwamba hakikisha
ukianzisha biashara angalia ile ambayo una moja kati ya vitu vifuatavyo, au
viwili au vyote ikiwezekana kuwa navyo vyote;
1.
Una mapenzi nayo.
2.
Una uzoefu nayo.
3.
Una ujuzi nayo.
4.
Ni hitaji muhimu kwa
watu na wanalihitaji kwelikweli, kwa maana nyingine ni biashara yenye soko
kubwa na la uhakika kwa asilimia nyingi.
Ukishachagua biashara
yenye moja ya sifa nilizotaja, ianze kwa kiwango kidogo(anza biashara na mtaji mdogo
kwanza), wakati bado hujaachana na kazi au shughuli unayoifanya sasa
ili kupima kama ina uwezo wa kukufanya uishi kwa kuitegemea muda wote(full
time) Hapa unafanya utafiti kwa vitendo na wala siyo kinadharia tena.
Baada ya hapo
ukishagundua biashara hiyo ni ya uhakika angalao inaleta faida hata usipopata
mshahara 'itakuweka mjini' basi ndipo uachane rasmi na kazi unayoifanya.
Kuanza biashara ndogo kwa mtaji mdogo hakumaanishi kwamba biashara hiyo unalenga
iwe ndogo siku zote hapana, unafanya hivyo huku maono yako yakiwa ni kuja
kuifanya iwe biashara kubwa baada ya kuachana na ajira kwa kuongeza mtaji uwe
mkubwa zaidi pamoja na muda wako wa kutosha.
SOMA: Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na kwanini uweke malengo makubwa maishani.
SOMA: Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na kwanini uweke malengo makubwa maishani.
Hata baada ya kumpa
msomaji wangu huyu majibu hayo bado hakuridhika akaendelea kutaka kujua zaidi
kwa kuniuliza kama ifuatavyo;
“OK nimekuelewa vizuri kiongozi lakin sasa ili
ujue biashara inalipa au hailipi mi najua inatakiwa uisimamie mwenyewe ili ujue
faida na hasara zake halaf kama ndo unamuachia mtu umuachie huoni kama hilo
swala LA kuacha kazi litakuwa na uzito ili nijue faida na hasara ya biashara
nitakayoianzisha”
MAJIBU:
Ndio maana nimesema
lazima kwanza ufanye utafiti wa kutosha wa kulithibitisha wazo lako la biashara
kivitendo kama linalipa kabla hata haujaacha kazi kwani kuna takwimu za
biashara nyingi kufa ndani ya muda mfupi mara tu baada ya kuanzishwa.
Kinachosisitizwa zaidi
hapo ni ule uwezo wa kuhimili gharama za maisha wakati ukiitengeneza biashara
yako ili isimame. Kumbuka kuwa ukianzisha biashara leo kuna kipindi fulani
kitapita hata miezi 6 na zaidi kabla haijaanza kutengeneza faida.
SOMA: Jinsi ya kufanya utafiti wa biashara yako/upembuzi yakinifu.
SOMA: Jinsi ya kufanya utafiti wa biashara yako/upembuzi yakinifu.
Ikiwa unacho kianzio,(mtaji
wa kutosha) utakaoweza kutenga hapo kiasi cha matumizi yako ya kila
siku pasipo kutegemea hiyo biashara basi hamna shida sana juu ya kuachana na
kazi na kuelekeza nguvu zako zote kwenye hiyo biashara.
Ila kama mtaji wa biashara yako ni mdogo, ni bora
ukafuata hiyo njia ya kuanza biashara katika levo ndogo ukiwa bado na ajira
yako lengo likiwa si kutengeneza faida kubwa bali network, soko na uzoefu wa kiasi fulani ili baadae ukiacha kazi uwe
unajiamini zaidi na biashara yako.
Unaweza hata ukaanza
katika levo(hatua) ambayo si ya kumwajiri mtu, just unaifanya katika muda wako wa ziada na ikiwa utaweka mtu basi
uhakikishe ni lazima ‘unacontrol’
mahesabu ya biashara yako kikamilifu(
effectively ) muda unapokuwa nje ya ajira yako. Na kwa kuwa nimeshakuambia
utaanza biashara kwa kiwango kidogo sana mwanzoni(biashara ndogo kwa mtaji kidogo), bila shaka kusimamia hesabu
haitakuwa kazi ngumu sana kwako, nusu saa au lisaa kwa siku itatosha kabisa,
ili mradi usipitishe hata siku moja bila kujua hesabu za biashara yako
zinaendaje, ni nini kimeingia na ni nini kimetoka, nani anadai na ni nani
anadaiwa.
SOMA: Jinsi ya kusimamia hesabu katika biashara ndogo unayomwachia mfanyakazi.
SOMA: Jinsi ya kusimamia hesabu katika biashara ndogo unayomwachia mfanyakazi.
Kumbuka katika levo
hiyo utakuwa haupotezi chochote kwani bado unao uhakika kazini(kwenye ajira yako), na katika biashara
yako pia unaendelea kupata ‘exposure’
kubwa hata kama hupati faida kivile. Lakini ‘at least una gain experience’
na kujua ni kitu gani kinachofanya kazi na kipi hakifanyi kazi.
Pia katika hatua hii
ya majaribio kwenye biashara, “usicheke na kima tafadhali”, hapa
kucheka na kima namaanisha kwamba usije ukamvumilia mtu yeyote atakayeonyesha
daliki zozote za kuihujumu biashara yako ndogo hasa yule pengine utakayemwachia
akuangalizie biashara muda haupo. Kuwa strictly sana kwani hapo ndipo
palipo na mtihani mkubwa kwa mtu yeyote yule anayeanza biashara mpya.
Kwakuwa huna cha
kuhofia, ajira yako ipo 'intact' hujaiacha bado, usimbembeleze
sana mtu kupita kiasi, akionyesha dalili kidogo tu za kuzingua mwambie kwaheri asijekukuharibia msingi wako bure, ndio
maana nimetangulia kusema kwamba katika stage
hii unaweza hata kuifanya muda wako wa ziada baada ya kazi kwani lengo lako kuu
hutafuti faida, bali uzoefu na uwezekano wa kupata faida baadae endapo utaamua
kuifanya full time kwa mtaji na muda wa kutosha.
SOMA: Jinsi gani naweza kutengeneza pesa kwenye mradi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti?
SOMA: Jinsi gani naweza kutengeneza pesa kwenye mradi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti?
Inamaana kwamba hiyo
biashara unaweza kuwekeza kiasi kidogo kwanza cha fedha kama biashara ya mtaji
mdogo, mfano umesema una kama milioni 5 hivi, wekeza kwanza labda milioni 1 zingine ziweke mahali(benki) zitulie tuli.
..................................................................
Ndugu msomaji wangu kama unamiliki biashara ya rejareja hususan Duka la vyakula mtaani au una ndoto ya kuanzisha biashara ya rejareja siku moja, nakushauri usikose kupitia kitabu kifuatacho japo kurasa mbili au tatu tu za mwisho ambazo kuna Mfumo maalumu unaomwezesha mmiliki wa duka la rejareja kusimamia kwa ufanisi mkubwa biashara yake, mfumo huo uitwao, "TWO IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM" umebuniwa kitaalamu kwa ajili ya kuhakikisha msaidizi au mfanyakazi hadokoi hata senti tano huku mmiliki akifanya majukumu yake mengine bila kuumiza kichwa.
..................................................................
Ndugu msomaji wangu kama unamiliki biashara ya rejareja hususan Duka la vyakula mtaani au una ndoto ya kuanzisha biashara ya rejareja siku moja, nakushauri usikose kupitia kitabu kifuatacho japo kurasa mbili au tatu tu za mwisho ambazo kuna Mfumo maalumu unaomwezesha mmiliki wa duka la rejareja kusimamia kwa ufanisi mkubwa biashara yake, mfumo huo uitwao, "TWO IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM" umebuniwa kitaalamu kwa ajili ya kuhakikisha msaidizi au mfanyakazi hadokoi hata senti tano huku mmiliki akifanya majukumu yake mengine bila kuumiza kichwa.
Bei ya kitabu cha karatasi(hardcopy) ni sh. 12,000/=, tunakuletea ulipo Dar, mikoani ongeza gharama ya basi.
Bei ya kitabu(nakala tete) softcopy ni sh.5,000/=
Kwa mahitaji: Whatsapp, 0765553030 au simu, 0712202244
0 Response to "Nataka kuacha kazi nianzishe biashara kwa mtaji wa milion 5 hadi10 nishauri nianze biashara ipi?"
Post a Comment