SEHEMU YA 1
Katika email za wasomaji wa makala zangu
nimewahi kukutana na maswali mengi ambayo baada ya kuyachunguza nimekuta yote
yalihitaji jibu moja linalofanana. Leo nimeamua kutoa majibu kwa swali hilo na
hapa chini nitatumia swali la mmoja wao kama lilivyotumwa na msomaji kutoka
Songea Mkoani Ruvuma. Aliuliza hivi;
“Kila nikitaka kuwa tajiri nashindwa, lakini
nashangaa kuona kuna wengine hufanikiwa kutajirika kirahisi tu, tafadhali
naomba kujua ninakosea wapi? A.J Mbawala.
Ili kuweza kulijibu swali hilo, ilinibidi
nitafute kwanza kiini cha watu kuwa masikini ni nini na ni sababu ipi
inayowafanya kuendelea kubakia katika umasikini huo. Sababu kubwa niligundua
kwamba masikini huwa hatujui jinsi ya kusimamia pesa zetu vizuri ili tuwe
matajiri. Masikini hufikiria kwamba ili mtu atajirike ni lazima kwanza awe
anaingiza kiasi kikubwa sana cha fedha lakini hiyo si kweli hata kidogo.
SOMA: Biashara nzuri ya kuanzia unapotaka kuwa tajiri na kufikia uhuru kamili wa kifedha.
SOMA: Biashara nzuri ya kuanzia unapotaka kuwa tajiri na kufikia uhuru kamili wa kifedha.
Ukweli ni kwamba ili mtu aweze kutajirika ni
lazima kwanza aweze kuwa na UHURU WA KIFEDHA. Ni baada tu ya mtu kuwa huru
kifedha ndipo huanza kutengeneza pesa bila ya kutumia tena nguvu nyingi na
hivyo kumfanya aweze kuendelea kuwa tajiri zaidi na zaidi. Hii kwa maneno
mengine tunaweza tukasema kwamba kutegemea kipato cha siku hadi siku katika
kukidhi tu mahitaji yale ya msingi pasipo kuwekea hata kidogo husababisha watu
wengi tuendelee kulia na umasikini siku zote.
Kutajirika
siyo kazi rahisi.
Kutajirika ni kazi ngumu lakini hii zaidi ni
kwa watu wale tu wa tabaka la chini na la kati kama mimi na wewe, siyo kwa
matajiri. Muhimu zaidi ni kwamba kile watu wa tabaka la chini na la kati
wanachokifanya katika shughuli zao za kila siku za kimaisha ndicho
kinachowafanya waendelee kubakia kuwa masikini na wala si kana kwamba kuwa
kwenye hayo matabaka ndiko kunakowafanya masikini. Watu masikini pia hujitahidi
kufanya kazi kwa nguvu sana lakini bado tu wanaendelea kuwa masikini.
SOMA: Kuwa Bilionea naweza kutumia njia zipi?
SOMA: Kuwa Bilionea naweza kutumia njia zipi?
Sababu kubwa ni utegemezi wa kipato cha siku
hadi siku au mwezi hadi mwezi. Kutegemea kipato cha siku hadi siku au mwezi kwa
mwezi ni sawa na mtoto mdogo kuwa na tabia mbaya. Ni vigumu sana kwa mfano mtoto
mwenye tabia mbaya ya kuiba sukari kwenye kopo au mboga jikoni kuacha, hili
ndilo huwafanya masikini wawe kama walivyo.
Hivyo hatua ya mwanzo kabisa kuelekea uhuru wa kifedha ni
kwa mtu kuanza kupunguza utegemezi kwenye kipato chake cha mwezi au cha siku.
Kivipi sasa? Kuna njia mbili(2) za
kufanya hivyo;
1. Kuondokana
kwanza na madeni yote mabaya
2. Kuanzisha
vitegauchumi kwa kutumia rasilimali zinazoingiza kipato
Kipato kitokanacho na vitegauchumi(miradi)
hiyo ni lazima kiwe na uwezo wa kuendesha maisha yako. Hata kama kipato chako
cha siku au mwezi kitakoma, vitegauchumi hivyo vinatakiwa viweze kukufanya
maisha yaendelee bila wasiwasi. Ninapozungumzia kipato cha siku hadi siku au
mwezi hadi mwezi namaanisha kile kipato tunachokipata aidha kutokana na kazi
zetu au kutokana na biashara zetu za kawaida za kila siku, siyo vitegauchumi
vile vya pembeni.
Njia ya kuondoka kwenye umasikini na kuelekea
kwenye uhuru wa kifedha ni ngumu na ni ngumu kwasababu wengi wetu hatujui NAMNA
YA KUFIKA PALE, na zaidi ni kwamba wengi wala hatufahamu ni nini maana ya Uhuru wa kifedha. Walimu
wetu, wazazi, marafiki zetu wote pia
hawakujua ni nini maana ya uhuru wa kifedha. Kwahiyo siyo ajabu hata
kidogo kwamba na sisi pia tumejikuta hatujui maana ya falsafa hii ya Uhuru wa
kifedha. Mtu masikini anapenda kuwa tajiri lakini haelewi chochote kuhusiana na
uhuru wa kifedha. Mtu kama huyo hawezi kamwe kutajirika.
Watu wanaotajirika haraka kwa kushinda bahati
na sibu mara nyingi wengi hujikuta wamerudia tena kuwa masikini wa kutupa
kwasababu unakuta hawana uelewa na dhana hii ya uhuru wa kifedha. Ikiwa mtu
anajua basi huwa hawezi kurudi tena kuwa masikini baada ya kushinda. Hii ndiyo
sababu ni kwanini mtu wa kawaida kutajirika inakuwa vigumu kiasi hicho.
SOMA: Mambo 8 ya kipekee yanayowapa watu furaha ya kweli, je pesa ipo?
SOMA: Mambo 8 ya kipekee yanayowapa watu furaha ya kweli, je pesa ipo?
Lakini mara tu mtu anapotambua umuhimu wa
Uhuru wa kifedha, safari yake kuelekea Utajiri huanzia hapo. Simulizi za safari
za watu wengi walivyotoka kwenye umasikini mpaka kuwa matajiri ni za kusisimua
mno, njiani walikutana na vikwazo vingi lakini msisimko, furaha na shauku kali
ya kutoboa na kuwa tajiri viliwafanya waendelee kupambana.
Hebu jaribu kuvuta picha, umenasa katika
handaki lililojaa giza nene kwa miezi kadhaa lakini ghafla kule unakoelekea
unaiona miali hafifu ya mwanga, sasa angalao unapata matumaini kuwa pengine
unakaribia njia ya kutoka nje ya lile handaki kuliona tena jua baada ya miezi
mingi ndani yake ukitembea gizani huku ukila tandu, mende na wadudu wengine
watambaao utadhani ni komandoo Check noris vile katika moja ya muvi zake kali….
Uhuru
wa kifedha ni sawa na miali hafifu ya mwanga wa matumaini kwenye handaki la
giza nene(Umasikini)
Hatimaye utatufikisha kwenye nchi kavu
salama(nje ya handaki) ambalo ndilo lengo letu kuu la kutajirika. Kila hatua ndogo(ya
ukuaji wa vitegauchumi vyetu) utazidi kutufikisha karibu zaidi na mlango wa
kutokea nje ya handaki.
SOMA: The sky is very wide, every star can shine(Mbingu ni kubwa mno kila nyota inaweza kung'ara.
SOMA: The sky is very wide, every star can shine(Mbingu ni kubwa mno kila nyota inaweza kung'ara.
Kadiri mtu atakavyokuwa na rasilimali
nyingi(Assets) katika miradi yake ndivyo pia atakavyokuwa karibu na uhuru wa
kifedha. Na mara tu tutakapoufikia uhuru wa kifedha, hakuna kitu chochote kile
kitakachoweza kutuzuia kuwa matajiri.
Anza safari yako leo kuelekea uhuru wa
kifedha. Mahali pa kuanzia itakuwa ni kufahamu kwanza ni kwanini masikini
wanaendelea kuishi na umasikini. Kuondoa sababu hizo kunatakiwa kuwa ndio kitu
cha kwanza kabisa kwenye safari hiyo.
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.
Nilipenda nizitaje kabisa sababu hizo hapa
katika makala hiihii lakini naona itakuwa ndefu sana, sipendi kukuchosha hivyo
nakuomba sana mpenzi msomaji wangu usikose kufuatilia makala ijayo, nitaelezea
yale yaliyobaki hasa hasa sababu kubwa zinazowafanya masikini waendelee kubakia
kuwa masikini. Itakuwa ni part ii ya somo hili. ASANTE SANA!
……………………………………………………….
TAARIFA: KWA ANAYEHITAJI KUJIFUNZA ZAIDI
HII NI KWA YULE TU AMBAYE HAJAJIUNGA BADO
NA GROUP LA (WASAP MASTERMIND GROUP) LA MICHANGANUO-ONLINE AU KUSOMA VITABU VYA
SELF HELP BOOKS TZ
Najua wapo wadau ambao mmejiunga kwa email
hivi karibuni na hivyo hamjapata fursa ya kufahamu Programu zetu nyingine kama
wale waliotangulia, hivyo naomba kuchukua nafasi hii kidogo kuwajulisha
Programu hizo.
PROGRAMU#1
SELF HELP BOOKS TANZANIA tuna vitabu
mbalimbali vya ujasiriamali katika lugha ya Kiswahili na miongoni mwavyo ni
hivi vikuu vitatu.
1.MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
2.MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
3. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI
WASIOPENDA KUITOA.
Vitabu vyote 3 softcopy kwa njia ya email
ni sh. Elfu 18 na hardcopy kama upo Dar es salaam unaletewa ulipo kwa sh. Elfu
37. Unaweza kupata kimojakimoja pia. Ukinunua vitabu vyote 3 softcopy au
hardcopy unapata pia offa ya kujiunga na MASTERMIND GROUP la wasap bure pamoja
na michanganuo kadhaa na vitabu vingine 4(softcopy) bila malipo yeyote.
PROGRAMU#2
MASTERMIND GROUP LA WATSAP
Tunalo group la masomo na mijadala ya kila
siku WASAP ambalo tunajifunza hasa Vitu 2 kwa undani, Jinsi ya kuandaa
michanganuo ya biashara mbalimbali zinazolipa haraka pamoja na masomo yenye
maudhui ya pesa(MZUNGUKO WA FEDHA KWENYE BIASHARA ZETU). Ada ya kujiunga ni sh.
Elfu 10 tu mwaka mzima na punde baada ya malipo tunakutumia kupitia wasap au
email vitu vyote hivi vifuatavyo;
1. Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya
Kiswahili.
2. Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara
hatua kwa hatua.
5. Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN
kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI
CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili
na kiigereza
9. Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
10.
Vielezo(Templates) za
michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
11.
Mfumo mpya wa usimamizi wa duka
la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo
la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti
5
12.
Somo muhimu sana la mzunguko wa
fedha.
13.
Ukurasa mmoja wa mchanganuo.
PROGRAMU#3
PACKAGE NZIMA(kifurushi) cha semina kubwa
ya jinsi ya kuandaa hesabu za mpango wa biashara(ADVANCED BUSINESS PLAN
FINANCIALS) katika mfumo wa PDF. Bei yake ni sh. 10,000(Bado ipo kwenye offa,
baadae itarudia bei yake ya kawaida sh. elfu 20)
UKITAKA PROGRAMU ZOTE 3 KWA PAMOJA KATIKA SIMU, KOMPYUTA AU
TABLET YAKO NI SH. ELFU 38 TU.
ASANTE SANA,
PETER A. TARIMO
Wasap:0765553030
Simu: 0712202244
self help books Tanzania
0 Response to "WENGINE HUFANIKIWA KUWA MATAJIRI, MIMI NIMESHINDWA, NAKOSEA WAPI?"
Post a Comment