Baada ya kujibu swali la jana
kutoka kwa mdau wa group la MICHANGANUO-ONLINE kuhusiana na wazo
la biashayenye hatari ndogo mwajiriwa serikalini anaweza akafanya kwa mtaji wa
milioni 5, leo tutaendelea kusoma majibu ya swali la mdau mwingine
tofauti, huyu ni mwanachuo na alipenda kushauriwa biashara nzuri anazoweza
akafanya kwa mtaji wa laki mbili akiwa angali chuoni akisoma(Kusoma na
biashara). Swali lake kama alivyouliza naliweka hapa chini kama lilivyo bila
kuedit kitu;
“Habari
za jioni ndugu zangu, naitaji ushauri kutoka kwenu jamani,, mm nipo chuo dodoma
apa, ninataka nianzishe biashara na nina mtaji kidogo tu almost laki 2 je ni
biashara gani naweza kufanya kwa mtaji huu nilio nao??”
MAJIBU YA BIASHARA UKIWA CHUONI:
Kwa kweli hebu nivae
viatu vyako kidogo nikiwa na maana kwamba nitajifanya kama vile mimi ningelikuwa ndio wewe mwana
chuoni Leo hii(sasa).
Kwa kadiri ya muda wa
chuo/shule ulivyokuwa mchache(miaka 2 tu au 3) na ukilinganisha na umuhimu wa
malengo mtu unayokuwa nayo kimaisha ya kwenda pale chuoni, kwa kweli
ningeahirisha biashara nikomae kwanza na chuo ili niweze kufaulu vizuri.
Biashara nitaweza kuja
kufanya muda wowote ule nitakao lakini sio chuo, muda wa chuo/shule kama ni
mwaka 1, 2, 3 au 4 ukishapita bwana, ni kazi kwelikweli kuja kupata tena chance kama hiyo, tuulize sisi tuliopitia
huko tutakueleza.
Inawezekana kufanya
biashara ukiwa chuoni, kwa huo mtaji wa sh. laki 2 lakini itakulazimu kwanza
uapply kitu kinachoitwa "bootstrapping" Kufunga mkanda kwa kiwango
kikubwa ikiwa utataka huo mtaji usije kukata.
Sababu ni
kwamba, kwanza kiwango cha huo mtaji ni kidogo, hautaweza kununua bidhaa nyingi
za kuuza labda iwe utatoa huduma.
Sipendi kuondoa
uwezekano wa kufanya biashara ukiwa chuoni wala kukukatisha tamaa bali tu
ninachotaka ufahamu, ni changamoto mbalimbali na ile risk ya kukosa vyote 2,
elimu na biashara.
Hata hivyo bado wapo
watu walioweza kumudu kufanya biashara wangali chuoni japo siyo wengi sana. Na
kama nilivyosema wengi wao ilibidi wajitume sana ili waweze 'kucope' au kuendana na muda mchache waliokuwa nao. Kuna baadhi ya
biashara kama vile;
✍Kuuza airtime, miamala ya kifedha kama tigo pesa, Mpesa, Airtel
money, ezy pesa, TTCL money na Halo pesa. Unaweza ukaongeza na vitu, vifaa au huduma zinavyoendana na hivyo mfano, flash zenye ubora wa hali ya juu, kusajili laini za simu mitandao mbalimbali(uwakala wa makampuni ya simu) nk.
✍Kama unayo laptop, jinunulie kaprinta kako hata ka sh. laki
moja, kaweke bwenini na uwatangazie wenzako kwamba unaprint kwa bei poa kuliko
steshenari za jirani.
✍Tumia smartphone yako kuanzisha biashara yeyote ya mtandaoni
mfano ya kuuza nguo, au bidhaa yeyote ile kali unayojua unaweza kwenda kutuma
muda haupo kwenye masomo. Bidhaa hiyo unaweza pia hata kuwauzia wanafunzi
wenzako watakaopendezwa nayo. Unaweza hata ukaamua
kuuza simu.nk.
Usijali hata ikiwa utanunua bidhaa moja tu kwa hiyo laki mbili lakini inayouzika kirahisi na yenye faida. Njia mbadala pia unaweza ukatangaza
bidhaa fulani ambazo unajua pa kuzipata mjini au kokote kirahisi lakini wateja wako
hawajui namna ya kuzipata. Kisha wakioda wewe ndio unakwenda kuchukua na
kuwapelekea au kuwatumia. Tafuta kitu ambacho hakitakupa usumbufu wala kula
muda wako mwingi
✍ Unaweza pia ukajiunga
na moja ya makampuni ya network marketing(riferral marketing) yanayoaminika na yasiyokuwa na
viingilio vikubwa.
Kabla ya a kufanya biashara ukiwa chuoni, pima kwanza mazingira yako kikamilifu ukiona utaathiri
kwa kiasi kikubwa matokeo yako ya mwisho, ni bora ukavumilia huku ukijifunza
ujasiriamali mitandaoni kidogokidogo, utakuja kuwa na muda mwingi tu wa kutosha
hapo baadae wa kufanya biashara ya ndoto yako mpaka wewe mwenyewe ukose pa
kuupeleka.
Wahitimu wa chuo kikuu
|
Uhalisia wa mambo ni
kwamba, kutokana na muda kuwa mfupi mno na mambo yenyewe kuwa ni mengi, chuoni
hapawezi kuwa mahali unapoweza kutimiza malengo makubwa sana ya kibiashara ila
ni mahali unapoweza kujiwekea msingi wako wa kuja kufanya biashara hapo baadae
kwa kufanya biashara simple kama
nilizozitaja hapo juu na nyinginezo.
Lakini pia kujifunza kwa
kufuatilia programu rahisi kama zilivyokuwa hizi za kwetu, Self Help Publishers ambazo
zimekwishaandaliwa tayari na unaweza kujifunza ukiwa tu na muda wa ziada mbali
na ule wa masomo yako ya chuo.
Ikiwa huna muda wa kutosha unachoweza kukifanya ni kuendelea tu kuyahifadhi masomo yako hayo kwani yanahifadhika na uzuri pia tunalo group la kudumu la watsap la MICHANGANUO-ONLINE ambalo utaweza kuja kuwasiliana na admin muda wowote akutumie(program nzima) masomo yote in case labda umeyapoteza.
...............................................mwisho..........
Hakikisha hukosi vitabu vyako hivi vifuatavyo, kwa maelezo zaidi unaweza pia kutembelea; SMART BOOKS TZ
Watsap: 0765553030
Simu: 0712202244
KUJIUNGA NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE LIPIA KIINGILIO AMBACHO NI SH. ELFU 10, KISHA TUMA UJUMBE KWA WASAP 0765553030.
Ikiwa huna muda wa kutosha unachoweza kukifanya ni kuendelea tu kuyahifadhi masomo yako hayo kwani yanahifadhika na uzuri pia tunalo group la kudumu la watsap la MICHANGANUO-ONLINE ambalo utaweza kuja kuwasiliana na admin muda wowote akutumie(program nzima) masomo yote in case labda umeyapoteza.
...............................................mwisho..........
Hakikisha hukosi vitabu vyako hivi vifuatavyo, kwa maelezo zaidi unaweza pia kutembelea; SMART BOOKS TZ
Watsap: 0765553030
Simu: 0712202244
KUJIUNGA NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE LIPIA KIINGILIO AMBACHO NI SH. ELFU 10, KISHA TUMA UJUMBE KWA WASAP 0765553030.
0 Response to "BIASHARA NZURI 4 MWANACHUO ANAWEZA KUFANYA NA MTAJI WA LAKI 2 HUKU AKISOMA"
Post a Comment