Bado tunaendelea na
mfululizo wa majibu ya maswali kutoka kwa wasomaji na wadau mbalimbali
wanaofuatilia masomo yetu hapa katika blogu ya jifunzeujasiriamali, katika Mastermind
group la MICHANGANUO-ONLINE na pia katika mitandao mingine ya kijamii
tunakopatikana. Leo hii nayaweka maswali mawili yaliyoulizwa na wadau wawili
katika Group na nimeona si vibaya nikayashirikisha hapa. Kila swali nitaliweka
katika makala yake na la kwanza ni hili lifuatalo bila ya kuongeza wala
kupunguza kitu kama alivyouliza;
“Jaman
I have 5m,and I don't have any business idea”
MAJIBU:
Kwa kweli hatari(risk)
ndiyo kitu kikubwa huwaogopesha zaidi wafanyakazi kuanzisha biashara na
hili ni ukweli hawaogopi bure kwani biashara bila ya kuwepo mfumo imara wa
usimamizi ni bora kuacha kabisa.
Mimi binafsi kwa upande
wangu nina maoni yafuatayo;
Kwa kuwa hata ukisema
usubiri mpaka muda wa kustaafu ndipo uje uanzishe mradi sidhani kama ni uamuzi
bora. Vyovyote vile iwavyo ukitaka kuja kuepusha stress baada ya kustaafu ni
lazima sasa ujifunze biashara au miradi iliyokuwa na risk(hatari) kidogo ili uwekeze
humo hizo pesa zako.
Najua tayari kuna
mipango ambayo imeshawekwa na mwajiri kama vile mifuko ya mafao lakini bado
inatakiwa kujaribu aina nyinginezo za uwekezaji utakaokulipa zaidi.
Mbali ya kuwepo baadhi
ya biashara zenye hatari kidogo lakini pia hatari ya mradi au biashara yeyote
ile hupungua kadiri mtu anavyokuwa na uelewa au kujifunza zaidi juu ya biashara
husika wala haijalishi ni biashara ya aina gani, yaweza kuwa ni biashara ya
duka, biashara ya mazao, biashara ya kusafiri au kuagiza bidhaa nje ya nchi,
biashara ya mtandao nk.
Baadhi ya biashara
zilizo na kiwango cha chini cha hatari ni kama vile,
✍Uwekezaji kwenye hisa.
✍Akiba ya kudumu ya benki(fixed deposit account)
✍Uwekezaji kwenye ardhi na majengo(unaweza ukanunua pagala
ukalikarabati na kuweka wapangaji)
✍Kuna biashara pia kama hizi za mitandaoni unazoweza kuziendesha
bila kutegemea msaidizi, msaidizi wako anakuwa ni teknolojia pekee ambayo
haiwezi kukudokolea.
✍Mwisho ni kwamba unaweza kuanzisha biashara yeyote hata zile
zenye risk kubwa lakini hapa ukawa mjanja 'kutokutumbukiza mayai yako yote katika kapu moja.
Anza kidogo kabisa
huku ukilenga hapo baadae kukua taratibu kadiri siku zinavyosogea. Mfano Kama
ukianzisha mgahawa basi uwe mdogo kabisa kusudi iwe rahisi wewe kujua kwa
urahisi kila kitu kinavyoendelea, iwe ni kama vile mahali pako pa
kujifunzia(field) na sio kujali unapata faida kubwa hapana.
Kwakuwa unakuwa
umewekeza kiasi kidogo sana cha mtaji, hata itokee riski gani haitakuumiza
kichwa sana na itakuwa moja ya funzo kwako ili baadae ukijikita kisawasawa
katika biashara usijekukwama. Utakuwa umekwishajifunza mbinu za biashara
husika.
Ni biashara gani
uanze, hiyo ni lazima itakuwa kichwani mwako tu, hamna binadamu asiyekuwa na
vitu anavyovipenda au ujuzi fulani, hobi, passion na vitu Kama hivyo.
Ikishindikana kabisa wewe fikiria tu ni hitaji gani watu wanaokuzunguka
linawasumbua hawalipati vizuri au hawalipati kabisa na wangetamani
kulipata.
Ukisubiri watu wengine
wakupe mawazo ya biashara yaliyo vichwani mwao hayataweza kufanya kazi.
By the way usikirupuke
ukapoteza milioni 5 zako bure. Tulia ufikirie kwa umakini na ukipata wazo la
biashara lianze kwanza kwa kiwango cha chini kabisa pasipo kuathiri kabisa muda
wa ajira yako inayokuweka mjini kwa Sasa. Zipo biashara mpaka za mtaji wa laki
moja(natolea
mfano) unazoweza ukaanzisha hatimaye ukaweza kupata uzoefu.
.....................................................................
Programu zetu zote kubwa zinaendelea kama kawaida na usisite kuagiza PACKAGE inayokufaa muda wowote ule utakaohitaji zikiwa bado kwenye offa zake kwani ukifika muda muafaka bei zitabadilika na kupanda au OFFA husika kutokuwepo tena.
KIFURUSHI(PACKAGE) YA 1 (18,000/= au 37,000/=)
Vitabu 3, softcopy kwa sh. elfu 18 vyote 3 na Hardcopy sh. elfu 37
1. MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
2. MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
3. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA
Pamoja na kuunganishwa na grupu la wasap bure ukipenda
KIFURUSHI(PACKAGE) YA 2 (10,000/=)
Tunakutumia vitabu, michanganuo na masomo yote yafuatayo kwa gharama ya shilingi elfu 10 tu.(Vyote ni softcopy); Ukitaka pia unajiunga na group bure.
KIFURUSHI(PACKAGE) YA 3 (20,000/=)
Semina maalumu ya jinsi ya kufanya hesabu za mpango wa biashara(Advanced Business Plan Financials) Bei yake ni shilingi elfu 20 na tunatuma kama softcopy kwa email.
.....................................................................
Programu zetu zote kubwa zinaendelea kama kawaida na usisite kuagiza PACKAGE inayokufaa muda wowote ule utakaohitaji zikiwa bado kwenye offa zake kwani ukifika muda muafaka bei zitabadilika na kupanda au OFFA husika kutokuwepo tena.
KIFURUSHI(PACKAGE) YA 1 (18,000/= au 37,000/=)
Vitabu 3, softcopy kwa sh. elfu 18 vyote 3 na Hardcopy sh. elfu 37
1. MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
2. MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
3. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA
Pamoja na kuunganishwa na grupu la wasap bure ukipenda
KIFURUSHI(PACKAGE) YA 2 (10,000/=)
Tunakutumia vitabu, michanganuo na masomo yote yafuatayo kwa gharama ya shilingi elfu 10 tu.(Vyote ni softcopy); Ukitaka pia unajiunga na group bure.
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu
kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu
kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu
kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.
5. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA:
Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza
9. Mchanganuo
wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
10.
Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara
inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
11.
Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2
IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja
au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
12.
Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.
13.
Ukurasa mmoja wa mchanganuo.
KIFURUSHI(PACKAGE) YA 3 (20,000/=)
Semina maalumu ya jinsi ya kufanya hesabu za mpango wa biashara(Advanced Business Plan Financials) Bei yake ni shilingi elfu 20 na tunatuma kama softcopy kwa email.
0 Response to "WAZO LA BIASHARA IPI YENYE HATARI KIDOGO NAWEZA KUFANYA KWA MTAJI WA MILIONI 5?: MWAJIRIWA SERIKALINI"
Post a Comment