Kwa ujumla sababu moja kuu ya watu kukopa pesa
duniani kutoka kwa wakopeshaji mbalimbali kama vile mabenki, taasisi za fedha
na watu binafsi mbali na zile sababu mahsusi moja moja nitakazozitaja huko
mbele katika somo hii ni ile ya watu hao kutaka kununua au kulipia vitu ambavyo
hawana uwezo wa kuvilipia kwa fedha taslimu wakati huo. Mkopo humwezesha mtu
aliye na kipato endelevu mfano ajira au biashara iliyokwishaanzisha kufanya
marejesho ya mkopo aliochukua kidogokidogo katika muda waliokubaliana.
Mkopo huwanufaisha wote wawili, mkopaji na
mkopeshaji, kwa mkopaji kupata kiasi chote cha pesa anachohitaji pasipo kuwa na
haja ya kuweka akiba kidogokidogo hadi atimize kiasi hicho, huku mkopeshaji
naye akinufaika kwa kupata riba inayotokana na marejesho ya mkopo huo. Kwa hiyo
ili mtu kuweza kuiboresha na kuilinda hali yake ya kifedha wakati fulani katika
maisha yake ni lazima ahitaji uwekezaji kutoka nje kama mkopo zaidi ya zile
fedha anazokuwa nazo mwenyewe mkononi.
SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake 2019, njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima.
SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake 2019, njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima.
Kuna aina mbalimbali pia za mikopo kulingana
na mahitaji ya wakopaji. Aina mbalimbali za mikopo nazo huwa na masharti au
vigezo tofauti tofauti kwa mfano ipo mikopo mkopaji atatakiwa kueleza bayana
ataenda kufanyia kitu gani baada ya
kuupata na mingine mkopaji akishapewa huachwa aende zake akapange mwenyewe ni
nini atakachokwenda kufanyia mkopo huo nk. Ipo mikopo ya muda mfupi na mikopo
ya muda mrefu, mikopo ya riba na mikopo isiyokuwa na riba kabisa. Mikopo yenye
dhamana na ile isiyolindwa na dhamana yeyote,
mikopo ya vikundi na mikopo ya mtu mmojammoja.
Kuna wakati mwingine kukopa hakuna maana
yeyote kwa mtu na kanuni kubwa kabisa kwenye kukopa inasema hivi; “Unatakiwa
kukopa tu pale kunapokuwa na uhitaji wa kufanya hivyo” Ili kunufaika na
fursa zilizopo katika mikopo zingatia na ulinganishe faida na gharama za
kuchukua mkopo. Kuna kitu kingine kimoja watu wengi huwa hawakijui, kwamba
wakopeshaji huweka riba kubwa kwenye ile mikopo yenye hatari kubwa kusudi kuja
kufidia hasara zitokanazo na mikopo
chefuchefu(mikopo isiyolipika) na kuweka riba ndogo kwa mikopo ile
isiyokuwa na hatari kubwa. Hatari katika mkopo ni kama vile mkopaji kutokuwa na
dhamana za kutosha au bima ya mkopo nk.
SOMA: Je, Mtanzania unakopesheka na taasisi za fedha au Benki?
SOMA: Je, Mtanzania unakopesheka na taasisi za fedha au Benki?
Unatakiwa pia kabla ya kuchukua mkopo,
ujiulize maswali yafuatayo;
· Je,
Utaweza kurejesha mkopo wako?
· Je,
gharama za huo mkopo zinakubalika?
· Ni
mkopeshaji yupi(Benki, taasisi au mtu binafsi) mwenye masharti na riba nafuu
zaidi ya wengine?
Kuyajibu maswali hayo na mengineyo muhimu kutakusaidia kupata mkopo unaostahili kwa ajili ya mahitaji yako. Ingawa kila mtu ni tofauti kulingana na mazingira yake mwenyewe, mifano ifuatayo inawakilisha sababu mbalimbali zinazowafanya watu wakope pesa. Baada kukuelezea sababu hizo 9, nitaenda pia kukutajia zile sababu miongoni mwa hizo 9 unazotakiwa kuziepuka kama ukoma, nikiwa namaanisha kuwa sababu hizo hazitakiwi kabisa kukusukuma ukakope vinginevyo utakuja kujutia na kusaga meno bure. Kuna watu wengi wamewahi kuuziwa majumba yao ya maana huku wakitolewa nje ya nyumba hizo mithili ya wakimbizi vile, wengine walizikimbia familia zao na hata wengine kufikia hatua ya kujitoa uhai kisa madeni yaliyotokana na sababu hizo hizo nitakazokutajia.
SOMA: Njia 7 za kupata mtaji wa biashara unayoipenda.
Hebu tuzione kwanza sababu zote 9
mchanganyiko wa zile nzuri na mbaya kabla hatujazichambua mbivu na mbichi;
1.Kukopa
kwa ajili ya kununulia rasilimali(Assets) mfano nyumba, gari, kiwanja, nk.
Kumiliki nyumba ni moja ya malengo makubwa
muhimu zaidi ya kiuchumi binadamu wote duniani hutamani kutimiza katika maisha
yao. Lakini pia kuna ununuaji wa asseti nyingine mbalimbali kwa ajili ya
biashara na hata kwa malengo mengine tu yasiyokuwa ya kibiashara. Tutakwenda
kufafaua hapa vizuri kwenye kipengele cha sababu za kuepukwa kama ukoma na zile
sababu zinazofaa kukumbatiwa.
SOMA: Mbinu za kubadilisha asseti mbaya zinazotafuna pesa zako kuwa asseti nzuri zitakazokupa pesa
SOMA: Mbinu za kubadilisha asseti mbaya zinazotafuna pesa zako kuwa asseti nzuri zitakazokupa pesa
2.Kukopa
kwa ajili ya kuanzisha biashara mpya.
Mtu kwa kutumia rasilimali nyingine alizokuwa
nazo kama vile kiwanja, nyumba nk. anaweza akakopa kwa dhumuni la kuanzisha
biashara mpya.
3.Kukopa
kwa ajili ya uendelezaji wa biashara ya zamani uliyokwishaianzisha kitambo.
Wale waliokuwa tayari na biashara
zilizokwisha anzishwa kitambo huenda kukopa ili kuzipanua au kuziboresha zaidi
biashara zao
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
4.Kwa
ajili ya kujiboresha binafsi/Mikopo ya kielimu/Vyuo vikuu nk.
Katika eneo
hili gharama za elimu au mafunzo kwa kiasi kikubwa hazina mjadala kwani faida
zake kwa mkopaji ni za uhakika. Kuna mahusiano makubwa sana kati ya mafanikio
ya mtu kiuchumi na elimu au mafunzo anayoyapata hivyo, ujuzi, cheti, stashahada
na hata shahada vina uwezo mkubwa wa kuongeza kipato cha mtu hapo baadae.
5.Kukopa
kwa ajili ya kwenda kulipia hasara mbalimbali zitokanazo na shughuli za
kibiashara; Mfano mtu baada ya kufungua biashara yake
mtaji ukakata sasa anaamua kwenda kukopa kusudi kurudi tena kwenye chati. Hii
hufanywa sana na wale wanaofanya biashara za hisa au katika masoko ya mitaji na
pia hata katika biashara ya ununuaji na uuzaji wa majumba na viwanja(Real
Estate Agency)
SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?
SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?
6.Kukopa
kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu na dharura mbalimbali za kimaisha.
Ugojwa haubishi hodi na unapoingia wakati
mwingine unakukuta huna hata senti tano mfukoni. Sasa hebu niambie utaacha mtu
wako wa karibu au hata wewe mwenyewe ufe wakati unaweza ukakopa na kuokoa
maisha kisha baadae ukapiga kazi na kuzirejesha?
7.Kukopa
ukalipie videni vidogovidogo vinavyokuumiza kichwa(Debt consolidation).
Kuna wakati mwingine mtu hujikuta ana madeni
madogomadogo mengi kutoka kwa wakopeshaji zaidi ya mmoja, madeni hayo yana
tabia ya kuwa na riba kubwa na masharti magumu kiasi kwamba kadiri muda
unavyokwenda ndivyo nayo yanavyozidi kuongezeka shauri ya riba kuzaana. Wakopeshaji
wengine huwa ni watu binafsi na wanakutisha hata na mapanga au visu endapo
hutowalipa kwa wakati pesa zao. Wengine ni wenye nyumba na wanakutishia kila
siku kukutoea vitu vyako nje tena kibabe(Kimafia) ili uadhirike mbele za watu.
Kuepukana na adha zoote hizi unaamua kumtafuta mkopeshaji mstaarabu mmoja tu
kama benki au taasisi yeyote ile rasmi itakayokukopesha pesa kwa masharti ya
kistaarabu na kuwalipa hao ‘wahuni’ ‘wakasepa’ na kero zao huku wewe ukiendelea
kulipa kila mwezi au wiki kidogokidogo.
SOMA: Mkopo wa benki au taasisi za fedha: soma hapa hutakaa uwalaumu tena.
SOMA: Mkopo wa benki au taasisi za fedha: soma hapa hutakaa uwalaumu tena.
8.Kukopa
kwa ajili ya kulipia gharama mbalimbali za maisha za kila siku.
Hii mara
nyingi hutokea kwa wale wenye vipato vya uhakika. Wanakopa wakijua kesho na
keshokutwa mshahara au kipato kitaingia tu penda kisipende. Wanaamini kabisa
kwamba hawawezi kupanda daladala wakati tax, bodaboda na hata ndege zipo, kuna
hata wengine hukopa kwa ajili ya sherehe mbalimbali kama vile za harusi nk.
9.Kukopa
kwa ajili ya kuiongezea thamani rasilimali uliyokuwa nayo tayari mfano nyumba,
gari, shamba nk.
Unaboresha kitu ili kipendeze zaidi kwa
malengo mbalimbali
Nimemaliza kuzitaja na kuzielezea kidogo
sababu kubwa 9 zinazowasukuma watu kukopa fedha. Pengine unaweza ukaongezea
hapo nyingine, siyo mbaya kwani naamini bado zipo nyingi nyingine. Sasa
nitakachokwenda kukifanya katika sehemu hii inayofuata, ni kuzigawa sababu hizo
9 katika makundi mengine makubwa 2, moja likiwa ni kundi la sababu za kuepukwa
kama ukoma na kundi la pili ni la sababu zile mtu unazopaswa kutokuziogopa hata
kidogo. Katika hizi 9 nilizozitaja, zipo sababu 4 za kuogopa kama ukoma na
nyingine 5 ni za kukumbatia. Nitaanza kwanza na hizo 4, kisha 5 huku kila moja
niikitolea ufafanuzi ni kwanini imeingia katika kundi husika.
SOAMA: Kabla ya kukoipa mkopo wa biashara yako, pambana kiume kwanza usijekuumbuka bure
SOAMA: Kabla ya kukoipa mkopo wa biashara yako, pambana kiume kwanza usijekuumbuka bure
Kuna sababu zingine zitakushangaza sana kwani
hutoamini kabisa kama zinaweza zikaingia katika kundi la kuogopwa kama ukoma,
hivyo kuwa makini sana hapa, yawezekana hapo kabla ulikuwa ukifikiri ni sababu
za kukumbatiwa kumbe siyo hivyo, zitakuchoma bure, kuzikumbatia hakuna tofauti
na mtu aliyekumbatia upupu.
SEHEMU
YA II
SABABU 4 ZA KUKOPA PESA UNAZOTAKIWA KUZIOGOPA
KAMA UKOMA VILE
1………..
………………………………………
Ndugu
msomaji wangu, somo hili linaendelea hadi mwisho usiku saa 3-saa4 kwa aliyejiunga katika masomo
ya kulipia. Kujiunga na group hilo(Michanganuo-online Premium group) ni bure,
ila utatakiwa kununua moja ya vifurushi vifuatavyo vya masomo kwa bei rahisi kabisa ya OFFA.
Katika Premium Group unapata mafunzo ya mwaka mzima ya fedha na jinsi ya kuandika mpango wa biashara hatua kwa hatua, toka Januari- Desemba pamoja na dondoo nyingine mbalimbali za biashara, ujasiriamali na mipango ya biashara halisi iliyokamilika kila kitu. Unapata pia fursa ya kuuliza swali lolote lile kutoka kwa wataalamu wa michanganuo(Business plan experts) na kujibiwa haraka. Aidha unaweza kujiunga na group letu jingine la bure(Michanganuo free group) kwa kiungo hiki, https://chat.whatsapp.com/EJ3MS2MtJepEjm9GaYtT8e
Nafasi kwenye group la Premium zilizobakia ni chache ili lijae(Chini ya watu 30 tu), pia offa hii inakaribia kuisha na kila kitu kitauzwa kwa bei yake ya kawaida. Kila item hapo chini ina bei yake, jumla vyote 13 kwa bei halisi vinagharimu si chini ya sh. elfu 80. Lakini tunakupa kila kitu kwa sh. elfu 10 tu au ukipenda kuchukua kifurushi cha 2 na cha 3 elfu 18 na elfu 28
Katika Premium Group unapata mafunzo ya mwaka mzima ya fedha na jinsi ya kuandika mpango wa biashara hatua kwa hatua, toka Januari- Desemba pamoja na dondoo nyingine mbalimbali za biashara, ujasiriamali na mipango ya biashara halisi iliyokamilika kila kitu. Unapata pia fursa ya kuuliza swali lolote lile kutoka kwa wataalamu wa michanganuo(Business plan experts) na kujibiwa haraka. Aidha unaweza kujiunga na group letu jingine la bure(Michanganuo free group) kwa kiungo hiki,
Nafasi kwenye group la Premium zilizobakia ni chache ili lijae(Chini ya watu 30 tu), pia offa hii inakaribia kuisha na kila kitu kitauzwa kwa bei yake ya kawaida. Kila item hapo chini ina bei yake, jumla vyote 13 kwa bei halisi vinagharimu si chini ya sh. elfu 80. Lakini tunakupa kila kitu kwa sh. elfu 10 tu au ukipenda kuchukua kifurushi cha 2 na cha 3 elfu 18 na elfu 28
1.Kifurushi
cha sh. Elfu 10 kinachojumuisha vitu vifuatavyo,
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu
kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu
kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu
kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.
5. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA:
Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza
9. Mchanganuo
wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
10.
Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara
inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
11.
Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2
IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja
au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
12.
Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.
13.
Ukurasa mmoja wa mchanganuo.
2.Kifurushi
cha sh. Elfu 18 kinachojumuisha vitu vifuatavyo
Unapata Kifurushi kizima cha kwanza pamoja na
vitu vingine vifuatavyo;
· Kitabu
cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
· Kitabu
cha MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYWASIYOPENDA KUITOA
3.Kifurushi cha sh. Elfu 28 kinachojumuisha vitu vifuatavyo;
Unapata vitu vyote kutoka kifurushi cha 1
& 2 pamoja na Semina kubwa ya Hesabu za mpango wa biashara(Advanced
Business Plan Financials).
KULIPIA KIFURUSHI CHCHOTE HAPO JUU, TUMIA
NAMBA ZIFUATAZO,
0765553030 au 0712202244
Jina hutokea, Peter Augustino Tarimo
Kisha tuma ujumbe wasap 0765553030, usemao,
NIUNGANISHE GROUP LA KULIPIA LA MICHANGANUO.
Nitakuunganisha muda huohuo pamoja na
kukutumia kila kitu
0 Response to "SABABU KUBWA 9 DUNIANI KWANINI WATU HUKOPA PESA, 4 KATI YAKE NI ZA KUOGOPA KAMA UKOMA"
Post a Comment