Kuwashirikisha mambo mbalimbali hakuwasaidii
tu wateja wako lakini pia kunakuweka wewe mwenyewe katika nafasi ya juu zaidi
kama mtu wa kutegemewa. Hata hivyo wafanyabiashara na wajasiriamali wengi
hulifanya jambo hili kupita kiasi na kusahau kumbe kuna hatari mbalimbali pia
zinazoweza zikajitokeza endapo watawashirikisha wateja wao mambo mengi kupitiliza.
SOMA: Makosa 12 yatakayofukuza wateja dukani kwako na kudhani umelogwa.
SOMA: Makosa 12 yatakayofukuza wateja dukani kwako na kudhani umelogwa.
Bila kupoteza muda wako mwingi hebu basi
tukazione hizo siri 5 zikoje;
1.Maswala
yako ya kifedha.
Usipende sana kulialia umasikini mbele ya
wateja wako wala kujitapa kuwa una pesa nyingi(ukwasi), unapofanya mambo haya 2
kupitiliza yanaweza kuwafanya wateja
wako kukaa mbali na wewe kwani wanaweza kuhisi mambo mawili, kwanza wanaweza
kufikiria biashara yako inachungulia kaburi(inafilisika)
au pengine bei unayowatoza ni kubwa kupita kiasi. Hivyo utaona wakikimbia mmoja
baada ya mwingine.
2.
Masuala ya ndani ya biashara yako.
Wateja hawana haja ya kuyajua matatizo yako
na wale wanaokusambazia mzigo, wala kujua matatizo yako na mwenye nyumba
ulikopanga fremu ya ofisi/duka lako.
SOMA: Kuanzisha kiwanda rahisi cha juisi ya matunda, Tanzania ya viwanda yaja jiandae.
SOMA: Kuanzisha kiwanda rahisi cha juisi ya matunda, Tanzania ya viwanda yaja jiandae.
3.Matatizo
ya wafanyakazi wako.
Kutoa malalamiko juu ya wafanyakazi wako kwa
wateja wako hakuwezi kusaidia kitu, sanasana kutazidi kukufanya uonekane kama
kwamba wewe ni mtu mbaya na mwenye roho mbaya. Ikiwa mfanyakazi wako
ataboronga hata iiwa ni mbele ya wateja basi wewe cha kufanya kama bosi ni
kuwataka radhi wateja kwa kosa hilo kisha rekebisha tatizo lililotokea halafu
sasa njoo baadae ushughulike na mfanyakazi wako wakati mkiwa wenyewe wawili tu bila
mtu mwingine.
4.Hali
halisi ya soko ilivyo.
Kila mtu na si wewe tu hata na wateja wenyewe
kuna wakati wanahisi hali ya kiuchumi kuwa ngumu. Hivyo usitegemee sana huruma
toka kwao kwa kulialia kuwa ‘vyuma
vimekaza, vyuma vimekaza’. Utawafanya wakushangae bure badala ya kukuonea
huruma.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako.
5.Kuhusiana
na wateja wengine.
Kila mteja angependelea kujihisi kama yeye
ndiyo mteja pekee, hivyo si vizuri hata kidogo kushea kupita kiasi stori za ni
nani anayenunua kwako,ananunua nini, ananunua kiasi gani na ananunua kupitia njia
zipi. Sisemi ni vibaya kwa mfano kuweka ushuhuda(Testimonies) katika ukurasa au page zako lakini, fanya hivyo kimkakati na pia kwa kiasi.
…………………………………………………
LEO
NINA HABARI MBILI NJEMA KWAKO,
Somo la leo lilisisitiza kutokutoa kila siri
kwa wateja wako lakini mimi nitakaribia japo siyo kabisakabisa kukupa “siri
zangu muhimu 2”
Habari
ya kwanza kabisa;
Ni ujio wa semina yetu ya kwanza kati ya 4
tulizoazimia kuzifanya kabla ya mwaka huu kumalizika. Kumbuka Mwezi Januari
niliahidi kupitia kaulimbiu yetu ya mwaka; “KIWANDA NI UTAJIRI, TUACHE MANENO
MANENO TUJENGE VIWANDA KWA VITENDO”, kuwa tutaandaa michanganuo bunifu
4 kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda(biashara za uzalishaji) ambazo zitakuwa kama mifano kwa ajili ya mtu
kuanzisha biashara ya kiwanda chochote kile kidogo na hata cha kati.
Kwa Miezi iliyobakia mwaka huu 2019 kuisha
tutafanya mchanganuo mmojammoja kila mwezi, kumbuka pia kwamba hii michanganuo
si ya kitoto!, na tayari nimekwishaifanyia utafiti mkubwa na kwa pamoja tena
nitaomba mawazo yenu wadau mtakaojiunga na semina hizi wakati tukiandika hatua
kwa hatua katika group.
Tutachambua kiwanda kimoja cha ufyatuaji wa
matofali ya block kilichopo maeneo ya Kiluvya jirani na jiji la Dar es salaam,
nimeshawasiliana na wahusika na tayari wameshanipatia taarifa zote muhimu kama
za Mahitaji ya kuanzishia kiwanda na soko.
Bila kupoteza muda wako mwingi, niseme tu
kwamba semina hii tunakwenda kuifanya kuanzia tarehe 15 katika group la MICHANGANUO-ONLINE, na kiingilio ni sh.
Elfu 10 tu, fedha ambayo itakuwezesha kushiriki tena michanganuo mingine yote 3
iliyobakia bila kuchajiwa zaidi. Namba za malipo ni 0765553030 au 0712202244 jina kama kawaida ni la kwangu
mwenyewe, Peter Augustino Tarimo.
Unaweza ukaanza kulipia sasa hivi kujihakikishia nafasi yako mapema.
Habari
ya Pili;
Ni OFFA ya “kufa mtu” inayoambatana na hiyo
semina. Kusema ule ukweli hii offa naitoa tu kwa shingo upande lakini ndani
kiroho kinaniuma na nafanya hivyo ni kwa
sababu tu nawapenda wadau wangu na si vinginevyo. Any way, nikuibie tu siri
moja ni kwamba, kwa kukupa offa hii ni sawa na kukupa kila kitu nilichokuwa
nacho katika Programu zangu zote, nakuwa sijabakiza kitu. Naamini ukiwa mjanja huwezi
kuikosa offa hii hata iwe vipi. Na naitoa tu hapa na si kokote kwingineko.
IKOJE
OFFA HII?
Natoa offa hii kwa watu 10 tu wa mwanzo
watakaojiunga na semina hii kisha baada ya hapo itafungwa rasmi, wengine
watashiriki semina na kupata tu vitu vya kawaida.
INA
NINI NDANI YAKE?
Nakupatia Instatly, punde tu unapolipia,
Programu zangu zote tatu zilizosheheni vitabu, michanganuo ya biashara, semina
na masomo yoote ya siku zilizopita. Kumbuka vitabu ni pamoja na vitabu vyangu
vikuu vya MICHANGANUO, DUKA na MIFEREJI 7 YA PESA. Hutasubiri mpaka
siku ya semina ndipo ufaidike na offa yako, bali offa hii unatumiwa mara moja
baada ya kulipa kiingilio chako cha sh. Elfu 10 hata kama ni sasa hivi
ninapoandika hapa.
Na haijalishi kama unatumia watsap au email
tu peke yake, kila kitu kipo katika mfumo wa softcopy utatumiwa hata kama huna
Whatsapp kwenye simu yako. Halikadhalika semina nayo si lazima uwe katika
watsap, masomo yote tunatuma pia kwa E-mail yako.
WAHI OFFA HII INGALI YA MOTOMOTO KABLA
HAIJAPOA KWA KUTUMA KIINGILIO CHAKO SH. ELFU 10 KWA NAMBA, VODACOM,
0765553030 au TIGO, 0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo.
Dondoo za semina tutaendelea kujuzana kadiri
ziku zinavyokwenda.
Ni mimi,Peter Augustino Tarimo
Mwalimu/kocha na mhamasishaji wako.
0 Response to "SHEA NA WATEJA WAKO KILA KITU LAKINI SIYO SIRI HIZI TANO(5)"
Post a Comment