SEHEMU
YA I
Kumiliki biashara ndiyo njia pekee ya haraka
inayoweza kumfanya mtu kuufikia uhuru kamili wa kifedha. Lakini siyo biashara
zote au kila aina ya biashara iliyokuwa na uwezo wa namna hiyo. Biashara
nyingine zinamwezesha mtu kuufikia uhuru kifedha taratibu mno wakati kuna
nyingine zinamwezesha mtu kutoka haraka zaidi.
Zipo biashara nyingi mtu anaweza kuanzisha
kama vile, biashara ya duka, biashara ya nguo, biashara ya mazao kama vile
mchele, mahindi, mpunga, mtama, karanga, ngano nk. Katika somo hili la leo
nitakwenda kuzungumzia biashara moja ya mtaji mdogo sana ambayo wengi walioamua
kuifanya wameweza kuona matokeo yake haraka sana na wametajirika au kuwa huru
kifedha. Biashara hiyo haina tofauti na Duka mtu unalotembea nalo kwani
hauhitaji fremu kubwa Kariakoo wala sijui wapi ndipo uweze kufanya biashara
yako.
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
Biashara nitakayoizungumzia inafanyika katika
mtandao wa Intaneti lakini ni tofauti na
zile biashara nyingi za kwenye mtandao watu wengi tulizozizoea. Wachache
wanaoijua hata hapa Tanzania wanatengeneza wengine hadi millioni 7 na zaidi kwa
mwezi huku wenyewe wakiwa wametumia kiasi kidogo sana cha mtaji.
Kabla hatujaendelea mbele zaidi hebu tuone
kwanza Uhuru wa kifedha maana yake ni
kitu gani. Mtu anakuwa huru kifedha pale kipato chake cha ziada (Passive
income) kinapozidi matumizi yake. Mfano
kama kipato cha mtu cha ziada ni sh. millioni moja kwa mwezi na matumizi yake
ni shilingi laki 6 kwa mwezi basi mtu huyo yupo huru kifedha. Hapo sijahusisha
kipato chake cha kila siku cha kawaida kama mshahara au biashara, nimezungumzia
tu kipato cha ziada.
SOMA: Je, unajua unaweza kumiliki kiwanja au nyumba bila kutoa senti 5 mfukoni? Soma kitabu cha dola miioni tano ujue yote
SOMA: Je, unajua unaweza kumiliki kiwanja au nyumba bila kutoa senti 5 mfukoni? Soma kitabu cha dola miioni tano ujue yote
Sasa utaona hapo kwamba mtu huyu anao uwezo
wa kuacha kazi yake ya kila siku au biashara na akaamua kuishi kwa kutumia
kipato chake cha ziada tu, na akamudu bila matatizo yeyote wala haja ya kufanya
kazi kama vile mwanzoni kabala ya kupata huo uhuru wa kifedha.
Kuwa huru kifedha unahitaji kumiliki
rasilimali(Assets) zitakazokuingizia pesa kila mwezi hata kama hufanyi kazi, na
njia pekee ya kuzipata hizo asseti ni kwa kupitia kuwekeza kidogokidogo katika
miradi mfano katika ardhi na majengo, kwenye hisa za makampuni au pia unaweza
kuwa na biashara ya kawaida tu lakini iliyo na mfumo unaoiwezesha kujiendesha
yenyewe, mfano mmojawapo ni zile biashara za kwenye mtandao wa intaneti nk.
Katika miradi niliyotaja hapo juu yote,
biashara inayojiendesha kimfumo ndiyo rahisi zaidi kuliko nyingine kwa mtu wa
kawaida. Uwekezaji kwa mfano kwenye ardhi na majumba unahitaji pesa nyingi sana mtu
wa kawaida kuweza kumudu. Sasa basi ni biashara ipi nzuri zaidi unayoweza
kuijengea mfumo hatimaye ikakupa uhuru kamili wa kifedha?
SOMA: Kipato cha ziada ambacho watu wengi hawakijui
SOMA: Kipato cha ziada ambacho watu wengi hawakijui
Wazo la biashara ya namna hiyo linatakiwa
liwe ni lile wazo mtu unaweza ukatumia nyenzo mbalimbali (Leverage)
kulitekeleza. Kutumia nyenzo(leveraging) maana yake ni kutumia rasilimali za
watu wengine kupata faida haraka. Kwa
mfano unaweza ukatumia muda, pesa, maarifa, bidhaa, au mfumo nk. vya watu
wengine katika kujiingizia faida. Nikupe mfano mmoja, mtaalamu wa
kutengeneza tovuti anaweza akasaidia
watu kutengeneza website zao na wakamlipa pesa.
Mtaalamu huyo akiamua mwenyewe kumtengenezea
mtu mmojammoja tovuti maana yake ni kwamba biashara yake haina mfumo endelevu
kwani siku tu akiugua au kupata dharura yeyote ile na kipato nacho hakuna. Lakini
endapo ataamua kutengeneza mafunzo(courses) ya jinsi mtu anavyoweza
kujitengenezea tovuti mwenyewe, akaelezea hatua kwa hatua kwa kutumia video nk.
ataweza kuziuza kozi hizo hata kama ikiwa atakuwa na safari ya mbali au
amelala. Lakini huduma ni ileile ya utengenezaji wa tovuti ila mfumo tu ndio uliobadilika.
SOMA: Biashara ndogondogo Tanzania zenye faida ya haraka ni hizi hapa zipo 4
SOMA: Biashara ndogondogo Tanzania zenye faida ya haraka ni hizi hapa zipo 4
Ili kufanya biashaa mtandaoni na kupata pesa
utahitaji vitu muhimu vifuatabvyo;
1. Uwezekano
wa kufikia mtandao wa Inaneti kupitia kompyuta au simu yako ya
mkononi(smartphone)
2. Jukwaa
au platform, na hii inaweza ikawa ni tovuti, au jukwaa lingine lolote lile
mfano kurasa katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, Instagram na
mingineyo. Jukwaa hilo ndilo litakalokuwezesha wewe kuwasiliana na wateja wako
mtandaoni.
3. Kuaminika
na kujenga mtandao imara. Bila kitu hiki biashara mtandaoni haiwezi ikaleta
matokeo mazuri kwani wateja ni watu wa kawaida kama wale wale unaofanya nao
biashara zingine nje ya mtandao.
SOMA: Njia mpya za kufanya mambo: Dunia, biashara, ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu
Karibu kila biashara siku hizi hata na zile zinazofanyikia kwenye eneo maalumu kama ofisini au katika fremu zinahitaji kuwa na uwepo wake katika mtandao wa Intaneti, ni trend haiwezi kukwepeka tena kirahisi sasa hivi na faida kubwa za biashara yako kuwa mtandaoni ni hizi zifuatazo;
Karibu kila biashara siku hizi hata na zile zinazofanyikia kwenye eneo maalumu kama ofisini au katika fremu zinahitaji kuwa na uwepo wake katika mtandao wa Intaneti, ni trend haiwezi kukwepeka tena kirahisi sasa hivi na faida kubwa za biashara yako kuwa mtandaoni ni hizi zifuatazo;
1. Kuwafikia
wateja wengi na wa mbali zaidi(Kitaifa na Kimataifa)
2. Hupunguza
gharama za uendeshaji wa biashara
3. Kuingiza
kipato(pesa) muda wowote ule hata ukiwa umelala.
Lakini vipi kama ikiwa huna uzoefu na mtandao wa
intaneti? Si ishu tena siku hizi kwani mambo yamefanywa kuwa rahisi mno tofauti
na ilivyokuwa miaka miwili mitatu iliyopita huko nyuma. Siku hizi tovuti/blog
mtu yeyote yule anaweza akaanzisha ilimradi tu awe ana uelewa wa kuifungua na
kuweka vitu ndani yake(contents). Na mitandao ya kijamii ndio usiseme kabisaa kwani hata mtoto wa miaka 7 anaweza akafungua ukurasa wake.
SEHEMU
YA II
Katika sehemu yetu ya pili tutakwenda kuiona biashara
ambayo watu wengi bado hawajaishitukia. Ungana na mimi leo saa 3 usiku katika
group jingine la Michanganuo-online-Premium ujue kila kitu kuhusiana na
biashara hiyo.
SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado
SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado
Kujiunga na group la Premium, lipia vitabu na masomo
yaliyoorodheshwa hapo chini, nitakutumia muda huohuo kisha kukuunganisha na
group hilo mara moja. Ni sh. Elfu 10 tu itakayokupa pia uanachama wa kudumu.
Pia utaweza kushiriki katika semina yetu ya tarehe 15 August 2019 ambapo tutakwenda kuandika hatua kwa hatua mchanganuo wa kiwanda cha ufyatuaji wa tofali za block. Mwisho Mchanganuo huo utakuwa na kila kitu, vipengele yote, mahesabu na katika lugha ya kiswahili na kiingereza.
Watu wa mwanzo 10, Nitawapa pia vitabu vya DUKA LA REJAREJA na kile cha MIFEREJI 7 ya fedha pamoja na SEMINA ILIYOPITA YA HESABU ZA MICHANGANUO(Advanced Business Plan Financials) tunayoiuza sh. elfu 20 utaipata free of charge!
ASANTE SANA
Peter A. Tarimo
1. Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA
UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko
chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018
part 2
4. Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika
michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.
5. Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO
WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu
vingi duniani.
6. SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika
mpango wa biashara.
7. Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya
ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE
RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza
9. Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha
matikiti maji.
10.
Vielezo(Templates)
za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
11.
Mfumo
mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM)
unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake
pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
12.
Somo
muhimu sana la mzunguko wa fedha.
13.
Ukurasa
mmoja wa mchanganuo.
0 Response to "DUKA UNALOTEMBEA NALO: BIASHARA NZURI UKIANZISHA INAKUPA UHURU KAMILI KIFEDHA"
Post a Comment