Tathmini
hii haifanywi tu na wale wanaofanya biashara hapana, bali hata na mtu
mwingine yeyote yule anayetaka kufanya maamuzi yanayoweza kumletea matokeo
chanya au hasi baadae.
NUFUVI au kwa kiingereza SWOT analysis ni
ufupisho wa maneno NGUVU, UDHAIFU, FURSA na VIKWAZO(Strength, Weaknesses,
Oportunity and Threats).
Umuhimu
wa kufanya NUFUVI ni nini?
1. Husaidia
katika kazi ya kutengeneza mikakati yako utakayoitumia ili kufikia malengo
unayokusudia.
2. Husaidia
kujua ni vipaumbele gani utakavyoweka katika biashara/mradi wako.
3. Humsukuma
mtu kuwa na mtazamo na mwelekeo mpya juu ya biashara anayoifanya kwa kutumia
vizuri nguvu na fursa zilizopo huku akikwepa udhaifu na vikwazo.
4. Husaidia
katika kazi ya kuandika mpango wako wa biashara kwani unafahamu kabla mema na
mabaya yote yanayoizunguka biashara husika.
Kufanya tathmini hii maana yake ni kwamba
unatafakari mazingira yote hasi na chanya yanayoizunguka biashara yako kwa nje na
kwa ndani. Hivyo katika NUFUVI kuna mazingira ya aina mbili, yale ya ndani
ambayo ni Nguvu na Udhaifu halafu yale ya nje ambayo ni Fursa na Vikwazo.
Unaweza pia kuyaweka katika makundi mawili kama hivi, Mazingira wezeshi(Nguvu
na Fursa) halafu Mazingira Pingamizi(Udhaifu na Vikwazo)
MAZINGIRA
YA NDANI(Nguvu & Udhaifu)
NGUVU:
Nguvu ni vile vitu vyote kwenye biashara au
kampuni yako vilivyokuwa na mchango chanya(mzuri) na ambavyo vipo ndani ya
uwezo wako. Vitu hivyo mfano ni;
· Rasilimali
unazozimiliki
· Ujuzi/elimu
uliyokuwa nayo
· Jina
zuri, heshima au sifa njema ya biashara yako
· Timu
nzuri ya wafanyakazi
· Wateja
ulio nao
· Eneo
zuri la biashara
· Teknolojia
ya kisasa
· Mtaji
wa kutosha
· Hakimiliki
ya kitu
· Na
nguvu shindani nyingine yeyote ile unayoweza kuwa nayo dhidi ya
washindani/wapinzani wako.
UDHAIFU:
Udhaifu ni igezo au vitu vyote vile
vinavyokinzana na nguvu ulizokuwa nazo katika biashara yako na ambavyo pia vipo
ndani ya uwezo wako. Nikisema ndani ya uwezo wako namaanisha unaweza
kuvirekebisha ikiwa utaamua. Vitu hivyo vinaweza vikawa ni vile vyote
nilivyovitaja katika NGUVU hapo juu lakini katika mtazamo HASI, nikimaanisha
kwamba ikiwa vitu hivyo utakuwa hauna basi itakuwa ni UDHAIFU kwako badala ya
NGUVU. Navyo ni kama hivi hapa chini;
· Kutokuwa
na rasilimali za kutosha kama mtaji
· Mapungufu
kwenye timu yako ya wafanyakazi au uongozi
· Vifaa
na teknolojia duni
· Kutokuwa
na jina sokoni
· Bei
isiyowaridhisha wateja
· Kifungashio
kibaya nk.
MAZINGIRA
YA NJE:(Fursa & Vikwazo)
FURSA:
Ni vitu au mazingira kutoka nje ya biashara
vyenye athari chanya au vinavyochangia mafanikio ya biashara yako. Mifano ni
hivi vifuatavyo;
· Kukua
kwa soko lako
· Mwelekeo
fulani wa soko unaohamasisha watu kununua kile unachouza, kwa mfano ikiwa
unatengeneza mifuko mbadala halafu kunakuwa na katazo la mifuko ya plastiki nk.
hiyo ni fursa
· Tukio
lolote lile linalotazamiwa ambalo biashara yako inaweza ikalitumia katika
kujitanua zaidi.
· Mabadiliko
yeyote yale ya kisheria au ya kiserikali yanayoweza yakaleta matokeo chanya
katika biashara yako.
· Mtazamo
chanya wa wateja juu ya biashara yako.
VIKWAZO:
Hivi ni vile vitu au vigezo hasi kutoka nje
ya biashara ambavyo huna uwezo wa kuvizuia visitokee lakini unaweza tu kuweka
mipango ya dharura kwa ajili ya kupunguza makali yake yasiweze kuiua biashara
yako endapo vitatokea. Navyo ni kama hivi vifuatavyo;
· Washindani
watarajiwa wanaoweza kuibuka muda wowote ule
· Uwezekano
wa wale wanaokusambazia bidhaa au kukuuzia jumla kupandisha bei
· Mabadiliko
ya teknolojia unayotumia
· Janga
lolote lile la asili au moto
· Wateja
kubadili mwenendo wao wa ununuaji kama
vile kupunguza kunuua kutokana na sababu mbalimbali
· Na
mwelekeo mwingine wowote ule wa soko unaoweza kuhatarisha biashara yako.
MFANO
WA JEDWALI LA NUFUVI(SWOT)
Tathmini hii siyo ngumu hata kidogo na hufanyika kwa
kuchora tu jedwali linaloonyesha sehemu kuu nne 4(vyumba 4) na katika kila
chumba basi unaorodhesha vigezo husika. Katika mfano nitakaoutoa hapa ni wa
biashara ya tofali za saruji tunayokwenda kuandika mchanganuo wake hatua kwa
hatua kwenye semina yetu siku ya Alhamisi August 15.
Ukishamaliza tathmini yako hii, sasa unaweza
ukaibadilisha kuwa mikakati ya kufanikisha biashara yako kama tutakavyokwenda
kuona kwenye mchanganuo wetu hatua kwa hatua siku ya Alhamisi. Kwanza kabisa
unatakiwa kutumia mazingira wezeshi ya ndani na nje(Nguvu na Fursa) kukabiliana
na Mazingira yote pingamizi ya ndani na nje(Udhaifu na Vikwazo).
....................................................
Mpenzi msomaji wangu ikiwa unapenda kujifunza zaidi jinsi ya kuandaa mpango wa biashara yako, basi karibu sana siku ya Alhamisi Tarehe 15 August katika kundi la watsap la MICHANGANUO-ONLINE GROUP. Mbali na semina hiyo pia nitakupatia offa kubwa ya vitabu, michanganuo na masomo mbalimbali yanayohusiana na Michanganuo ya biashara.
Mpenzi msomaji wangu ikiwa unapenda kujifunza zaidi jinsi ya kuandaa mpango wa biashara yako, basi karibu sana siku ya Alhamisi Tarehe 15 August katika kundi la watsap la MICHANGANUO-ONLINE GROUP. Mbali na semina hiyo pia nitakupatia offa kubwa ya vitabu, michanganuo na masomo mbalimbali yanayohusiana na Michanganuo ya biashara.
Offa hii si ya kukosa hata kidogo kwani
ukisema uje uvinunue baadae gharama yake ni karibu mara 9 zaidi.
Kujiunga na semina hiyo lipia kiingilio
chako sh. Elfu 10 na nitakuunganisha muda huohuo pamoja na kukutumia kila kitu
nilichoahidi halafu utasubiri semina siku ya Alhamisi na nyinginezo
zitakazofuata bila kuchajiwa pesa ya ziada. Siku ya mwisho kulipia ni tarehe 14
usiku.
0 Response to "NUFUVI(SWOT ANALYSIS), TATHMINI MUHIMU KABLA HUJAANZA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO"
Post a Comment