Kuna uwezekano mkubwa sana kwamba mambo mengi
mimi na wewe tuliyokwishajifunza juu ya pesa tokea utotoni hayakuwa na ukweli
wowote ule au yawezekana pia yana ukweli lakini uliokuwa mdogo sana. Yamkini
tumekuwa tukiambiwa kwamba, “ukishafikisha
umri wa miaka zaidi ya 40, wewe mafanikio kifedha tena sahau”, au “kama una umri chini ya miaka 25 kumiliki
biashara za maana ni sawa na ndoto za alinacha”.
Lakini ndugu yangu mpendwa nikueleze tu ule
ukweli kwamba, jinsi ya kutengeneza pesa nyingi hakuna uhusiano wowote ule na
umri wa mtu, kiwango chake cha elimu, jinsia wala eneo na kabila atokalo.
Hakuna pia uhusiano na uzoefu wake wa siku zilizopita kwani unaweza kuwa
ulikuwa ukimiliki pesa nyingi miaka ya nyuma, ukala bata sana, lakini kwa sasa
hivi unaomba mia ya maji ya kunywa(Kandoro).
SOMA: Vipaji uwezo akili ni vitu watu tunazaliwa navyo au kujifunza?
SOMA: Vipaji uwezo akili ni vitu watu tunazaliwa navyo au kujifunza?
Kupata pesa nyingi pia hakuhusiani na miaka
uliyokaa darasani wala kiwango cha akili ulichokuwa nacho(IQ). Hakuna mtu
aliyekuwa na IQ kubwa kama kina, Albert Einstain, Christopher Michael Langan na
wengineo lakini je, uliwahi kusikia mahali popote pale wakitajwa kuwa waliwahi
kuwa mabilionea huko Marekani zaidi ya umaarufu tu walionao katika fani zao?
Karibu kila binadamu mwenye akili timamu za
kawaida anaweza akajifunza kwa urahisi kabisa jinsi ya kutengeneza mamilioni ya
shilingi lakini ni ukweli uliokuwa mchungu sana kwamba watu 97 kati ya 100 wanaozaliwa huishia kuishi maisha
yao yote bila ya kujishughulisha hata kidogo na na elimu hii ya jinsi ya kupata
pesa. Tena mbaya zaidi ni kwamba tatizo hili huzidi kupewa nguvu na kuendelezwa
kwa kupitia njia ya kurithishana kizazi kimoja hadi ya kingine.
SOMA: Wanaofanikiwa katika maisha huamini vitu hivi (4) vinne
SOMA: Wanaofanikiwa katika maisha huamini vitu hivi (4) vinne
Mifumo ya kielimu katika nchi zetu kote
Duniani imejengwa kuzifundisha akili za vijana jinsi ya kuondoa ujinga na kwa
kweli mifumo hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kukidhi azma hiyo lakini
kwa upande mwingine ikisahau kabisa somo muhimu mno la Jinsi ya kupata fedha. Si ajabu hata kidogo kukuta mtu amefikia
ngazi ya udaktari kwenye ngazi ya uchumi lakini bado akiwa na uelewa mdogo sana
wa jinsi ya kujipatia pesa.
Kwa kuwa pesa ndiyo njia kuu ya kulipia
bidhaa na huduma za watu wengine, na kwakuwa ndiyo njia itumiwayo Duniani kote,
kutokuwa na uelewa wa kutosha katika eneo hili la pesa ndio chanzo kikubwa
kabisa cha matatizo yasiyotakiwa wala kustahili kuwepo. Mara zote Duniani kuna
kundi dogo la watu “wateule” wanaokadiriwa kufikia asilimia 3% tu ya watu wote.
Watu hawa ndio waliokuwa na uelewa mkubwa zaidi wa pesa(Money consciousness).
SOMA: Siri 10 alizotumia Aliko Dangote, tajiri namba 1 Afrika kutajirika
SOMA: Siri 10 alizotumia Aliko Dangote, tajiri namba 1 Afrika kutajirika
Uelewa huu wa pesa ndio chanzo kikubwa cha
utajiri na mafanikio ya kushangaza waliyokuwa nayo. Kama ulivyokuwa uelewa wa
fedha pia kuna ujinga wa fedha(Kinyume
cha uelewa wa fedha). Uelewa au
utambuzi wa fedha kama ulivyokuwa ujinga wa pesa, vyote 2 huweza kurithishwa
kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine.
Sasa
basi Pesa ni kitu gani hasa?
Hebu tuone pesa ni kitu gani, Pesa ni malipo
mtu unayopata baada ya kutoa huduma fulani. Kwa kadiri unavyotoa thamani kubwa
zaidi katika huduma hiyo ndivyo navyo unavyolipwa kiasi kikubwa zaidi cha pesa.
Kufikiria jinsi tunavyoweza kutoa huduma bora hakutusaidii tu kupata pesa zaidi
bali pia hutupatia fursa ya kukua kiakili na kiroho.
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala
Makaratasi au sarafu tunazoweka mifukoni
mwetu siyo pesa. Pesa ni wazo. Mchakato wa kuingiza pesa hauna uhusiano wowote
ule na makaratasi wala sarafu hizi za shaba, bali una uhusiano wa moja kwa moja
na akili zetu(fikra/mawazo)
Katika vitabu na ‘courses’ mbalimbali tunazosoma tunajifunza mbinu nyingi za kuongeza
mauzo na kuboresha biashara kusudi tuweze kupata pesa nyingi zaidi, nisawa tu
hilo wala halina shaka, lakini ni lazima tukumbuke pia kwamba juhudi zoote hizo
haziwezi zikazaa matunda ya kudumu wala furaha ya muda mrefu ikiwa kama
hatutazingatia na upande huu wa pili wa Utambuzi wa fedha Kiroho na Kiakili.
SOMA: Saikolojia ya pesa na kanuni 10 za kufuata ili uwe mtu uliyefanikiwa kimaisha.
SOMA: Saikolojia ya pesa na kanuni 10 za kufuata ili uwe mtu uliyefanikiwa kimaisha.
Ili kuweza kupata mafanikio ya kweli kifedha
mtu ni lazima aanze kujisikia vizuri na pesa, “aipende fedha”, hili linaweza
kuonekana kama ni jambo la ajabu kidogo lakini ukweli ni kwamba watu wengi
hawajisikii vizuri na pesa na hii ndiyo sababu kubwa ni kwanini hawafanikiwi
kupata pesa nyingi. Katia somo letu la siku ya jana nilielezea vizuri zaidi
eneo hili la kutokujisikia vizuri na pesa au kutokupenda pesa. Umasikini kwa
kiasi kikubwa unasababishwa na utambuzi Hasi wa pesa. Mtu aliye na uelewa wa
kimasikini juu ya pesa huutafsiri uelewa huo kwenye karibu kila jambo
alifanyalo kuanzia kufikiri, kuona, kusikia, kunusa na hata kuhisi. Kila kitu
kwake ni vikwazo na uhaba tu.
Producer maarufu wa sinema nchini Marekani
Mike Todd aliwahi kutamka maneno haya; “Kufilisika ni hali ya muda mfupi tu
inayopita, lakini kuwa masikini ni hali ya kiakili”-Mike Todd. Na
alikuwa sahihi kabisa kwani ni kweli upo ushahidi wa matajiri waliowahi
kupoteza kila kitu walichokuwa nacho kwa sababu ya makosa mbalimbali ya
kibinadamu mfano hata Steve Jobs wa Apple, lakini hiyo haikuwafanya wabakie
kuwa masikini daima, badala yake kwa muda mfupi tu waliweza tena kurudisha kila
kitu kwa msaada wa utambuzi wao sahihi wa kifedha.
Njia
ya kupata fedha halisi, siyo makaratasi wala shaba.
........................................................
Mpenzi msomaji wa blogu hii baadhi ya makala za fedha kama hii huwa tunaweka hapa sehemu tu na sehemu inayobakia tunamalizia katika group la masomo ya kila siku watsap(MICHANGANUO-ONLINE). Tunafanya hivi kwa lengo la kutaka yule anayependa kujifunza zaidi basi aweze kupata fursa hiyo kwa kuchangia sehemu ndogo ya gharama za kuandaa masomo hayo adimu(exclusive).
Hata hivyo katika blogu hii zipo makala nyingine nyingi nzuri tunazoendelea kuziweka free kabisa bila kuchaji chochote kwa wasomaji wetu wapendwa ambao kwa namna moja ama nyingine bado hawajajaliwa kupata kiingilio cha group, kwani si nia yetu kuwaacha nyuma hata kidogo .
Hata hivyo katika blogu hii zipo makala nyingine nyingi nzuri tunazoendelea kuziweka free kabisa bila kuchaji chochote kwa wasomaji wetu wapendwa ambao kwa namna moja ama nyingine bado hawajajaliwa kupata kiingilio cha group, kwani si nia yetu kuwaacha nyuma hata kidogo .
Ikiwa basi unapenda kujiunga na masomo hayo kwa undani zaidi ikiwa ni pamoja na kupata vitabu, michanganuo na semina mbalimbali zote zilizopita katika hilo group, unalipia ada ya sh. elfu 10 tu ambayo ni bei iliyokuwa kwenye offa maalumu. Baada ya muda mfupi ujao offa hii haitokuwepo tena tunataraji kuitoa.
Lipia leo hii kupitia namba zangu, 0765553030 au 0712202244 nikutumie offa zote hizi hapa chini na pia tarehe 15 Septemba uingie katika Semina yetu ya 2 ya mchanganuo wa Kiwanda, mwezi AGOST tulikuwa na kiwanda cha Tofali za block. Mwezi huu wa SEPTEMBA tutakuwa na mchanganuo wa aina yake ambao tofauti na michanganuo mingine yote uliyowahi kusoma, huu utakuwa na ubunifu wa kipekee wa aina yake unaomwezesha mtu kwenda kuapply moja kwa moja mbinu hizo katika kiwanda chake kidogo cha USAGISHAJI WA NAFAKA. Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi za semina hii kila siku hapa....
Baadhi ya OFFA nilizosema ni hizi hapa chini;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu
kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu
kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu
kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.
5. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA:
Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza
9. Mchanganuo
wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
10.
Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara
inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
11.
Semina na mchanganuo wa Biashara: Kiwanda cha
tofali za saruji Kiluvya.
12.
Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2
IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja
au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
13.
Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.
14.
Ukurasa mmoja wa mchanganuo.
0 Response to "PESA TUONAZO NI MAKARATASI TU, JIFUNZE NJIA YA KUPATA PESA ZA UKWELI(HALISI)"
Post a Comment