Mpenzi msomaji wa blogu hii ya Jifunzeujasiriamali,
napenda kukujulisha kwamba zile semina zetu 4 za kuchanganua biashara bunifu za
viwanda sasa zinakaribia kuanza rasmi na siku ya Alhamisi tarehe 15 ndio
tutaanza na kiwanda kidogo cha kufyatua tofali za block kilichopo Kiluvya mkoa
wa Pwani.
Semina hii itaanza saa 5 asubuhi kwa maelezo kuhusu
utafiti wa biashara hiyo, kisha baadae ndipo tutaandika hatua kwa hatua
mchanganuo huo mzima tukianza na Maelezo ya mradi mpaka Sura ya mwisho ya
vielelezo. Kisha mwishoni kabisa tutaandika Muhtasari wa mchanganuo wetu.
Siku ya pili tutachambua kwa undani hesabu za mchanganuo
huo ili kila mshiriki aweze kuelewa vyema jinsi ya kukokotoa makisio ya taarifa
zote muhimu za fedha hasa makisio ya faida na hasara, mtiririko wa fedha,
Mizania ya biashara, Mauzo ya kurudisha gharama(Break even Analysis na Muda
mradi utakaporudisha mtaji uliotumika(Pay back Period)
Ikiwa unapenda kushiriki Semina hii unakaribishwa na
utaratibu uliopo ni kwamba, Unalipa kiingilio shilingi Elfu 10 kupitia namba
zifuatazo, 0712202244 au 0765553030 jina
Peter Augustino Tarimo. Muda wa mwisho ni siku ya Jumatano tarehe 14 usiku. Ada
hii utaweza kushiriki Michanganuo mingine yote 3 iliyobakia hadi mwezi Novemba.
Tuna offa kubwa kwa wale watakaoshiriki ya kupewa vitabu
na masomo yetu mbalimbali ya siku zilizopita. Offa ya vitu vilivyoorodheshwa
hapo chini ni ya muda mfupi sana hivyo watakaowahi tu ndio watanufaika nayo.
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu
kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu
kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu
kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.
5. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA:
Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza
9. Mchanganuo
wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
10.
Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara
inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
11.
Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2
IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja
au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
12.
Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.
13.
Ukurasa mmoja wa mchanganuo.
14.
SEMINA ya Mahesabu ya mpango wa
biashara(ADVANCED BUSINESS PLAN FINANCIALS)
SOMA PIA;
1.Ratiba ya masomo yatakayofundishwa katika semina ya mpango wa biashara.
2. Yaliyomo katika Semina ya jinsi ya kuandaa Hesabu za mpango wa Biashara.
1.Ratiba ya masomo yatakayofundishwa katika semina ya mpango wa biashara.
2. Yaliyomo katika Semina ya jinsi ya kuandaa Hesabu za mpango wa Biashara.
0 Response to "SEMINA YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA KIWANDA CHA TOFALI ZA SEMENTI - BADO SIKU 4 TU"
Post a Comment