Katika makala hii ya leo nitajibu swali juu
ya moja kati ya changamoto inayowakumba wajasiriamali wengi hasa pale
wanapotaka kuanzisha biashara zao. CHANGAMOTO YA MTAJI. Karibu usome kujua
changamoto hii ni vipi tunaweza kukabiliana nayo na hatimaye kuishinda.
Karibu kila mtu utakayemgusa kuhusiana na
kuanzisha biashara/ujasiriamali, kitu cha kwanza atakachokuambia ni; “Sina
mtaji, mtaji nitautoa wapi, mtaji nilio nao ni kidogo mno hutoshi nk.
Kwa wale waelimishaji wanaotoa elimu ya ujasiriamali kama mimi ukiwauliza ni
changamoto zipi kubwa wasomaji au wasikilizaji wa semina na masomo yao
wanazokutana nazo watakuambia changamoto kubwa wanayoombwa utatuzi wake ni hii
ya jinsi ya kupata mtaji kwa ajili ya kuanzishia biashara.
SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara mbili ya mtaji utakaowekeza?
SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara mbili ya mtaji utakaowekeza?
Swali nitakaloenda kujibu leo, lilitoka kwa
mfuatiliaji wangu mmoja kwa njia ya email, na nitalitaja jina lake moja tu,
Fredi. Fredi aliniuliza kama ifuatavyo,
Nashukuru Sana Kwa mafunzo yako lakini changamoto kwetu Sisi vijana ni moja na changamoto hiyo ndio inayotufanya mawazo mengi kuozea ndani, changamoto hiyo ni MITAJI Vipi tutapataje MITAJI ??
MAJIBU
Ngoja
nikuambie kitu kimoja Fred, Ukweli watu wengi wasioukubali ni kwamba,
haiwezekani kuanzisha kitu wakati tayari unacho. Kanuni ya kimaumbile
inajieleza wazi kwamba, “mtu huwa anataka
kuanzisha kitu au kuwa na kitu kwa sababu kitu hicho hana” Sijui kama
umenipata lakini nitafafanua zaidi usihofu.
SOMA: Biashara 5 za mtaji kidogo kuanzia elfu 2, kumi mpaka laki moja unazoweza kuanza zikakutoa.
SOMA: Biashara 5 za mtaji kidogo kuanzia elfu 2, kumi mpaka laki moja unazoweza kuanza zikakutoa.
Katika
kuielezea vizuri dhana hii, nitatumia mfano au kanuni mbili maarufu (Siyo za
kwangu, sijazitunga mimi) namimi nilijifunza tu mahali pengine. Kanuni hizo 2
ndiyo zinazoelezea pande zote mbili, ule wa wanaotaka kuanzisha biashara wakiwa
tayari na mitaji mkononi na upande wa pili ni wa wale wanaoanzisha biashara
wakiwa hawana kitu chochote kile kama mtaji isipokuwa mawazo yao pekee. Zishike
vizuri kanui hizi zinaweza kukusaidia.
(1)
Kumiliki –
Kufanya – Kuwa au (To have – To do – To Be)
(2)
Kuwa – Kufanya
– Kumiliki au (To Be – To do - To have)
1. Maana ya kanuni ya kwanza,
miliki-fanya-kuwa (have-do-be) ni kwamba, Ili uweze kuwa mtu fulani(kuwa)
unahitaji kwanza uwe unamliki kitu fulani(miliki) ndipo uweze kufanya kitu
fulani(kufanya) kitakachokuwezesha kuwa yule unayetaka kuwa. Kwa wale wote
wanaofikiria kwamba hawawezi kuanza biashara bila kwanza kuwa na mtaji wapo
kwenye kundi hili la (have-do-be). Mtu anafikiri ili
atajirike ni lazima awe na pesa kwanza ndipo afanye biashara itakayompeleka
kwenye utajiri au, Ili mtu awe na mahusiano mazuri ni lazima apendwe kwanza
ndipo na yeye aweze kupenda.
SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado.
SOMA: Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado.
Ikiwa wewe ni muumini wa kanuni hii ya kwanza
ya kuwa nacho kwanza ndipo utende, haitatokea siku uje ufanikiwe kamwe, labda
tu itokee umeshinda bahati na sibu jambo ambalo hutokea kwa nadra mno na kwa
watu wachache. Akili ya ‘mpaka uwe nacho’
itakuzuia kabisa kuanza kitu na hata kama utalazimisha vyovyote vile bado akili
hiyohiyo itakuja kukuambia tu ‘ACHA’
pale biashara kwa bahati mbaya itakapokuja kupitia vipindi vigumu kama cha kukosa pesa(mdororo),
hata ikiwa ni wa muda mfupi. Ni vigumu sana kuwa na hamasa ya kuendelea
kuwekeza katika biashara yako ukiwa na mawazo ya (To have – To do – To be)
2. Kwenye kanuni ya 2, Unakuwa kwanza vile
unavyotaka uwe, kabla ya mambo mengine yote(You be), kisha Unafanya(you
do) na mwishoni ndio unamiliki kitu(You
have). Huwa ukipanga namba mfano 3+5 jibu lake ni sawa tu na kusema 5+3
lakini kwa kanuni hizi 2 mambo ni tofauti kidogo, kumiliki – kufanya – kuwa siyo sawa na kusema, kuwa – kufanya – kumiliki. Wakati kanuni ya kwanza haileti matokeo
mazuri ile ya pili ndiyo kanuni ya kimafanikio kwa wale wote wanaoanza biashara
wanapaswa kuitumia.
SOMA: Kwanini vitabu na semina za elimu ya pesa na mafanikio haviwasaidii watu wngi?
SOMA: Kwanini vitabu na semina za elimu ya pesa na mafanikio haviwasaidii watu wngi?
Mwandishi mmoja, Stephen Covey aliwahi kusema
kwamba,
“Katika maisha kila mtu huumbika mara
mbili, kwanza ni katika akili yake na pili ni katika mwili wa nyama(material
world)” - Stephen Covey
Tunapozungumzia (Kuwa – Kufanya – Kumiliki) tunaingia moja kwa moja kwenye mpango wa
biashara. Wakati ukifanya mpango wa biashara yako unaweza kuwa huna chochote
kile mfukoni lakini mpango wa biashara unakusukuma wewe kuifahamu biashara yako
nje ndani kabla hata haujaianzisha. Unatengeneza Maono*Vision). Maono au vision
ndio ‘To be yako/ jinsi unavyotaka uje kuwa’ miaka kadhaa ijayo. Na ndio maana
katika mpango wa biashara huwa Visio na Mission tunaviweka vitu vya mwanzo
mwanzo kabisa ili kutupa picha ya jinsi tunavyotaka tuje tuwe kabla hata hatujawa
kiuhalisia.
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako
SOMA: Jinsi mpango wa biashara unavyoweza kuongeza mafanikio ya biashara yako
Kuamua unataka kuwa nani maishani(To be) huwa haigharimu kitu chochote
kile ni mawazo tu ila kinachohitajika hapo ni muda wa kufikiria pamoja na
kufanya utafiti. Unawekeza muda wako katika mchakato wa kuwa yule unayetaka
kuwa. Maarifa yote utakayoyapata kutokana na mchakato huo ndiyo sasa
yatakayokulazimisha kufanya VITENDO,
na Vitendo mwishowe ndiyo vitakavyosababisha MATOKEO umiliki kitu.
Maneno haya matatu, KUWA – KUFANYA – KUMILIKI yanaweza yakabadilisha kabisa maisha yako
ikiwa utaamua kuyazingatia. Kwa mfano watu wakishafahamu kuwa wewe ni muaminifu
wanaweza kukupa mali kwa malikauli tu bila ya kutoa pesa na utakapokwenda kuuza
tayari unamiliki faida yake bila kuwa na mtaji wakwako mwenyewe. Hivyo
Utahitaji tu muda wa kupalilia aina nyinginezo za mitaji tofauti na pesa ili
kupata cha kuanzia na si lazima uwe na mtaji PESA.
SOMA: Biashara ndogondogo 7 zenye faida kubwa unazoweza kuanzisha bila mtaji kabisa.
SOMA: Biashara ndogondogo 7 zenye faida kubwa unazoweza kuanzisha bila mtaji kabisa.
Mtaji mwingine ni maarifa, tenga muda wako
kidogo wa kupata maarifa mbalimbali mfano hata maarifa ya kuanzisha viwanda
vidogovidogo kupitia Group la MICHANGANUO-ONLINE na mwisho wa siku unaanzisha
kiwanda chako kidogo kwa mtaji kidogo sana au bila ya mtaji kabisa wa fedha.
Usije ukakubali mawazo yako yakaozea ndani kwa ndani kisa eti ni mtaji. Kuna
mitaji ya aina nyingi zaidi ya pesa unayoweza ukaitumia kuanzisha biashara
yako, kinachohitajika ni ubunifu tu na muda wako, na baada ya muda pesa
zitakuja zenyewe.
Sisemi kwamba mtaji wa pesa siyo muhimu hapana, pesa za kutosha ni muhimu sana hasa pale ambapo unakuwa sasa umeshatengeneza biashara endelevu inayoingiza pesa. Ijapokuwa pesa inazoingiza siyo nyingi sana lakini angalao una uhakika ni lazima kila siku au kila mwezi iingize kiasi fulani cha fedha bila kutegemea mtaji kutoka nje.
SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji wa kutosha ni wasa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini
Sasa ikifikia hatua hii ndiyo muda muafaka wa kwenda kutafuta pesa nje kama vile kutoka mabenki na taasisi nyinginezo mbalimbali za kifedha kwani unao uhakika biashara itakuwa na uwezo wa kuzirejesha.
Sisemi kwamba mtaji wa pesa siyo muhimu hapana, pesa za kutosha ni muhimu sana hasa pale ambapo unakuwa sasa umeshatengeneza biashara endelevu inayoingiza pesa. Ijapokuwa pesa inazoingiza siyo nyingi sana lakini angalao una uhakika ni lazima kila siku au kila mwezi iingize kiasi fulani cha fedha bila kutegemea mtaji kutoka nje.
SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji wa kutosha ni wasa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini
Sasa ikifikia hatua hii ndiyo muda muafaka wa kwenda kutafuta pesa nje kama vile kutoka mabenki na taasisi nyinginezo mbalimbali za kifedha kwani unao uhakika biashara itakuwa na uwezo wa kuzirejesha.
……………………………………………………..
TAARIFA HII NI KWA ANAYEHITAJI TU.
Taarifa au matangazo ninayoyatoa hapa chini
hayahusiani na somo ulilosoma bali hii ni njia tu ya kukujulisha mambo mengine
tunayotarajia kuwa nayo au tayari yapo.
1.KITABU
KIPYA!
Kile kitabu nilichoahidi katika makala
iliyopita kimetoka rasmi hapo jana tarehe 5 September 2019 na kinaitwa, SAIKOLOJIA NA UTAMBUZI WA HALI YA JUU
KIFEDHA. Kitabu hiki bei yake ni shilingi 10,000/= na ukikinunua ndani ya
wiki hii unapata na offa INAYOISHIA YA VITU14, Semina yetu ya kiwanda cha tofali za saruji ya
mwezi uliopita pamoja na kujiunga na Group la MICHANGANUO-ONLINE.
Kupata kitabu hicho na OFFA zote nilizotaja
lipia sh. Elfu 10 kupitia namba, 0765553030 au 0712202244 na ujumbe wa wasap au SMS
usemao, “NITUMIE KITABU CHA SAIKOLOJIA
YA PESA NA OFFA INAYOISHA MUDA WAKE”
2.SEMINA
YA KIWANDA SEPTEMBA 15
Semina yetu ya pili kuhusu viwanda vidogo
zimebakia siku 10 tokea siku ya leo. Semina itahusu, KIWANDA CHA USAGISHAJI NAFAKA na mchanganuo wake unatarajiwa kuwa
na ubunifu wa kipekee hasa katika eneo la Soko. Si semina ya kukosa kabisa
ikiwa wewe ni mtu mwenye maono ya kumiliki kiwanda siku moja. Kujiunga na
semina hiyo lipia kama nilivyoeleza hapo juu kwenye taarifa ya Kitabu kipya.
3.MASOMO
YA KILA SIKU YA FEDHA
Ndani ya group la MICHANGANUO ONLINE masomo
ndiyo yanashika kasi kila siku, masomo yetu ni ya kipekee, huwezi kuyapata
mahali pengine popote pale. Kujiunga lipia kama ilivyoelezwa kwenye namba 1
hapo juu.
4. KIWANDA
CHANGU MWENYEWE
Niliahidi katikati ya hizi semina za kila
mwezi za viwanda nitazindua kiwanda changu mwenyewe, na wewe nitakushirikisha
katika uzinduzi huo. Namshukuru Mungu maandalizi yanaenda vizuri na tayari
nimeshaanza kuzalisha prototype(bidhaa za mfano) Ni aina ya kiwanda kidogo
lakini unaweza ukakiweka katika viwanda vya kati ikiwa mtu unazo rasilimali
nyingi kidogo. Cha kuvutia zaidi kiwanda hiki umetumika ubunifu zaidi, mtaji wa
pesa ni kidogo sana. Naamini nitawafundisha na wengine wengi watakaopenda
kuanzisha katika maeneo yao. Habari zaidi nitaendelea kukujuza kabla ya siku ya
uzinduzi wenyewe rasmi.
ASANTE KWA MUDA WAKO,
PETER A. TARIMO
WHATSAPP: 0765553030
0 Response to "KUPATA MTAJI WA BIASHARA CHA MSINGI NI WAZO NA MUDA WAKO, PESA BAADAE"
Post a Comment