PANADO YA UKOSEFU WA PESA NA KANUNI (2) ZA KUSHIKA KABLA HUJAENDA KUKOPA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

PANADO YA UKOSEFU WA PESA NA KANUNI (2) ZA KUSHIKA KABLA HUJAENDA KUKOPA

maumivu makali ya kichwa
Katika Ulimwngu wa leo ni jambo la kawaida kusikia matangazo kwenye redio au Tv yakisifia ubora wa dawa za kupunguza maumivu ya aina mbalimbali kuanzia maumivu ya kichwa, mgongo, tumbo, kiuno, maumivu ya mwili mzima au hata maumivu yatokanayo na magojwa makubwa kabisa ambayo madaktari wana namna ya kumpa mgojwa nafuu hata ikiwa hakuna tiba kamili. Tukirudi katika Ulimwengui wa pesa pia mikopo  kama isipotumika kwa umakini huwa haina tofauti sana na hizi dawa za kupunguza maumivu kama panadol au asprin.

Mkopo hasa ule wa matumizi ya kawaida unaweza ukampunguzia mtu dalili za maumivu yatokanayo na ukosefu wa pesa kwa muda mfupi tu na huku tatizo likiwa bado lipo palepale. Udhaifu kipesa ni tatizo la watu wengi iwe ni katika matumizi tu ya kawaida au hata fedha kwa ajili ya biashara. Moja ya suluhisho la tatizo hili ni mkopo ambao kwa wengi unakuwa ni kama Panado huku kwa baadhi ya wale waliokuwa makini ukiwa kama quinine(dawa ya kutibu tatizo moja kwa moja)

Kwanini na ni lini Mkopo unakuwa Panadol?
Mkopo unatuongezea matatizo ya kifedha badala ya kuyatibu pale unapotupatia ahueni ya muda tu kwa kutuaminisha  uwongo kwamba, sasa tumeondokana na umasikini. Kumbuka mara nyingi wakati unapokwenda kuomba mkopo inamaana kwamba tayari wewe hali yako ni tete na huna uwezo wa aidha kuendesha maisha yako binafsi au kuendesha biashara yako kwa fedha zako mwenyewe. Hivyo mkopo dhumuni lake kuu ni kutatua hili tatizo kwa muda. Lakini mkopo huo unaweza kukudhoofisha zaidi siku za baadae kutokana na sababu kwamba utarejesha mkopo na riba juu ingawa pia unaahidiwa kulipa kidogokidogo. Kulipa kidogokidogo kunakupa tu unafuu wa kisaikolojia lakini ukweli ni kwamba mzigo upo palepale ukikuelemea.

Sasa basi mkopo unakuwa kama panadol pale ambapo ukishamaliza kuuchukua unakwenda kufanya matumizi ya kawaida ya kimaisha kama vile kununulia chakula au mahitaji mengine ya nyumbani vikiwemo vifaa au vyombo mbalimbali vya ndani kama vile sofa, friji sufuria, sahani nk. Haijalishi kama umechukua mkopo kwa ajili ya biashara au kwa ajili ya matumizi ya kawaida kama ule wanaochukua waajiriwa wengi makazini mwao, mkopo usiokuwa wa biashara inayozalisha pesa ni shida! na lazima ukuumize tu.

Sasa ni muda muafaka wa kwenda kuziona zile kanuni kuu mbili(2) nilizokuahidi pale mwanzoni, zikoje?..

Kanuni 2 za kuzingatia, piga ua, kabla hujaamua ukakope pesa kwa ajili ya matumizi yeyote yale iwe biashara au binafsi.


Kanuni (1)........................................


Mpenzi msomaji, ungependa kuyasoma masomo haya yote kwa ukamilifu wake? Usikose kuungana na mimi katika MASTREMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE nimekukusanyia masomo yote mazuri tunayojifunza kila siku!

Unapolipia kiingilio chako cha shilingi elfu 10, unakuwa mwanachama, lakini pia nakutumia offa ya masomo, michanganuo, seminars na vitabu mbalimbali muda huohuo. OFFA hii ya vitu vingi utachagua mwenyewe usome nini kwa jinsi ilivyokuwa na wingi wa vitu. OFFA ni ya muda mfupi na inakaribia kuisha.

Pia utapata fursa ya kushiriki katika seminar zetu za kila mwezi juu ya michanganuo ya biashara za viwanda vidogovidogo bunifu. Mwezi huu tarehe 15 tutakuwa na semina ya kiwanda cha USAGISHAJI NAFAKA baada ya mwezi uliopita kuwa na ya KIWANDA CHA TOFALI ZA SARUJI. Semina hizi zinaamsha ari ya mtu kuanzisha kiwanda anachokitaka.

Kwa yule asiyependa kujiunga na magroup au wasiotumia WHATSAPP, email inatosha kwani tunatuma masomo na vitu vyote kwa email pia.

Namba za malipo ni 0765553030 au 0712202244 baada ya kulipia tuma ujumbe wasap au SMS ya kawaida ukisema; 

"NIUNGANISHE NA GROUP PAMOJA NA OFFA INAYOKARIBIA MWISHO"

0 Response to "PANADO YA UKOSEFU WA PESA NA KANUNI (2) ZA KUSHIKA KABLA HUJAENDA KUKOPA"

Post a Comment