KITABU CHA MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA TOLEO JIPYA 2020 (NEW EDITION) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KITABU CHA MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA TOLEO JIPYA 2020 (NEW EDITION)

SIRI YA MAFANIKIO BIASHARA YA REJAREJA
Kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA, DUKA LA REJAREJA 2020 NEW EDITION kimefanyiwa mabadiliko makubwa na tayari kimeshaanza kuuzwa ijapokuwa uzinduzi wake utafanyika rasmi ifikapo Januari 2020 mwakani. Bei yake pia itabadilika kidogo na kuwa shilingi elfu 15 badala ya elfu 10 ya zamani kwa kitabu cha karatasi(hardcopy), na sh. elfu 5  nakalatete (Softcopy).

Hata hivyo mabadiliko hayo ya bei bado hayajaanza rasmi, wateja wataendelea kujipatia kitabu hicho kipya kwa bei ileile ya zamani(Hii ni offa kwa mwezi huu wa Novemba na Desemba tu). Bei mpya zitaanza mwezi Januari tarehe itakayotangazwa baadae.

BAADHI YA MABADILIKO MAKUBWA YALIYOFANYIKA.
Sura za kitabu zimeongezewa vipengele vipya sambamba na vile vilivyokuwepo zamani. Kwa ujumla Kitabu kimekuwa na kurasa(Pages) 140 badala ya kurasa(Pages) 105 zilizokuwepo katika kitabu cha zamani(Old version)

Jalada upande wa mbele(Front Page):
Tukianza na jalada ukurasa wa mbele kabisa, pamewekwa maneno juu kabisa yanayosema, “New Edition 2020” . Jalada pia limengarishwa zaidi na kuwa na mng’ao wa kuvutia tofauti na lile la zamani.

Jalada upande wa nyuma(Back Page):
Pamoja na ‘nakshinakshi’ ndogondogo lakini pia ukurasa huu pameongezwa picha ya Mwandishi wa kitabu hiki kwenye kona kabisa upande wa kulia kwako halafu juu pamewekwa Bei mpya itakayoanza rasmi Januari mwakani, sh. 15,000/=

UKURASA WA YALIYOMO.
Badala ya kuonyesha kurasa zenye Sura peke yake, toleo hili katika YALIYOMO tumeweka kurasa zote zilizobeba vipengele vikuu katika kila sura husika kumrahisishia msomaji kazi ya kufungua kipengele akitakacho mara moja bila usumbufu. Sura kuu zipo 5 kila moja na vipengele vyake vya kutosha.(Vilivyooongezwa na kuboreshwa)

SURA YA KWANZA
Katika kipengele cha, “HATUA 10 ZA KUANZISHA BIASHARA YA REJAREJA (DUKA)” kipengele kidogo cha, “Jinsi ya kupata mtaji wa biashara yako ya duka la rejareja”, zimeelezewa mbinu mbalimbali watu wanazotumia kupata mtaji wa kuanzisha maduka yao lakini kitu cha pekee zaidi kwenye kipengele hicho ni Shuhuda za watu mbalimbali wakielezea namna walivyoanzisha biashara ya duka.

Miongoni mwa shuhuda hizo ni ule wa Mwandishi wa kitabu hiki Bwana Peter A. Tarimo akielezea njia alizotumia mpaka akaweza kuanzisha duka lake mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es salaa akiwa hana mtaji hata wa senti tano mfukoni. Ushuhuda huo unaambatana na picha mbalimbali(za mnato) alizopiga akiwa kwenye biashara hiyo katika nyakati tofauti ikiwemo picha moja(huwezi kuamini) aliyoipiga siku ya kwanza kabisa wakati anaanza moja.

Picha hizo 8, zote ni za rangi (FULL COLOUR) kwa hiyo zinaonekana ‘live’ kabisa bila chengachenga zozote kwenye nakala zote mbili za kitabu(hardcopy na softcopy)  


SURA YA PILI
Katika kitabu toleo lile la zamani, sura hii ilizungumzia mada mbalimbali zinazohusiana na mbinu mbalimbali za kuwavuta wateja kama ‘sumaku’ na miongoni mwa mbinu hizo tulikuwa tumegusia kwa uchache baadhi ya mbinu na ‘technics’ za kienyeji zinazotumiwa na baadhi ya wamiliki wa maduka lakini pia zile za Kisasa au za Kisayansi.

Mbinu hizo hususan zile za kienyeji(Kiafrika) zisizokuwa za Kisayansi(naamini ndugu msomaji unanielewa ninaposema mbinu za kienyeji au za kitamaduni) ikiwa nimekuacha basi wala usijali, tafuta kitabu hiki utanipata vizuri zaidi.

Basi katika toleo hili Mbinu hizo za kuwavutia wateja ‘tumezitolea uvivu’ na kuja na “ripoti kamili” baada ya utafiti wa kina tulioufanya kwa kuzunguka baadhi ya Mikoa ya Tanzania ukiwemo Mkoa wa Mwanza, Ruvuma, Kilimanjaro, Moro, Pwani na Tanga. Tuna mbinu za aina mbili tulizokuja nazo, zile za Kisayansi na zile za Kienyeji. Nikisema za kisayansi namaanisha mbinu za Kimasoko za kawaida zinazofundishwa vyuoni na mashuleni lakini zile za kienyeji au za kiasili hazifundishwi rasmi mahali popote pale, bali watu wanazijua tu kupitia masimulizi ya mdomo kwa mdomo mitaani, kizazi hata kizazi.

Ni katika sura hii pekee unapoweza kupata ufafanuzi na elimu ya kutosha kabisa kuhusiana na dhana mbalimbali ambazo pengine hapo kabla ulikuwa huzielewi vizuri zina mchango gani katika biashara. Dhana hizo kwa mfano, Ushirikina, Uganga, Uchawi, Chuma-ulete na Miujiza mingine ya kiimani katika biashara hususani ile ya duka la rejareja zimeelezewa kwa kina kabisa, faida na madhara yake.

Kwanini maduka mengine utakuta wateja wamejaa muda wote lakini mengine muuzaji anashinda akipiga miayo mchana kutwa?, Sura hii imeelezea kila kitu. Kwanini wengine huona wanauza sana lakini wakati wa kufunga hesabu zao usiku mauzo yanakuwa kidogo, ni nini kinachukua mauzo hayo na ni nini cha kufanya mauzo yasipotee tena?, yoote haya sura hii inayajibu bila kigugumizi.


SURA YA TATU
Katika Sura hii ya tatu nayo  pamoja na vipengele vile vya toleo la zamani lakini kuna kipengele kimoja kipya kabisa ukurasa wa 63. Kama uliwahi kusoma somo la Fizikia sekondari au hata somo la Sayansi primary darasa la tatu bila shaka ulijifunza kuhusiana na kitu kimoja kinachoitwa NYENZO au kwa kimombo LEVER(Leveraging).

Nyenzo au ‘lever’ maana yake ni kitu kinachoweza kikarahisisha kazi fulani. Tuchukulie mfano wa mtu anayetaka kubeba jiwe kuubwa! kutoka sehemu ‘A’ na kulifikisha sehemu ‘B’. Kutokana na ugumu au uzito wa kazi hiyo mtu huyu itambidi atumie mti, chuma ama kifaa kingine chochote kile kwa ajili ya kulibiringisha jiwe hilo mpaka kulifikisha eneo “B”.

Na kwenye biashara hususani ya duka la rejareja pia kuna nyenzo muhimu sana mbili ambazo zikitumiwa kwa usahihi zina uwezo wa kumfanya mmiliki wa duka kukuza duka lake haraka au hata kufungua maduka mengi ndani ya kipindi kifupi kabisa mpaka watu wakashangaa. Kuna kitu kingine pia cha kusisimua sana kwenye hiyohiyo nyenzo kiitwacho, Sheria ya Kidole(The Rule Of Thumb). Ufafanuzi wake ni moja ya vitu vipya katika toleo jipya la kitabu hiki 2020.


SURA YA NNE
Kwa kweli moja ya kitu kikubwa sana kilichosababisha tukifanyie marekebisho makubwa kitabu hiki ni JINSI YA KUSIMAMIA HESABU ZA DUKA LA REJAREJA HASA PALE MTU ANAPOAMUA KUMUAJIRI MFANYAKAZI AU MSAIDIZI.

“Nilikuwa nikipatwa na mshangao mkubwa baada ya baadhi ya wateja walionunua kitabu changu toleo la zamani kurudi na kuzidi kuniuliza niwapatie njia wanazoweza kutumia ili kudhibiti hesabu za maduka yao wasiibiwe na wafanyakazi/wasaidizi”- PETER A. TARIMO

Dada mmoja anayefanya kazi katika kampuni moja ya simu baada ya kuomba mkopo kazini kwake aliamua kufungua duka la rejareja mtaani kwake akamweka kijana pale, lakini baada ya muda mchache alianza kuhisi kijana anamuibia, ghafla akamtimua na kuanza kutafuta kijana mwingine. Kwa muda wa miezi 6 alikuwa keshabadilisha vijana zaidi ya 4 wasichana kwa wavulana na duka bado likazidi kuzorota.

Nilipozungumza naye akanieleza, nikagundua duka lake alikuwa akilisimamia kwa mazoea, siku haendi kazini kama jumapili na siku za sikukuu humwambia mfanyakazi apumzike kisha yeye hukaa dukani mwenyewe kwa madai kwamba anacheki kile alichokiita “movement ya wateja” kama kipimo cha iwapo mfanyakazi anamuibia au la. Lakini alisahau kwamba mauzo ya weekend au siku za sikukuu hayafanani kabisa na  ya siku za kawaida. Hivyo bila shaka nikagundua sababu kubwa ya kuwatimua wale wafanyakazi ilikuwa ni tofauti kubwa ya mauzo baina ya siku alizokuwa akikaa yeye na zile walizokuwa wakikaa wafanyakazi wake.”-PETER A. TARIMO

Tofauti na toleo lililopita, katika toleo hili jipya la 2020, tumeonyesha “EXACTLY” kabisa bila chengachenga zozote zile ni nini hasa cha kufanya ili hata ukimwachia mtu biashara yako ya duka basi hesabu uzikute vilevile na faida kamili iliyoongezeka. Namaanisha Stoku unayoacha uje uikute thamani yake iko vilevile na faida iliyoongezeka pia uikute haijapungua.

Tumeelezea pia mifumo mbalimbali ya usimamizi wa duka la rejareja pamoja na mfumo unaomfaa zaidi mtu ambaye ndiyo kwanza anaanzisha biashara hii, bado hajapata uzoefu wala mtaji mkubwa.

Uzuri mmoja ni kwamba baadhi ya mifumo  iliyopendekezwa humu katika hili toleo ni ile ambayo haimhitaji mtu akasomee IT kwanza ndipo aje aitumie, mtu mwenye elimu ya kawaida kabisa na hata ambaye hajasoma hata darasani, ilimradi tu anajua kusoma na kuandika anaweza akaitumia.

SURA YA TANO
Katika toleo la zamani kwenye “Mchanganuo Kamili wa Biashara ya Duka la Rejareja(MSUYA SHOPPING CENTRE LILILOPO KITUO KIKUU CHA MABASI UBUNGO TERMINAL)” kuna kasoro ndogondogo zilizokuwepo na zote zimerekebishwa katika toleo hili, majedwali na chati zilizokuwa hazisomeki vizuri zote nazo zimeboreshwa upya.


JINSI YA KUKIPATA KITABU HIKI

(A) Kitabu cha karatasi(HARDCOPY)
Dar es salaa, Ukija Mbezi kwa wakala wetu mkuu kabla ya January 2020 unapata kitabu hiki kwa sh. 10,000/= tu ila baada ya hapo bei itabadilika na kuwa sh. 15,0000/= Vinapatikana BGIGHT STATIONARY iliyopo Mbezi Kibanda cha Mkaa kituo cha bajaji au bodaboda ni  Mwembeni jirani na Shule ya Sekondari St. Augustino(TAGASTE)

Mikoani tunatuma kwa njia ya mabasi ila gharama ya basi  na mtu wa kukipeleka Stendi-Ubungo huongezeka kutegemea aina ya basi na umbali kinapofika. Lakini mikoa mingi gharama ya kifurushi (parcel) ni sh. elfu 10, mtu wa kukipeleka stendi Ubungo sh. elfu 2,  hivyo jumla inaweza kufika mpaka sh. elfu 22 au chini ya hapo kulingana na gharama watu wa basi watakayochaji.


(B) Kitabu kwa njia ya mtandao(SOFTCOPY)
Kabla ya Januari, Ukilipia kitabu SH. 5,000/=  kupitia namba zetu za simu, 0765553030 AU 0712202244 na sisi tutakutumia nakala yako kupitia e-mail muda huohuo bila kuchelewa. Huwa hazizidi dakika 5 toka malipo mpaka kupokea kitabu. Jina hutokea PETER AUGUSTINO TARIMO.


ASANTE SANA, UKAUANZE MWAKA 2020 KWA MTAZAMO MPYA KABISA!

0 Response to "KITABU CHA MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA TOLEO JIPYA 2020 (NEW EDITION)"

Post a Comment