Duniani kuna vitu
ambavyo umewahi kusikia kwamba havipitwi na muda(timeless/classic) au kwa maana
nyingine ni kwamba kadiri muda unavyozidi kupita basi navyo ndio vinazidi tu
kuwa bora. Nitajaribu kuvitaja baadhi ya vitu hivyo hapa chini japo najua
kunaweza kuwa na vitu vingi zaidi ya hivyo.
DHAHABU:
Nikianza na madini
haya adimu duniani ni kwamba inasemekana hata kabla ya kugunduliwa kwa hela
yalikuwa ndiyo yanayotumika kama njia kuu ya kubadilishana vitu kutokana na
dhahabu kuwa ‘timeless’. Dhahabu uitie kwenye moto mkali, uitwangetwange kwa
mawe, sijui uifanyie shuruba gani ndio kwanzaa! inazidi kung’ara.
MVINYO (WINE)
Ukitaka kujua maajabu
ya mvinyo nenda nchi kama Ufaransa, zipo chupa za mvinyo zimehifadhiwa ardhini
miaka mia tatu(300) iliyopita, huwezi amini lakini bado unaambia ndio kwanza
zinazidi ‘kuwiva’ na ubora wake
kuongezeka mara dufu sambamba na thamani au bei yake kuongezeka pia. Si ajabu
ukaambiwa chupa moja tu ya mvinyo kama huo ni shilingi za kibongo mamilioni.
![]() |
Mvinyo wa miaka 300
|
MUZIKI MZURI:
Kuna baadhi ya nyimbo
zilizowahi kuimbwa miaka mingi iliyopita lakini kila unapozisikiliza utadhania
zimerekodiwa jana. Si lazima mziki ninaouona mimi ‘classic’ na mtu mwingine
auone hivyohivyo lakini zipo nyimbo asilimia kubwa ya watu utasikia wakisema ni
classic. Kwa mfano Kuna vibao kama
vilivyopigwa na bendi ya Less Wanyika zaidi ya miaka 30 iliyopita kama hiki cha
“Ufukara siyo kilema” hapo chini, ukiusikiliza leo hii mashairi na hata
midundo yake utadhani ni mpya.
Vibao vya kizungu pia
vipo vingi ila hapa nitatolea mfano
mmoja wa kibao cha msanii ‘Michael Learns to Rock’ kilichotoka tangu mwaka 1996, “Breaking
my heart” . Ukikisikiliza hata leo bado ni kama kimetoka jana. Kuna
mamia ya nyimbo zisizopitwa na wakati tukiziorodhesha hapa hapatatosha.
VITABU:
Vitabu navyo halikadhalika vinaingia kwenye orodha, siyo
kila kitabu hapana kuna baadhi yake na unapozungumzia vitabu visivyopitwa na
wakati kwa kweli vipo vingi na katika tasnia mbalimbali pia. Mimi leo sitataja
orodha ya vitabu hivyo kidunia, nitafanya hivyo siku nyingine ila ninachotaka
kuelezea hapa tu ni juu ya vitabu 3 vya
Self Help Books Tanzania. Si kama labda najifagilia au kuvutia kamba kwangu
kwakuwa ni mdau wa kampuni hii hapana, bali kuelezea tu ukweli ulivyo.
KWANINI
VITABU HIVI NI TIMELESS(CLASSIC)
Sababu kubwa ni
kwamba, maudhui ya vitabu hivi yanahusu Biashara, Ujasiriamali na Mafanikio kwa
ujumla wake vitu ambavyo pia kila siku mwanadamu amekuwa akishughulika navyo.
Binadamu anapozaliwa haijalishi ni katika zama zipi lakini ni lazima atafute
mafanikio katika nyanja mbalimbali hususani katika kipato kwa njia mbalimbali
kubwa ikiwa ni Biashara na Ujasiriamali
Biashara
& Ujasiriamali
kwa maana pana zaidi inagusa mpaka Ajira
na shughuli nyingine zote zikiwamo hata zile za kujitolea kama vile kwenye Dini
mbalimbali, Wachungaji, Mapadre, Mashehe, Maimamu na Watumishi wengine wa Mungu.
Unapopata maarifa yaliyokuwemo katika vitabu hivi unakuwa na wewe miongoni mwa
watu wasiopitwa na wakati(classic
person)
Narudia tena, sina
maana kuwa classic books ni hivi “Self
Help Books” tu peke yake hapana, ila nasema kwamba ni miongoni mwake, vipo
vingine vingi hata hapa Tanzania ingawa unapaswa uwe makini kuchuja kipi ni
kipi.
Kitu kingine ni
kwamba unaweza kukuta kitabu ni classic lakini mwandishi akawa mvivu na kuweka
vitu vichache huku akilenga kuja kutoa toleo la kitabu kingine aweze kupata
pesa nyingi, lakini sisi Self help Books hatupo hivyo. Mpaka watu wengi
wameniuliza mara nyingi Swali hili, “Kwani nyie Self Help Books hampati hasara kuchapisha vitabu vyenye kurasa nyingi namna
hiyo?”
Mimi huwajibu tu
kwamba, waendelee kufurahia vitabu vyetu kwani dhamira yetu kubwa ni kuona
wanafanikiwa kimaisha na hususani katika Nyanja za biashara na ujasiriamali.
Katika kuzidi
kuvifanya vitabu hivi kuwa timeless au classic basi mwaka huu wa 2020 tumeamua
kuvifanyia marekebisho makubwa vitabu vyetu vyote 3. Ingawa maudhui
hayajabadilika lakini kuna baadhi ya vitu vilivyoongezwa ili kuboresha zaidi
uelewa wa msomaji. Mabadiliko mengine mfano bei siyo makubwa sana na ni kwa
baadhi tu ya vitabu hasa kile cha BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA ingawa pia
madadiliko hayo bado hayajaanza rasmi.
Tumeboresha pia
upatikanaji wa vitabu vyetu kwa kuhakikisha kwamba yeyote anayehitaji kitabu
popote pale alipo tunamtumia au anapata kwa mawakala wetu Dar es salaam na
mikoani.
JINSI
YA KUPATA VITABU 3 VYA SELF HELP BOOKS (3 TIMELESS CLASSIC BOOKS)
1.
HARDCOPY(VITABU VYA KARATASI)
Vinapatikana katika
Steshenari iitwayo BRIGHT STATIONERY iliyopo Mbezi Kibanda cha mkaa. Ukifika Kibanda cha mkaa, panda bajaji au
bodabona waambie wakushushe kituo cha KWA MOTA . Ni jirani na shule ya
secondary ya ST. AUGUSTINO (TAGASTE)
Ukitaka uletewe
kitabu/vitabu ulipo Dar es salaam
utaongeza gharama za basi sh. 2,000/=.
Mikoani tunatuma kwa
njia ya mabasi na gharama za basi hutegemea aina ya basi na umbali ulipo lakini
‘maximum’ ni sh. elfu 10 mikoa mingi kwa bahasha (percel) moja ya vitabu.
2.
SOFTCOPY(KWA NJIA YA MTANDAO-EMAIL)
Tunatuma kitabu/vitabu
popote pale mteja anapokuwa amelipia kitabu/vitabu. Ni ndani ya dakika 5 tu na
hazizidi 10 toka kutuma mpaka kupokea vitabu/kitabu
Ukitaka vitabu
vingine na Michanganuo ya Biashara kutoka Self Help Books Tanzania unaweza
ukatembelea DUKA LETU LA MTANDAONI LIITWALO (SMART BOOKS TANZANIA) HAPA na kuchagua ni
kipi unachohitaji.
0 Response to "VITABU 3 VISIVYOCHUJA KAMWE (THREE TIMELESS CLASSIC BOOKS OF ALL TIMES)"
Post a Comment