Ni kauli maarufu na
iliyozoeleka na watu wengi kwamba ili mtu aweze kuanzisha biashara yake
mwenyewe hitaji kubwa ni mtu huyo kwanza kuwa na sifa zote za ujasiriamali. Kauli
hii kwa kiasi kikubwa imekuwa ikiwafanya wajasirimali wengi wachanga kujawa na
hofu ya kuchukua hatua ya kuanzisha biashara zao na kuendelea kubakia kwenye
ajira zinazowabana muda wote wa maisha yao au kuendelea kufanya shughuli
zinazowawezesha kupata mlo wa siku tu ilimradi maisha yanasonga mbele.
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.
SOMA: Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa hata kama umelala.
Lakini tunaporudi
katika uhalisia wa mambo, siyo rahisi kwa mtu anayetaka kuanzisha biashara
aweze kuwa na sifa zote kamili za ujasiriamali. Ndio maana basi katika Makala
hii nimejaribu kuziorodhesha dalili muhimu ambazo pindi uzionapo na wewe ni
muajiriwa mahali, basi ni muda muafaka kwako wa kufikiria kuanzisha biashara
yako mwenyewe na wala usianze tena kufikiria juu ya kutimiza vigezo vyote vya
kuwa mjasiriamali bora ndio uanze. Utatimiza mbele kwa mbele
SOMA: Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri mwenyewe?
SOMA: Kwanini ni rahisi zaidi kutajirika ukiwa kwenye ajira kuliko kujiajiri mwenyewe?
Si lazima uachane na
kazi yako ghafla hapana, unaweza kuanza kidogo kwa kufungua biashara ya ndoto
yako lakini katika ngazi ya awali kabisa huku ukijpanga mdogomdogo(Start small but keep thinking big),
mfano mzuri ni pale mtu anapoanzisha café ya kuuza maziwa, chai na vitafunwa
kumbe yeye lengo lake kichwani ni kuja kumiliki mkahawa mkubwa kama wa Mc
Donald’s. Si kama fedha za kufungua mkahawa anakuwa hana, ila anataka kwanza
apate uzoefu wa biashara ya vyakula kabla hajajiingiza mzimamzima.
Kuna biashara za aina
nyingi, nyingine ni za uwekezaji usiohitaji muda wako hata sekunde moja
ukishawekeza mfano uwekezaji katika hisa, mifuko ya fedha nk, achilia mbali
kwenye ardhi na majengo. Kwa hiyo hapa hamna “excuse” hata kidogo ikiwa unakumbana na dalili hizi nitakazokwenda
kuzielezea hapo chini.
SOMA: Hatua 6 za uwekezaji fedha zako usipate hasara au kufeli.
SOMA: Hatua 6 za uwekezaji fedha zako usipate hasara au kufeli.
Tena isitoshe basi
suala la uwekezaji si lazima uache ajira yako ndipo uwekeze, unaweza ukaitumia
nguvu hii ya ajabu matajiri wengi waliyowahi kuitumia kama inavyofafanua makala
ya kipekee(exclusive report) tutakayojifunza leo Januari tarehe 11 usiku saa 3
kwenye Mastermind group la wasap la Michanuo-online isemayo, “AJABU LA 8 LA DUNIA: NGUVU YA KUSHANGAZA IWEZAYO KUMTAJIRISHA MTU
BILA YA KUTOA JASHO” .
Kimsingi kabisa ni
kwamba ajira siyo kitu kibaya hata kidogo kama watu wengi wanavyodhania, bali katika
mzunguko wa maisha ya binadamu ajira inapaswa tu iwe ni daraja la kuvukia
kuelekea katika biashara au uwekezaji binafsi(Uhuru wa kifedha).
SOMA: Ajira siyo laana, bali ni mtaji wa uhakika kuliko aina nyingine zote za mitaji.
SOMA: Ajira siyo laana, bali ni mtaji wa uhakika kuliko aina nyingine zote za mitaji.
Katika maajabu hayo
ya 8 ya dunia, nguvu kuu inayotajwa hutegemea sana vigezo au vitu vingine
muhimu 3 na kimoja kati yake ni MUDA. Ndiyo maana katika somo hilo nakushauri
kama wewe ni kijana jitahidi sana usilikose somo hilo kwani lina ujumbe mzito
na muhimu mno kwako, sina maana wazee au wenye umri mkubwa haliwahusu hapana,
bali vijana lina umuhimu wa kipekee zadi kwao somo hili adimu.
Baada ya hayo
machache hebu tuzione dalili hizo kuu 5 ambazo kama mwanzoni mwa mwaka huu wa
2020 unaziona katika eneo lako la kazi/ajira, basi hujachelewa, chukua hatua
kungali mapema.
1.
Hakuna tena kupandishwa daraja wala promosheni.
Na hata kama kukikiwepo
basi kunakuzidishia tu msongo wa mawazo badala ya kukupa faraja. Usikubali
katika ajira yako uishi na msongo wa mawazo (stress) au karaha, labda tu iwe wewe ndiye mtu unayelipwa pesa
nyingi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote katika kampuni/biashara hiyo.
SOMA: Stress za pesa zinavyoweza kuzima kabisa ndoto za mtu na hatua za kuchukua haraka.
SOMA: Stress za pesa zinavyoweza kuzima kabisa ndoto za mtu na hatua za kuchukua haraka.
2. Sasa
unao uwezo wa kufanya vitu kwa weledi zaidi.
Ukiona dalili kwamba
uwezo wa utendaji wako wa kazi unazidi hata ule wa bosi wako, basi fahamu ni
muda muafaka kwako wa kuanzisha biashara yako mwenyewe kwani bosi wako au mabosi wako kamwe
hawataweza kukupatia nafasi ya kuonyesha unawazidi kiutendaji.
3. Una
mawazo mazuri.
Unajaribu kutoa
mawazo mazuri jinsi ya kuboresha biashara lakini kwa bahati mbaya, si bosi wako
wala meneja anayehangaika kulitambua hilo. Watu pekee wanaotamba juhudi zako
wanabakia kuwa ni wale wateja unaowahudumia tu.
SOMA: Unapoajiri au kuajiriwa zingatia umuhimu wa kujua ni nini unachokitaka.
SOMA: Unapoajiri au kuajiriwa zingatia umuhimu wa kujua ni nini unachokitaka.
4. Unahisi
kuchoshwa na mwenye kukosa hamasa.
Ujuzi na taaluma yako
hauvitumii ipasavyo na wala havithaminiwi tena kama inavyostahili na mabosi
wako. Unaona kabisa uzoefu wako unapotea bure na wewe huna tofauti na wale
wafanyakazi wanaofanya mazoezi bure(internship). Uonapo dalili hii,
usiendelee kupoteza muda, ni wakati wako muafaka sasa na wewe kwenda kuitwa
Mkurugenzi(CEO)
5. Baada
ya kunyimwa promosheni na maslahi uliyostahili.
Sasa umehamishiwa
ofisi nyingine nje kabisa ya mji au iliyopo mkoa wa mbali. Hapa huna chaguo
jingine zaidi ya kuanzisha Biashara/Kampuni yako mwenyewe
mwisho
……………………………………………….
TAARIFA
MUHIMU SANA!
1. MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP 2020
Napenda kukufahamisha
mpenzi msomaji wa blogu ya jifunzeujasiriamali kwamba Group lako la MICHANGANUO-ONLINE kwa mwaka 2020 ndio
linaanza rasmi leo tarehe 11 Januari, saa 3 usiku baada ya kazi ya kusajili
wanachama upya.
Somo la leo saa 3
usiku linasema hivi;
“AJABU
LA 8 LA DUNIA: NGUVU YA KUSHANGAZA IWEZAYO KUMTAJIRISHA MTU BILA YA KUTOA
JASHO”
Utaratibu rasmi wa
ratiba zetu utatolewa kwenye group lakini kwa ujumla tu ni kwamba mwaka huu
kaulimbiu yetu kuu bado ni ileile ya Viwanda ila tumebadili kidogo maneno na kuiita, “THE 2020 TANZANIA INDUSTRIAL REVOLUTION IS POSSIBLE, PLAY YOUR PART”
Mwenyezi Mungu akipenda tunatarajia 2020 hii tufanye mambo makubwa sana katika
sekta hii ya viwanda vidogo.
Tutaaanza kwanza na
kumalizia kiporo cha michanganuo ya viwanda bunifu vitatu(3) vya mwaka jana
ambayo hatukuweza kuimalizia kutokana na muda mwingi kuishia katika maandalizi
ya kiwanda changu nilichotarajia kuwaonyesha lakini kwa bahati mbaya muda
tuliokadiria haukutosha, kazi likuwa nzito.
Kisha baada ya hapo
tutakuwa na uzinduzi wa hicho kiwanda chenyewe ambacho kama nilivyoahidi tangu
2019 kitakuwa ni cha ubunifu wa kipekee sana na nitawaonyesha wadau kwa njia ya
picha za video jinsi kilivyoundwa A – Z, na ni kwa namna gani kinavyofanya kazi.
Mpaka sasa hivi kimeshaanza uzalishaji wa awali na bidhaa zipo sokoni.
Nikuibie tu siri
kidogo, ni kwamba kiwanda hicho kinatumia mtaji mdogo sana wa pesa, sehemu
kubwa ni nguvu na utaalamu binafsi tu vinavyohitajika. Ni teknolojia ambayo
hapa Tanzania sijapata kuiona na hata katika baadhi ya nchi zingine ipo lakini
haijarahisishwa kama tulivyofanya sisi. Kwahiyo ni kitu cha kipekee sana hapa
Tanzania.
2. SEMINA YA KUANDAA MCHANGANUO WA BIASHARA YA KIWANDA CHA UNGA
SUPER WA DONA TAREHE 20/01/2020
Semina hii pamoja na
nyingine za viwanda tofauti 2 zilikuwa zifanyike toka mwaka jana 2019 lakini
hatukuweza kutekeleza na tarehe 20/01/2020 ndiyo siku tutakayofanya semina hii
ndani ya group letu halafu semina nyingine zitafuata siku zijazo.
JINSI YA KUJIUNGA NA GROUP
Ili mtu uweze
kujiunga na MASTERMIND GROUP LA
MICHANGANUO-ONLINE na kufaidi masomo ya fedha kila siku pamoja na semina
hizi za mara kwa mara za viwanda bunifu unatakiwa kulipa ada ya mwaka mzima
ambayo ni shilingi 10,000/=(Elfu kumi tu)
Namba zetu unazoweza
kulipia ni; 0765553030 au
0712202244 na jina ni Peter
Augustino Tarimo. Ukishalipa nitumie ujumbe wa watsap au sms kwenye 0765553030
usemao, NIUNGE NA MASTERMIND GROUP 2020.
Nitakuunganisha ndani ya dk. 3 tu pamoja na kukutumia offa ya masomo yote yaliyopita bure.
Wahi pia na offa ya
kupata masomo, semina na michanganuo yote iliyopia 2019 kabla ya tarehe 15 kupita. Tarehe 15
ikipita ofa hii itakuwa imeisha muda wake na utaweza kujiunga na group na
kupata masomo na semina za 2020 tu peke yake.
Aidha nafasi za group
zilizobakia pia siyo nyingi, hivyo ni vizuri kuwahi ili zisijekujaa ukakosa
nafasi yako 2020 na mambo yote mazuri tuliyoandaa.
ASANTE NA KARIBU SANA KUNDINI
Mwanaviwanda wako/Industrialist
PETER AUGUSTINO TARIMO
WATSAP: 0765553030
SIMU: 0712202244
0 Response to "2020 UKIONA DALILI HIZI 5 BASI UJUE NI MUDA SAHIHI WA KUANZISHA BIASHARA YAKO MWENYEWE"
Post a Comment