Nguvu hii ndiyo sababu kubwa kwanini Matajiri
ni matajiri na Masikini ni masikini.
Kitu kingine cha ajabu ni kwamba nguvu hii haina ubaguzi, pale inapotumiwa
vizuri na mtu yeyote yule awe masikini, awe tajiri, awe Mzungu , awe Mwafrika,
awe mlemavu, awe ni mtu wa dini yeyote ile au kabila, wote wana nafasi sawa
ikiwa wataamua kuitumia nguvu hii kwa faida yao. Hutoa matokeo sawasawa kwa
yeyote aitumiaye.
Inavyofanya kazi ni kama upanga ukatao pande
zote mbili, huku na huku. Maana yake ni kwamba unapoitumia vizuri
inakutajirisha na unapoitumia vibaya pia inakutia umasikini wa maisha mpaka
unaingia kaburini, na ukicheza hata kizazi chako chote kitakuwa masikini. Nguvu
hii inaitwa RIBA AMBATANI au kwa
kimombo wanaiita “COMPOUND INTEREST”
SOMA: Kwanini mikopo ya riba mitaani, michezo ya upatu na baadhi ya viccoba si salama kujiunga?
SOMA: Kwanini mikopo ya riba mitaani, michezo ya upatu na baadhi ya viccoba si salama kujiunga?
Mwanasayansi Mashuhuri zaidi Duniani Albert
Einstain aliwahi kutoa kauli maarufu sana juu ya riba ambatani akisema hivi;-
“Nguvu
kubwa zaidi Ulimwenguni ni Riba ambatani, yeyote yule anayeitumia vyema
humtajirisha ….. na yeyote yule anayeifuja humgharimu”-Albert Einstain
Riba
Ambatani(Compound Interest ni kitu Gani?
Hebu tuanze na maana ya Riba yenyewe kwanza,
Riba kwa lugha rahisi kabisa ni faida inayopatikana baada ya mtu au taasisi
kukopesha fedha zake kwa mtu mwingine au taasisi. Au pia Riba inaweza kuwa ni
gharama(hasara) inayotozwa baada ya mtu au taasisi kukopa pesa.
SOMA: Sababu kubwa 9 Duniani kwanini watu hukopa pesa, 4 kati yake ni za kuogopa kama ukoma.
SOMA: Sababu kubwa 9 Duniani kwanini watu hukopa pesa, 4 kati yake ni za kuogopa kama ukoma.
Mabenki na taasisi za kifedha huchaji Riba
wanapokopesha, halikadhalika mtu unapokwenda kukopa fedha huchajiwa riba. Riba
pia hutolewa na makampuni mbalimbali kama gawio la hisa kwa wanahisa
waliowekeza fedha zao, ijapokuwa hawaiti riba lakini gawio halina tofauti kubwa
na riba.
Kwa hiyo hii Riba(faida) ama Interest kwa kimombo zipo za aina mbili, Riba
rahisi(Simple Interest) na Riba tata/ambatani(Compound Interest). Tuchukulie
mfano umeweka fedha zako sh. 1,000,000/=
kwenye akaunti ya benki inayolipa riba ya asilimia 1% kwa mwaka. Hii inamaana
kwa kutumia riba rahisi utapata shilingi elfu 10 kila mwisho wa mwaka kama
riba. Kwa miaka tuseme miwili utapata shilingi elfu 20 kama riba ukiweka na
salio la mwanzo jumla itakuwa shilingi 1020,000(Milioni moja na elfu ishirini)
SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake: njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima.
SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake: njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima.
Tukija kwenye Riba tata au ambatani(compound
interest) mambo ni tofauti , Riba ya mwaka wa kwanza sh. elfu 10 mwaka wa pili riba
hii nayo itazaa. Kwahiyo badala ya elfu 20 mwaka wa pili hesabu itakuwa hivi; asilimia
1% ya 1,010,000 ya mwaka wa pili sawa na sh. 20,100 jumlisha na ile riba ya
mwaka wa kwanza sh. Elfu 10, hivyo jumla utapokea riba ya shilingi 20,100
badala ya 20,000 tu tuliyoona kwenye ‘simple interest’.
Unaweza kufikiria ni kwa namna gani ongezeko
la riba kidogo namna hii sh. 100 linaweza likafanya maajabu ya kumtajirisha mtu
bila jasho, lakini fahamu kwamba Riba ambatani huanza kidogo sana kama
tutakavyoona hapo chini na kwa kadiri muda unavyopita nayo huongezeka haraka
kimaajabu(Exponentially). Haina tofauti na mti unavyoota.
SOMA: Je wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya 4 madogomadogo?
SOMA: Je wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya 4 madogomadogo?
Mche wa mti unapokuwa mdogo sana huota
taratibu kabisa, seli mpya huzaliwa huku nazo zikizaa nyingine sambamba na zile
za zamani. Baada ya miaka kama 7 hivi huko, mti huo hautaujua tena kwa jinsi
utakavyokuwa ukikua kwa kasi, matawi na shina vikiongezeka huku mizizi nayo
ikienda mbali kutafuta virutubishi zaidi. Miaka kadhaa baadae mti huu unakuja
kukushinda hata kuukata mwenyewe mpaka unaamua kuutafutia chain saw na watu wa kukusaidia.
Kila nguvu yeyote kubwa hapa Duniani
unayoiona ilianza hivyo hivyo, mto mkubwa kama vile Nile na Amazon mwanzo wake
ni vijito vidogovidogo, baada ya muda na umbali wa kilomita nyingi vijito hivyo
vilibadilika na kuwa mito mikubwa isiyoweza kuzuilika kirahisi. Hivyohivyo na
mabonge ya barafu yanayobiringika toka milimani, huanza kama kigololi kidogo na
baadae kadiri kinavyobiringika huongeza kasi na uzito hatimaye kuangamiza hata
kijiji kizima.
SOMA: Kanuni ya siri ya Cocacola, birika la ajabu na wazo la dolla millioni moja.
SOMA: Kanuni ya siri ya Cocacola, birika la ajabu na wazo la dolla millioni moja.
Je, ungependa kufahamu vitu 3 muhimu
vinavyoifanya riba ambatani kutimiza maajabu yake kwa ukamilifu Zaidi? Na vipi
kama ungeliijua miradi inayoweza kukupatia riba ambatani na ukaanza kuifanya
mara moja? Halikadhalika jinsi riba ambatani inavyoweza kumtajirisha mtu hata
pasipo kufanya kazi(bila ya kutoa jasho). Na je, ungetaka riba ambatani ikufanyie
maajabu unapaswa utimize kigezo kipi? Kuna wakati pia riba ambatani inaweza
kugeuka kuwa adui mkubwa kwako, ni wakati gani huo na vipi unaweza ukakwepa
isigeuke?
Na mwisho kabisa ni Riba ambatani katika
Ulimwengu wa Kiislamu, tunazungumzia nguvu hii ya ajabu, je wenzetu Waislamu
wanaichukuliaje kulingana na muongozo wa dini yao? Inamaana Uarabuni na zile
nchi za Kiislamu au hata taasisi zinazoheshimu Utamaduni wa Kiislamu hapa nchini hakuna matajiri
wanaoitumia nguvu hii ya riba ambatani? Kama hamna sasa wanapatajepataje faida
katika biashara zao?
Masomo haya hapa ni kama tone dogo tu la maji ndani ya bahari kubwa. Unaweza kuyapata yote kwa ukamilifu wake baada ya kujiunga
na kundi letu la masomo ya fedha la kila siku whatsapp la MICHANGANUO-ONLINE MASTER MIND GROUP
Kujiunga na group hili kuna ada ya mwaka mzima ambayo shilingi 10,000/= tu. Ada hii ni kwa ajili ya Vitabu mbalimbali, semina na masomo utakayopokea kwa mwaka mzima wa 2020.
Aidha kwa anayewahi kabla ya tarehe 15 January kujiunga na group atapata OFFA kubwa ya Vitabu, semina na Masomo mbalimbaili vilivyopita mwaka 2019. Offa hiyo hii hii hapa chini;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu
kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1
3. Kitabu
kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2
4. Kitabu
kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.
5. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.
6. SEMINA:
Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.
7. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)
8. Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza
9. Mchanganuo
wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
10.
Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara
inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.
11.
Semina na mchanganuo wa Biashara: Kiwanda cha
tofali za saruji Kiluvya.
12.
Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2
IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja
au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5
13.
Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.
14.
Ukurasa mmoja wa mchanganuo.
Kujiunga Lipia ada ya mwaka Sh. 10,000/= kwa namba, 0765553030 au 0712202244 kisha tuma ujumbe wa whatsapp au wa kawaida kwenye namba, 0765553030 usemao; "NIUNGANISHE GROUP LA MICHANGANUO-MASTERMIND2020 PAMOJA NA OFFA INAYOMALIZIKA"
Baada ya hapo nitakutumia kla kitu kama ilivyoelezwa hapo juu pamoja na kukuunganisha na group ndani ya dk.5
KARIBU SANA!
Peter Augustino Tarimo
Mwandishi,Mhamasishaji na Mwanaviwanda 2020.
0 Response to "AJABU LA 8 LA DUNIA: NGUVU YA KUSHANGAZA INAYOWEZA KUMTAJIRISHA MTU BILA YA KUTOA JASHO"
Post a Comment