Naomba usininukuu vibaya, katika somo hili sizungumzii
matatizo ya pesa yatokanayo na magojwa, ajali au kufiwa, bali ni matatizo yote
ambayo mara nyingi hutokana na matakwa yetu wenyewe au matumizi ya hiyari ya pesa.
Umewahi kuwaza siku moja kwamba hata kama ungeoliongezewa
mshahara mara 2 ya ule wa sasa bado usingeliweza kumaliza matatizo yako ya
fedha yanayokukabili?. Kuna wakati mwingine mtu hata angepata mshahara sawa na ule anaopata bosi wake bado
ataendelea tu kuhaha kuwa matatizo hayaishi.
SOMA: Unategemea mshahara wa mwezi au kipato kimoja? hizi hapa mbinu za kujinasua na kuishi maisha mazuri unayotamani.
SOMA: Unategemea mshahara wa mwezi au kipato kimoja? hizi hapa mbinu za kujinasua na kuishi maisha mazuri unayotamani.
Chanzo cha hali kama hii kinaweza kikaelezwa kwa ufasaha
na kanuni moja mashuhuri ijulikanayo kama Parkinson’s
Law ambayo kimsingi inasema hivi; “Matumizi yanapoona kipato kinaongezeka, nayo
pia huongezeka kuhakikisha yanakwenda sambamba nayo” Na hii ndiyo
sababu kubwa watu wengi sana hulalamika kuwa wanapokuwa hawana pesa mfukoni
hakuna tatizo lolote linalojitokeza, lakini mara tu wanaposhika kiasi fulani cha
pesa mfukoni, huibuka tatizo linalohitaji kiasi kilekile cha pesa walichoshika.
Ni maajabu sana haya!
Watu tunadhani yakwamba dawa ya kukomesha matatizo yetu
mbalimbali ya kimaisha basi ni kupata
pesa zaidi, lakini ukweli mara nyingi huwa ni kuyazidisha zaidi matatizo hayo na
hili lipo wazi kabisa kwani tuna mifano ya watu wengi tena mashuhuri Duniani na
hapa Tanzania.
SOMA: Watu na pesa: yapo makundi matatu(3) duniani, je wajua wewe upo kundi gani?
SOMA: Watu na pesa: yapo makundi matatu(3) duniani, je wajua wewe upo kundi gani?
Unamkunbuka gwiji wa Muziki wa Pop Duniani Michael
Jackson maarufu kama Wacko Jacko, wakati fulani aliwahi kuwa Billionea mkubwa
lakini huwezi kuamini mpaka siku anaingia kaburini Wacko alikuwa akikabiliwa na
madeni ya kutisha, siku za mwisho za uhai wake zilitawaliwa na huzuni ya
kutisha. Ni nini alichokosea au kufanya ndivyo sivyo, nitakujulisha taratibu
kwenye somo hili adimu.
Naye Mrembo mweusi wa Kimarekani na Muimbaji mashuhuri
Whitney Houston licha ya kuchuma mamillioni ya pesa kipindi cha uimbaji wake,
baada tu ya kifo chake alikutwa na dolla elfu 29 tu katika akaunti yake ya
benki huku akiwa na madeni lukuki. Hali ni hivyohivyo kwa watu wengine maarufu
kama vile Marehemu Brenda Facy na wengineo wengi. Kwa upande wa hapa Bongo nisingelipenda
niwataje live kwani nadhani utakuwa unawajua mwenyewe.
SOMA: Vipaji, uwezo, akili ni vitu watu wanazaliwa navyo au kujifunza?
SOMA: Vipaji, uwezo, akili ni vitu watu wanazaliwa navyo au kujifunza?
Watu wote hawa waliwahi kushika pesa za ajabu, sasa
ingelikuwa kama pesa zaidi zina uwezo wa kuondoa matatizo, watu hawa mashuhuri walishindwa
vipi kuyaondoa matatizo yao hata kwa kuomba mashabiki wawachangie mia mia mpaka
wakaishia kufilisika namna hii?
Ni nini suluhisho la tatizo hili na linasababishwa na
kitu gani hasa? Je, unakabiliwa na madeni makubwa yaliyotokana na matumizi yako
mwenyewe yasiyokuwa ya lazima? Basi somo hili litakufaa sana hakikisha leo saa
3 hulikosi ndani ya MASTERMIND GROUP LA WASAP LA MICHANGANUO-ONLINE.
Kujiunga Lipia ada ya mwaka mzima sh. Elfu 10 tu uweze
kuwahi na Semina ijayo ya jinsi ya kuandaa mchanganuo wa kiwanda cha unga wa
Dona(Super) siku ya ya tarehe 20/1/2020
0 Response to "KWANINI TUNAISINGIZIA PESA KILA TATIZO LINALOTUPATA KATIKA MAISHA YETU?"
Post a Comment