MCHANGANUO WA BIASHARA YA CAR WASH, KUOSHA MAGARI, MTAJI NA VIFAA VINAVYOHITAJIKA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MCHANGANUO WA BIASHARA YA CAR WASH, KUOSHA MAGARI, MTAJI NA VIFAA VINAVYOHITAJIKA


Katika safu ya maswali na majibu leo hii kuna mdau wetu mmoja katika group la Michanganuo-online aliyetaka kujua kwa ufupi mchanganuo wa biashara ya Car Wash au uoshaji wa magari, bei za vifaa pamoja na mtaji, aliuliza hivi kwa njia ya whatsapp;


Biashara ya uoshaji wa magari maarufu kama “car wash” ni biashara ambayo mahitaji yake hutegemea unataka uanzishe biashara ya ukubwa gani. Kwa mfano kuna,

·      Carwash ndogondogo za hali ya chini kabisa,
·      Car wash za kati na
·      Car wash kubwa za hali ya juu(full car engine and body washing)

Tukiacha Car wash za hali ya chini kabisa ambazo mtaji wake hauhitaji zaidi ya madumu yako mawili, ndoo, kitambaa na eneo lenye mto au kijito cha maji, car wash yeyote ile ya kati au kubwa itahitaji vitu(vifaa) muhimu vifuatavyo;

1.   Pressure washer(Compressors)
2.   Vacuum cleaner
3.   Tanki la maji
4.   Brashi, ndoo, mataulo na vyombo vingine vidogovidogo
5.   Madawa kwa ajili ya kuoshea magari kama shampoo na sabuni

Vilevile vifaa vilivyotajwa hapo juu vipo vya hadhi ya juu sana kutoka nchi za Ulaya na Marekani kama vile, USA, Ujerumani, Ufaransa, na Uingereza(UK). Lakini pia kuna vifaa vya bei chee vinavyofanya kazi kama hiyohiyo vya Mchina.

PRESSURE WASHER(COMPRESSOR)
Baadhi ya vifaana zana vya kuoshea magari(car wash tools)

Mfano Pressure washer kutoka Ulaya kama vile KARCHER, BOSCH, SIMPSON nk. huweza kuanzia Tsh. 500,000/= hadi tsh. 2,000,000/= wakati vile vya mchina kutoka nchini China vinavyofanya kazi kama hiyohiyo huanzia tsh. 150,000/= mpaka 200,000/= na kuendelea kutegemeana na aina na ukubwa wake katika vipimo vya Kilowatt au Horsepower. Kuna vifaa pia vinavyotumia umeme na vinavyotumia mafuta(dizeli)

Halikadhalika vifaa vinginevyo kama Vacuum cleaner, kuna za kuanzia shilingi za kitanzania 30,000/= mpaka laki 3(300,000/=) na kuendelea kulingana na aina, nchi itokako na ukubwa kama nilivyotangulia kusema.

Kutokana na maelezo hayo sasa hapa chini nitaweka makadirio ya haraharaka tu ya kuanzisha biashara ya uoshaji wa magari(car wash business) katika category 3(makundi matatu), car wash ya hali ya chini kabisa, car wash ya hali ya kawaida ya kati na ya tatu ni car wash ya hali ya juu yenye mpaka winchi ya kunyanyulia magari wakati wa kuosha (car washing lift).


Mchanganuo wa biashara ya Car Wash ya hali ya chini kabisa;

Eneo la kukodi kwa mwezi

30,000
Tenki la maji lita 1000 au 500 used

70,000
Ndoo mabeseni na madumu                   

30,000
Sabuni za unga
10,000
Madodoki na Brush
10,000
JUMLA
150,000

Car wash ya hali ya chini kabisa(Mtaji kati ya laki 1 hadi laki moja na nusu)  ikiwa eneo halina mto, kijito au chanzo kingine chochote kile cha maji karibu, itabidi kuwepo na chombo kikubwa kwa ajili ya kuhifadhia maji kama vile tenki ukubwa wowote utakaoona unamudu kununua. Pia waweza kuosha magari kienyeji kwa kutumia tu brashi, madodoki na vitambaa, lakini huwezi kutoza bei kubwa sawa na car wash zenye vyombo vya kisasa.


Mchanganuo: Car Wash ya kawaida(hali ya kati)
Pango(Eneo)miezi 6       
300,000
Leseni na vibali
100,000
Pressure washer
250,000
Vacuum cleaner
60,000
Tank la maji
500,000
Mfumo wa maji
300,000
Madawa, shampoo sabuni nk.

50,000
Vyombo, ndoo, brush nk
50,000
Mengineyo
100,000
JUMLA
1,710,000 

Kwa hiyo kwa makadirio ukiwa na shilingi kuanzia milioni moja na nusu(1,500,000) mpaka 2,000,000/=  unaweza kuanzisha car wash yako ya kawaida yenye vifaa vyote muhimu. Kwa kuanzia unaweza ukanunua vifaa used kutoka Ulaya/Marekani au hata ukaamua kununua vifaa kutoka china.                                                  

Mchanganuo wa Car Wash ya hali ya Juu:
Pango(Eneo)miezi 6       
1,200,000
Leseni na vibali
200,000
Pressure washer
1,500,000
Vacuum cleaner
300,000
Car wash lift
1,500,000
Tank la maji
1,200,000
Mfumo wa maji
500,000
Mfumo wa umeme
500,000
Madawa, shampoo sabuni nk.

500,000
Vyombo, ndoo, brush nk
300,000
Mengineyo
300,000
JUMLA
8,000,000

Unaweza pia kusoma makala zifuatazo;

1. Mchanganuo wa biashara ya duka la kuuza vinywaji baridi mchanganyiko na maji.

2. Jinsi ya kuandika mchanganuo wa biashara ya kiwanda cha tofali za saruji.

3. Mchanganuo wa kuanzisha biashara ya kampuni ya Ulinzi(Nyuki security)

4. Biashara ya mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado.

5 Responses to "MCHANGANUO WA BIASHARA YA CAR WASH, KUOSHA MAGARI, MTAJI NA VIFAA VINAVYOHITAJIKA"

  1. Ombi langu ni moja hamna group la WhatsApp mniunge ilituwe tunapata habari mala kwa mala.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Karibu sana kaka, group la watsap lipo linaitwa, MICHANGANUO-ONLINE. Sharti moja tu ni kwamba, ili mtu aweze kushiriki anapaswa kulipia kitabu chetu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI sh. elfu 10 ambacho pamoja na vingine tunavyomtumia vitamwezesha kushiriki masomo yetu ya michanganuo ya biashara ndani ya group hilo kila siku

      Delete
  2. Air watts are calculated using the formula, (Air Flow (in CFM) x Vacuum (in inches of water lift))/8.5 = Air Watts. cheap vacuum cleaner

    ReplyDelete
  3. The plan of action would permit him to, in any event in his speculative strategy, assist administrators with improving and offer them backing and demographic for a reasonable expense, while building the client records and customer base. Best Jump Starters for Cars

    ReplyDelete
  4. Your drapes and curtains will be returned free of dust and allergens.
    We Wash 24 Laundry Service

    ReplyDelete